Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

`

Mungu ananuia kuangamiza ulimwengu kwa gharika, anamwagiza Nuhu kuijenga safina

(Mwa 6:9-14) Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu: Nuhu alikuwa mtu wa haki na mkamilifu katika vizazi vyake, na Nuhu alitembea pamoja na Mungu. Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, dunia ilijaa dhuluma. Mungu akaingalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; maana kila mwenye mwili alikuwa amejiharibia njia yake duniani. Na Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu dunia imejawa na dhuluma kupitia kwao; na, tazama, Nitawaharibu pamoja na dunia. Ujitengenezee safina ya mti wa mvinje; utatengeneza vyumba ndani ya safina, na uifunike ndani na nje kwa lami.

(Mwa 6:18-22) Lakini nawe Nitalifanya agano langu kuwa thabiti; nawe utakuja katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao pamoja nawe. Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwaweka hai pamoja nawe; watakuwa mume na mke. Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna watakuja kwako, ili uwaweke hai. Na ujichukulie chakula cha kila namna kinacholika, ukikusanye kwako; nacho kitakuwa ni chakula chenu, na chao. Ndivyo alivyofanya Nuhu; kulingana na vyote ambavyo Mungu alimwamuru, hivyo ndivyo alivyofanya.

….

Katika enzi hiyo, Mungu alinuia kumuita Nuhu ili kufanya kitu muhimu sana. Kwa nini ilikuwa lazima Afanye hivyo? Kwa sababu Mungu alikuwa na mpango kwa moyo Wake wakati huo. Mpango Wake ulikuwa kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Kwa nini auangamize ulimwengu? Maandiko yanasema hivi: “Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, dunia ilijaa dhuluma.” Mnaona nini kutoka kwenye kauli “dunia ilijaa dhuluma”? Ni ajabu duniani wakati ulimwengu na watu wake wanapotoka kwa kupindukia, na ni hivi: “dunia ilijaa dhuluma.” Katika lugha ya leo, “ikajaa dhuluma” inamaanisha kila kitu kimechanganyika. Kwa binadamu, inamaanisha kwamba katika nyanja zote za maisha hakuna mpangilio, na mambo yamejaa fujo kweli na ni magumu kudhibiti. Katika macho ya Mungu, inamaanisha watu wa ulimwengu wamepotoka sana. Wamepotoka hadi kiwango gani? Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu hawezi tena kuvumilia kuangalia na hawezi tena kuwa na subira kuhusu hali hiyo. Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu anaamua kuwaangamiza. Wakati Mungu alipoamua kuuangamiza ulimwengu, Alipanga kupata mtu wa kuijenga safina. Kisha Mungu akamchagua Nuhu kufanya kitu hicho, ambacho ni kumruhusu Nuhu kuijenga safina. ...

Kwamba Nuhu alihitajika ni ukweli mdogo, lakini hoja kuu ya kile tunachozungumzia sasa—tabia ya Mungu, mapenzi Yake kiini Chake halisi katika rekodi hii—si rahisi. Ili kuelewa dhana hizi mbalimbali za Mungu lazima kwanza tuelewe ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hutamani kuita, nakupitia hii, tuweze kuelewa tabia yake, mapenzi yake na kiini chake halisi. Kufanya hivi ni muhimu. Hivyo katika macho ya Mungu, mtu huyu ni wa aina gani ambaye yeye humwita? Huyu lazima awe ni mtu anayeweza kuyasikiza maneno Yake. Wakati huohuo, lazima mtu huyu awe yule wa kuwajibika, mtu atakayetekeleza neno la Mungu kwa kuliona kuwa jukumu na wajibu ambao anahitajika kukamilisha. Basi mtu huyu anahitajika kuwa mtu anayemjua Mungu? La. Hapo nyuma, Nuhu hakuwa ameyasikia sana mafundisho ya Mungu wala kupitia kazi yoyote ile ya Mungu. Hivyo basi, maarifa ya Nuhu kumhusu Mungu yalikuwa madogo mno. Ingawaje imerekodiwa hapa kwamba Nuhu alitembea na Mungu, aliwahi kuuona ubinafsi wa Mungu ? Jibu ni bila shaka la! Kwa sababu katika siku hizo, wajumbe wa Mungu tu ndio waliowaendea watu. Ingawa waliweza kuawakilisha Mungu katika kusema na kufanya mambo, walikuwa wakipitisha tu mapenzi na nia Zake. Ubinafsi wa Mungu haukufichuliwa kwa binadamu uso-kwa- macho. Kwenye sehemu hii ya maandiko, chote tunachoona tu ni kile ambacho mtu huyu Nuhu alilazimika kufanya na maagizo ya Mungu kwake yalikuwa gani. Hivyo basi ni kiini kipi kilichoonyeshwa na Mungu hapa? Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu dunia imejawa na dhuluma kupitia kwao; na, tazama, Nitawaharibu pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaingalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; maana kila mwenye mwili alikuwa amejiharibia njia yake duniani.” Kauli hii “maana kila mwenye mwili alikuwa amejiharibia njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu,wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioaminii, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika.

….

Katika hali hizi, Mungu anajali kuhusu nini zaidi? Si vile wale wasiomfuata Yeye kabisa au wale wanaompinga Yeye kwa vyovyote vile wanamshughulikia Yeye au kumpinga Yeye, au namna ambavyo mwanadamu anamdanganya Yeye. Anajali tu kuhusu kama wale wanaomfuata Yeye, walengwa wa wokovu Wake katika mpango Wake wa usimamizi, wamewekwa kamili na Yeye, na kama wametimiza utoshelezi Wake. Kuhusiana na watu wale wengine bali na wale wanaomfuata Yeye, Anawatolea tu adhabu kidogo mara kwa mara ili kuonyesha ghadhabu Yake. Kwa mfano tsunami, mitetemeko ya ardhi, kuibuka kwa volkano na kadhalika. Wakati huohuo, Anawalinda kwa dhati na kuwashughulikia wale wanaomfuata Yeye na karibu wanaokolewa na Yeye. Tabia ya Mungu ni hii: Kwa mkono mmoja, Anaweza kuwapatia watu Anaonuia kutekeleza subira na ustahimilivu kamili wa kupindukia na kuwasubiria wao kwa muda mrefu Anavyoweza; kwa mkono mwingine, Mungu anachukia na kuchukizwa kwa dhati na watu wa aina ya Shetani wasiomfuata Yeye na wanaompinga Yeye. Ingawaje Hajali kama hawa watu wa aina ya Shetani wanamfuata au wanamwabudu Yeye, bado Anawachukia wao huku akiwa na subira na wao katika moyo Wake, na Anapoamua mwisho wa hawa watu wa aina ya Shetani, Yeye pia anasubiria kufika kwa hatua za mpango Wake wa usimamizi.

kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha

Inayofuata:Kuhusiana na Baraka za Mungu kwa Nuhu Baada ya Gharika

Unaweza Pia Kupenda