Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

433 Kupata Mwili kwa Mungu Kwawafunua Watu Wote

1 Nitatimiza moja baada ya lingine, kupitia uungu Wangu, kila kitu ambacho Nimenena kutoka kwa ubinadamu Wangu wa kawaida. Hii ndiyo sababu Ninaendelea kusema kuwa kile Ninachosema kitafanyika bila ya utata wowote; badala yake, yote yatakuwa wazi na dhahiri sana. Kila kitu Ninachosema kitatimizwa, na hakika hakitatendeka ovyoovyo. Sizungumzi maneno matupu na Sifanyi makosa. Yeyote atakayethubutu kunipima atahukumiwa, na hakika hataweza kuponyoka kiganja cha mkono Wangu. Mara maneno Yangu yanapozungumzwa, ni nani anayethubutu kupinga? Ni nani anayethubutu kunidanganya au kunificha chochote?

2 Mimi ni Mungu mwenye hekima. Ninatumia ubinadamu Wangu wa kawaida kuwafichua watu wote na tabia ya shetani, kuwafichua wale wenye nia mbaya, wale wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na kwa njia nyingine bila wao kufahamu, wale wanaonipinga, wale wasio waaminifu Kwangu, wale wanaotamani fedha, wale ambao hawaudhukuru mzigo Wangu, wale wanaojihusisha na ulaghai na udanganyifu pamoja na ndugu zao, wale wanaozungumza kwa maneno matamu ili kuwafanya watu wafurahi, na wale ambao hawawezi kuratibu na ndugu zao kwa umoja kwa kujitolea. Kwa sababu ya ubinadamu Wangu wa kawaida, watu wengi sana hunipinga kwa siri na kushiriki katika ulaghai na udanganyifu, wakidhani kuwa ubinadamu Wangu wa kawaida haujui.

3 Na watu wengi sana wanatilia maanani maalum ubinadamu Wangu wa kawaida, wakinipa vitu vizuri nile na kunywa, wakinitumikia kama watumishi, na wakininenea yaliyo ndani ya mioyo yao, huku wakati wote wakitenda tofauti kabisa pasi na ufahamu Wangu. Binadamu vipofu! Hamnijui kabisa—Mungu ambaye huangalia ndani sana ya moyo wa mwanadamu. Bado hamnijui Mimi hata sasa; bado mnafikiri Sijui kile unachonuia. Fikiria jambo hilo: Ni watu wangapi ambao wamejiangamiza kwa sababu ya ubinadamu Wangu wa kawaida? Amka! Usinidanganye tena. Lazima uweke tabia na mwenendo wako wote, kila neno na tendo lako mbele Yangu, na ukubali ukaguzi Wangu wa hilo.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 76” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Mungu ni wa Kawaida Jinsi Usemavyo?

Inayofuata:Watu Wanamchukulia Kristo kama Mwanadamu wa Kawaida

Maudhui Yanayohusiana

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga. Maneno Yako ya…