Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

69 Mazungumzo ya Dhati na Mungu

1

Ee Mungu! Nimefurahia mwingi sana wa upendo Wako,

kuna mengi moyoni mwangu ninayotaka kukwambia.

Kupitia kwa maneno Yako mlango wa moyo wangu ulifunguliwa, niliisikia sauti Yako.

Maneno Yako ni ukweli, yanauimarisha moyo wangu kama maji ya chemichemi.

Ninapofikiria maneno Yako, moyo wangu huchangamka na ni mtulivu, wenye amani na furaha.

Kwa kupitia na kutenda maneno Yako, naelewa ukweli mwingi.

Katika maneno Yako naona haki, utakatifu na upendo Wako wa kweli.

Zaidi na zaidi nahisi uzuri Wako, Wewe, Unastahili sana upendo wa mwanadamu.

Katika imani nimefurahia amani na furaha, niko karibu zaidi nawe.

Nimeona hukumu ya siku za mwisho ni muhimu sana kwa binadamu wapotovu.

Naamua kufuatilia ukweli kutekeleza wajibu wangu kulipiza upendo Wako kwangu.

2

Ee Mungu! Kuna mengi moyoni mwangu ninayotaka kukwambia.

Neno Lako kama upanga mkali unauchoma moyo wangu,

unaupasua uovu ulio rohoni mwangu.

Nimejaa tabia ya shetani, mwenye kiburi, mgumu,

mara nyingi nasema uongo na kukudanganya.

Nimeona hukumu ya siku za mwisho ni muhimu sana kwa binadamu wapotovu.

Naamua kufuatilia ukweli ili nitakaswe na kulipiza upendo Wako.

3

Katika wajibu wangu, nafanya mabadilishano na Wewe,

moyo wangu umejaa matumaini ya makuu.

Hakika ni hukumu na kuadibu Kwako ambako kumenitakasa na kuniokoa.

Bila hilo ningeanguka katika maafa kwa sababu ya kukupinga.

Bila ukweli unaoonyeshwa na Wewe katika siku za mwisho,

miaka yangu ya imani katika Bwana ingekuwa bure.

Nimeona hukumu ya siku za mwisho ni muhimu sana kwa binadamu wapotovu.

Naamua kufuatilia ukweli ili nitakaswe na kulipiza upendo Wako.

Iliyotangulia:Mwenyezi Mungu, Anayependeza Zaidi

Inayofuata:Nisingekuwa Nimeokolewa na Mungu

Maudhui Yanayohusiana

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…