Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Napaswa Kuufikiria Moyo wa Mungu

1 Nimebarikiwa kusikia sauti ya Mungu na kuletwa mbele Yake. Kula na kunywa maneno ya Mungu, nimehudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo na kuona kuonekana kwa Mungu. Kupitia hukumu na utakaso wa Mungu kweli ni kuinuliwa na Mungu. Ningewezaje, nilivyo mpotovu, kustahili kuona uso Wake? Nikiwa na wokovu wa Mungu mbele yangu, najawa na machozi. Kama siwezi kulipiza upendo Wake basi nitakuwa na aibu sana kumtazama. Kama nina dhamiri na akili kweli, kwa nini basi siwezi kufikiria mapenzi ya Mungu? Badala yake, nina tamaa ya raha za kimwili na ninaishi chini ya ushawishi wa giza.

2 Mara nyingi mimi husumbuka na kushindwa kutekeleza wajibu wangu vizuri. Tabia zangu za kishetani ni za kina sana na kweli ni ngumu sana kuziondoa. Kutokuwa na ukweli lakini bado mwenye kiburi, mimi nimepungukiwa mantiki sana. Nangoja kwa hamu hukumu zaidi kali ili nipate kubadili haraka. Kuona wasiwasi wa Mungu, natamani kujitahidi kwa bidii zaidi. Usafishaji wote ni wa kustahili ili kupata ukweli. Ni kwa sababu tu ya upogoaji na ushughulikiaji Wake ndiyo naishi kwa kudhihirisha mfano kiasi wa binadamu. Kupitia katika uzoefu, najua kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu ni baraka Zake.

3 Mungu amelipa gharama isiyopimika ili kutuokoa: hukumu na majaribu, watu, matukio, na vitu vingi sana vinavyofanya huduma. Kwa watu waliopotoka kama hao kufikia wokovu si jambo rahisi. Asante kwa Mungu kwa ajili ya hukumu na kuadibu Kwake; nimepata maisha mapya. Baraka hii kubwa imenijia, ningekosaje kulia machozi ya shukrani? Kufurahia upendo wote wa Mungu, ningeendeleaje kujiishia mwenyewe? Napaswa kumtukuza na kumshuhudia Mungu katika maisha haya, na ni hapo tu ndipo moyo wangu unaweza kutulia. Nitatafuta kupata ukweli kwa nguvu yangu yote na niwe mtu anayempenda Mungu. Nitaishi kwa kudhihirisha roho ya Petro wa wakati wa sasa na ning’ae kwa uangavu. Moyo Wangu unafurahia katika kuuridhisha moyo wa Mungu na naishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli.

Iliyotangulia:Baada ya Hukumu Hatimaye Ninajijua

Inayofuata:Mzinduko Kupitia Hukumu

Maudhui Yanayohusiana