Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 15. Kutoka katika Siasa Isiyo na Kadri hadi Kutafuta kuwa Msaliaji

1. Uhamaji wa Watu kuelekea kwenye Siasa Isiyo na Kadri

Je, nyote mmekuwa mkitafuta nini hivi karibuni? Je, imekuwa mabadiliko ya tabia na kuwa na ushuhuda wa Mungu? Haijakuwa hiyo! Nawaona watu wengi tena wakitafuta kufa kwa ajili ya Mungu ili kumuaibisha Shetani. Je, mnasubiri tu kuadhibiwa badala ya kupanga kutenda ukweli ama kutafuta kubadilishwa kwa tabia, kulipiza upendo wa Mungu? Baada ya kusoma “Usaliti (1) “na “Usaliti (2), “watu walikuwa na mipango ya kufa. Wote waliamini kuwa lengo la mwisho la kazi ya Mungu lilikuwa watu kufa ili kumuaibisha Shetani. Kwa hivyo watu hawakutarajia kujipatia lolote, na hawakutafuta kwa njia nzuri, wala hawakuwa na hiari kuteseka. Je, ufuatiliaji wa aina hii si wa kuhamia katika siasa isiyo na kadri? Madhumuni ya kazi na maneno ya Mungu ni kwamba watu waweze kuingia ndani zaidi na vyema zaidi katika ukweli, na katika mabadiliko ya tabia. Nia si kuwa watu wafe, na si kuwaadhibu watu baada ya wao kubainisha tabia zao halisi zilivyo. Ni ili tu watu wote wayatafakari baadhi ya maswali muhimu kiasi kidogo zaidi, ili waweze kuona wazi zaidi hali yao wenyewe, na kuingia kwa haraka zaidi baada ya wao kuelewa mahitaji ya Mungu. Kama watu wote wangekufa na kuadhibiwa, basi kazi ya Mungu ingekuwa ya nini kwa kweli? Na matokeo ya kuwaokoa watu yangekuwa gani? Kama kusudi la kazi ya Mungu lingekuwa kwamba watu wafe, je, kungekuwa na mtu yeyote jasiri wa kutafuta mabadiliko ya tabia? Je, si huku kungekuwa kuwaelekeza watu kwa shida kubwa? Wakati huo watu wote wangefikiri: “Nitaadhibiwa kwa vyovyote vile, nitaridhika tu na kuishi, pasipo haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu lolote. Hata nikitenda kwa namna gani, nitakufa. Nitaadhibiwa. Je, ni nini faida ya kuutafuta ukweli? “Wasingekuwa na ujasiri mwingi. Watu wana magumu mengi hata wanapoongozwa kutoka kwa upande wa hakika. Kuwa na watu kutafuta mabadiliko ya tabia na kufa kwa vyovyote vile, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokolewa kwa sababu huu ni ukinzani wenyewe. Kumshuhudia Mungu hakuwezi kufanywa kutoka kwa upande hasi; sharti kufanywe kutoka kwa upande wa hakika. Ni kwa njia hii tu ndipo watu watakuwa na nguvu. Kwa kuwa vimo vya watu ni vya chini kabisa, hawaoni waziwazi jinsi ya kuingia ndani kutoka kwa upande wa hakika. Kutoa nadharia tete zaidi kwa upande ulio hasi, basi wamechanganyikiwa kuhusu upande wa hakika, na kusalimu amri. Ukisema: “Kama tutaadhibiwa baadaye, basi tunapaswa kutenda kwa njia gani sasa, tunapaswa kumpenda Mungu vipi?” Je, watu wanaweza kufanya msemo huu kufanya kazi? Ukisema zaidi, “Kuwa shahidi mzuri wa Mungu, “kila mtu atasema kwa unyonge, “Ukisema hivyo! “Kwa aina hii ya mawasiliamo watu wote wanasubiri tu kupokea adhabu. Hakuna mtu ambaye atafikiri kuhusu vitu kama vile kumpenda Mungu ama kutenda ukweli, ama kuwa shahidi wa Mungu. Je, mbari ya aina hii ya wanadamu inaweza kuokolewa?

2. Kuwa Msaliaji Ni Kile Ambacho Watu Wanapaswa kuwa Wakitafuta

Mwanzoni, kundi hili la watu lilitafuta kuwa wafalme na kushika madaraka. Wakati mwishowe, Mungu alipokuja kufanya kazi Yake na kusema kuwa watu wote walikuwa watendaji-huduma, walijitosa huku ndani ili wasitoke nje. Hata wakipewa baraka, hawazitaki. Hawaamini kugeuzwa kwao kuwa watu wa Mungu. Hawaamini pia wanapoambiwa kuwa wao si watendaji-huduma. Je, haya siyo mawili yanayozidi kadri? Watu daima hupenda kuvuka mpaka. Hebu tusikitaje kile ambacho kimepita awali. Tunaweza kusema kuwa ni mkondo tu wa mabadiliko ya tabia ya lazima, bila haja ya kutaka kuchunguza zaidi. Sasa lazima utafakari: Je, ninapaswa kuwa na mpango upi wa msingi zaidi? Je, ni njia ipi sahihi ya kumfidia Mungu? Nitakuelekeza kwenye njia, ambayo inahakikisha kuwa nyote mtakuwa na njia ya kufuata. Ambayo ni kutafuta kuwa msaliaji. Bila kujali madaraka au hadhi ya baadaye, jishughulishe tu na kile unachopaswa kukifanya, unapotafuta kusalia. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kutafuta; ni sawa. Si tamaa inayopita kiasi, kwa kuwa wanadamu ambao huokoka hakika watakuwa watu wazuri. Hakika watakuwa na ushuhuda mzuri wa Mungu, na hakika wataridhisha mapenzi Yake. Kutafuta kuokoka kwa hivyo si matakwa yaliyopita kiasi, badala yake ni kitu ambacho watu wanapaswa kutafuta. Hili linakubaliana na kazi ya Mungu ya kuwaokoa watu. Ikiwa unajitayarisha kuadhibiwa, basi lazima wewe ni mtu mbaya. Je, mtu mbaya anawezaje kuwa shahidi wa Mungu? Watu wote wanaopokea adhabu ni watu ambao hawampendi Mungu. Watu wanaompenda Mungu wanawezaje kwenda jahanamu? Je, isingekuwa mpayuko wa bure kwa watu wanaoenda kuzimu na wanaadhibiwa kuzungumzia kuwa shahidi wa Mungu? Kama watu wote wangeenda kuzimu, kazi ya Mungu ingekuwa bila maana. Kama watu wote wangekufa, kazi ya Mungu isingekuwa na maana hata zaidi, kwa kuwa “zao” la kazi ya Mungu lingekufa lote. Ingekuwa mzaha kiasi gani? Je, si kweli kuwa hii nadharia tete ina nafasi ya kushindwa? Je, si ukinzani mkuu? Kwa hivyo nyote mnapaswa kufanya mpango wa msingi unaowezekana, kuishi baadaye, ikiwa ni kama mtendaji-huduma, kama mmoja wa watu wa Mungu, kama mmoja wa wana wa Mungu, ama kama mtu wa hadhi ya juu. Yote unayopasa kufikiria ni kuhusu kila ambacho unahitaji kufanya, ili kwamba kwa kibali cha Mungu uokoke, kwa sababu Mungu anatumai kuwa na watu na wasaliaji wengi. Je, hili halifanyi utafutaji wenu kuwa rahisi zaidi? Kuwa nawe kutafuta kwa njia hii, nina uhakika hutakuwa na wasiwasi tena kuhusu jinsi ya kuwa na ushuhuda wa Mungu baada ya kifo! Hatimaye, unatakiwa kuelewa: Ufuatiliaji wa kawaida sio matakwa ya kupita kiasi. Katika imani yao katika Mungu, watu hawapaswi kuwa na matakwa ya kupita kiasi. Wanayopaswa kuwa nayo ni ufuatiliaji wa kawaida.

Iliyotangulia:Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

Inayofuata:Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo