Sura ya 23. Jinsi ya kuelewa Umoja wa Mwili na Roho

Baadhi ya watu huuliza, “Mungu huangalia kwa makini moyo wa binadamu, na mwili na Roho wa Mungu ni moja. Mungu hujua kila kitu ambacho watu husema, kwa hivyo Mungu anajua kwamba sasa ninamwamini?” Kujibu hili swali huhusisha jinsi ya kuelewa Mungu mwenye mwili na uhusiano kati ya Roho Wake na mwili. Baadhi husema, “Mungu ni halisi kwa njia thabiti.” Wengine husema, “Yeye ni halisi kwa njia thabiti. Lakini mwili Wake na Roho Yake ni moja, kwa hivyo Yeye anapaswa kujua hilo!” Kumfahamu Mungu ni hasa kuelewa kiini Chake na sifa za Roho Wake, na mwanadamu hapaswi kujaribu kuamua kama mwili wa Mungu hujua kitu chochote fulani au kama Roho Wake hujua kitu chochote; Mungu ni mwenye hekima na wa ajabu, Asiyeeleweka kwa mwanadamu. Fikiri kwamba wakati ulilala usiku, roho yako iliondoka na kisha ikarudi. Ungependa kujua mahali ilipoenda? Unaweza kuguza roho iliyo ndani yako? Unajua ni nini roho yako inafanya? Mwili, Roho, na mtu ambaye ndani ya mwili wake Roho amethibitishwa—haya ni masuala ambayo hamjayaelewa kwa wazi. Wakati Mungu anakuwa mwili na Roho amethibitishwa katika mwili, kiini cha mtu atokeaye ni kitakatifu, tofauti kabisa na kiini cha mtu wa kibinadamu na roho ya aina gani hukaa ndani ya mwili wa mwanadamu; ni mambo mawili tofauti kabisa. Kiini cha mwanadamu na roho yake yamefungwa kwa huyo mtu. Roho wa Mungu amefungwa kwa mwili Wake, lakini bado Yeye ni mwenye nguvu zote. Wakati Anafanya kazi Yake akiwa ndani ya mwili, Roho Wake pia hufanya kazi kila mahali. Huwezi kuuliza kuona asili ya kudura hii au kuiona wazi. Hakuna njia ya kuiona wazi. Kumetosha wewe kuona jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi miongoni mwa wale walio chini wakati mwili hufanya kazi Yake. Roho ana sifa ya kuwa na nguvu zote; Yeye huudhibiti ulimwengu mzima na huwaokoa wale Anaowachagua, na pia Yeye hufanya kazi ili kumpa kila mtu aliye chini nuru, wakati mwili unafanya kazi Yake wakati huo huo. Huwezi kusema kwamba mwili unakosa Roho wakati Roho hufanya kazi miongoni mwa walio chini. Ukisema hivyo, je, hutakuwa umekataa kupata mwili kwa Mungu? Hata hivyo, kuna mambo ambayo mwili haujui. Huku kutojua ni kipengele cha kawaida na cha vitendo cha Kristo. Kwamba Roho wa Mungu amefahamika kikamilifu ndani ya mwili huthibitisha kuwa Mungu mwenyewe ndicho kiini cha mwili huo. Roho Wake tayari ajua kitu chochote kile ambacho mwili Wake haujui kwa sababu ya kipengele Chake cha vitendo, hivyo mtu anaweza kusema kwamba Mungu tayari Ajua kitu hicho. Ukikataa kipengele cha Roho kwa sababu ya kipengele cha vitendo cha mwili na kukataa kwamba mwili huu ni Mungu Mwenyewe, basi umetenda kosa sawa na Mafarisayo. Baadhi husema, “Mwili na Roho wa Mungu ni moja, hivyo Mungu anajua ni watu wangapi tumemshindia Kwake hapa? Anaweza kujua, kwa maana haijasemwa kuwa mwili na Roho ni moja? Roho hujua na mwili pia hujifunza kuhusu hilo, kwa sababu Wao ni sawa!” Kuzungumza kwako hivi kunakataa mwili. Mwili hujumuisha kipengele Chake cha kawaida na cha vitendo: kuna vitu ambavyo mwili unaweza kujua na kuna vitu vingine ambavyo mwili hauhitaji kujua. Hicho ni kipengele Chake cha kawaida na cha vitendo. Baadhi husema, “Roho hujua, hivyo mwili bila shaka hujua.” Jambo kama hilo liko nje ya mawanda ya uhalisi, na kwa hivyo wewe unakataa kiini cha mwili. Vitu vingine kuhusu Mungu mwenye mwili ni tofauti na vile wanadamu huvifikiri: havionekani, havishikiki, ni vya siri. Kama Anao uwezo wa kujua kitu bila kuzuiwa na eneo ama jiografia, basi huo si mwili ila mwili wa kiroho. Baada ya Yesu kusulubiwa kwa msalaba na kisha kufufuka, Aliweza kupitia kwa mlango, lakini huyo alikuwa Yesu aliyefufuka. Yesu kabla ya ufufuo hangeweza kupita kwa ukuta; hakuna namna. Alizuiliwa na eneo, jiografia na wakati. Hicho ndicho kipengele cha kawaida cha mwili. Suala moja lazima lipimwe na kuzungumziwa kikamilifu. Unasema tu kwamba mwili na Roho wa Mungu ni moja na hivyo mwili hujua kile Roho hujua, lakini mwili huunganisha kipengele cha kawaida na cha vitendo. Zaidi kuna jambo hili lingine. Wakati wa kufanya kazi Yake katika Mwili ni Yeye Mwenyewe anayeifanya: Roho na mwili wote wamehusishwa katika kazi hiyo. Inafanywa hasa na mwili; mwili ni msingi. Roho hufanya kazi kuwapa watu nuru, kuongoza, kusaidia, kulinda na kuwachunga, wakati mwili unachukua jukumu kuu katika kazi. Hata hivyo, kama Anataka kumjua mtu, ni suala rahisi. Wakati mwanadamu mmoja anataka kumwelewa mwingine, hatajua kiwango cha uovu wa vitendo vya mwingine isipokuwa avione. Lakini Mungu mwenye mwili daima Ana hisia kuhusu jinsi mtu fulani aliye chini hutenda na Ana uwezo wa kufanya hukumu. Haiwezekani kuwa kwamba Yeye hana utambuzi kama huo. Kusema kwamba Yeye hajui mtu fulani ni suala la semantiki, lakini haiwezekani kuwa kwamba Hajui chochote kuhusu mtu huyo. Kwa mfano, Yeye hujua na kuelewa jinsi yeyote kati yenu hutenda na kile ambacho mtafanya, na uovu gani mtafanya na kwa kiwango gani. Wengine husema, “Kama Mungu huelewa yote, je, anajua mahali niko sasa hivi?” Yeye hajui hili; si muhimu kujua hili. Kukuelewa wewe kwa kweli sio kujua pahali ulipo kila siku. Hakuna haja ya kujua hilo. Kuelewa ni nini utafanya kwa asili kunatosha, na ni cha kumridhisha Yeye kufanya kazi Yake. Mungu ni wa vitendo katika jinsi Anavyojishughulisha na kazi Yake. Sio kama watu wanavyofikiri kwamba wakati Mungu humjua mtu, lazima Ajue alipo mtu huyo, kile anachofikiri, kile anachosema, kile atakachofanya baadaye, jinsi anavyovaa, jinsi anavyoonekana na kadhalika. Kwa kweli, kazi ya wokovu ambayo Mungu hufanya kimsingi haihitaji kujua mambo hayo. Mungu hulenga tu kujua dutu ya mtu na mchakato wa uendeleaji katika maisha yake. Wakati Mungu anakuwa mwili, maonyesho ya mwili ni ya vitendo na ya kawaida, na hali hii ya vitendo na ukawaida imepagawa ili kukamilisha kazi ya ushindi na wokovu wa wanadamu. Lakini, hakuna yeyote anayepaswa kusahau kuwa hali ya vitendo na ukawaida wa mwili ni udhihirisho wake wa kawaida zaidi wakati Roho wa Mungu huishi katika mwili Wake. Kwa hiyo, unasema, je Roho anajua? Roho anajua. Yeye anajua, lakini Je, Yeye huzingatia mambo haya? Yeye hazingatii, hivyo wala mwili haujali kuhusu masuala haya. Lolote litokealo, Roho na mwili ni moja, na hakuna mtu anayeweza kukataa hili. Wakati mwingine una mawazo ndani ya moyo wako—Je Roho anajua kile unachofikiri? Bila shaka Roho anajua. Roho huangalia moyo na hujua kile watu hufikiri, lakini kazi Yake si kuwa na ufahamu wa mawazo ya kila mtu tu. Badala yake, Yeye anastahili kuonyesha ukweli kutoka ndani ya mwili ili kubadili mawazo ya mioyo ya watu. Mawazo yenu juu ya mambo mengine yako machanga sana. Mnafikiri kwamba Mungu anapaswa kuwa mjua yote. Watu wengine huwa na shaka na Mungu mwenye mwili ikiwa Mungu hajui kitu wanachofikiri Anapaswa kujua. Haya yote ni kwa sababu watu wana ufahamu usiotosha wa dutu ya Mungu kupata mwili. Kuna baadhi ya vitu nje ya mawanda ya kazi ya mwili ambavyo Yeye hatasumbuka navyo. Hii ni kanuni ya jinsi Mungu hufanya kazi. Mnaelewa mambo haya sasa? Niambieni, mnajua nyinyi ni wa Roho gani? Unaweza kugusa roho yako mwenyewe? Ikiwa unaweza kuhisi au kugusa roho yako, basi siyo sehemu yako. Ni kitu kisicho cha wewe; ni kitu cha ziada kilicholetwa kutoka nje ya wewe. Unaelewa? Unaweza kuhisi nafsi yako? Unaweza kugusa nafsi yako? Unaweza kuhisi ni nini roho yako inafanya? Hujui, siyo? Ikiwa unaweza kufahamu vitu fulani kama hiki, basi ni roho nyingine ndani yako inafanya kitu kwa nguvu—ikidhibiti vitendo na maneno yako. Ni kitu kisichohusiana na wewe, kisicho cha mwili wako mwenyewe. Wale wenye roho ovu hujua hili vyema zaidi. Ingawa mwili wa Mungu hujumuisha kipengele Chake cha vitendo na cha kawaida, kama binadamu mtu hawezi kufafanua bila kuzuiwa au kufikia mahitimisho juu Yake. Mungu hujishusha hadhi na kujificha Mwenyewe ili kuwa kama mwanadamu; matendo Yake ni yasiyoweza kueleweka.

Iliyotangulia: Sura ya 21. Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Inayofuata: Sura ya 27. Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki