Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia

Ni nini mnafahamu kuhusu mabadiliko katika tabia? Asili ya mabadiliko katika tabia na mabadiliko katika mwenendo ni tofauti, na mabadiliko katika matendo pia ni tofauti—yote ni tofauti kwa asili. Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia yao katika imani yao kwa Mungu, matokeo yakiwa mabadiliko yanayofanyika katika mienendo yao. Baada ya kuamini katika Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa, hawaibi mali ya uma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao pekee—na hata wanaenda kiasi cha kutoipeleka kotini wanapopata hasara ama wamekosewa. Bila shaka, baadhi ya mabadiliko yanafanyika katika mienendo yao. Kwa sababu, baada ya kuamini katika Mungu, kukubali njia ya kweli inawafanya kuhisi vizuri kabisa, na kwa sababu wameonja neema pia ya kazi ya Roho Mtakatifu, wanakuwa na bidii hasa, na hata hakuna kitu chochote ambacho hawawezi kupuuza ama kufanya. Ilhali mwishowe—baada ya kuamini kwa miaka tatu,tano, kumi ama thelathini—kwa sababu hakujakuwa na mabadiliko katika tabia ya maisha yao, wanateleza nyuma kwa njia zao za kitambo, kiburi chao na majivuno vinakua, na wanaanza kupigania nguvu na faida, wanatamani pesa ya kanisa, wanafanya chochote kinachofaidi maslahi yao, wanatamani cheo na raha, wanakuwa vimelea wa nyumba ya Mungu. Wengi wa viongozi, hasa, wameachwa. Na je ukweli huu unathibitisha nini? Mabadiliko katika kisicho zaidi ya mienendo ni kisicho endelevu. Kama hakuna mabadiliko katika tabia ya maisha ya watu,basi sasa ama baadaye upande wao wa uovu utajionyesha. Kwa sababu kiini cha mabadiliko katika mienendo yao ni juhudi, ikiongezwa na kazi ya Roho Mtakatifu katika wakati huo, ni rahisi sana kwao kuwa na juhudi, ama kuwa wazuri kwa muda. Kama wasioamini wanavyosema, “Kufanyia mtu tendo nzuri ni rahisi, kilicho kigumu ni kufanya matendo mazuri maisha yote.” Watu hawana uwezo wa kufanya matendo mazuri maisha yao yote. Mienendo yao inaelekezwa na maisha; chochote ambacho maisha yao, pia mienendo yao ni hivo, na kile tu kinachofichuliwa kwa asili inawakilisha maisha, na asili ya mtu. Vitu vilivyo vya bandia havidumu. Mungu Anapofanya kazi kuokoa mwanadamu, sio kupamba mwanadamu na mienendo mizuri—kazi ya Mungu ni ili kubadilisha tabia za watu, kuwafanya wazaliwe kama watu wapya. Hivyo, hukumu ya Mungu, adibu, majaribu, na usafishaji wa mwanadamu ni yote ili kubadilisha tabia yake, ili aweze kupata kutii kabisa na uaminifu kwa Mungu, na kusifu Mungu kwa kawaida. Hili ndilo lengo la kazi ya Mungu. Kuwa na tabia nzuri siyo sawa na kumtii Mungu, pia kwa uchache zaidi si sawa na kulingana na Kristo. Mabadiliko katika tabia yanazingatia mafundisho, na kuzaliwa na juhudi—hayazingatii maarifa ya kweli ya Mungu, ama juu ya ukweli, kwa uchache zaidi, hayazingatii uongozi wa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna nyakati ambazo baadhi ya yale watu wanafanya yanaongozwa na Roho Mtakatifu, haya siyo maonyesho ya maisha, ila sio sawa na kumjua Mungu; haijalishi mienendo ya mtu ni nzuri aje, haithibitishi kwamba wanamtii Mungu, ama kwamba wanaweka ukweli katika matendo. Mabadilikoya tabia ni udanganyifu wa muda, ni udhihirisho wa bidii, na siyo maonyesho ya maisha hayo. Kwa hivyo unapoona baadhi ya watu ambao, wanapokuwa katikati ya bidii, wanaweza kufanya vitu kwa ajili ya nyumba ya Mungu na hata kuacha vitu, usiwasifu. Kile unaweza kufanya ni kuongoza watu hao kuelekea ukweli, kuelekea njia ya maisha—huwezi kuweka kupunguza shauku yao. Watu wenye bidii hukuwa na motisha sana sana na huwa na matarajio; wengi wao wanatamani njia ya kweli, na ni watu ambao Mungu Ameamulia awali na Amechagua. Watu wengi wenye bidii ni waumini wa kweli wa Mungu; kama mtu ni muumini mpya na hana bidii, hili linatatiza. Ni wale wenye bidii ndio walio rahisi kuelekezwa kwa njia sahihi. Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimanishi kuwa wako na ukweli. Juhudi ya watu inaweza tu kuwafanya kuzingatia mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida muhimu, na mafundisho hayawezi kusimama kwa niaba ya ukweli. Wale ambao wamebadilisha tabia zao ni tafouti. Wana ukweli ndani, wanatambua masuala yote, wanajua jinsi ya kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kutenda kulingana na kanuni za ukweli, jinsi ya kutenda kumridhisha Mungu, na wanaelewa asili ya upotovu wanaofichua. Wakati mawazo yao wenyewe na dhana yanapofichuliwa, wanaweza kutambua na kunyima mwili. Hivi ndivyo mabadiliko ya tabia hudhihirishwa. Kitu cha muhimu kuhusu mabadiliko ya tabia ni kwamba yana ukweli na uwazi, na unapotekeleza vitu, vinaweka ukweli katika matendo na usahihi wa karibu na upotovu wao hauonekani mara nyingi. Kwa ujumla, mtu ambaye tabia yake imebadilika anaonekana kuwa na busara na mwenye utambuzi, na kama tokeo la kuelewa kwake kwa ukweli, haki ya kibinafsi na kiburi havifichuliwi sana. Ana uwezo wa kuona kila kitu kwa uwazi, basi awatakuwa na kiburi baada ya kupata uwazi huu. Ana uwezo wa kuwa na ufahamu uliopimwa juu ya ni wapi mahali pa mwanadamu, jinsi ya kutenda kwa busara, jinsi ya kuwa mtu mwenye wajibu, kile cha kusema na kisicho faa kusemwa, na kile cha kusema na kile cha kutenda kwa watu wapi. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa watu wa aina hii ni wenye busara kiasi. Wale wanaobadilisha tabia zao wanaishi kweli sura ya binadamu, na wana ukweli; hawapitii ushawishi wa wengine. Wale ambao wamekuwa na mabadiliko katika tabia zao wako imara kabisa, hawasitisiti, na haijalishi wako kwa hali gani, wanajua jinsi ya kufanya wajibu wao sawasawa na jinsi ya kufanya vitu kumridhisha Mungu. Wale ambao tabia zao zimebadilika hawalengi kitu cha kufanya ili kujifanya waonekane wazuri katika kiwango cha juujuu— wana uwazi wa ndani kwa kile cha kufanya ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo, kutoka nje wanaweza kosa kuonekana wenye shauku ama kama wamefanya kitu chochote kubwa, lakini kila kitu wanachofanya kina maana,kina thamani, na kina matokeo ya kweli. Wale ambao tabia zimebadilika wana uhakika kuwa na ukweli mwingi— hii inaweza kuthibitishawa na mitazamo yao kwa vitu na kanuni zao katika vitendo vyao. Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko kwa tabia hata kidogo. Hiyo si kusema kwamba mtu mwenye uzoefu mwingi kutenda ubinadamu wao ni lazima kuwa na mabadiliko kwa tabia; inafanyika sana pengine wakati baadhi ya sumu ya kishetani katika asili ya mtu inabadilika kwa sababu ya maarifa yao ya Mungu na kuelewa kwao ukweli. Hivyo ni kusema, sumu hizo zimetakaswa na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unachukuwa mizizi katika mtu huyo, na unakuwa maisha yake, na inakuwa msingi wa uwepo wake. Hapo tu ndipo anakuwa mtu mpya, na tabia yake basi inabadilika. Hii siyo kusema kwamba tabia yake ya nje imekuwa ya upole kuliko hapo awali, kuwa alikuwa na kiburi lakini sasa maneno yake ni ya busara, kwamba hakuwa anasikiza mtu yeyote laikini sasa anaweza kuwasikiza wengine—mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko ya tabia. Bila shaka mabadiliko kwa tabia inajumulisha hali hizi, lakini kitu cha maana sana ni kuwa maisha yao ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unageuka kuwa maisha yao, baadhi ya sumu ya kishetani ndani imetolewa, mtazamo wa mtu huyo umebadilika kabisa, na hakuna unaozingatia yale ya dunia. Anaona njama na sumu ya joka mkubwa jekundu kwa uwazi; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika— hili ndilo badiliko la muhimu na kiini cha kubadilika kwa tabia. Kwa msingi upi ndio watu waliishi kabla ya hayo? Watu wote wanaishi kwa ajili yao wenyewe. Kila mwanadamu kwake mwenyewe na shetani anakuwa nyuma zaidi— hii ndiyo jumla ya asili ya mwanadamu. Kuamini Mungu inafanywa kwa mtu binafsi, na pia kupata baraka ni hivyo hata zaidi. Kutupilia vitu mbali kwa ajili ya Mungu,kujitumia kwa Mungu, na kuwa mwaminifu kwa Mungu— haya yote yanafanywa kwa mtu binafsi. Kwa jumla, yote ni kwa ajili ya kupata baraka kwa mtu binafsi. Katika dunia, kila kitu ni kwa faida ya mtu binafsi. Kuamini Mungu ni kupata baraka, na ni kupata baraka ndipo mtu anatupa kila kitu, na mtu anaweza kustahimili mateso mengi ili kupata baraka. Hii yote ni ushahidi wa kutegemea nadharia wa asili ya upotovu ya mwanadamu. Ingawa, badiliko kwa tabia ni tofauti. Jinsi anafaa kuishi maisha yenye maana, jinsi anafaa kutekeleza wajibu wa mtu ili kufaa kuitwa binadamu, jinsi anafaa kumwabudu Mungu, na jinsi anafaa kumtii na kumridhisha Mungu— anaamini kuwa huu ndio msingi wa kuwa mtu na ni wajibu wake kulingana na kanuni ya mbingu na nchi isiyobadilika. Vinginevyo, hatafaa kuitwa binadamu, hakutakuwa na haja, na atakuwa amejawa na utupu. Watu wanafaa kuishi ili kumridhisha Mungu, kufanya wajibu wao vizuri, na kuishi maisha yenye maana, ili hata wanapokufa, watahisi wametosheka bila majuto yoyote, na hawatakuwa wameishi bure. Kutoka kufananisha hali hizi mbili, tunaona kuwa ile ya mwisho ni mtu ambaye tabia yakeimebadilika, na kwa sababu tabia ya maisha yake imebadilika, mtazamo kwa maisha imebadilika bila shaka. Na maadili tofauti, hatawahi tena kuishi kwa ajili yake mwenyewe, na imani yake kwa Mungu haitawahi tena kuwa kwa ajili ya kupata baraka kwake mwenyewe. Ataweza kusema, “baada ya kumjua Mungu, kifo ni nini kwangu? Kumjua Mungu imenifanya niishi maisha iliyo na maana. Sijaishi bure na sitakufa nikiwa na majuto— sina malalamishi.” Je huu sio mtazamo wa maisha iliyobadilika? Kwa hivyo, chanzo kubwa cha mabadiliko kwa tabia ya maisha ya mtu ni kuwa na ukweli ndani, na kuwa na maarifa ya Mungu; mtazamo wa mtu kwa maisha umebadilika, na maadili ni tofauti na ya awali. Mabadiliko yanaanza kutoka ndani, na kutoka kwa maisha; kwa kweli siyo tu mabadilko ya nje. Baadhi ya waumini wapya, baada ya kumwamini Mungu, wameacha dunia ya kilimwengu nyuma; wanapokutana na wasioamini hawana cha kusema, na ni vigumu sana kukutana kwao na jamaa na marafiki, na wasioamini wanasema, “Mtu huyu kweli amebadilika.” Kwa hivyo wanafikiria, “Tabia yangu kweli imebadilika— wasioamini wanasema nimebadilika.” Kwa weli, tabia yao kweli imebadilika? La hasha. Haya tu ni mabadiliko ya nje. Hakujakuwa na mabadiliko yoyote katika maisha yao, na asili yao ya kitambo imebaki kuwa na mizizi ndani yao, bila kuguzwa hata kidogo. Wakati mwingine, watu wanashikwa na juhudi kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu; baadhi ya mabadiliko ya nje yanatokea, na wanatenda vitendo chache nzuri. Lakini hii siyo sawa na mabadiliko kwa tabia. Uko bila ukweli, mtazamo wako kwa vitu haijabadilika, hata bila tofauti na ule wa wasioamini, na maadili yako na mtazamo wa maisha hayajabadilika. Hauna hata moyo unao heshimu Mungu, ambao angalau unafaa kuwa nayo. Hakuna kitu ambacho ni mbali na mabadiliko kwa tabia yako. Ili kupata mabadiliko kwa tabia , kitu cha umuhimu kabisa ni kutafuta kuelewa Mungu na kuwa na maelewano ya kweli juu Yake. Ona Petro— Mungu Alipotaka kumkabidhi kwa Shetani, alisema, “unaweza nikabidhi kwa Shetani. Wewe ni Mungu, wewe ni mwenyezi. Kila kitu kiko mikononi Mwako; nitakosa aje kukusifu kwa kila kitu Unachofanya? Lakini kama ningekujua kabla nife hiyo ingekuwa afadhali.” Alihisi kuwa katika maisha ya watu, kumjua Mungu ilkuwa kitu cha umuhimu zaidi; baada ya kumjua Mungu aina yoyote ya kifo ingekuwa sawa, na jinsi yoyote Mungu Angeshughulika nayo ingekuwa sawa. Alihisi kuwa kumjua Mungu ilikuwa kitu cha muhimu sana; kama hangepata ukweli, hangetosheka kamwe, lakini pia hangelalamika kwa Mungu. Na hii roho ya Petro, na tamanio hili la kutaka kutafuta maarifa ya Mungu, mtazamo wake kwa maisha kwa kweli ulibadilika. Kutoka kwa kauli hii tunaweza kuona kuwa tabia yake ilibadilika, kuwa alikuwa mtu ambaye tabia yake ilibadilika, na mwisho wa uzoefu huu, Mungu Alisema kuwa alikuwa mtu mwenye uelewa mkubwa zaidi juu ya Mungu, na alikuwa Yule aliyempenda Mungu kwa kweli.

Kama mtu hana ukweli, tabia yake haiwezi kamwe kubadilika. Hata kama ni kiongozi kanisani, hataweza kufanya kazi halisi ya kiongozi; atakuwa anafanya kazikwa jina pekee, na atakuwa akifanya kazi tu ya uendeshaji. Wale tu wanaoweza kwa kweli kutekeleza unyunyizaji wa kanisa kusambaza ukweli na maisha ni wale walio na ukweli. Sasa hivi, uko kwenye wakati wa mazoezi, katika muda wako wa kuingia. Wakati utakapokuja ambao hakika umeingia katika uhalisi wa ukweli, hapo tu ndipo utaweza kuwaongoza watu wengine. Ni wale tu walio na ukweli na wale ambao tabia ya maisha yao imebadilika ndio vingozi wanaofaa jina hilo.

Iliyotangulia: Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine

Inayofuata: Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki