Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu

Je, ni vitu vipi vya asili ya mwanadamu? Unajua tu kuhusu upotovu wa mwanadamu, uasi, upungufu, dosari, fikra, na dhamira, lakini huwezi kugundua sehemu za ndani za asili ya mwanadamu—unafahamu tu safu ya nje, lakini huwezi kugundua chanzo chake. Baadhi hata hufikiri haya mambo ya juu kuwa ni asili ya mwanadamu, wakisema, “Ona, ninaelewa asili ya mwanadamu; ninatambua ufidhuli wangu. Je, hiyo si asili ya mwandamu?” Je, haitoshi kuikubali kikanuni pekee? Ufidhuli ni kitu cha asili ya mwanadamu; huu ni ukweli kabisa. Je, kuelewa asili ya mtu binafsi ni nini? Inawezaje kujulikana? Je, inajulikana kutoka kwa vipengele vipi? Aidha, vitu hivi vinavyofichuliwa kutoka kwa vipengele hivi tofauti vinapaswaje kutazamwa kwa uthabiti? Tazama asili ya mtu kupitia shauku yake. Jinsi gani? Mathalani, baadhi ya watu hususan hupenda kudansi. Wengine hususan huwapenda waimbaji ama magwiji wa kuigiza filamu. Watu wengine hususan huabudu hulka fulani. Kwa kutazama mapendeleo haya, ni nini asili ya watu hawa? Nitatoa mfano mwingine ambao ni rahisi: Watu wengine humpenda mwimbaji fulani mno, na kwa kiasi gani? Kiasi kwamba wanapenda sana kila ambalo mwimbaji hutenda, kila tabasamu, kila neno, na kila tendo. Wanatawaliwa na tama ya mwimbaji, wakipiga picha kila anachovaa mwimbaji na kuiiga. Je, kiwango hiki cha kupenda mno kinaonyesha nini kuhusu asili ya mtu? Kinaonyesha kuwa moyo wa mtu kama huyu una vitu hivyo tu, wala hauna Mungu. Vitu ambavyo moyo wake huwaza, hupenda, na kutafuta ni vitu vyote vinayofichuliwa na Shetani; vinamiliki moyo wake, na vinakabithiwa moyo wake. Je, unaona tatizo ni lipi? Ikiwa kitu kinapendwa kupita kiasi, basi kitu hicho kinaweza kuwa maisha ya mtu na kumiliki moyo wake, kudhihirisha wazi kuwa mtu huyo ni mwabudu sanamu asiyemtaka Mungu moyoni mwake ila anampenda ibilisi. Hivyo, tunafikia uamuzi kuwa asili yake ni ile inayopenda na kuabudu ibilisi, haipendi ukweli, na haimtaki Mungu. Je, hii ni njia sahihi ya kuangalia asili yake? Ni sahihi kabisa! Hivi ndivyo asili ya mtu inavyochanguliwa. Kwa mfano, watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja na kuongea; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, kuwazingira. Wanapenda kuwa na kimo katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Je, tunagundua nini kuhusu asili ya mtu kutokana na aina hii ya mwenendo? Hebu tuchanganue asili yake: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia kama hii ana asili ya aina gani? Je, ingewezaje kusemwa kwa ufupi? Watu wa kawaida hawawezi kuelewa hili lakini wanaweza tu kuona mwenendo. Uhusiano kati ya tabia na asili ya mtu ni upi? Je, asili yake ni gani? Huwezi kuitambua, sivyo? Kama kweli anatennda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni mfidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwambudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, kuwa na kimo akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Je, hii si asili yake? Unaweza kuelewa wazi asili yake kutoka kwa mienendo hii. Kwa mfano, baadhi ya watu hususan hupenda kujinufaisha kwa gharama ya wengine na kutafuta upenedeleo wao katika kila jambo. Kila wanachofanya lazima kiwanufaishe la sivyo hawatakifanya. Hawajishughulishi na chochote isipokuwa pale ambapo kinawapa faida na wana nia zao wenyewe zilizofichika za kila kitu. Wanazumgumza mema juu ya yeyote anayewanufaisha na kumtukuza yeyote anayewapendeza. Hata wapendwa wao wanapokuwa na matatizo, watasema kuwa wapendwa wao wako sahihi na kujaribu kabisa kuwakinga na kuwatetea. Je, mtu wa aina hii ana asili ipi? Je, unaweza kuona waziwazi asili yake kulingana na hii mienendo? Wanajitahidi ili kujinufaisha pasipo na haki kwa kupitia matendo yao na kujishughulisha na tabia ya kimapatano kila wakati na kila mahali, hivyo unaweza kuhakiki kuwa asili yao ni ile ya kutamani faida kwa moyo wao wote. Wanajipenda katika kila kitu. Hawataamka mapema ispokuwa kunaposhirikisha faida. Wao ndio watu wachoyo zaidi, wasioridhika, hivyo asili yao ni kupenda pesa na wala si kupenda ukweli. Je, hilo haliwakilishi asili yao? Baadhi ya watu hupendezwa mno na wanawake, daima wakifikiria kuwahusu wanawake katika kila wanalofanya, wakiwasaka wanawake popote waendapo. Wanawake warembo ni walengwa wa mapenzi ya mtu kama huyu na wao huwa na heshima kuu moyoni mwake. Yeye yuko radhi kutoa uhai wake kwa ajili ya wanawake wazuri. Anaweza kutoa chochote—wanawake ndio wameujaza moyo wake. Je, asili yake ni ipi? Asili yake ni kuwapenda wanawake na kuwaabudu, hivyo yeye ni mkware mwenye asili yenye uovu na ulafi. Je, hii si asili yake? Mienendo yake inafichua asili yenye uroho—havunji sheria tu mara kadhaa ama kutenda vibaya kidogo kuliko watu wa kawaida—na moyo wake tayari umemilikiwa kabisa na vitu hivi ambavyo vimekuwa asili yake, kiini chake. Hivyo, vitu hivi vimekuwa dalili za asili yake.

Sehemu za ndani za asili ya mtu daima hujifichua, kila wakati. Kila anachofanya mtu, bila kujali ni nini, kinaweza kufichua asili ya huyo mtu. Watu wana madhumuni yao ya kila kitu wanachokifanya, na ikiwa ni ukarimu, kuhubiri injili, ama kazi ya aina yoyote nyingine, waweza kufichua sehemu za asili yao bila ufahamu wowote kuihusu, kwa sababu asili ya mtu ni maisha yake, na watu husukumwa na asili zao muda wote wanaoishi. Asili ya mtu haifichuliwi mara moja tu ama kwa utukizi; badala yake, inaweza kuwakilisha kiini cha mtu kabisa, na kila kitu kinachobubujika kutoka ndani ya mifupa ya mtu na damu ni kiwakilishi cha asili na maisha yake. Baadhi ya watu huwapenda wanawake wenye sura nzuri. Wengine hupenda pesa. Wengine hususan hupenda hadhi. Wengine hususan huthamini sifa njema na mfano wao binafsi. Wengine hususan hupenda ama huabudu sanamu. Na watu wengine hasa ni wafidhuli na wenye majivuno, bila kusalimu amri kwa yeyote mioyoni mwao na kujikakamua kupata kimo, wanapenda kuwa kuonekana vizuri zaidi ya wengine na kuwa na mamlaka juu yao. Kuna aina mbalimbali za asili tofauti, na zinaweza kutofautiana miongoni mwa watu, lakini vipengele vyao vya pamoja vinampinga na kumsaliti Mungu. Kwa njia hiyo zote zinafanana.

Hebu sasa tumwangalie mtu mchoyo. Uchoyo unaweza kusemwa kuwa msingi wa asili ya mtu; kila mtu ana msingi huu ndani yake. Baadhi ya watu ni wachoyo kupita kiasi, na kiasi bila kadiri kama hiki kinawakilisha asili yao. Kila mtu ni mchoyo kiasi, lakini kuna tofauti. Wanapojihusisha na wengine, watu wengine wanaweza kuwalinda na kuwatunza, kuwahangaikia, na kuwafikiria katika kila kitu wanachofanya. Watu wengine hawako hivi; fikiria kuhusu yule ambaye ni mchoyo hususan anapowapokea ndugu: Jamaa yake hula chakula kizuri kabisa, lakini ndugu wanapokuja anawapakulia chakula kidogo duni. Wakati ambapo kuna mambo mazuri anayaweka mbele ya watoto wake, mume, ama familia yake. Ndugu wanapokuja anawafanya walale sakafuni, lakini jamaa yake wanapokuja anawafanyia mpango wakustarehesha zaidi, na kila kitu kikiwa sawa. Mtu wa aina hii hawafikirii wengine hata kidogo. Ni vyema vya kutosha kwake kuwakubalia kukaa wanapokuja, na hivyo wanapougua ama kuwa na magumu mengine hata hayafikirii, akitenda ni kama hayafahamu. Hajali ama kujishughulisha na wengine hata kidogo. Anajijali mwenyewe na kujali jamaa yake pekee. Hii asili yake ya uchoyo inaamua kuwa hayuko radhi kuwajali wengine. Anahisi kwamba kuwatunza wengine ni hasara kwake na jambo la kukera. Pengine watu wengine watarazinisha, wakisema, "Mtu mchoyo hajui jinsi ya kuwatunza wengine?" Basi kwa nini yeye ni mwema sana kwa jamaa yake mwenyewe, na kwa nini anazingatia mahitaji yao kikamilifu? Je, yeye mwenyewe anajuaje anachokosa na kile ambacho kinafaa kuvaliwa au kuliwa wakati fulani? Je, ni kwa nini hawezi kuwa hivyo kwa wengine? Hakika, anaelewa haya yote, lakini ni mchoyo, na hilo limeamuliwa na asili yake. Ni kama tu vile kuna baadhi ya wanawake ambao wamekosea kwa muda hapo awali, lakini hilo haliwafanyi wao kuwa wakware. Mtu mwovu ni yule anayevuruga kila anapoenda kwa mazoea, asiyejua aibu na asiyekuwa na mfumo wa maadili na unyofu—mtu kama huyu ana asili ya uzinzi. Daima anafichua asili yake bila kujali anachotenda au nini anachofanyia kazi. Baadhi ya watu hujinufaisha na nafasi hii ya kuhubiri injili ili kushiriki katika mwenendo kama huu, lakini je, mtu huyu asingetenda hivi asingekuwa akihubiri? Hata katika hali ile, angekuwa bado anashiriki katika hayo kisirisiri. Baadhi ya watu husema, “Asingefanya hivi asingekuwa akihubiri, sivyo?” Je, wajua? Yeye ni wa asili hii, na hawezi kujizuia. Vitu hivi ndivyo hujaa moyoni mwake. Hata hakuna sababu yake ya kutoshiriki katika vitu hivi. Hata akikaa kwa muda bila kufanya vitu kama hivi, ni kwa sababu mazingira hayaidhinishi ama hakuna watu wanaostahili. Hivi ndivyo mambo ya asili ya mtu yalivyo; hayawezi kuthibitiwa. Baadhi ya watu hasa hupenda mavazi na urembo na hujishaua kupita kiasi. Asili ya mtu kama huyu ni ya ubatili. Yeye hubadilisha mavazi yake mara nyingi kwa siku. Anapomwona mtu akivalia nguo nzuri ama akijipodoa vizuri, anapoteza usingizi asipofikia mambo hayo. Lazima pia apate vitu hivyo hata ikiwa lazima aazime pesa ama kulipa thamana yoyote inayowezekana, na kama hawezi kuvipata hana moyo wa kumwamini Mungu, anakosa tamaa ya kuenda mikutanoni, hawezi kufyonza neno la Mungu anapolisoma, na akili yake inajawa na mambo hayo siku nzima. Mambo hayo yanamiliki akili yake, na ni yale anayoyawaza siku nzima. Mtu wa aina hii ni wa juujuu kabisa, zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Hii ni ishara ya asili yake, kitu kilicho ndani ya mifupa yake. Mambo ya asili si vitu vinayofanywa wakati wa udhaifu tu ila vinaendelea kuwepo kotekote maishani. Kila anachofanya mtu kinabeba harufu yake, kinabeba ishara ya sili yake. Hata ikiwa hizo ishara hazionekani wakati mwingine, zimo ndani yake. Kwa mfano, mtu mdanganyifu anapozungumza ukweli mara moja, kwa kweli bado kuna usemi ndani ya usemi wake na uongo umechanganywa ndani. Mtu mdanganyifu humshawishi yeyote kwa hila zake, wakiwemo jamaa yake—hata wanawe. Bila kujali uko wazi kwake kiasi gani, atatafuta kukufanyia mchezo. Hii ndiyo sura ya kweli ya asili yake, na ni wa asili hii. Ni vigumu kubadilika na yu hivi kila wakati. Mathalani, watu waaminifu wakati mwingine watasema kitu kijanja na cha hila, lakini mtu huyu aghalabu huwa mwaminifu na hufanya vitu kwa uaminifu bila kujinufaisha na wengine kwa njia isiyo ya haki katika shughuli zake nao. Anapozungumza na wengine, yeye hasemi vitu kimaksudi ili kuwajaribu; bado ni mwamnifu kwa kiasi na anaweza kuufungua moyo wake na kuwasiliana na wengine. Kila mtu husema yeye ni mtu mwaminifu, lakini bado kuna nyakati nyingine ambazo yeye huzungumza kwa hila fulani. Hii tu ni dalili ya asili potovu na haiwakilishi asili yake kwa sababu yeye si mtu wa aina hiyo. Inapofikia asili ya mtu lazima uelewe ishara ya hiyo asili ni zipi na tabia potovu ni nini; sharti uweze kutofautisha waziwazi kati ya hayo mawili. Sasa, jaribu kuchanganua asili yako. Baadhi watasema, “Wakati mwingine mimi huzungumza kwa ukali” ama “Mimi si wa malezi bora na sina tabia nzuri” ama “Wakati mwingine kuna najisi ninapotekeleza wajibu wangu,” lakini hawazungumzi kuhusu asili yao ilivyo ama iwapo ubinadamu wao ni mzuri. Kwa njia hii, hawawezi kujua asili yao wenyewe. Huwezi daima kujisitiri ama kuwa na soni. Lazima uchambue zaidi ndani yako mwenyewe. Ikiwa huwezi kuchambua hutakuja kujua asili yako, na iwapo hujui asili yako hutaweza kubadilika. Lazima hasa uwe dhabiti kuhusu unavyokuja kujijua mwenyewe; huwezi kujidanganya ama kuwa mzembe ama kujipumbaza.

Kuelewa asili yako kimsingi ni kuelewa wewe ni mtu wa aina gani. Aina ya mtu uliye ni aina ya asili uliyo nayo. Kwa mfano, kusema kuwa mtu yuko hivi na vile ndiko kunaelezea zaidi asili yake. Aina ya asili aliyo nayo huamua yeye ni mtu wa aina gani. Maisha ya mtu ni asili yake tu. Je, unawezaje kuona jinsi asili ya mtu ilivyo? Lazima uwasiliane naye zaidi na kuchunguza zaidi yeye ni mtu wa aina gani. Chochote kinachojitokeza zaidi kumhusu na kiwakilishi cha kiini chake na sifa bainifu vinaweza kusemwa kuwa kitovu cha asili yake. Hulka ya kiini cha mtu ni silika ya asili yake. Inapofika kuona kwa kweli mtu ni wa aina gani, kumwangalia kwa njia ni sahihi kabisa. Kiini cha mtu kiwacho chote, hiyo ndiyo asili yake. Mtu ni wa aina inayoamuliwa na asili yake. Kwa mfano, ikiwa sifa ya kutokeza ya mtu ni kuwa anapenda hususan pesa, basi asili yake ni mpenda pesa, ikifupishwa kwa maneno mawili. Kama mfano mwingine, ikiwa sifa ya kutokeza ya mtu ni upendo wa wanawake—daima huwafuata wanawake sana—basi anapenda maovu na ana asili yenye uovu. Baadhi ya watu hupenda kula sana. Ukiweza kumpa mtu wa aina hii vinywaji kadhaa na nyama au kumuagizia chakula kizuri, atatenda kwa kukupendelea; hivyo huyu mtu ana asili ya uroho, kama nguruwe. Kila mtu ana kasoro yake kuu, ambayo huweka athari yake juu ya kila wakati wa maisha ya mwanadamu na hupenyezwa katika vyote vinavyomhusu huyo mtu na inakuwa madhumuni ya kila afanyalo. Kitu hicho kinawakilisha asili ya mtu. Na unaweza kusema kwamba asili yake ndiyo sehemu yake ya udhaifu mkuu zaidi. Dosari yake kuu ni asili yake. Baadhi ya watu wanaonekana kuwa na ubinadamu mwema na hawadhihirishi dosari yoyote kuu usoni, lakini sifa yao inayojitokeza ni udhaifu. Hawana malengo ya maisha ama hamu ya kupata lolote na wanamalizia maisha kwa kubahatisha. Wanapotea ukisema maneno machache ya kuumiza, na wanakuwa hasi wakati wowote kwa sababu ya kitu kimoja au kingine, kiasi kwamba hawataki tena kuamini. Asili ya kipekee ya mtu huyu ni udhaifu, na asili yake ni ile ya mwoga asiyejiweza. Baadhi ya watu ni wa kuchukuliwa haraka na hisia kuvuka mipaka. Kile wanachokisema ama kufanya kila siku na mienendo yao vipo katika dunia ya hisia. Wanahisi upendo kwa huyu mtu na yule mtu na kila siku lazima walipize upendo na kurudisha hisia nzuri; kila kitu wanachokifanya kiko katika eneo la hisia. Ona jinsi shauku ya mtu kama huyu ni nzito! Mume wake asiyeamini anapofariki bado atalia kwa siku tatu. Wengine wanataka kumzika, lakini bado anasema, “La, yeye ni mume wangu.” Ana hisia hata kwa mtu aliyekufa—hisia zake ni kali mno. Unaweza kusema kuwa hisia ndizo dosari yake kuu, udhaifu wake mkuu ambao unaweza kumpeleka katika maangamizi na kumharibu. Hisia zake zenye mhemko wa kupita kiasi zinamaanisha kuwa yeye hana ukweli na anatenda bila kanuni. Anaonyesha tu nadhari kwa mwili na ni mtu mjinga na aliyekanganyikiwa. Asili yake ni ile ya kutia uzito mahususi kwa hisia. Hivyo, ikiwa unatafuta kubadilisha tabia yako, basi lazima utambue asili yako. “Mito na milima vinaweza kubadilika, lakini msingi wa asili ya mtu hauwezi.” Iwapo asili ya mtu ni mbaya zaidi na haiwezi kubadilika kamwe, Mungu hatamwokoa. Usidhani kuwa asili inaweza kubadilishwa. Je, “kubadailishwa kwa tabia” ni nini? Lazima uwe mpenzi wa ukweli, uikubali hukumu na kuadibiwa na neno la Mungu unapopitia kazi Yake, na kupitia aina zote za mateso na kusafishwa, ambayo kwayo unatakaswa kutokana na sumu ya kishetani iliyo ndani yako. Huku ndiko kubadilishwa kwa tabia. Ikiwa asili ya mtu ni mbaya zaidi, iwapo yeye ni mtu mwovu, basi Mungu hatamwokoa, na Roho Mtakatifu hataweza kufanya kazi ndani yake. Kwa njia nyingine, ni kama daktari anapomponya mgonjwa: Mtu anayepata nimonia anaweza kutibiwa, lakini anayepata saratani ya mapafu hawezi kuokolewa. Mabadiliko katika tabia yanamaanisha kuwa mtu, kwa sababu anapenda na anaweza kuukubali ukweli, hatimaye huja kujua asili yake ya uasi na ya kumpinga Mungu; anaelewa kuwa upotovu wa mwanadamu ni wenye kina zaidi na kuelewa upumbavu na udanganyifu wa mwanadamu. Anajua uduni wa mwanadamu na kusikitisha kwake, na hatimaye anaelewa kiini cha asili ya mwanadamu. Kwa kujua haya yote, anaweza kujikana na kujinyima kabisa, kuishi kwa neno la Mungu, na kutenda ukweli katika kila kitu. Mtu wa aina hii anamjua Mungu na tabia yake imebadilishwa.

Wanadamu wote wamepotoshwa na Shetani, na asili ya mwanadamu ni kumsaliti Mungu. Lakini, miongoni mwa wanadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kuna baadhi yao wanaoweza kulitii neno la Mungu na kuukubali ukweli; hawa wanaweza kupata ukweli na kutimiza kubadilishwa kwa tabia zao. Kuna wale ambao hawautafuti ukweli kwa ari ila bado wanafuata katika imani. Wanatenda yale unayowaambia kufanya na wana utu stahifu. Wako radhi, kwa kiasi fulani, kutumia rasilmali, kuacha ya malimwengu, na kuvumilia mateso. Mtu wa aina hii atakuwa na uwezo wa kusimama na kupokea wokovu. Hata hivyo, tabia yake haitabadilishwa kwa sababu haufuatilii ukweli kwa dhati. Anatoshelezwa tu na kuelewa kanuni. Yeye husikia kanuni, hufikiri kuwa ni nzuri na kuifuata, na baada ya kuelewa kanuni yeye hutekeleza wajibu wake, kwa kiasi. Anaweza kutenda kwa njia yoyote ambayo inamfaa kwake kutenda. Hata hivyo, hana bidii kuhusu ukweli; moyo wake umetiwa giza, na anashindwa kuelewa kabisa umuhimu wa ukweli. Mtu wa aina hii pia anaweza kupokea wokovu na kusamehewa, lakini tabia yake haiwezi kubadilishwa. Kupata mabadiliko ya tabia kunahitaji upendo wa ukweli na uwezo wa kuukubali ukweli. Je, kupokea ukweli ni nini? Ina maana kuwa bila kujali una tabia gani potovu ama ni sumu gani ya joka kuu jekundu inayopotosha asili yako, unaukiri unapofichuliwa na neno la Mungu na kulitii neno la Mungu kwa kusadiki kabisa. Na, unajijua mwenyewe kulingana na neno la Mungu. Hivi ndivyo inavyomaanisha kukubali neno la Mungu. Bila kujali kile ambacho Mungu anasema, bila kujali kinavyochoma moyo, bila kujali Anayatumia maneno gani, unaweza kulikubali mradi uwe ukweli, na unaweza kulikiri mradi lipatane na uhalisi. Unaweza kulitii neno la Mungu bila kujali unalielewa kwa kina kiasi gani, na ukubali na kutii mwanga wa kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu ambayo hupitishwa na ndugu. Wakati ambapo ufuatiliaji wa ukweli wa mtu huyu umefikia mahali fulani, anaweza kupata ukweli na kufikia kubadilishwa kwa tabia yake. Mtu ambaye hapendi ukweli anaweza kuwa wa ubinadamu mwema, lakini ni mzembe kuhusu ukweli na haufuatilii kwa dhati; anaweza kufanya kazi fulani nzuri, kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu, na kutoa vitu vingine kwa ajili ya Mungu, ila hawezi kupata kubadilishwa kwa tabia. Unaona kwamba, kwa kulinganisha, ubinadamu wa Petro ulikuwa kama ule wa mitume wengine ama ndugu, lakini alionekana vizuri katika utafutaji wake wa ukweli wenye ari. Alitafakari kwa dhati kila kitu ambacho Yesu alikisema. Yesu aliuliza, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Akajibu moja kwa moja, “Ee, nampenda tu Baba aliye mbinguni ila sijampenda Bwana aliye duniani!” Baadaye alielewa: “Hili si sawa!” Mungu aliye duniani ndiye Mungu aliye mbinguni. Je, si Mungu yule yule mbinguni na duniani? Kupenda kwangu Mungu aliye mbinguni pekee bado si halisi. Sharti nimpende Mungu duniani, kwani ndipo upendo wangu u halisi tu Alielewa kile ambacho Yesu alikuwa amesema kwa kutafakari neno la Mungu. Je, ni nini maana halisi ya kile alichosema? Ili kumpenda Mungu, mtu lazima apende Mungu mwenye mwili duniani ili upendo uwe halisi. Kumpenda Mungu asiye dhahiri na asiyeonekana hakuna uhalisi ama si kwa vitendo. Kumpenda Mungu halisi na Anayeonekana ni ukweli. Petro alipata ukweli ndani ya maneno ya Yesu na alielewa mapenzi ya Mungu. Imani ya Petro kwa Mungu ilizingatia ufuatiliaji wa ukweli waziwazi, na mwishowe akatimiza upendo wa Mungu wa vitendo, Mungu aliye duniani. Petro hususan alikuwa na ari katika ufuatiliaji wake wa ukweli. Kila wakati Yesu alipomshauri, alitafakari maneno ya Yesu kwa bidii. Pengine alitafakari kwa miezi, mwaka, ama miaka kabla ya Roho Mtakatifu kumpatia nuru na akaelewa maana ya neno la Mungu. Kwa njia hii, aliingia katika ukweli, na baada yake kuingia katika ukweli tabia ya maisha yake ikabadilishwa na kufanywa upya. Mtu asipoufuatilia ukweli, kamwe hatauelewa. Unaweza kuyasema maneno ya ukweli mara elfu kumi na bado ni herufi na kanuni tu. Baadhi ya watu watasema tu, “Kristo ndiye ukweli, njia na uzima.” Kurudia kwako haya, hata mara elfu kumi, ni bure; huelewi maana yake. Kwa nini unasema kuwa Kristo ndiye ukweli, njia na uzima? Je, unaweza kuelezea kwa ufasha ufahamu wako wa hayo ambayo uliyapata kwa kupitia? Je, umeingia katika uhalisi wa ukweli na njia na uzima? Neno la Mungu limetolewa kwenu ili myapitie na kuyajua; kulisema tu neno hakuna maana.

Unapoelewa na kuingia katika neno la Mungu, basi utaweza kujijua. Usipoelewa neno la Mungu, basi huwezi kujijua. Unaweza tu kumaizi unapokuwa na ukweli; bila ukweli huwezi kumaizi. Unaweza tu kuelewa kabisa jambo unapokuwa na ukweli; bila ukweli huwezi kuelewa jambo. Unaweza tu kujijua unapokuwa na ukweli; bila ukweli huwezi kujijua. Asili yako inaweza tu kubadilishwa unapokuwa na ukweli; bila ukweli asili yako haiwezi kubadilishwa. Ni baada tu ya wewe kuwa na ukweli ndipo unaweza kuyatumikia mapenzi ya Mungu; bila ukweli huwezi kuyatumikia mapenzi ya Mungu. Ni baada tu ya kuwa na ukweli ndipo unaweza kumwabudu Mungu; bila ukweli ibada yako itakuwa tu utendaji wa kaida za kidini. Haya yote yanategemea kupata ukweli kutoka kwa neno la Mungu.

Baadhi watasema, “Inamaanisha nini hasa kupata ukweli kutoka kwa neno la Mungu?” Huwezi kupata ukweli kwa kuzungumzia kanuni tu mara kwa mara; ina maana gani kupitisha vitu hivi sisisi? Sharti utoe ufumbuzi wa maana ya neno la Mungu, kuelewa msingi wake na athari iliyodhamiriwa. Kuna ukweli katika neno la Mungu, maana katika neno Lake, mwangaza katika neno Lake. Kuna vitu vingi ndani ya neno Lake; si jambo rahisi la kukariri maana yake halisi. Nitakupa mfano rahisi. Mungu asema, “Lazima muwe watu waaminifu. Msiwe wenye hila.” Je, mstari huu unamaanisha nini kwa kweli? Baadhi husema, “Je, haukuambii tu uwe mtu mwaminifu na wala si mwenye hila?” Mtu akiuliza, “Je, unamaanishaaje vingine?” mtu huyo ataendelea, “Ni uwe mtu mwaminifu na usiwe mwenye hila tu.Ni vitu hivyo viwili tu” “Mtu huwa mwamnifu kivipi hasa?” Mtu mwaminifu ni nini? Je, dalili kuu za mtu mwaminifu ni zipi?” “Mtu mwaminifu ni mtu yule anayeongea ukweli na kabisa na hadanganyi.” “Mtu mdanganyifu ni nini?” “Mtu mdanganyifu ni mtu mwenye kutoa maneno yenye maana isiyo dhahiri. Mtu asiyesema maneno yenye maana isiyo dhahiri na ambaye hunena ukweli usio zimuliwa ni mtu mwaminifu.” Bila kujali unauliza kiasi gani, utapata kiasi hiki tu kutoka kwake; kufikiria kwa mwanadamu ni rahisi sana. Je, neno la Mungu linasema nini kumhusu mtu mwaminifu? Kitu cha kwanza kuhusu mtu mwaminifu ni kuwa hana tashwishwi kuhusu wengine. Je, Mungu anamaanisha nini kuhusu hili? Kwa nini Mungu anasema hili? Tafakari hilo na kuliwazia; watu hawawezi kuelewa hilo. Pili, mtu mwaminifu anaweza kuukubali ukweli. Neno la Mungu linasema hasa kuwa mtu mwaminifu anatosheleza hali hizi mbili. Unaweza kuelewa maana halisi ya mtu mwaminifu ktika neno la Mungu, linazungumzia nini hasa, ufafanuzi kamili wa mtu mwaminifu ni nini, na unaweza kupata ufafanuzi sahihi; utajua kutoka kwa neno la Mungu ni mienendo gani mingine ambayo mtu mwaminifu huonyesha, mtu wa aina gani ni mdanganyifu, ni mtu wa aina gani ambaye ni mwaminifu; na mtu mwaminifu anavyotenda. Tazama tena mtu mwaminifu kutoka kwa mtazamo wa mienendo hii, na kisha utaelewa jinsi watu waaminifu na waongo walivyo na watu waongo wanavyochukulia neno la Mungu, Mungu, na watu wenigne. Katika njia hii utafikia ufahamu wa kweli wa neno la Mungu na kuelewa jinsi tofauti kati ya neno Lake na ufahamu wa mwanadamu wa mtu mwaminfu na mdanganyifu ilivyo kuu. Inapoangaliwa kutoka ndani ya neno la Mungu, kuna maelezo mengi zaidi kwa “Unapaswa kuwa mtu mwaminifu. Usiwe wale wadanganyifu.” Unapoelewa maana ya neno la Mungu kwa kweli, basi unajua mtu mwaminifu ni nini, na mtu mdanganyifu ni nini; na unapoweka kwenye vitendo utajua hakika jinsi ya kutenda kama mtu mwaminifu, na utakuwa na njia ya kuwa mtu mwaminifu, ambayo hakika inaweza kutosheleza kiwango cha Mungu. Je, una umahiri wa kiwango hiki? Iwapo kweli unaelewa maneno haya na kuyaweka katika vitendo, basi unaweza kupata kibali cha Mungu. Iwapo huelewi msemo huo, basi huwezi kuwa mtu mwaminifu, na kabisa hutaweza kupata kibali cha Mungu. Kuja kwako kufahamu kweli maana hasa ya neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri tukwamba unaweza kutafsiri maana halisi ya maneno yote ya Mungu, na kila mtu husema kutafsiri kwako ni kuzuri na kukupa hongera, hivyo inamaanisha unaelewa neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata baadhi ya nuru kutoka ndani ya neno la Mungu na umeelewa maana halisi ya neno la Mungu, ikiwa unaweza kusema maana ya neno la Mungu ni nini na ni nini athari ya mwisho linaloleta, ni wakati tu haya yako wazi ndipo kuna kiwango fulani cha kuelewa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo mazuri ya herufi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyotafsiri herufi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu na ni bure! Je, neno la Mungu linapasa kutafsiriwa vipi?

Je, neno la Mungu linapasa kueleweka vipi? Msingi ni kuelewa neno Lake kutoka ndani ya neno Lake. Kila mara Mungu anenapo hakika Haneni kwa ujumla tu. Ndani ya kila sentensi kuna maudhui yenye maelezo ambayo yana uhakika wa kufichuliwa zaidi katika neno la Mungu, na yanaweza kuonyeshwa kwa njia tofauti. Mwanadamu hawezi kuelewa njia ambazo Mungu huonyesha ukweli. Neno la Mungu lina undani na haliwezi kuingiliwa na njia ya mwanadamu ya kufikiria. Watu wanaweza kugundua maana kamili ya kila kipengele cha ukweli mradi watie bidii, na maelezo yanayosalia yanajazwa kabisa Roho Mtakatifu anaponurisha ufahamu wako wa hali dhabiti kwa kupitia. Sehemu moja ni kuelewa neno la Mungu kwa kupitia neno Lake, kutafuta maudhui mahsusi ya neno Lake. Sehemu nyingine ni kuelewa athari za neno la Mungu kwa kulipitia na kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Kimsingi ni kwa njia hizi mbili ndipo ufahamu wa kweli wa Mungu unatimizwa. Ukitafsiri kupitia herufi ya neno ama mawazo ya namna yako ya kufikiria, basi ufahamu wako si wa kweli hata ikiwa unaweza kuitafsiri kwa lugha ya ushawishi wa juu sana. Usipofanya kwa usahihi, utapotoka hata kutoka katika muktadha na kuelewa neno la Mungu visivyo, na hilo ni la taabu hata zaidi. Hivyo, ukweli unapatikana kikanuni kwa kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu unapokuja kujua neno la Mungu. Ukweli hauwezi kupatikana kutoka kwa ufahamu tu ama utafsiri wa herufi ya neno Lake. Kama unahitaji tu kutafsiri herufi ya neno Lake, basi ni nini maana ya kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu? Katika hali hiyo kiwango fulani cha masomo kingeweza kufanya kazi, na wasiosoma wangekuwa kwenye hatari kabisa! Kazi ya Mungu haiwezi kufahamika na akili ya mwanadamu. Ufahamu wa kweli wa neno la Mungu unategemea hasa kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; hii ni namna ya kuupata ukweli.

Inapofikia kujua asili ya mwanadamu, kitu cha muhimu zaidi ni kuijua kutoka kwa mtazamo wa maoni yake ya dunia, maoni ya maisha, na maadili. Wale wote walio wa ibilisi wote huishi kwa ajili yao wenyewe. Kanuni zao na wanavyoishi ni hasa maneno hayo yanayotoka kwa Shetani kama vile, “Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa.” Maneno ya mashetani hao, wakuu, na wanafalsafa wa dunia yamekuwa maisha yao. Mengi ya maneno ya Konfyushasi, ambaye anadhaniwa kuwa “mjuaji” na watu wa Kichina hususan yamekuwa maisha ya mtu. Pia kuna misemo maarufu ya Ubudha na Utao na misemo maarufu zaidi yanayosemwa mara kwa mara na watu mashuhuri; haya yote ni muhtasari wa falsafa ya Shetani na asili ya Shetani.Pia ni vielezo vizuri sana na maelezo ya asili ya Shetani. Sumu hizi ambazo zimtiliwa mioyoni mwa wanadamu zote hutoka kwa Shetani; hakuna hata chembe yao inayotoka kwa Mungu. Uongo huu na upuuzi pia ni upinzani kwa neno la Mungu hasa. Ni wazi kabisa kuwa uhalisi wa vitu vyote vyema hutoka kwa Mungu, na vitu vyote hivyo hasi ambavyo humtia sumu mwanadamu hutoka kwa Shetani. Hivyo, unaweza kumaizi asili ya mtu na yeye yu wa nani kutoka kwa maoni yake ya maisha na maadili. Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Uongo wao na upuuzi vimekuwa uzima wa mwanadamu na asili. “Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa” ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na kuwa maisha ya mwanadamu. Kuna baadhi ya maneno mengine ya falsafa ya maisha ambayo pia ni kama haya. Shetani huwasomesha watu kupitia utamaduni mzuri wa kila taifa na kuwapelekea wanadamu kuanguka ndani, na kumezwa na lindi kuu la mtanuko la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu. Ebu fikiri kumwuliza mtu ambaye amekuwa mtendaji katika jamii kwa miongo swali lifuatalo, “Umeishi duniani kwa muda mrefu sana na kutimiza mengi sana; je, unafuata misemo ipi maaarufu?” Watasema, “Muhimu sana ni ‘Wale ambao hutoa zawadi kwa wale wenye madaraka rasmi hawagongwi nao, na wale wasiojipendekeza hamna wanachofanikisha.” Je, hufikiri kuwa hotuba kama hii ni uwakilisho wa asili yake? Asili yake si kuepuka mbinu zozote za kupata hadhi, kuwa na madaraka rasmi ndiko kunakompa uzima. Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu na katika wanavyoshughulikia mambo, na katika mienendo yao na maafikiano na wengine—karibu wawe bila hata chembe ya ukweli—kwa mfano, falsafa yao ya maisha, kanuni zao za mafanikio, au njia zao za kufanya vitu. Kila mtu anajazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, kinachobubujika kwa mifupa na damu ya watu ni vitu vya Shetani vyote. Kila mtu ambaye hutimiza mafanikio ya kidunia ana njia yake na siri ya kufaulu, hivyo si siri hiyo ni uwakilisho mzuri zaidi wa asili yake? Unaweza kuona kuwa asili ya watu hawa ni yenye hila sana–ni wenye madaraka rasmi ya juu na wameyafanya mambo makuu duniani. Asili yao ni yenye kudhuru kwa siri na ya sumu—wana uwezo wa kufanya lolote. Mwanadamu amepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na asili ya mwanadamu imepotoka waziwazi, ni yenye uovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—ni asili inayoasi dhidi ya Mungu kabisa. Asili ya mwanadamu inaweza kujulikana na kila mtu ikichanguliwa hivi.

Ni tu pale ambapo mtu anamjua Mungu na kuwa na ukweli ndipo huishi nuruni; na ni pale tu ambapo maoni yake ya dunia na maoni yake ya maisha yanabadilika ndipo anabadilika kimsingi. Anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli; anapomtii Mungu kabisa na kuishi kwa neno la Mungu; anapohisi kuhakikishiwa na kuchangamshwa ndani ya moyo wake; moyo wake unapokuwa huru bila giza; na anapoishi kikamilifu na kwa huru na bila kuzuiwa kenye uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli. Aidha, ukweli wote ulio nao unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe, kama mwadamu halisi anayeishi maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, nini linaweza kuwa la maana zaidi kuliko hili? Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli. Katika dunia hii ya sasa iliyo chini ya miliki ya Shetani, kupitia miaka elfu ya historia ya mwanadamu, ni nani aliyepata uzima? Hamna. Je, mbona hivi? Wote ni watu ambao wamempinga Mungu. Kila kitu ambacho wameishi maisha yao kwacho na kudumu kinatoka kwa Shetani na kilikubalika kutoka kwa Shetani na hasa ni upinzani kwa neno la Mungu na kilikubaliwa kutoka kwa Shetani na hasa ni upinzani kwa neno la Mungu. Hivyo, ni viumbe wanaompinga Mungu, wanaopitia laana Yake, na hawana uzima wa kuzungumzia. Hata ingawa wanataka “kuacha sifa inayodumu,” kufanya majina yao yapitishwe kwa mamia ya vizazi,” na “kuwa na jina linalodumu,” haya yote ni upuuzi. Hakika, walilaaniwa na Mungu kitambo, wasiweze kupata mwili mpya asilani. Maneno ya watu mashuhuri, yoyote yale, kimsingi hayakubaliani na Mungi, na wote huadhibiwa katika kiwango cha kumi na nane cha jahanamu baada ya wao kufa. Mungu tu ndiye ukweli. Mungu hudhibiti mbingu na dunia na vyote vilivyomo na ana mamlaka juu ya vyote. Kutoamini Mungu, kutomtii Mungu ni kutokuwa na uwezo wa kupata ukweli. Ukiishi kulingana na neno la Mungu, utahisi uwazi, udhabiti, na utamu usioweza kulinganishwa ndani kabisa ya moyo wako; utakuwa umepata uzima kwa kweli. Bila kujali mafanikio ya kisayansi ya wanasayansi duniani ni makuu kiasi gani, wanapokaribia kifo, wanahisi kuwa mikono mitupu; hawajapata lolote. Hata Eisten na Newton, wakiwa na maarifa mengi zaidi, walihisi utupu, na hilo ni kwa kuwa hawakuwa na ukweli. Newton na Galileo, hususan, wote walimwamini Mungu na walikuwa Wakristo; waliteswa na kanisa la Ukatoliki ila hawakutafuta ukweli. Walijua tu ilikuwa vyema kumwabudu Mungu. Walisoma sayansi tu na kugundua kuwa hakika kuna Mungu, na wakamwamini Mungu hadi mwisho, wakaishia kusadiki asilimia mia moja kuwa Mungu yupo na kusadiki asilimia mia moja kuwa Aliumba mbingu na nchi na vitu vyote. Walitafuta tu maarifa ya kisayansi na hawakutafuta kumjua Mungu. Hawakuupata ukweli, wala kupata uzima wa kweli. Njia mnayotembelea leo si njia yao. Mnachotafuta ni kumjua Mungu, jinsi ya kumtii Mungu, jinsi ya kumwabudu Mungu, jinsi ya kuishi maisha yenye maana—tofauti kabisa na kile walichotafuta. Sasa, Mungu mwenye mwili amewaambia kuhusu vipengele vyote vya ukweli na kukupa njia ya ukweli na uzima. Kutotafuta ukweli kutakuwa upumbavu kwenu.

Sasa mnahisi kama bado mmepungukiwa, kwamba kuna ukweli mdogo sana ndani yenu, kwamba hamhisi kustawika ndani yenu. Hili ni kwa sababu kuingia kwenu kumekuwa kwa juujuu sana, na bado hamna uzoefu wa kina. Unapokuwa umeelewa neno la Mungu kwa kweli na kuingia katika neno la Mungu utakuwa na nguvu, na nguvu inayojaa mwilini mwako na haiwezi kutumiwa vikamilifu. Wakati huo, utahisi mchangamfu ndani yako zaidi na zaidi, na njia itakuwa angavu zaidi kadri unavyozidi kuitembelea. Watu wengi sasa wanamwamini Mungu ila hawajaingia katika njia iliyo sawa. Bado wanahisi watupu na watepetevu, wakati mwingine hata kuhisi kana kwamba kuishi kote ni mateso, utupu wote—hata wanatamani kufa! Hivi ndivyo mtu alivyo kabla ya moyo wake kuwa na maono. Mtu wa aina hii hajapata ukweli na hamjui Mungu bado, hivyo bado hahisi furaha nyingi ya ndani. Hususan nyinyi ambao mmepitia mateso na ugumu wakati wa kurudi nyumbani, mmeteseka na pia mna fikra za kifo na kutokuwa na radhi kuishi; huu ndio udhaifu wa mwili. Baadhi ya watu hata hufikiri kuwa ikiwa wanamwamini Mungu basi wanapaswa kuhisi ridhaa ndani yao. Katika Enzi ya Neema Roho Mtakatifu bado alitoa amani na furaha kwa watu. Sasa kuna amani na furaha kidogo sana; hakuna ridhaa kama iliyokuwa wakati wa Enzi ya Neema. Leo kumwamini Mungu kunaudhi. Unajua tu kuwa ridhaa ya mwili ni nzuri kupita chochote kingine. Hujui kile ambacho Mungu anafanyia kazi leo. Mungu anaruhusu miili yenu iteseke ili kubadilisha tabia yenu. Hata ingawa miili yenu inateseka, mna neno la Mungu na mna baraka ya Mungu. Huwezi kufariki hata ukitaka: Je, unaweza kukubali bila malalamiko kutomjua Mungu na kutopata ukweli? Sasa hasa ni kuwa bado watu hawajapata ukweli tu, na hawana maisha. Sasa watu wako katikati ya mchakato wa utafutaji wa wokovu, hivyo lazima wayapitie baadhi ya hayo wakati huu. Leo kila mtu duniani hujaribiwa: Mungu bado anaumia—je, ni vyema kwamba usiteseke? Bila kusafishwa kupitia maafa makubwa hakuwezi kuwa na imani halisi, na ukweli na uzima havitapatikana. Kutokuwa na majaribio na usafisho kusingesaidia. Unaona, Petro alijaribiwa kwa miaka saba mwishowe (baada ya kuhitimu miaka hamsini na mitatu). Aliyapitia mamia ya majaribio katika miaka hiyo saba, na baada tu ya hiyo miaka mitatu na mitatu na moja zaidi ndipo alipopata uzima na mabadiliko ya tabia yake. Hivyo, unapopata ukweli kwa kweli na kuja kumjua Mungu unahisi kuwa maisha yanapaswa kuishwi kwa ajili ya Mungu. Kutoishi kwa ajili ya Mungu ni jambo la kujutia sana. Ungeishi maisha yako kwa majuto machungu na toba iliyopita kiasi. Bado huwezi kufa. Sharti ukaze ngumi yako na kuendelea kuishi kwa ari; lazima uishi maisha kwa ajili ya Mungu. Watu wanapokuwa na ukweli ndani yao basi wanakuwa na azimio hili na kamwe hawatamani kufa tena; kifo kinapokutisha, utasema, “Ee Mungu, siko radhi kufa; bado sikufahamu!” Bado sijalipiza upendo Wako! Lazima nife baada tu ya kukujua Wewe vyema. Je, mmefikia kiwango hiki? Bado, siyo? Baadhi ya watu hupitia dhiki ya kifamilia. Baadhi ya watu hupitia dhiki ya ndoa. Baadhi ya watu hawana maskani ya kuishi ama hata mahali pa kuishi; wanaweza tu kuishi katika maskani ya wengine popote waendapo, na wanataka kuwachukulia kama ni wao na kufurahia uhuru mdogo, lakini hilo haliwezekani kwa kuwa wako katika makazi ya wengine, hivyo wanateseka mioyoni mwao. Je, mateso mnayokumbana nayo sasa si sawa na mateso ya Mungu? Mnateseka pamoja na Mungu, na Mungu yuko pamoja na watu katika mateso yao, siyo? Leo nyinyi nyote mna sehemu katika mateso ya Kristo, ufalme, na subira, na kisha, mwishowe Mtapata utukufu! Aina hii ya mateso ina umuhimu. Kutokuwa na azimio hakutasaidia. Ni lazima uelewe umuhimu wa mateso ya leo na kwa nini lazima uteseke hivyo. Tafuta ukweli mdogo kutoka kwa hili na kuelewa machache ya nia ya Mungu, na kisha utakuwa na azimio la kuvumilia mateso. Ikiwa huelewi nia ya Mungu na unatafakari tu kuhusu mateso yako, basi kadri unavyozidi kuyawaza ndivyo itazidi kuwa vidumu kuvumilia—hilo lasumbua—na hivyo mateso ya kifo yanaanza. Ukiuelewa ukweli utasema, “sijaishi vya kutosha! Mbona nife? Bado sijapata ukweli! Lazima nitumie rasilmali yangu kwa ajili ya Mungu sawasawa. Lazima niwe na ushuhuda mzuri wa Mungu. Lazima nilipize upendo wa Mungu. Baada ya hapo, haijalishi jinsi nitakavyokufa. Kisha, nitakuwa nimeishi maisha ya kutosheleza. Bila kujali ni nani mwengine anayekufa, sitakufa sasa; lazima niendelee kuishi kwa ushupavu. Hivyo, vitu hivi vyote lazima viangaliwe waziwazi, na ukweli sharti ueleweke kutoka kwa vitu hivi. Watu wanapokuwa na ukweli, wanakuwa na nguvu. Wanapokuwa na ukweli, miili yao inajawa na nguvu isiyoisha. Wanapokuwa na ukweli, wanakuwa na radhi. Bila ukweli, wao ni kama makapi laini ya tofu. Na ukweli, wao ni dhabiti na wenye kutiwa moyo, na hawahisi kuwa mateso yao ni mateso bila kujali wanavumilia mangapi. Kuteseka kwenu huku kunaleta nini? Mungu mwenye mwili bado Anateseka! Ninyi ni watu ambao wanapotoshwa na Shetani na wenye asili inayoasi dhidi ya Mungu. Nyote mmeyafanya mambo mengi yanayomuasi Mungu bila ufahamu, katika kumpinga Mungu. Mnapaswa kuhukumiwa na mnapaswa kuadibiwa. Mtu anayeugua hawezi kuogopa kuteseka anapotibiwa, hivyo ni vyema kwenu, ninyi mnaotaka tabia zenyu potovu kubadilishwa na kuupata uzima, kutoumia kidogo? Mateso yenu yanapasa kuvumiliwa; lazima yavumiliwe. Mateso haya hayaanguki juu ya yasiyo na kosa, na hata zaidi hayalazimishwi kwanu. Mnayoyapata sasa si lolote ila ugumu wa safari yenu ya mara kwa mara na uchovu mdogo kutoka kwa kazi yenu. Wakati mwingine mnapitia usafisho kiasi katika neno la Mungu. Wakati mwingine mnakuwa na ufahamu wa upotovu wenu wenyewe na kuhisi kuwa kamwe hambadiliki, na kwa kiasi mnateswa na asili yenu potovu. Wakati mwingine kuna sehemu ya neno la Mungu ambalo hamwezi kulielewa asilani, ama mioyo yenu inachomwa inaposoma neno la Mungu na mnahisi kuumizwa. Ama, ninyi hufanya kazi yenu vibaya na daima kuyafanya makosa, mkijilaumu, mkichukia kwamba hamwezi kustahimili na kwamba hamwezi kufanya kazi. Mnateseka kwa njia hizi zote. Wakati mwingine mnawaona wengine wakiendelea na mnahisi kuwa kuendelea kwenu ni kwa asteaste sana, kwamba mnalipokea neno la Mungu polepole sana, kwamba mwanga ni nadra kabisa. Mnayapata mengine kwa njia hizi; je, kuna mateso yapi mengine kando na ya aina hizi? Hamfanyishwi kazi yoyote kubwa, na hamna wakuu ama mabwana wanaowachapa wala kuwalaani, na hakuna anayewafanya kuwa watumwa. Hamyapiti yoyote hayo, siyo? Dhiki mnazopitia sizo dhiki halisi kabisa. Fikiria kuhusu hilo kwa muda mdogo—je, hali si hiyo? Wakati mwingine mazingira yenu yanawatisha, yakiweka akili zenu katika hali ya wasiwasi, yakiwazuia kuwa na mapunziko, na mnateseka kidogo kuishi na hofu. Lazima muelewe ni nini maana ya kutoa kwenu kwa familia yenu na kutumia rasilmali yenu kwa ajili ya Mungu na kwa nini mnataka kufanya haya. Ikiwa ni ili kutafuta ukweli, kutafuta uzima, na kufanya machache ili kutimiza jukumu lenu na kulipiza upendo wa Mungu, basi hiyo ni ya haki kabisa, kitu kizuri, na ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya ulimwengu. Katika hali hii, hamtawahi kuwa na majuto, na mtaweza kuachilia familia zenu bila kujali hali. Sivyo? Ikiwa u wazi juu ya umuhimu huu basi hutakuwa na majuto, na hutakuwa mbaya. Ikiwa, hata hivyo, huji kutumia rasilmali yako kwa ajili ya Mungu, basi haina maana, na unapaswa kurudi haraka, na punde unapoona jambo hilo waziwazi tatizo litatatuliwa na hakutakuwa na haja ya wasiwasi; yote yako mikononi mwa Mungu.

Sasa ninyi nyote mnapitia dhiki kiasi ya majaribio. Baadhi yenu mna ukweli fulani; wengine hawana. Baadhi ya watu huupokea kwa njia hii; wengine hupokea kwa njia nyingine. Bila kujali unavyoupokea, mradi kuna ukweli ndani yako na unaupokea kwa njia sahihi, mateso yako yatakuwa na maana na thamani, utakuwa na ushupavu, na utafanikiwa hadi mwisho. Usipopokea ukweli ila upokee tu fikra za mwanadamu na mawazo, basi kuteseka kwako hakuna maana kwa sababu hujaupata ukweli. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika kila kitu na sharti uutafute ukweli katika kila kitu. Je, unatafuta vipi ukweli katika mambo ya kula na kuvaa mavazi na mambo ya maisha ya binafsi? Je, kuna ukweli wa kutafuta ndani ya vitu hivi? Baadhi husema, “Lolote usemalo, kula vizuri ni vyema; kuvaa vizuri ni vyema. Kula au kuvaa vibaya ni hasara.” Je, kuna ukweli katika maoni haya? Hamna! Je, ni muhimu kwa maisha ya mtu kula vizuri na kuvaa vizuri? La hasha! Ukiwekwa kwa njia nyingine, ikiwa mtu anaweza kumjua Mungu kweli na kuwa na ukweli, kila anachofanya ni kuwa na ushuhuda wa Mungu, kinamridhisha Mungu. Bila kujali anavaa na kula vibaya kiasi gani, kuna thamani katika kuishi kwake, na anapata kibali cha Mungu—je, hicho si kitu cha maana zaidi? Kuvaa mavazi ya aina gani si kwa maana ya kimsingi kabisa. Baadhi husema, “Inapofika wakati wa kumtafuta mwenzi ni bora zaidi kuvaa vizuri.” Hata hilo si hakika. Fikiria kupatana na mwenzi ambaye anavutia kabisa, mwenye sura nzuri kabisa. Unavaa nguo nzuri; anavutiwa na wewe na kukuoa. Lakini iwapo mtu huyu ni ibilisi, basi atakuletea huzuni! Ukikutana na ibilisi unaopokuwa umevalia nguo zilizochanika na kofia la mabua, na asivutiwe na wewe, je, hujaepuka msiba? Hutabarikiwa kwa lazima kwa kuvaa nguo nzuri. Bado utalaaniwa kwa ajili ya kuchukua kwa njia mbaya. Na, mtu aliyevaa nguo mbovu na ambaye anamiliki ukweli atabarikiwa na Mungu vilevile. Hivyo, kuna ukweli wa kutafuta katika jinsi unapaswa kushughulikia kula na kuvaa. Na kuna ukweli zaidi wa kutafutwa katika jinsi unavyopaswa kuchukulia utendaji wa wajibu wako. Unapaswaje kuchukulia Agizo la Mungu? Hili ni jambo zito sana! Ikiwa huwezi kukamilisha kile ambacho Mungu humwaminia mtu, hufai kuishi katika uwepo wa Mungu na unapaswa kuadhibiwa. Ni amri ya mbingu na kanuni ya dunia ya mwanadamu kumaliza kile ambacho Mungu humwaminia; hili ni jukumu la juu kabisa la mwanadamu, muhimu kama maisha yake. Ikiwa hulichukulii Agizo la Mungu kwa uzito, basi unamsaliti Mungu kwa njia kuu zaidi; hili ni la huzunisha zaidi kuliko Yuda na linastahili kulaaniwa. Hivyo, Mungu anamwagiza mwanadamu: Huku ni kutukuzwa kukuu na mapendeleo maalum kutoka kwa Mungu, jambo la utukufu kuu zaidi. Kila kitu kingine kinaweza kuachwa—hata ikiwa itamlazimu mtu kutoa maisha yake bado lazima atimize Agizo la Mungu. Unaona, kuna hata ukweli zaidi wa kutafutwa hapa.

Mabadiliko ya tabia na kutafuta ukweli yanahusiana kwa undani sana. Ikiwa unaelewa ukweli wa kwa nini watu huishi na jinsi unapaswa kuyaangalia maisha, basi maoni yako kuhusu maishai hayatabadilika? Kuna ukweli zaidi ndani ya hili kutafutwa. Je, kuna ukweli gani katika kumpenda Mungu? Je, ni kwa nini mwanadamu sharti ampende Mungu? Je, umuhimu wa kumpenda Mungu ni upi? Ikiwa mtu yuko wazi kuhusu ukweli wa kumpenda Mungu na anaweza kumpenda Mungu moyoni mwake—kama moyo wake unaweza kumpenda Mungu kiasi kidogo—basi ana maisha ya kweli na ndiye mbarikiwa zaidi. Wale wanaotafuta ukweli katika kila kitu huendelea kwa haraka zaidi maishani na wanaweza kutimiza mabadiliko ya tabia. Wale wanaotafuta ukweli katika kila jambo ni wale wanaopendwa na Mungu kabisa. Iwapo mtu hutegemea fikra na kanuni ama hutii amri katika mambo yote, basi hataendelea, daima hatakuwa na ukweli, na sasa ama hivi karibuni ataondolewa—Mungu humchukia kabisa mtu wa aina hii.

Iliyotangulia:Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako

Inayofuata:Sura ya 42. Kwa Kutafuta Ukweli tu Ndio Unaweza Kupata Mabadiliko katika Tabia Yako