20. Ndoto Yangu ya Kuwa Mwelekezi

Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Sikuwahi kuwa na ufahamu wa vitendo kuhusu kifungu hiki. Nilidhani kwamba imani ilimaanisha tu kusoma neno la Mungu mara nyingi, kutekeleza wajibu wangu kwa uangalifu, na kutenda kama Mungu anavyotuambia, kwamba haya yalitosha kupata kibali cha Mungu. Nilijiuliza, kwa nini lazima tupitie hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu? Pia, Mungu anapowahukumu watu, je, Yeye hawalaani? Kwa nini inasemekana kwamba kuadibu na hukumu ni wokovu na ulinzi? Ni baada tu ya mimi binafsi kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ndipo mwishowe nilipata ufahamu wa kibinafsi kuhusu kifungu hiki.

Wajibu wangu ulikuwa kuimba katika kwaya. Nilikuwa na maoni fulani juu ya kuwasilisha maonyesho yetu, kwa hivyo msimamizi wetu aliniagiza nifanye mpango pamoja na kikundi cha waelekezi. Niliposikia habari hiyo, nilifurahi sana na nikamshukuru Mungu kwa kuniinua. Nilipojiunga na kikundi cha waelekezi kwa mara ya kwanza, nilihisi kwamba nilikuwa na upungufu sana, kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa bidii na kumtegemea, na nilikuwa mwangalifu sana katika kila kitu nilichosema na kufanya. Lakini baada ya muda kidogo, maoni yangu mengine yalipoidhinishwa na kukubaliwa na kina ndugu, nilihisi kwamba nilikuwa nikifanya vizuri, na kwamba labda ulikuwa wakati wa talanta yangu kuangaza. Nilianza kuongea zaidi na kuwa mwenye kujiamini polepole. Hasa nilipokuwa nikijadili kazi na wengine, nilitaka kujionyesha sana, na wakati mwingine nilidakiza ili kuongea kabla ya mwenzangu kuongea. Dada yule ambaye nilishirikiana naye alizuiwa nami kidogo. Nilijua kuhusu hilo, lakini badala ya kumsaidia na kumuunga mkono kutokana na upendo, nilimwambia atafakari juu yake mwenyewe kwa sauti ya kuhoji na ya kudunisha. Baada ya kunisikia nikisema hivyo, mbali na hali yake kutokuwa nzuri zaidi, pia alianza kuwa hasi, na hata akasema kwamba hakutaka kufanya wajibu huu tena. niliwaza, “Hiyo ni bora zaidi kwani nitachukua nafasi yako.” Lakini baada ya hapo, hali yake ilianza kuboreka polepole kupitia kula na kunywa neno la Mungu. Nilimshukuru Mungu kwa maneno yangu, lakini ndani ya moyo wangu, sikuridhika sana. Nilihisi kwamba nafasi nzuri ilikuwa imepotea. Nilivunjika moyo sana, nikijiuliza ni kwa nini msimamizi hakutambua kipaji changu, na kwa nini hakuona uwezo wangu. Ili kujithibitisha, nilianza kuwa katili hata zaidi na mwenye bidii zaidi, na nikajitosa katika kuboresha ujuzi wangu. Baadaye, maoni yangu mengine yaliungwa mkono na watu wengi zaidi katika timu na nikahisi kwamba nilikuwa na uwezo wa kuwa mwelekezi.

Baadaye kidogo, msimamizi aliniagiza nifuate kikundi cha kupiga picha za sinema. Niliposikia hivyo. niliwaza, “Hiki ndicho waelekezi hufanya hasa! Inaonekana kwamba wananifundisha ili niwe mwelekezi!” Kadiri nilivyozidi kufikiria hilo, ndivyo nilivyozidi kufurahi. Mara baada ya kufika mahali pa kupigia picha, sikumsubiri mtu yeyote aniambie la kufanya. Nilichukua megafoni na nikachukua msimamo wa mwelekezi, nikimwambia kila mtu kitu cha kufanya. Kina ndugu waliokuwako huko walionyesha matatizo kadhaa katika jinsi nilivyofikiri juu ya wajibu wangu, lakini niliwapuuza. Hata niliwaza, “Mnafikiri ninyi ni bora kuniliko? Je, mmewahi kuwa na maoni gani mazuri?” Nilijali tu kuonyesha “maono yangu ya kipekee” Nilitaka tu kumaliza kupiga picha za wimbo huo, nikifikiri baadaye nitakuwa mwelekezi.

Msimamizi alinitafuta baada ya kupiga picha, na nikawaza, “Hakika anataka kunipandisha cheo.” Ajabu ni kwamba, alikuwa amekuja kuonyesha matatizo kadhaa yaliyokuwa katika wajibu wangu. Alisema kwamba nilikuwa mwenye kiburi, dhalimu na dikteta, kwamba sikuwa nimesikiliza ushauri wa ndugu zangu hata kidogo, na kwamba kila mtu alihisi kuwa alizuiwa sana nami. Kumsikia akisema hivyo kulikuwa kama kwamba kumwagiwa maji baridi ya ndoo kichwani pangu. Nilihisi kana kwamba bidii hiyo ilikuwa imekomeshwa kabisa. Niliwaza, “Eti mimi nina kiburi? Bila shaka, mimi huchukulia tu wajibu wangu kwa makini.” Nilivunjika moyo sana na sikuridhika. Msimamizi aliona kwamba sikujaribu kujielewa, kwa hivyo aliniomba nirudi kwenye kwaya. Kupata habari hiyo kuliniumiza sana. Siku chache tu zilizopita, nilidhani kwamba nilishikilia mamlaka kwenye jukwaa, lakini sasa nilirudishwa kwenye kwaya bila heshima. Je, watu watanionaje? Nilikuwa pia na malalamiko juu ya msimamizi. Niliwaza, “Kwa nini nisisalie katika kikundi cha waelekezi? Je, sijalipa gharama? Nimefanya kazi kwa bidii, hata kama haijakuwa kamilifu.” Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba nilikosewa. Kule kwenye kwaya, sikuwa na nguvu ya kufanya mazoezi. Nilishindwa kupumua vizuri na sauti yangu haikulingana na sauti za wengine. Nilihisi kwamba singeweza kuvumilia kutofaulu kuingia katika kikundi cha waelekezi, lakini nilikuwa mwanakwaya mbaya zaidi. Nilihisi kwamba sikuwahi kushindwa vibaya jinsi hiyo. Wale wengine waliona hali yangu na wakajaribu kunisaidia na kuniauni. Lakini nilihisi aibu zaidi. Nilitamani tu dunia ipasuke niingie ndani. Katika kipindi hicho, nilihisi kuwa sikuwa na msaada kabisa, na sikujua nilipaswa kutenda ukweli upi. Nilichoweza tu kufanya ni kwenda mbele za Mungu na kuomba, “Mungu, sijui jinsi ya kupitia haya yote, na sielewi mapenzi Yako. Nahisi mwenye taabu sana. Naomba Uniongoze ili nielewe mapenzi Yako katika haya.”

Baada ya kuomba, nilisoma kifungu cha neno la Mungu. “Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. Watu hawajawahi kuweka kando tamaa yao ya starehe. … Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujitoa nje ya uhasi? Je, si daima ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo?” (“Mbona Hutaki Kuwa Foili?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilihisi kwamba neno la Mungu lilieleza hali yangu kikamilifu. Baada ya kujiunga tena na kwaya, je, uhasi, malalamiko, na suitafahamu zangu havikutokana tu na kutoridhika kwangu kwa ajili ya kukosa cheo kile? Nilifikiria pia jinsi ambavyo, nilipokuwa katika kikundi cha waelekezi, uwezo wangu wa kujionyesha kwa dhati, kutolala usiku kucha, kuteseka, na kulipa gharama haukuwa kwa sababu nilitaka kujali mapenzi ya Mungu na kutekeleza wajibu wangu vizuri ili kumridhisha Mungu, lakini ulikuwa kwa sababu lengo langu la pekee lilikuwa kupata wadhifa wa mwelekezi. Yule dada aliyekuwa mbia wangu alipohisi kwamba alizuiwa na alikuwa katika hali mbaya, mbali na kutojaribu kumsaidia na kumwauni kutokana na upendo, pia nilikuwa na hamu ya kumwondoa ili niweze kuchukua mahali pake. Wakati wa kupiga picha, wakati muhimu kama huo, nilikuwa dhalimu na dikteta na nilikataa kusikiliza ushauri wa kina ndugu, kwa hivyo tulilazimika kurudia kupiga picha nyingi za sinema, na hivyo kuchelewesha maendeleo ya kazi ya nyumba ya Mungu sana. Katika kwaya, kwa kuwa sikuwa nimepata cheo nilichotaka, nilikuwa hasi, nilikuwa na malalamiko, na suitafahamu, na hata nilifikiri kuhusu kuacha kazi yangu, na sikutekeleza wajibu wangu vizuri. Kadiri nilivyozidi kufikiria hilo, ndivyo nilivyozidi kugundua kuwa sikuwa na mantiki. Nyumba ya Mungu ilikuwa imenipa nafasi ya kufanya mazoezi kwa kuniweka katika kikundi cha waelekezi, lakini badala ya kuthamini hilo sana, nililenga sifa na cheo changu. Sikulala usiku kucha, niliteseka, na nikalipa gharama kwa ajili tu ya cheo hicho, na hata nikageuza wajibu wangu kuwa jukwaa la kujionyesha. Jitihada kama hiyo iliweza tu kumfanya Mungu anidharau na kunichukia. Nilizingatia pia ukweli kwamba sikuwa na ujuzi wa kitaalamu, lakini nilikuwa nimepata mwangaza na nuru ya Roho Mtakatifu kwa kuwa tu na hamu ya kujitahidi. Lakini nilipopata mafanikio kidogo tu, badala ya kufikiria jinsi ya kumshukuru Mungu, nilitumia vitu hivi kama mtaji kwangu na nikaiba utukufu wa Mungu bila aibu. Kadiri nilivyozidi kufikiri, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba nilikosa kabisa dhamiri na mantiki. Nilijiuliza, mawazo yangu yalikuwaje tofauti na ya wasioamini? Nilipogundua hilo, nilipiga magoti mbele ya Mungu na kutubu, “Mungu, nilishindwa kutimiza wajibu wangu vizuri. Nilitafuta sifa na cheo, nikaizuia sana kazi ya nyumba ya Mungu, na kusababisha madhara mengi kwa ndugu zetu. Mungu! Nilikosea, na sitaki kuendelea kufuatilia haya. Nataka kutekeleza wajibu wangu nikiwa imara.”

Baadaye, kwa sababu ya ukuzaji wa Mungu, kama kazi ya kanisa ilivyohitaji baada ya muda mfupi, nilirudi kwenye kikundi cha waelekezi na kuendelea kufanya kazi pamoja na wale kina ndugu. Wakati huu kwenye kikundi cha waelekezi, nilijikumbusha kila wakati kwamba nilipaswa kushikilia nafasi yangu, kwamba sikufaa kufuatilia sifa na cheo changu tena. Lakini, kwa kuwa sikuelewa asili yangu mwenyewe, na kwa kuwa sikuwa bado nimebaini kiini na matokeo ya kufuatilia sifa na hadhi, muda mfupi baadaye, wakati ambapo maoni yangu mengine yalipata idhini na kukubaliwa na kila mtu tena, tamaa hiyo ya hadhi ilianza tena kuongezeka ndani yangu, hadi kufikia hatua ambayo niliwaza, “Nataka kurudi na kufanya jambo kubwa, nataka kumwonyesha kila mtu jinsi nilivyo na uwezo.”

Baadaye katika mazoezi, wakati ambapo kila mtu alikuwa amesimama msitarini kulingana na maelekezo yangu, wakati huo nilihisi tena kama mwelekezi anayesimamia kila kitu, na tamaa yangu ya hadhi ikaanza kukua mpaka sikuwa tena na hamu yoyote ya kuomba au kumtegemea Mungu, na nilizama kabisa katika furaha ya kuwaelekeza wengine. Haikuchukua muda mrefu kabla ya matatizo kutokea katika wajibu wangu. Vizuizi vilizuka kwenye mipango yangu kila wakati, na ghafla, nilichanganyikiwa na sikujua jinsi ya kutatua matatizo haya. Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimegonga mwamba, na sikuweza kuhisi nuru au mwongozo wa Roho Mtakatifu hata kidogo. Hasa kina ndugu walipotaja matatizo kadhaa yaliyokuwa katika utekelezaji wa wajibu wangu, nilikuwa mwepesi sana wa kuathiriwa, nikijiuliza iwapo walihisi kwamba sikuwa na uwezo wa kuetekeleza wajibu huu. Msimamizi alipokuja kunijulia hali, nilihisi kama nilikuwa katika hali ya wasiwasi. Niliwaza, je, nitahamishwa? Je, hii inamaanisha kwamba sitaweza kufanya wajibu huu tena? Kina ndugu walipokuwa na maoni fulani ambayo yalikuwa bora kuliko yangu, nilihisi wasiwasi hata zaidi. Je, mtu mwingine atapandishwa cheo badala yangu? Nilishinda kila siku katika hali ya wasiwasi kila wakati, na ilinichosha sana. Sikupendezwa na wajibu wangu hata kidogo. Shida zilizokuwa katika wajibu wangu zilisalia, lakini nilihisi kwamba nilikuwa nimepotea kabisa, na sikuthubutu kuwaambia ndugu zangu kuhusu hilo, nikiogopa kwamba mara watakapojua ukweli kunihusu, watadhani kwamba sistahili wajibu huu. Kwa hivyo, nilijizuia, nikaficha hilo, na kujifanya, na kwa hivyo sikuweza kutimiza wajibu wangu. Niliishi katika hali ya kutafuta hadhi, nikijisumbua kuhusu kile ambacho ningepoteza, na hali yangu ilizidi kuwa mbaya hadi mwishowe, iliathiri kazi ya nyumba ya Mungu moja kwa moja, na kuchelewesha kazi sana, na mwishowe, nilihamishwa. Siku ambayo nilihamishwa, nilihisi kwamba kwa mara nyingine nilikuwa nikiacha kazi ya kuwaelekeza wengine kwa kuwa mmoja wa wale walioelekezwa. Ghafla, nilikuwa nimeshushwa tena kutoka mahali pa hadhi. Wakati huo, sikuweza kuelewa kabisa. Nilijiuliza ni kwa nini niliendelea kujikuta katika hali hii. Nilitaka kuwa mwelekezi. Je, hilo kwa kweli lilikuwa jambo gumu sana? Je, haikuwezekana kunipa nafasi kwa kweli? Nilipofikiria hayo sana, nilizidi kuwa hasi na kufadhaika. Kina ndugu wengine wote waliimba nyimbo za kumsifu Mungu. Lakini kwangu, kwa kuwa nilikabiliwa na upotezaji wa cheo changu, fedheha, na mabadiliko katika wajibu wangu, na hasa hayo mateso ya kutamani kitu ambacho huwezi kukipata, zile siku chache za mazoezi zilikuwa kama miaka mingi ya masumbuko makali. Nilianza hata kuwa na mawazo ya kumsaliti Mungu, ya kutotaka tena kutekeleza wajibu wangu kule. Nilihisi kuwa nilikuwa nimenaswa katika taabu kuu kupita kiasi kiasi kwamba sikuwa na uwezo wa kushinda. Sikujua kile ambacho ningefanya ili kubadili hali yangu.

Kisha jioni moja, nilipinda kifundo cha mguu wangu nilipokuwa nikishuka orofani. Ndugu zangu wote walikuwa wakishiriki kwa bidii katika mazoezi wakati huo, huku nilichoweza kufanya ni kulala kitandani tu, nikishindwa kusonga. Sikuweza kutekeleza wajibu wowote hata kidogo. Kwa kweli sikuwa na maana. Sikuweza kujizuia kukumbuka yale yaliyofichuliwa kutoka ndani yangu nilipoanza kutekeleza wajibu huu kwa mara ya kwanza, kwamba nilitaka kurudi kufanya jambo kubwa sana, lakini sasa, nilikuwa nimeanguka chini kwa aibu … Moyo wangu uliuma nilipokuwa nikifikiria hilo, na sikuweza kujizuia kujiuliza, kwa nini maisha yangu yalikuwa ya taabu hivyo? Kwa nini sikuweza kujizuia kufuatilia sifa na hadhi? Nilimwomba Mungu tena na tena.

Halafu kifungu cha neno la Mungu kikanijia akilini. “Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarufu na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida,wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kwa ajili ya umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa na watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo, bila kujua, watu huvumilia pingu hizi na kutembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa. Kwa ajili ya umaarufu huu na faida hii, binadamu humwepuka Mungu na kumsaliti, na wanazidi kuwa waovu zaidi na zaidi. Kwa njia hii, hivyo kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili). Niliposoma kifungu hiki cha neno la Mungu, nilielewa kwamba Shetani hutumia umaarufu na faida kuwadanganya na kuwadhibiti watu, na kwamba kadiri watu wanavyozidi kufuatilia umaarufu na faida, ndivyo wanavyozidi kutaabika na kupotoka. Hapo zamani, sikuwahi kufikiri kwamba kulikuwa na kosa katika hayo, na falsafa za kishetani kama vile “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake,” “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo” yalikuwa mambo ambayo niliyachukulia kama wito wa kufuata. Nilidhani kwamba huo ulikuwa ufuatiliaji ambao watu walipaswa kuwa nao, na mambo hayo ndiyo tu yalikuwa na kusudi, kwa hivyo shuleni na katika wajibu wangu katika nyumba ya Mungu, niliishi kulingana na falsafa hizi za kishetani, huku nikifuatilia sifa bahau, hadhi, na kufanya wengine waniheshimu. Nilijaribu kujitokeza na kuwa bora zaidi. Sikuweza kuvumilia kuwa mtu wa kawaida, kwa hivyo nilipopata nafasi ya kufanya kazi katika kikundi cha waelekezi tena, nilishikilia kupata cheo kama mwelekezi, kwa sababu nilidhani kwamba wengine wangenistahi kwa njia hiyo pekee na ningeweza kuwaamrisha wengine. Ndiyo sababu nilifurahia sana wakati ambapo kwa mara nyingine nilisimama mbele ya jukwaa, na kuwaamuru wengine. Nilihisi kwamba nilifaa kuvumilia mateso yoyote au kulipa gharama yoyote kwa ajili ya sifa na faida, lakini bila sifa au faida, nilihisi mwenye taabu, kana kwamba maisha hayakuwa na maana. Nilidhani kwa kweli kwamba nilikuwa nimefungwa kwa pingu zisizoonekana na wazo la kuwa na sifa, na nilitaka kuzivua, lakini sikuweza. Sikuweza kabisa kufanya kazi kwa amani pamoja na ndugu zangu katika hali kama hiyo. Nilivuruga na kuizuia tu kazi ya nyumba ya Mungu. Nilizidi kuona kwamba kufuatilia sifa na faida kwa kweli si njia sahihi. Mungu huwachukia watu wanaoishi katika hali hii, na watu wengine huchukizwa nayo pia. Ninapofikiri juu ya kuinuka na kuanguka kwangu, mara mbili, naona kwa kweli huu ulikuwa wokovu mkubwa wa Mungu kwangu. Tamaa yangu ya hadhi ilikuwa kubwa sana, kiasi kwamba ilibidi nipitie majaribio haya na kusafishwa ili nilazimike kwenda mbele za Mungu ili kutafakari juu yangu, kujifahamu, na kutubu kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo niliweza kufuatilia ukweli na kuepukana na tabia hizi potovu za kishetani. Huu ulikuwa wokovu wa Mungu kwangu. Niliona binafsi jinsi ambavyo kuadibu, hukumu, upogoaji, ushughulikiaji, majaribu na utakaso wa Mungu kwa kweli ni wokovu na ulinzi Wake mkuu kwa watu! Ingawa michakato hii iliumiza kwa kiwango fulani, ilinisaidia sana kubadili tabia yangu ya maisha. Mara nilipogundua hayo, nilisujudu ili kuomba na kutubu: “Mungu! Nilikosea, kweli nilikosea. Nimejua taabu na mateso ya kuishi chini ya ushawishi wa Shetani na kufuatilia sifa, faida, na hadhi. Ulinihukumu, Ukanifundisha nidhamu, na kuniamsha kwa njia hii. Haya yote yalikuwa wokovu na upendo Wako mkuu kwangu. Mungu, sitamani tena kufuatilia sifa, faida, na hadhi. Sitayashindania haya tena. Bila kujali ni agizo lipi au wajibu gani utanijia katika siku za baadaye, nitatii.” “Natamani tu kutekeleza wajibu wa kiumbe.” Baada ya kuomba, nilihisi kwamba nilitiwa moyo sana, niliona pia waziwazi kwamba Shetani alikuwa ametumia sifa na faida kuniletea taabu na mateso.

Kufumba na kufumbua, kanisa liliniarifu kwamba, ninaweza kushiriki tena katika mazoezi almradi hilo lisiathiri uponyaji wa kifundo changu cha mguu. Kusikia habari hii kulinifurahisha sana, na nilithamini nafasi yangu ya kufanya wajibu huu. Hata kama ilikuwa sehemu moja ndogo tu, kwangu, ilikuwa ya thamani sana, na ngumu kupata. Hasa, haya yalikuwa katika onyesho ambalo nilishughulikia: Kundi la waumini wanaishi maisha ya taabu, wanateswa na joka kubwa jekundu. wanazungukwa na kila aina ya sumu ya kishetani, wanakandamizwa hadi kufikia kiwango ambacho wanapumua kwa shida. Wanalia, wanapambana, lakini hakuna kinachosaidia, na ni wakati tu nuru ya Mungu inapoangazia nchi hiyo ya giza ndipo kila mtu anaweza kuondokana na utumwa wa nguvu za giza kwa sababu wanasikia sauti ya Mungu na wanapata wokovu wa Mungu. Kushughulikia onyesho hilo kulinigusa sana, kwa sababu nilihisi kwamba nilikuwa katika hali sawa na hiyo. Nilikuwa utumwani katika mahali pa giza kwa muda mrefu sana, nilikuwa nimeteseka sana kwa ajili ya utumwa wa sifa, faida na hadhi, kwa hivyo kila wakati mwale wa mwanga uliposhuka, niliguswa sana na nikamshukuru Mungu sana kwa kuniongoza ili niondokane na utumwa wa sifa, faida, na hadhi. Baada ya kurudi katika kwaya, Sikufikiria tena jinsi ya kujitokeza na kuwa bora zaidi. Nilitaka tu kuwa kiumbe mdogo, na bila kujali nilichohitaji kufanya, nilifurahia kutia bidii katika wajibu wangu na kuwa mnyenyekevu.

Msimamizi yule alikuja kunitembelea baadaye na akaniomba nimwonyeshe dada mmoja mpangilio wa nafasi jukwaani. Mwanzoni, niliwaza, “Ni vizuri kwamba siwezi kwenda jukwaani, lakini sasa sina budi kumwonyesha mtu mwingine mpangilio wa nafasi jukwaani.” Lakini baadaye niligundua tamaa yangu ya hadhi ilikuwa ikijitokeza tena. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu, na kisha maneno ya wimbo mmoja ulinijia. “Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi au malalamishi yoyote. Ulipanga kwamba ningezaliwa katika nchi hii na miongoni mwa watu hawa, na ninapaswa tu kuwa mtiifu kabisa chini ya utawala Wako kwa sababu kila kitu ki ndani ya yale Umepanga” (“Mimi ni Kiumbe Mdogo Sana tu Aliyeumbwa” Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilishiriki kikamilifu katika mazoea yaliyofuata, na nikampa dada huyu mapendekezo mengi. Niliwaza moyoni, pengine sipati matokeo mengi, lakini nilihisi salama sana nilipotekeleza wajibu wangu kwa njia hiyo. Msimamizi alinipangia nimwonyeshe dada mwingine mpangilio wa nafasi jukwaani. Licha ya kulazimika kuhakikisha kwamba mpango wa nafasi ulikuwa sahihi, pia ilibidi nimtungie miondoko. Nilipopokea wajibu huu, Nilihisi kwamba Mungu alikuwa akinijaribu. Hakukuwa na sifa, faida, na hadhi. Mungu alitaka kuona iwapo nitajitolea kikamilifu katika wajibu wangu. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu kwa dhati, na chini ya mwongozo Wake, kila kitu kilikwenda kwa utaratibu, na haraka sana. Nilipomkabidhi dada yangu wajibu wangu. niligundua kwamba sikuwa nimewahi kuhisi salama katika wajibu wangu. Hakukuwa na kufanya mapatano kwa ajili yangu mwenyewe, na wajibu huo haukuchafuliwa na nia zangu. Nilikubali wajibu huu kutokana na ufahamu wangu kuhusu neno la Mungu, na kwa sababu nilitaka kutenda ukweli. Nilihisi kwamba kutekeleza wajibu wangu kwa njia hiyo kulikuwa haki kabisa.

Wakati fulani baadaye, kina ndugu wengine waliniambia, “Unaonekana kuwa mnyenyekevu zaidi katika wajibu wako. Huudhiki upesi na kuwa na kiburi kama hapo zamani.” Niliposikia hayo, nilitambua fika kuwa haya yalikuwa matokeo yaliyofanikishwa ndani yangu na hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake. Ni Mungu aliyeniongoza, hatua kwa hatua, katika kuondokana na utumwa wa sifa, faida, na hadhi. Muda mfupi baadaye, msimamizi aliniarifu kuwa nitapewa wajibu wa mwelekezi. Siwezi kueleza jinsi nilivyosisimka niliposikia habari hiyo. Nilihisi kwamba sikuwa na kiburi sana na kuridhika kama nilivyofanya mwaka mmoja kabla nilipopewa wajibu huo, na niliweza kuelewa hilo lilikuwa agizo, jukumu nililopewa na Mungu, na niliweza kuelewa vyema nia njema za Mungu. Niligundua kwamba kupitia hayo yote hakukuwa ili kufanya maisha yangu yawe magumu au kuniangamiza. Kulikuwa ili kutakasa asili yangu potovu na nia zangu zilizochafuliwa. Kupitia kile ambacho neno la Mungu lilifunua na kile ambacho ukweli ulifunua, niliona kwa kweli jinsi ambavyo nilikuwa nimepotoshwa na Shetani, na kwamba bila kuhukumiwa, kuadibiwa, kushughulikiwa, na kufundishwa nidhamu na maneno ya Mungu, singeweza kamwe kuepukana na tabia hizi potovu au kuepukana kabisa na nguvu za giza na utumwa wa Shetani. Wakati huo tu ndipo nilipata kujua kwamba kuadibiwa, kuhukumiwa, kujaribiwa, na kusafishwa na Mungu kwa kweli ni ulinzi na wokovu mkuu wa Mungu kwangu.

Iliyotangulia: 18. Tuzo za Kutimiza Wajibu wa Mtu

Inayofuata: 22. Roho Yangu Yakombolewa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

8. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo

Petro alikamilishwa kwa sababu alimpenda Mungu kweli na kwa sababu alikuwa na hiari na uvumilivu wa kutafuta ukweli. Ingawa niko mbali na hilo, sitaishi kwa namna ya kuchukiza na isiyovutia tena ili kujihifadhi; niko tayari kufanya kumpenda Mungu kuwa lengo langu katika kutafuta na nitatumia juhudi zote na kulipa gharama katika kutimiza wajibu wangu. Kweli nitaubeba mzigo wa majukumu yangu na kutia ukweli katika vitendo wakati ninatimiza wajibu na kuingia katika uhalisi wa kumpenda Mungu.

9. Ukombozi wa Moyo

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki