Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Mungu atawaadhibu Watenda Dhambi

1 Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya wanadamu na kuchukia matendo yao maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha wanadamu ambao wanafikiria kama Mimi. Sijawahi kuwasahau wale ambao hawana fikira sawa na Zangu; Nimewachukia sana moyoni Mwangu. Hata hivyo, alimradi ni watu wanaoweza kunisaliti Mimi, haijalishi ni katika hali gani, kamwe Sitaweza kusahau na Nitawakumbuka moyoni Mwangu huku Nikisubiri fursa ya kulipiza matendo yao maovu. Mahitaji Niliyoyaleta yote ni masuala ambayo kwayo mnapaswa kujikagua wenyewe. Natumaini nyote mnaweza kuyazingatia kwa uzito na kwamba hamshughuliki na Mimi kiuzembe.

2 Hivi karibuni, Nitayachunguza majibu mliyonipa dhidi ya mahitaji Yangu. Kabla ya wakati huo, Sitahitaji kitu kingine zaidi kutoka kwenu na Sitawapatia onyo zaidi la dhati. Badala yake, Nitatekeleza mamlaka Yangu. Wale ambao wanapaswa kubakizwa watabakizwa, wale ambao wanapaswa kutuzwa watatuzwa, wale wanaopaswa kukabidhiwa kwa Shetani watakabidhiwa kwa Shetani, wale wanaopaswa kupokea adhabu kali watapokea adhabu kali, na wale ambao wanapaswa kuangamia watateketezwa. Kwa njia hiyo, kamwe hakutakuwepo na yeyote wa kunisumbua katika siku Zangu. Siku hiyo ifikapo, unaweza kufikiria ikiwa utakuwa ukiishi katikati ya shangwe na vicheko, au katika kulia na kusaga meno yako? Ni hatima ya aina gani unatarajia utakuwa nayo? Je, umewahi kutafakari kwa uzito ikiwa unaniamini asilimia mia moja au una mashaka nami asilimia mia moja? Ikiwa unatumaini kwamba Ning’oe nanga mapema ili Nitimize maneno Yangu, basi unapaswa kuchukuliaje maneno na matendo yako mwenyewe?

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Unajua Kudura Yako Itakuwa Ipi?

Inayofuata:Kila Siku Uishiyo Sasa ni Muhimu

Maudhui Yanayohusiana

 • Upendo wa Kweli wa Mungu

  I Nasimama mbele ya Mungu wangu tena leo. Moyo wangu una mengi ya kusema ninapoona uso Wake wa kupendeza. Nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura ny…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…

 • Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani

  Ⅰ Nimerejea katika familia ya Mungu, nikiwa mwenye msisimko na furaha. Nina bahati ya kukujua Wewe Mwenyezi Mungu, nimekupa moyo wangu. Ingawa nimepi…

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Ⅰ Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. Ⅱ…