Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Kupitia Utunzaji wa Uangalifu wa Mungu wa Wokovu wa Mwanadamu katika Maafa

Muling , Beijing

Agosti 16, Mwaka wa 2012

Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, Beijing ilipata mvua kubwa zaidi katika miaka sitini. Katika mvua hiyo kubwa niliona matendo ya Mungu na kuona jinsi Yeye huwaokoa mwanadamu.

Siku hiyo adhuhuri, dada zangu watatu na mimi tulikuwa tumekutana. Nje mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha. Saa kumi u nusu jioni mume wangu, ambaye hakuwa muumini, alirudi akitwambia kwamba kulikuwa na maji mengi kwa mzunguko kiasi kwamba watu hawakuweza kupitia. Hata hivyo, saa kumi na moja jioni aliondoka kwa haraka sana kwenda kwa zamu yake ya usiku kazini. Wakati huo sikuhisi kitu chochote kisicho cha kawaida, na nilienda kupika chakula cha jioni kama kawaida. Saa moja usiku, mpangaji wetu kwa ghafla alibisha mlango akiniita, na nilipotoka kuangalia, kile nilichoona kilinipa mshtuko mkubwa: Maji ya mvua yalikuwa tayari yamejaza ua na yalikuwa yakiingia kwa pembe za mashariki na magharibi za nyumba, wakati maji yaliyokuwa juu ya ardhi yaliendelea kuongezeka. Mwanangu wa kiume nami tulijaribu kuzuia mtiririko wa maji, lakini hatukufaulu. Katika kukata tamaa, nikapiga magoti ndani ya maji, nikimwita Mungu, “Ee Mungu, nakuomba unifungulie njia.” Wakati huo tu kampuni ya mume wangu ikapiga simu na kuuliza kama alikuwa nyumbani, na nilipokuwa nikichukua simu maji yalikuwa tayari yakija katika sehemu kuu ya nyumba. Nilitambua sasa jinsi mambo yalivyokuwa mazito, na nikaanza kuhangaika juu ya mume wangu bila kujua ni nini kilichokuwa kimemtokea. Nilipiga magoti tena ndani ya maji ili kumwita Mungu katika wasiwasi wangu, “Ewe Mungu! Ni katika kukakabiliana na mafuriko haya ya ghafla tu ambapo ninajihisia mwenyewe hasira Yako, na kutambua uasi wangu mwenyewe na usaliti. Ungependa tugeuze mioyo yetu kukuelekea Wewe, na kuishi kwa urahisi kwa kukutegemea Wewe, lakini bado ninaendelea kushikilia familia, mume wangu na mtoto wangu na siwaachilii. Ewe Mungu! Ni sasa tu ninapoelewa kuwa kati ya wanadamu hakuna mtu anayeweza kumletea yeyote chochote, na hakuna mtu anayeweza kumwokoa yeyote; ninaweza kukutegemea Wewe tu. Mume wangu amekuwa zaidi ya saa 4 njiani kwelekea kazini, lakini bado hajafika kwa kampuni, na sijui kinachoweza kuwa kilitokea njiani. Bila kusita namwaminia mikononi Mwako, na kila kitakachotendeka, bila kusita ninatii mpango Wako na utaratibu Wako!” Niliendelea kuomba jinsi hii tena na tena, na takriban saa tatu usiku mume wangu kwa ghafla akasimama mbele yangu kama ameloweka kabisa. Nilimshukuru Mungu bila kukoma katika moyo wangu kwa kumwokoa. Wakati huu maji ndani ya chumba yalikuwa tayari yamepanda hadi sehemu ya chini ya paja langu na nilimchukua mume wangu nikisema, “Omba pamoja nami, maisha yetu ni ya Mungu kutoa.” Mume wangu alikubali kwa kichwa, na tukapiga magoti katika maji pamoja katika sala. Tulipokuwa tukiomba, ghafla nikasikia mpangaji wetu akipaaza sauti, “Maji yanapungua! Yanapungua!” Katika moyo wangu nilifurahi; nje mvua ilikuwa ikishuka, hivyo maji yanawezaje kuwa yakipungua? Huu ulikuwa ni uweza wa Mungu! Ni kupendeza kwingi kulikoje, uaminifu mwingi ulioje alio nao Mungu; Anampenda mtu sana kabisa. Sisi ni duni sana na waasi, Mungu hutuhurumia sana, na husikiliza kilio chetu na kutuokoa kutoka kwa majanga. Mimi kweli sijui ni maneno gani ambayo yanaweza kuonyesha shukrani yangu na ibada ya Mungu.

Baada ya mvua hii nzito, mume wangu, mama mkwe wangu na wenzangu pia walimwamini Mungu, na nikamshukuru Mungu kwa wokovu wao. Kwa njia ya uzoefu huu nilielewa kweli kwamba Mungu hushusha maafa sio kuwaangamiza wanadamu lakini kuathiri wokovu wao. Kwa upande mmoja, Yeye hutupa tahadhari, watoto tulio vipofu na waasi ambao humwamini Yeye lakini bado tuko shingo upande na humdanganya na kumsaliti Yeye. Kwa upande mwingine, ni zaidi kuziokoa roho zote fukara ambazo kwanza zilikuwa Zake lakini bado zinaishi chini ya utawala wa Shetani. Njia hii ya wokovu ina utunzaji mwingi wa uangalifu wa Mungu. Kama maneno ya Mungu yanavyosema: “Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza ‘mbegu za maafa’ ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi” (“Tamko La Kumi” ya Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Siwezi kujizuia kutoa sifa zangu kwa Mungu tena: “Ee Mungu, upendo Wako ni wa kweli sana, kwa maana nimeona kwamba bila kujali Unachokifanya yote ni kwa sababu ya kutuokoa. Sasa ninafurahia uweza Wako na hekima na ninaona upendo Wako, wokovu Wako, na hata zaidi naona wazi nia Zako za shauku. Siwezi tena kuwa asiyejali na asiyekuwa na shukrani. Ninatamani tu kufanya liwezekanalo ili kueneza injili Yako ya ufalme, ili kurejesha roho zaidi zilizopotea kwa familia Yako, na kwa njia hii kwa hakika kuutoa moyo wangu Kwako ili nipate upendo Wako mkubwa kama malipo!”

Iliyotangulia:Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

Inayofuata:Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu

Maudhui Yanayohusiana

 • Ujana Usio na Majuto Yoyote

  Xiaowen, Jijini Chongqing “Upendo ni hisia safi, safi bila ya dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki ma…

 • Vigezo vya Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

  Kutoka leo, napenda kuchukua kirai “tafuta ukweli na kuwa na hisi ya haki” kama vigezo vya mwenendo wangu, kutafuta kuingia ndani zaidi katika ukweli, kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kujitahidi kuwa mtu mwema kwa dhati hivi karibuni ambaye yu dhahiri juu ya upendo na chuki na ambaye ana hisi ya haki.

 • Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

  Baada ya kusoma hili, nilihisi kama kwamba nilikuwa nikiamka kutoka ndotoni. Kwa hiyo, kuokolewa na Mungu hakukuwa rahisi kama nilivyokuwa nimefikiri hata hivyo; inategemea watu kupitia kazi na maneno ya Mungu kila hatua ya njia, kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, ushughulikiaji na upogoaji, pamoja na kupitia machungu ya kila aina ya maudhi na kero. Ili waweze kufikia ufahamu halisi wa tabia zao potovu na hatua kwa hatua kujiondolea upotovu, na hatimaye waweze kutegemea maneno ya Mungu na kutegemea ukweli kumshinda Shetani na kuvuka mipaka ya nguvu za giza katika kila aina ya mazingira. Kufikia matokeo haya tu ndio kuokolewa na Mungu kwa kweli.

 • Kiini cha Kutumia Mamlaka Vibaya Kwa Ajili ya Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

  Ee Mungu, asante kwa nuru Yako ya haraka, kwa kuzuia tabia yangu ya ubaguzi, kwa kuniruhusu kuona vyema zaidi uso wangu wa Shetani ukitenda kama adui Yako. Kuanzia siku hii kwendelea, ninapenda kufuata mabadiliko katika tabia, na wakati ninapokutana na watu au vitu ambavyo havinipendezi, nitajifunza kujiweka kando, kuunyima mwili, na katika vitu vyote kuyalinda maslahi ya kanisa, kufanya kila linalowezekana ili kutimiza majukumu yangu.