Umeme wa Mashariki Unatoka Wapi?
Kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu tunaona kuwa kazi ya Mungu na neno la siku za mwisho ni umeme ambao huangaza kutoka Mashariki. “Umeme” ni mwanga mkubwa, kumaanisha neno la Mungu, njia ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho. Kifungu “unavyotokea mashariki” kinamaanisha hutoka China, na “kumulika pia magharibi” kikimaanisha kuwasili katika nchi za Magharibi. Mwisho, “ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” kinahusu Mungu kupata mwili na kwanza akijifichua Mwenyewe na kuanza kazi Yake nchini China katika Mashariki. Huko Analifanya kundi la watu ambao kwa kweli wanamjua Mungu, na wao ni washindi kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Kisha kupitia watu hawa, injili ya siku za mwisho itaenea Magharibi, ili kila mmoja atapokea wokovu wa Mungu wa siku ya mwisho. Hili limefanikishwa sasa na ni ukweli ambao unaweza kuonekana na kila mtu!