Nimepata Furaha ya Kweli

24/12/2019

Na Zhang Hua, Kambodia

Nilizaliwa katika familia ya kawaida ya ukulima. Ingawa familia yangu haikuwa tajiri, baba na mama yangu walipendana na kunitendea vyema sana. Maisha ya familia yetu yalikuwa tele na kubarikiwa kabisa. Baada ya kukua, nilijiambia: Ni lazima nipate mume ambaye atanitendea vyema na ni lazima nianzishe familia ya furaha na iliyoridhika. Hii ndiyo muhimu zaidi. Sitafuti utajiri, nahitaji tu kuwa na uhusiano wa upendo na mume wangu na maisha ya amani ya familia.

Nilikutana na mume wangu kupitia kwa mtu tuliyemfahamu sote wawili. Sikumpenda kwa sababu alikuwa mfupi kiasi, lakini baba na mama yangu walimpenda. Waliniambia: “Ana moyo mzuri, na atakutendea vyema.” Niliona kwamba mume wangu aliwatendea watu kwa uaminifu sana na alionekana kuwa mtu ambaye angetendea familia yake vyema. Nilifikiri, “Ni sawa kuwa yeye ni mfupi kiasi. Ilimradi anitendee vyema, ni sawa.” Matokeo yake ni kwamba, nilikubali ndoa na mwaka wa 1989, tulioana. Baada ya kuoana, mume wangu alinitendea kwa wema sana na alinitunza vizuri sana. Maisha yangu ya ndoa yalikuwa ya furaha sana na tele. Bwanangu alinitendea vyema, na nilikumbuka hilo moyoni mwangu. Pia nilimtunza kwa makini na kufikiri kumhusu katika kila masuala. Baada ya mabinti zetu wawili kuzaliwa, ili kuruhusu bwanangu kuwa na amani kazini, nilibaki nyumbani na kutunza familia. Wakati huo, binti yangu mdogo alipata ugonjwa mara nyingi. Wakati mmoja, usiku, ghafla alipata homa. Bwanangu alikuwa akifanya kazi zamu ya usiku na hakuwa nyumbani. Katika hofu kubwa, niliamua kumleta binti yangu hospitalini mimi mwenyewe. Wakati mume wangu alipata habari kuhusu hili, alitaka kurudi nyumbani. Hakutaka niteseke sana. Nilikuwa mwenye furaha sana kwamba mume wangu alikuwa na moyo wa aina hii. Baadaye, watoto hao wawili walienda shuleni nje ya kijiji. Nilikodi pahali ili kuandamana nao walipokuwa wakisoma na kuwatunza. Ili mradi ningeweza kushughulikia suala fulani, singemsumbua mume wangu kulihusu. Ingawa wakati mwingine, ilikuwa vigumu na nilikuwa nimechoka kiasi, uhusiano wetu kama mume na mke ulijawa na upendo na msaada wa pande mbili. Nilihisi kwamba maisha yangu yalikuwa yamebarikiwa kweli.

Wakati huo, pesa ambayo bwanangu alipata ilikuwa ya kutosha tu kukimu gharama yetu ya kila siku. Ingawa maisha yetu yalikuwa magumu kiasi, sikuwahi kulalamika kwake. Nilihisi kwamba mume na mke wanapaswa kushiriki katika furaha na huzuni za maisha. Baadaye, hali ya kiuchumi katika mahali pa kazi pa bwanangu iliharibika na aliona vigumu kupeleka nyumbani nusu ya malipo yake yaliyotangulia kila mwezi. Punde, hatungeweza kulipa karo za shule za watoto wetu. Katika juhudi ya kupunguza shinikizo ya bwanangu, niliomba pesa kutoka kwa jamaa zetu mara nyingi. Nilifikiri, “Taabu hizi ni za muda mfupi pekee. Mambo yatakuwa bora hatimaye.” Kwa sababu tuliomba pesa kwa muda mrefu sana, deni zetu zikawa kubwa zaidi na zaidi. Mume wangu nami sote tulihisi kwamba shinikizo ilikuwa kubwa sana. Katika mwaka wa 2013, bwanangu alianza kufikiri kuhusu kuenda ng’ambo kupata pesa. Niliposikia hili, ingawa sikutaka, nilifikiri, “Akienda ng’ambo kwa miaka mbili ama tatu kupata pesa kiasi, tunaweza kulipa deni fulani zetu na kuendeleza hali ya familia yetu.” Hata zaidi, watoto wetu wanakua na tunataka kuwapa mazingira mazuri. Kwa ajili ya familia yetu, ninakubali aende ng’ambo kufanya kazi.

Bwanangu alienda Kambodia kwa miaka tatu. Katika miaka hii tatu, nilibaki nyumbani na kutunza watoto na wazazi wetu wazee. Mwanzoni, bwanangu angepiga simu nyumbani mara nyingi na kuonyesha kwamba alijali familia. Pia angetuma pesa nyumbani. Badaye, alipungua tena na tena kupiga simu na angetuma pesa kidogo sana nyumbani. Mwishowe, ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba hakutuma nyumbani pesa yoyote na ilichukua muda mrefu sana kabla yeye kupiga simu nyumbani. Nilikuwa na wasiwasi kuwa kitu kilikuwa kimemfanyikia. Matokeo yake ni kwamba, nilileta mabinti zetu nami kumwona. Tulipofika Kambodia na niliona kuwa mume wangu alikuwa salama salimini, nilifarijika sana. Kwa kuwa hii ilikuwa mara yetu ya kwanza Kambodia, nilikuwa tayari kukaa hapo na mabinti zetu kwa kipindi cha muda na kuandamana na mume wangu kabla ya kuenda nyumbani. Hata hivyo, niligundua kwamba kila wakati niliandamana na mume wangu nje ya nyumba, watu ambao walimjua mume wangu wangeniangalia na sura ya ajabu. Kwa sababu hatukuzungumza lugha sawa, sikujua walikuwa wakisema nini. Baada ya wiki moja, mume wangu ghafla alileta mtoto mgeni mikononi mwake mbele yangu. Alimwambia mtoto huyo, “Haraka msalimie shangazi yako.” Wakati huo, nilikodoa macho tu bila kuonyesha hisia kwa sababu sikujua kilichokuwa kikiendelea. Nilipomwuliza mume wangu, niligundua kwamba huyu alikuwa mtoto ambaye alimpata na mwanamke aliyekutana naye Kambodia. Nilikuwa na hasira mbaya sana na sikujua nifanye nini. Nilipomshutumu, alijibu kwa baridi, “Hili ni kawaida sana. Watu wengi hapa hufanya hili!” Nilipomsikia akisema hili, nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba mwili wangu mzima ulitetemeka. Singewahi kufikiri kwamba mume wangu nami tulikuwa tumependana kwa miaka mingi sana, ilhali sasa angeweza kusema kitu baridi na katili na kufanya jambo lisilo na haya hivyo. Nikiwa na hasira, nilimzaba kofi kwa ukali mara mbili. Nilifadhaishwa na usaliti wa bwanangu. Ukweli wa usaliti wake ulikuwa kama radi kutoka kwa anga angavu kwangu. Hakuwahi kuonyesha ishara yoyote ya awali kwamba angetenda hivi. Singekubali hili kumhusu. Nilikaa chini sakafuni na kulia kwa uchungu. Nilijiuliza tena na tena, “Mbona bwanangu anifanyie hili? Bwana ambaye nilikuwa namjua alienda wapi?” Inaweza kuwa kwamba ahadi yake ya upendo usioisha, wema wake na utunzaji wake yote yalikuwa bandia? Nilitoa kila kitu kwa familia hii. Sikuwahi kumwuliza bwanangu anipe pesa ama raha za mwili. Hata hivyo, sasa … Usaliti wa bwanangu ulikuwa fedheha kubwa kwangu. Nilihisi kwamba sikuwa na heshima yoyote ya kuendelea kuishi.

Siku zilizofuata, nililia sana kila siku. Nilidharau mwanamke huyo na kumdharau mtoto huyo. Nilimwambia bwanangu kwamba nilitaka kutangua ndoa na nilikuwa tayari kuwapeleka mabinti zangu nyumbani na kuacha hii inayodaiwa kuwa familia. Sikufikiri kwamba mume wangu hangekataa tu kunipa talaka lakini pia hakutaka kumwacha huyo mwanamke. Kisha, niligundua kwamba baadhi ya jamaa zangu tayari walijua kwamba mume wangu alikuwa amepata mwanamke mwingine na alikuwa na mtoto naye. Waliniweka gizani tu kuhusu hilo. Nilihisi hata zaidi kwamba sikuwa nikiishi na heshima yoyote. Nilitoa kwa kujitahidi kwa ajili ya familia hii. Singewahi kufikiri kwamba ningelipizwa na usaliti na udanganyifu. Moyo wangu ulikuwa umevunjika … Usaliti huu tayari ulikuwa mchungu sana. Kilichofanya iwe hata vigumu zaidi kwangu kukubali kilikuwa kwamba watu waliomjua bwanangu na mwanamke huyo wangeniangalia kwa ajabu na pia wangenihakiki. Awali, ilikuwa bwanangu ambaye alikuwa amenisaliti na ilikuwa mwanamke huyo ambaye alivunja familia yangu. Hata hivyo, sasa, machoni pa watu wengine, mimi nilikuwa mdukizi. Siwezi kuelezea uchungu huo niliokuwa nikihisi wakati huo. Wakati unajikokota mtu anapohisi mwenye huzuni. Niliishia kupoteza zaidi ya kilo 10 ya uzito.

Wakati huo nilipokuwa nimevunjika moyo kabisa, nilikutana na wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Wakati jirani yangu Lin Ting alipata habari ya tukio hili, alikuja kwangu na kuhubiri injili kwangu. Alisema, “Mwamini Mungu. Mungu anaweza kukusaidia.” Hata hivyo, kwa sababu ya kushawishiwa na ukana Mungu, ningemwamini vipi Mungu tu! Sikumpa jibu lolote. Baadaye. Lin Ting aliniongelesha mara nyingine tena, “Soma maneno ya Mungu. Mungu anaweza kukuokoa na kukusaidia kujinasua kutoka kwa uchungu wako.” Alisema mambo kwa uaminifu sana kiasi kwamba nilihisi kuguswa kihisia. Nilihisi aibu kumkata tena na kama matokeo, nilipata nakala ya kitabu Neno Laonekana katika Mwili. Nilifungua kitabu hicho na kusoma fungu lifuatalo: “Wanadamu, baada ya kuuwacha utoaji wa uzima kutoka kwa Mwenye uweza, hawajui azma ya kuishi, lakini hata hivyo wanaogopa kifo. Hawana usaidizi wala msaada, lakini bado wanasita kufumba macho yao, na wanajitayarisha kuendeleza uwepo wa aibu ulimwenguni humu, magunia ya miili wasio na hisia za roho zao wenyewe. Unaishi hivi, bila matumaini, kama vile wafanyavyo wengine, bila lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa watu ambao, wakiwa wanapiga kite katika mateso yao, wanatamani sana kufika Kwake. … Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Niliposoma maneno ya dhati ya Mungu, nilijawa na machozi na kuhisi kwamba Mungu huyu kweli anaelewa wanadamu. Nilipokabili usaliti wa bwanangu, nilitaka kufa lakini sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo wala sikuwa tayari kukubali kufa kwa njia hiyo. Nilipoteza mwelekeo wa maisha yangu na lengo na hata nilitaka kusalimu amri mwenyewe. Niliposoma maneno ya Mungu, ningeweza kuona matumaini ya maisha na moyo wangu ulipata amani. Hata ingawa bwanangu alikuwa amenisaliti, ningemtegemea Mungu. Sikuwa pekee yangu. Mwenyezi Mungu alisema, “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote.” Nilikuwa tayari kumtegemea Mungu kwa sababu nilikuwa mtu ambaye alikuwa amesononeka na sikuwa na mtu aliyenijali. Nilihitaji kumbatio la Mungu. Nilihisi kwamba kila siku ilikuwa ya kuumiza na ya kuchosha sana. Sikutaka kuendelea hivi. Kwa kuwa Mungu anawaelewa wanadamu vyema sana, bila shaka Angeniongoza mbali kutoka kwa uchungu huu. Matokeo yake ni kwamba, nilianza kusoma maneno ya Mungu pamoja na Lin Ting. Tuliwasiliana nia za Mungu na kujifunza kuimba nyimbo za ibada kwa Mungu. Lin Ting aliniambia, “Unapopitia nyakati ngumu, mwombe Mungu na kusoma maneno ya Mungu. Mungu anaweza kufariji moyo wetu ulioumizwa.” Nilifanya alichoniambia nifanye. Nilipoona video za muziki na video za nyimbo ambazo ndugu wa kanisa la Mwenyezi Mungu walipiga filamu, nilianza kuhisi mwenye furaha zaidi moyoni mwangu. Nilihisi kwamba ni familia ya Mungu pekee ilikuwa na upendo wa kweli na kwamba furaha ya kweli ingeweza kupatikana tu na ndugu zangu. Hii hasa ilikuwa hali nilipoona video, “Furaha Katika Nchi ya Kanaani.” Moyo wangu uliruka pamoja na ndugu waliokuwa wakiimba na kucheza. Mateso yangu na moyo wenye huzuni ulichangamka mara moja na tabasamu hatimaye ikaanza kuonekana usoni mwangu. Mara moja, nilihisi kwamba hii ilikuwa familia ambayo kwa kweli nilitaka. Matokeo yake ni kwamba, nilifurahia maisha ya kanisa pamoja na ndugu zangu.

Baadaye, nilisoma maneno fulani zaidi ya Mungu: “Shetani kutumia kwa manufaa yake mitindo ya kijamii kumpotosha mwanadamu. Hii mitindo ya kijamii ina mambo mengi. Watu wengine husema: ‘Je, inamaanisha mitindo ya karibuni, vipodozi, kutengeneza nywele na chakula cha kidomo?’ Je, ni kuhusu mambo haya? Hii ni sehemu ya mitindo, lakini hatutaki kuzungumzia haya hapa. Tunataka tu kuzungumza kuhusu mawazo ambayo mitindo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inasababisha watu kutenda duniani, malengo ya maisha na mtazamo ambao inaleta kwa watu. Hii ni muhimu sana; inaweza kudhibiti na kushawishi hali ya akili ya mwanadamu. Moja baada ya nyingine, hii mitindo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, kumfanya kuendelea kupoteza dhamiri, ubinadamu na mantiki, na unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote. … Wakati upepo wa mwenendo unavuma, pengine ni idadi ndogo ya watu tu watakuwa waanzisha mitindo. Wanaanza kwa kufanya jambo la aina hii, kukubali wazo la aina hii ama mtazamo wa aina hii. Wengi wa watu, hata hivyo, katikati ya kutojua kwao, bado watazidi kuambukizwa, kufanywa wenyeji na kuvutia na aina hii ya mwenendo, hadi wote bila kujua na bila kujitolea wanamkubali, na wote wanazama na kudhibitiwa na yeye. Moja baada ya nyingine, mitindo ya aina hii inawafanya watu ambao si wa mwili na akili timamu, wasiojua ukweli, na hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi, mitindoinawafanya kukubali mitindokwa furaha vilevile mtazamo wa maisha, na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani kuhusu jinsi ya kukaribia maisha na jinsi ya kuishi ambayo Shetani ‘amewapa.’ Na hawana nguvu, wala uwezo, wala ufahamu wa kupinga” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili). Niliposoma sehemu hii ya maneno ya Mungu, nilifikiri kuhusu kile bwanangu alikuwa ameniambia: “Hili ni kawaida sana. Watu wengi wanalifanya hapa!” Je, si fikira za bwanangu zinaonyeshwa katika ukweli ambao unafichuliwa na maneno ya Mungu ya jinsi mitindo miovu ya jamii iliyopambanishwa na Shetani inapotosha na kusimilisha watu? Kabla ya bwanangu kutoka nchini, angetunza jamii yake na kunitunza mimi na watoto wetu. Hata hivyo, katika miaka mitatu mifupi tangu aondoke nyumbani kufanya kazi, alifuata kabisa mitindo miovu ya jamii na kusaliti familia yake mwenyewe. Kisha nilifikiri: Katika jamii ya sasa, kuwa hawara si jambo la aibu. Kwa kweli, ni kitu ambacho kinafanyika mara nyingi kabisa. Wanadamu wengi wamedhuriliwa na fikira ya sumu ambayo ni kama ifuatayo: “Bendera nyekundu nyumbani haianguki, bendera za rangi nyingi nje zinarukaruka katika upepo mwanana.” Bila aibu wana mapenzi nje ya ndoa. Kwa kuwa hawakatishwi tamaa na aibu, wanatiwa motisha na fahari. Bwanangu hataki kunipa talaka, ilhali pia hataki kumwacha mwanamke huyo. Je, hajadhibitiwa na fikira na maono ya ina hii? Kupitia kusoma maneno ya Mungu, niliweza kuelewa hili: Kwa kweli, kila mtu ni mwathiriwa. Kila mtu amedanganywa na fikira ovu za Shetani. Hii ndiyo maana tumepotoshwa hadi kiwango ambapo hatuna maadili na aibu. Je, watu wamepata nini wakitimiza tamaa zao za binafsi pekee? Kwa kweli wamepata furaha? Kuhusu mume wangu na mwanamke huyo, sidhani kwamba wana furaha zaidi kuniliko. Aidha, watoto wetu ni waathiriwa wasio na hatia. Je, si taabu ambayo familia yangu imekabiliana nayo ni matokeo ya upotovu na madhara ya Shetani? Ninapofikiri kujihusu, kama singekutana na wokovu wa Mungu, pia ningeharibiwa na mitindo miovu ya jamii. Nilidhani kwamba kwa kuwa mume wangu alipata mwanamke mwingine pia mimi vivyo ningetafuta wanaume wengine. Mimi si mwanamke asiyetakiwa hata kidogo. Nashukuru kwamba Mungu aliniokoa wakati ambapo nilikuwa karibu kumezwa na Shetani. Aliniruhusu kuja mbele Yake na kupokea ulinzi Wake. Vinginevyo, ningeangamizwa na mwelekeo muovu wa jamii hii.

Baadaye, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu kina uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa maneno ya Mungu, nilihisi upendo Wake kwa wanadamu na Yeye kuwajali, na pia nilikuja kuelewa kwamba, ingawa Shetani anaweza kutumia kila aina za mitindo ya kijamii kutupotosha na kutudhuru, Mungu hajawahi kuacha kujaribu kutuokoa. Badala yake, Mungu kila mara na kwa kimya anatulinda, akitayarisha kila aina za hali tofauti ili tuweze kurudi mbele Zake na kukubali wokovu Wake. Nikikumbuka wakati ambapo nililazimika kukabili usaliti wa mume wangu, nilijua kwamba nilikuwa nikiishi katika hali ya chuki na uchungu wakati huo. Isingekuwa utunzaji na rehema ya Mungu ambaye alitumia maneno Yake kunifariji na kunitia moyo ili niweze kubaini hila na njama za udanganyifu ambazo Shetani hutumia kuwapotosha watu, na kuona vyema madhara maovu ambayo mitindo miovu ya Shetani hutusababishia, basi ningebaki milele nikiishi katika hali ya chuki na uchungu bila kuwahi kuweza kujinasua kutoka kwa hali hiyo. Hata ningejisababishia maangamizi ili tu kusuluhisha chuki yangu ya ndani. Kwa sababu ya kupitia tukio hili, sikuwa tu nimepitia upendo wa Mungu, lakini pia kweli nilikuja kuhisi kwamba ni Mungu pekee anayeweza kuwaokoa wanadamu dhidi ya kupotoshwa na kudhuriwa na Shetani, na ni Mungu pekee anayeweza kutuongoza kwenye njia ya nuru katika maisha. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniokoa kutoka kwa uchungu huo mkuu!

Siku hizi, nikiendelea kusoma maneno zaidi ya Mungu, naelewa ukweli kiasi na ninaweza kubaini hali nyingi. Simchukii tena bwanangu ama mwanamke huyo. Wako huru kuchagua aina ya maisha wanayotaka kuishi. Kuhusu jamaa na marafiki, ninaweza kuwashughulikia kwa utulivu. Siwalaumu tena jamaa zangu kwa sababu sote tumepotoshwa na Shetani na sote ni waathiriwa wake. Sasa, nahudhuria mikutano mara nyingi na ndugu zangu. Tunasoma maneno ya Mungu na tunawasiliana na kushiriki uzoefu wetu binafsi. Tunafaidika kila siku kutoka kwa maneno ya Mungu. Ndani ya mioyo yetu, tuna amani na furaha na maisha yetu yamejaa matumaini. Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza katika njia sahihi ya maisha na kwa kunipa familia ya kweli. Hapa, nimepata furaha ya kweli! Niko tayari kumfuata Mungu milele!

Iliyotangulia: Nimepata Makazi ya Kweli
Inayofuata: Mungu Yuko Kando Yangu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Niliupata Mwanga wa Kweli

Kuanzia hapo kuendelea, sikucheza tena michezo ya video wala kupoteza wakati kwa kwenda kwa KTV. Nilipokuwa na wakati, ningesoma maneno ya Mungu au ningekusanyika na ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa ushirika ambapo tungeimba na kumsifu Mungu. Kila siku ilikuwa na wingi wa mambo. Sikujisikia tena mtupu na nisiyejiweza. Aidha, nilikuwa dhahiri kuhusu malengo yangu ya maisha. Nilijua kwamba maana ilikuwa ipatikane kupitia kwa mtu kutimiza wajibu wake mwenyewe mbele ya Mungu na kuishi kwa ajili ya Mungu kama moja wa uumbaji wake.

Bahati na Bahati Mbaya

Baada ya kupitia maumivu na mateso ya tukio hili la ugonjwa, nilitafakari juu ya jinsi nilivyokuwa chini ya udhibiti wa mtazamo wa maisha ya Shetani usio sahihi wa “kujitahidi kuwa bora zaidi kuliko kila mtu mwingine.” Muda huu wote, nilijitahidi kujitokeza miongoni wa wenzangu na kuishi maisha yenye wingi ili wengine wangenipenda na kunitamani. Hata hivyo, sijawahi kufikiri nini nitapata badala yake yalikuwa maumivu na huzuni. Sikupata hata amani na furaha kidogo.

Mungu Yuko Kando Yangu

Na Guozi, Marekani Nilizaliwa katika familia ya Kikristo, na nilipokuwa na umri wa mwaka mmoja, mama yangu alikubali kazi mpya ya Bwana...