Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maarifa Yanayohitajika ya Kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema

13

Iwapo tunaweza kuyatafakari kwa dhati maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo hufichua umuhimu na asili ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema, tutaweza kutambua kikamilifu kuwa kazi ya Bwana Yesu Kristo katika Enzi ya Neema ilikuwa kazi ya ukombozi, na ilikuwa kazi ya upatanisho na Mungu wa mwanadamu mpotovu. Maneno na kazi ya Bwana Yesu Kristo katika Enzi ya Neema yote yalihusisha kazi ya ukombozi, na yote ilikuwa kuwafanya watu kumkubali Yesu kama Mwokozi wao, kuja mbele ya Mungu kuzikubali dhambi zao zote, kupata msamaha wa Mungu, na kuweza kuitegemea neema ya Mungu ili kuishi mbele Yake. Ilikuwa yote kuwafanya watu kuweza kufurahia neema na baraka zote walizopewa na Mungu baada ya kumgeukia, kutambua kuwa Yeye ni Mungu wa huruma na upendo, kumuomba mara kwa mara, kumwabudu ili kuishi katika neema na baraka walizopewa na Yeye. Ilikuwa yote kuwafanya watu kueneza injili na kuwa na ushuhuda wa wokovu wa Mungu baada ya kutambua kuwa Bwana Yesu Kristo ndiye Mwokozi, na waweze kuichukua ahadi ya Yesu na wajue jinsi ya kujitayarisha kupata wokovu wa siku za mwisho. Hiyo inatosha kuwafanya watu kuona kuwa yale ambayo Bwana Yesu Kristo Aliyafanya katika Enzi ya Neema yote yalikuwa kazi ya kumkomboa mwanadamu. Bwana Yesu Kristo kusulubiwa msalabani na kuwa sadaka ya dhambi kunahusishwa kwa karibu na kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Katika Enzi ya Sheria, Waisraeli walijua uongozi wa Mungu na walijua jinsi ya kufuata sheria na amri Zake, lakini kwa sababu ya upotovu wa ubinadamu, bado kila wakati walikuwa wakikiuka sheria na kanuni, wakitenda dhambi dhidi ya na kumkosea Mungu. Hii iliwafanya watu kutambua dhambi ni nini, na kutenda dhambi ni nini, kujua ni dhambi gani ambazo watu hutenda na jinsi ya kufanya dhabihu ili kupata msamaha wa Mungu baada ya kutenda dhambi. Kutoka kwa hii, tunaweza kuona kuwa matokeo ya kwanza yaliyopatikana kutoka kwa sheria na amri za Mungu yalikuwa kuwafanya watu wajue dhambi ni nini, na jinsi wanavyopaswa kufanya dhabihu baada ya kutenda dhambi ili waweze kusamehewa na Mungu. Hii ndio maana Bwana Yesu Kristo Alikuja katika Enzi ya Neema kukamilisha kazi ya upatanisho wa Mungu kwa mwanadamu. Hii hakika ni ya maana sana. Katika Enzi ya Sheria, kutoa dhabihu, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani zilikuwa zinatatua dhambi moja tu, na kutoa msamaha mmoja, lakini katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu Kristo Alikuwa wa milele, sadaka kamili ya dhambi, na wakati mmoja Alizisamehe dhambi za mwanadamu milele. Hii iliwaruhusu watu kuona jinsi upendo wa Mungu kwa mwanadamu ulivyo mkuu, na kuwa tabia Yake haijumuishi tu haki, ukuu, na ghadhabu, lakini pia hujumuisha huruma na upendo, na hasa kuwa neema ambaye huwa Anapeana kwa mwanadamu ni kubwa sana na nyingi. Mara dhambi za watu zinaposamehewa, wanaweza kufurahia neema Yake yote kama awali. Inaweza kuonekana kuwa upendo Wake kwa mwanadamu ni wa kweli na neema Yake kwa kweli ni kuu na isiyo na kipimo. Bwana Yesu Kristo Hakuwa tu sadaka ya dhambi kwa binadamu mpotovu na kwa kitendo hicho kimoja Alizisamehe dhambi za mwanadamu milele, lakini pia Aliwafundisha watu ukweli mwingi wa Enzi ya Neema kuwafanya kupendana, kuvumiliana, kuwasamehe wengine mara sabini mara saba, na pia kuwasamehe wengine milele na kuwaombea maadui wao. Hakukosa tu kuondoa sheria na amri, lakini Alifanya kazi ya Enzi ya Sheria kuwa kamilifu, ili wale wote ambao walikubali kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu Kristo wangeweza kukusanyika inavyofaa na kumuomba Mungu, kumwabudu Mungu, kueneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu—hii ni kuwa na ushuhuda. Ni bayana kuwa kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema yote ilijengwa kwa msingi wa kazi Yake katika Enzi ya Sheria. Bwana Yesu Kristo kwa kweli alifanyika kuwa sadaka ya dhambi na kutimiza kazi ya kumkomboa mwanadamu, na katika hatua moja akazisamehe milele dhambi zote za mwanadamu mpotovu za kumpinga Mungu, akiwafanya kustahili kuja mbele ya Mungu, kumuomba, na kumwabudu. Hata hivyo, Bwana Yesu Kristo kuwa sadaka ya dhambi sio sawa na kumuokoa mwanadamu kikamilifu na kukamilisha mpango wa Mungu wa usimamizi. Kuna watu wengi katika dini ya Kikristo ambao huamini kuwa Bwana Yesu Kristo kusema “Imekwisha” msalabani ilimaanisha kuwa alikuwa tayari ameikamilisha kazi ya Mungu ya kumuokoa mwanadamu. Hii sio sahihi—hili tu ni wazo na fikira za mwanadamu ambazo huonyesha kuwa watu hawana ufahamu hata wa kiwango kidogo wa kazi ya Mungu. Iwapo kazi ya Yesu ya ukombozi ilikuwa tayari imemuokoa mwanadamu kikamilifu, basi watu wa kidini leo hawangekuwa wanaomba na kuziungama dhambi zao kila siku, na madhehebu makuu hayangekuwa yenye huzuni na kuwa na ukiwa kama ilivyo sasa. Bwana Yesu Kristo pia kwa hakika Hangesema “Nakuja kwa haraka.” Ni kurudi tu kwake Bwana Yesu Kristo, kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho iliyo kazi kamili ya kumuokoa mwanadamu. Kupitia hukumu na kuadibu, upogoaji na ushughulikiaji, na majaribio na usafishaji, Mwenyezi Mungu anatatua suala la upotovu wa wanadamu ili waweze kuacha kikamilifu vifungo na vizuizi vya ushawishi wa Shetani, na kuwa watu ambao humtii na kumwabudu Mungu kwa kuwa hakika wanamjua. Ukweli unatosha kuonyesha kuwa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu Kristo ilikuwa tu inatengeneza njia kwa Mungu kumuokoa mwanadamu kikamilifu katika siku za mwisho, na ni kwa kukubali tu kazi Yake katika siku za mwisho ambapo watu wanaweza kupata wokovu kamili. Huu ni ukweli kamili usioweza kupingwa.

Kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu Kristo ilipanua mawanda ya kazi ya Mungu kwa haraka nchini Israeli, na kuieneza kikamilifu kwa ulimwengu wa Mataifa yasiyo ya Wayahudi na hadi mwisho wa dunia. Hivi ndivyo kazi ya Mungu ilipanuka kutoka Israeli hadi kwa ulimwengu wote katika Enzi ya Neema, na watu wengi katika kila nchi na kila eneo walikuja mbele ya Mungu, kumuomba, na kumwabudu. Jina Lake limeenea kwa kila nchi na kila eneo. Ni wazi kutoka kwa hili kuwa mpango wa Mungu wa usimamizi wa kumuokoa mwanadamu nusu yake tayari ilikuwa imekamilika huku pia ukitengeneza njia kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho.

Iwapo umuhimu halisi wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema utajumuishwa katika sentensi moja, itakuwa kuwa Mungu mwenye mwili Alijifanya Mwenyewe kuwa sadaka ya dhambi kwa ubinadamu uliopotoka ili kumkomboa mwanadamu. Umuhimu halisi wa kazi ya Enzi ya Neema unaojitokeza zaidi ni ule wa “ukombozi.”

kutoka katika “Ni Hatua Tatu Tu za Kazi ya Mungu ambazo Ni Kazi Yake Kamili ya Kumuokoa Mwanadamu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha

Maudhui Yanayohusiana