Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maarifa Yanayohitajika ya Kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme

8

Maarifa Yanayohitajika ya Kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme

Baada ya kuyasoma maneno kuhusu umuhimu wa Kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, iwapo unaweza kuyatafakari kwa moyo, hakika utaweza kupata maarifa na ufahamu fulani kwa kazi Yake katika siku za mwisho. Iwapo basi unaweza kusoma kitabu, Neno Laonekana katika Mwili, ambacho kimeonyeshwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu wakati wa kazi Yake katika siku za mwisho na upitie miaka kadhaa ya kazi Yake katika siku za mwisho, hakika zaidi utaweza kwa kweli kuelewa kuwa kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme ni hukumu na kuadibu ili kumkomboa mwanadamu kikamilifu. Kupitia hii, unaweza kupata wokovu na kufanywa kuwa mkamilifu.

Ili kuelewa kazi ya Mungu katika siku za Mwisho, kwanza ni lazima uwe wazi kuhusu ni kwa nini Anafanya kazi ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho. Baada ya Bwana Yesu Kristo kukamilisha kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, watu wote wa Mungu waliochaguliwa wangeweza kuja mbele ya Bwana Yesu Kristo, kuungama dhambi zao na kutubu, na kusamehewa. Pia wangeweza kufurahia neema nyingi waliyopewa na Mungu, lakini hakukuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaweza kuondoa vikwazo na pingu za asili yao ya dhambi baada ya ubinadamu kupotoshwa na Shetani. Kila mmoja aliendelea kutenda dhambi hata baada ya kumkubali Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wake na kusamehewa dhambi zake. Waliishi katika mzunguko unaojirudia wa kutenda dhambi na kukubali dhambi zao. Hiyo ndiyo maana, hata ingawa wale wote walikuwa wamekombolewa na Bwana Yesu Kristo walikuwa wamesamehewa dhambi zao na walifurahia neema yote waliyokuwa wamepewa na Mungu, walikuwa wameshindwa kabisa kuondoa vizuizi na pingu za asili ya kishetani ambazo humwelekeza mwanadamu kwa dhambi. Ndio maana watu wote hupaza sauti kwa uchungu: “Kwa kweli nina huzuni! Ninaweza kufanya nini ili hatimaye niondoe vizuizi vya asili yangu ya kishetani na kupata wokovu wa kweli?” Ni wazi kuwa mwanadamu mpotovu hana njia yoyote ya kutatua asili yake mwenyewe ya dhambi, hakuna anayeweza kujiweka huru kutoka kwa udhibiti wa asili yake mwenyewe ya kishetani. Wote hawawezi kujizuia ila kuendelea kutenda dhambi na kuishi katika dhambi, hii ndio maana ingawa dhambi za ubinadamu uliopotoka zimesamehewa, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kawaida ya ubinadamu, hivyo ni vipi ambavyo wangeweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli ya binadamu? Huu ndio uzoefu halisi wa watu wote wa Mungu waliochaguliwa ambao waliikubali kazi ya Mungu ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Hivyo kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu mwenye mwili hufanya Yeye binafsi katika siku za mwisho ni kazi ya kuuokoa kikamilifu ubinadamu uliopotoka kutoka kwa asili yake ya dhambi ya kishetani na kuibadilisha tabia yao ya maisha. Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli wote wa hukumu na kuadibu ili kumuokoa mwanadamu kikamilifu. Huwa Hatumii ukweli tu katika maneno Yake kuweka wazi na kuhukumu nafsi ya asili potovu ya kishetani ya ubinadamu na ukweli wa upotovu wao, lakini pia Hutumia njia za kupogoa ushughulikiaji na majaribio na usafishaji kutatua na kubadilisha tabia za watu za kishetani. Hii huuruhusu ubinadamu potovu kutambua kwa kweli asili yao wenyewe ya kishetani na ukweli wa upotovu wao, na kuona kwa hakika kuwa ubinadamu potovu umejaa tabia za kishetani kama vile ubinafsi na kustahili dharau, udanganyifu na uhalifu, ulafi na uovu, na kuchoka na ukweli. Kwa kupogolewa na kushughulikiwa, na kupitia majaribio na usafishaji, watu wanaweza kuelewa ukweli na kuijua kazi ya Mungu, jambo ambalo hufanya mitazamo yao ya masuala, mitazamo yao ya maisha, na maadili kupitia mabadiliko ya kimsingi, na hii itafuatwa na mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Haya yote ni matunda yaliyozaliwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, na mabadiliko yanayoletwa na haya ni makubwa kwa kiwango kikubwa kuliko yale yaliyoletwa na kusamehewa kwa dhambi baada ya kumwamini Bwana Yesu Kristo katika Enzi ya Neema. Yanatosha kuthibitisha kuwa ni hukumu na kuadibu kwa Mungu tu katika siku za mwisho ambako ni kazi ya kumuokoa kamilifu mwanadamu. Kando na hii hakuna njia nyingine yoyote ya ubinadamu potovu kuwa huru kikamilifu kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani na kumgeukia Mungu kwa kweli, kumtii, na kupatwa na Yeye ili kutimiza wokovu kamili.

Mwanadamu aliyepotoka sana ni lazima apitie hukumu na kuadibu kwa Mungu kabla aweze kuokolewa. Hii ni kwa kuwa watu wamepotoka sana na wamemilikiwa kikamilifu na maarifa na falsafa za Shetani na wamejaa tabia za kishetani. Ni kwa njia ya hukumu na kuadibu tu ambapo Mungu anaweza kumtakasa na kumuokoa mwanadamu, hii ndio sababu katika kuendeleza kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, kwanza Alionyesha ukweli kumshinda mwanadamu. Mungu anapotumia ukweli kumshinda kikamilifu mwanadamu mpotovu, na anashawishika kwa kweli, ni wakati huo tu ambapo ataona kuonekana Kwake kwa kweli, na ni wakati huo tu basi ataweza kuinama chini mbele ya Mungu na kujuta kabisa. Wakati huo, mwishowe wataona kuwa kwa hakika wao ni watu ambao humpinga Mungu na kwa sababu hiyo watajua kiburi na kujipenda kwao wenyewe, kuwa hakuna nafasi kabisa ya Mungu katika mioyo yao, kwa kweli hawajakuwa wakiishi kulingana na mshabaha wa wanadamu, na kuwa kwa kweli wamepotoshwa sana, kwa njia ya kusikitisha na Shetani. Ni baada tu ya mwanadamu kushindwa na maneno ya Mungu ambapo anaweza kwa kweli kuelewa ukweli na asili muhimu ya kupotoshwa kwake na Shetani, na ni wakati huo tu ambapo anaweza kukubali kwa kweli kuwa baada ya kumwamini Mungu ndani ya dini fulani kwa miaka hiyo yote, hakuelewa zaidi ila maarifa kidogo kutoka kwa Biblia na barua na mafundisho kidogo, na kuwa hana uhalisi wa ukweli kabisa. Kwa kweli wao ni maskini, wa kusikitikiwa, vipofu, na uchi. Ni wakati huo tu ambapo watu wanaweza kuanza kuwa wanyamavu mbele za Mungu, kukubali na kutii rasmi hukumu na kuadibu kwa maneno Yake, na kuanza kuingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu. Haya ni matokeo ya kwanza ya kushinda yaliyotimizwa na hukumu na kuadibu kwa Mungu. Ni kama tu wakati wa Enzi ya Sheria, wakati ambapo Ayubu alikuwa akipitia majaribio na baada ya kuyasikia maneno ya Mungu, alishindwa kikamilifu. Iwapo watu wameshindwa tu na maneno ya Mungu ndio wao ni watu ambao hukiri na kuukubali ukweli, na kisha wanaweza kuingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu na kuwa watu ambao wanaweza kuokolewa. Wale wote ambao bado wanaweza kuuchukia na kuukataa ukweli na kuwa maadui wa Mungu hata baada ya kuyasikia maneno mengi Yake wako katika aina ya wapinga Kristo. Kwa kweli hakuna njia yoyote yao kuokolewa, na watu hao watakuwa vifaa vya uondolewaji na adhabu. Ni lazima wokovu ujengwe kwa msingi wa kushindwa kwa maneno ya Mungu. Kama tu vile Mungu amesema: “Mnapaswa kujua kwamba dhamira Yangu ni kuzima kabisa na kuangamiza yule mwovu kati ya binadamu, ili asiweze tena kuasi dhidi Yangu, sembuse kuwa na pumzi ya kupinga au kuleta fujo kwa Kazi Yangu. Hivyo, kulingana na wanadamu, imekuja kumaanisha kushinda” (“Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi”). “Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa” (“Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)”).

Haya ndio matokeo ya mwanzo yaliyotimizwa na kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu, hii ni kusema, matokeo ya kazi Yake ya kushinda. Kuwafanya watu kuwa wakamilifu kwa Mungu kumejengwa kwa msingi wa kuwashinda, na iwapo wale wanaoshindwa wanaweza kuufuatilia ukweli na kutii kazi yote ya Mungu ya hukumu na kuadibu, basi tayari wameingia katika njia ya kuokolewa na kufanywa kuwa wakamilifu. Kila mmoja anapaswa kuwa wazi kuwa ubinadamu una kiwango hiki cha kiburi, udanganyifu wa kibinafsi, kutokuwa na sheria, na kukosa mantiki kwa kuwa tu hawajawahi kushindwa. Wanakosa kabisa maarifa ya kibinafsi na wamemkataa na kumpinga Mungu hadi kwa kiwango hiki cha ujinga, ambayo ni sababu ni kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu tu ambapo ubinadamu uliopotoka unaweza kupata utakaso na wokovu. Hii pia ndio njia ya pekee ya binadamu mpotovu kuokolewa na kufanywa kuwa mkamilifu.

Hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa ubinadamu uliopotoka hufichua kikamilifu tabia Yake ya haki, na huwaletea fursa ya ajabu ya kumjua Mungu. Iwapo hawatapitia hukumu na kuadibu kwake, kamwe hawatawahi kuijua tabia Yake ya haki. Mara wanapopitia hukumu na kuadibu kwa haki Yake, uadhama, na ghadhabu, ni wakati huo tu ambapo wanaweza kuhisi ukweli kuwa tabia Yake haitavumilia makosa yoyote, na kupitia wenyewe kwamba kwa kweli Mungu anaweza kuchunguza sehemu za ndani kabisa na kulinda mioyo yao wote, kuwa anafahamu vyema asili potovu za watu, na asili za kishetani, na pia kuelewa ukuu na hekima ya Mungu. Kwa kuwa wanaweza kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanaweza kupata maarifa ya kweli ya tabia ya Mungu na asili, hivyo kupata wokovu na ukamilishaji Wake. Ni wazi kuwa utaratibu wa ubinadamu uliopotoka kuokolewa ni mchakato wa kukubali kuonekana kwa Mungu, na ni utaratibu wa kujua tabia Yake ya haki.

Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya binadamu mpotovu kupata wokovu na kufanywa kuwa kamilifu, na tabia ya Mungu ya haki ambayo Amefichua katika kazi Yake katika siku za mwisho. Yote ni kwa sababu ya kujua tabia ya Mungu ya haki na kutambua ukuu na hekima ya Mungu ndipo watu waliochaguliwa wamekuja kumcha Mungu na kuepuka maovu, na hasa ni kwa kuijua tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho ndipo wameelewa ukweli wote ambao Ameonyesha. Hii ndio maana mitazamo ya watu ya mambo, mitazamo ya maisha, na maadili yao yamepitia mabadiliko ya kimsingi, kutimiza polepole mabadiliko katika tabia katika maisha yao. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuukataa, na ni kama tu Alivyosema Mungu:

Watu wameiona tabia Yake kwa sababu ya kazi Yake ya kuadibu na hukumu, na kwa hiyo wanamcha mioyoni mwao. Mungu anapaswa kuchiwa na kutiiwa, kwa sababu uungu Wake na tabia Yake havifanani kama ule wa watu walioumbwa na vikuu juu ya vile vya watu walioumbwa. Mungu sio kiumbe Aliyeumbwa, na ni Yeye tu anayestahili kuchiwa na heshima na taadhima; mwanadamu hana sifa ya kupewa hivi” (“Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu”).

Haki Yangu, uadhama na hukumu vitadumu milele na milele. Mwanzoni, Nilikuwa mwenye upendo na rehema, lakini hii si tabia ya uungu Wangu kamili; haki, uadhama na hukumu ni tabia Yangu tu—Mungu Mwenyewe mkamilifu” (“Sura ya 79” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni).

Haki ni utakatifu, na ni tabia ambayo haivumilii makosa ya mwanadamu, na yale yote ambayo ni machafu na hayajabadilika ndiyo shabaha ya chukizo kwa Mungu. Haki ya Mungu si sheria, lakini amri ya utawala: Ni amri ya utawala katika ufalme, na hii amri ya utawala ni adhabu ya haki kwa yeyote asiye na ukweli na hajabadilika, na hakuna kiwango cha wokovu” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu”).

Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu” (“Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu”).

Haijalishi kama kutakuwa na kuhukumu kwa haki au utakasaji usio na huruma na kuadibu, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kunao uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake, au uwekaji wazi wa aina za mwanadamu, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu” (“Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu”).

Mungu sasa ameanza rasmi kuwakamilisha watu. Ili kufanywa kuwa kamili, watu lazima wapitie ufunuo, hukumu, na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kupitia majaribio na usafishaji wa maneno Yake (kama vile jaribio la watendaji huduma). Kuongezea, watu lazima waweze kustahimili jaribio la kifo. Yaani, mtu ambaye kweli hufanya mapenzi ya Mungu anaweza kutoa sifa kutoka ndani ya kina cha moyo wake katikati ya hukumu ya Mungu, kuadibu, na majaribio, na anaweza kutii Mungu kwa ukamilifu na kujitelekeza mwenyewe, hivyo kumpenda Mungu kwa moyo wa uaminifu, nia moja, na utakatifu; huyo ndiye mtu kamili, na pia ni kazi ambayo Mungu anataka kufanya, na kile ambacho Mungu anataka kutimiza” (“Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu”).

Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[1] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haikuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso na minyanyaso ya nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku?” (“Kazi na Kuingia (9)”)

Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili, na tabia kamili ya Mungu ikionyeshwa kwako, hili linakuletea nini mwilini mwako? Tabia ya haki ya Mungu ikionyeshwa kwako, bila shaka mwili wako utapata uchungu mkubwa. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili” (“Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli”).

Japokuwa kwa sasa unapitia mateso na usafishaji kwa sababu ya hukumu, mateso haya ni ya thamani na ya maana. Japo kuadibu na hukumu ni usafishaji na ufichuzi usio na huruma kwa mwanadamu, uliokusudiwa kuadhibu dhambi zake na kuadhibu mwili wake, kazi hii haijanuiwa kukashifu na kuuzima mwili wake. Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi. Ninyi wenyewe mmeipitia sana kazi hii na, ni wazi, haijawaongoza kwenye njia mbaya. Yote ni kukuwezesha kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, yote ni kitu ambacho kinaweza kutimizwa na ubinadamu wa kawaida. Kila hatua ya kazi hufanywa kwa misingi ya mahitaji yako, kulingana na udhaifu wako, kulingana na kimo chako halisi, na hamjatwikwa mzigo msioweza kuubeba. Japo huwezi kuliona hili wazi kwa sasa, na unajihisi Ninakuwa mgumu kwako, japo unadhani kuwa Ninakuadibu na kukuhukumu na kukuadibu kila siku kwa kuwa Ninakuchukia, na ingawa unachokipokea ni kuadibu na hukumu, hali halisi ni kuwa yote ni mapenzi kwako, pia ni ulinzi mkubwa kwako” (“Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)”).

Haki Yangu, uadhama na hukumu havionyeshi huruma kwa Shetani. Lakini kwa ajili yenu, vipo ili kuwaokoa, lakini ninyi hamwezi tu kuielewa tabia Yangu, wala hamjui kanuni za matendo Yangu” (“Sura ya 90” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni).

Mwishowe, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo ni dhalimu ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, ili kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, na upendo tu, si Mungu wa hekima, na maajabu tu, si Mungu mtakatifu tu, bali, hata zaidi ni Mungu anayemhukumu mwanadamu. Kwa waovu miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwenye kuchoma, kuhukumu na kuadhibu; kwa wale ambao wanapaswa kukamilishwa, Yeye ni mateso, usafishaji, na majaribu, na vilevile faraja, ruzuku, utoaji wa maneno, kushughulika na kupogoa. Na kwa wale ambao wanaondolewa, Yeye ni adhabu na vilevile malipo” (“Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili”).

Ni kwa Mungu kuwa mwili tu katika mahali palipo nyuma mno kimaendeleo na pachafu mno ndiyo Yeye anaweza kudhihirisha ukamilifu wote wa tabia Yake takatifu na yenye haki. Na kupitia kwa nini ndiyo tabia Yake yenye haki inadhihirishwa? Kupitia kwa hukumu ya dhambi za watu, hukumu ya Shetani, karaha kuelekea dhambi, na chuki kwa maadui Zake ambao wanaasi dhidi Yake na kumpinga Yeye” (“Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Kushinda Huzaa Matunda”).

Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. Ndani Yangu kila kitu ni cha wazi; chochote Ninachosema kukamilisha kinakamilika na chochote Ninachosema kuanzisha kinaanzishwa, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuiga mambo haya kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa pekee” (“Sura ya 96” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni).

Ni kwa sababu ya hukumu hizi ndiyo mmeweza kuona kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu. Ni kwa sababu ya utakatifu na haki yake ndiyo Amewahukumu kuwapatilizia hasira Zake juu yenu. Kwa sababu Yeye anaweza kudhihirisha tabia yake ya haki anapotazama uasi wa wanadamu, na kwa sababu Anaweza kudhihirisha utakatifu Wake anapotazama uchafu wa wanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na bila doa, lakini ambaye pia Alizaliwa katika nchi ya uchafu” (“Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Kushinda Huzaa Matunda”).

Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu!” (“Sura ya 44” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni)

Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?” (“Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)”)

Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo” (“Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote”).

Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti” (“Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”).

Umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili” (“Fumbo la Kupata Mwili (2)”).

Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la mwili Wake wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. … Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni uhaki wa Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa” (“Fumbo la Kupata Mwili (2)”).

Imedhihirika kikamilifu kutoka kwa njia za Mungu zinazofanya kazi za hukumu na kuadibu ya kuokoa na kuwafanya watu kuwa wakamilifu kikamilifu katika siku za mwisho kuwa wokovu na ukamilishaji Wake wa watu hutimizwa wote kwa njia ya kufichua tabia Yake ya haki. Mara tabia Yake ya haki, uadhama, hukumu, na ghadhabu inapofichuliwa kikamilifu, binadamu mpotovu kwa kawaida atatenda kulingana na jinsi yao. Wale wote ambao hupenda ukweli na wanaweza kuukubali na kutii kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu, na kisha watapata wokovu na kufanywa kuwa wakamilifu. Wale wote ambao hukataa ukweli, ambao huchukia ukweli, kwa hakika, watampinga, kumkataa na kumshutumu Kristo, na watakataa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho. Hasa, viongozi na wachungaji wengi kutoka vikundi na madhehebu mbalimbali ya ulimwengu wa kidini watakuwa nguvu za wapinga Kristo ambao humpinga na kumkataa Kristo. Hii ndio maana watawekwa wazi na kuondolewa, na mwishowe watapewa adhabu. Watakuwa vifaa vya hukumu ya Mungu katika hasira Yake kali sana. Kazi ya Mungu katika siku za mwisho huakisi kikamilifu pale ambapo upotovu huko, ni lazima hukumu ifanyike, na pale ambapo pana dhambi, ni lazima kuwe na kuadibu. Hii ndiyo sheria ya mbinguni iliyoamrishwa na Mungu na hakuna anayeweza kuiepuka. Ubinadamu potovu hupinga na kumsaliti Mungu, na iwapo hautapitia hukumu na kuadibu Kwake, hautavumiliwa na Mungu. Hii ndio maana ni kanuni ya mbinguni isiyoweza kubadilishwa na mapenzi ya Mungu yasiyoweza kukiukwa kuwa ubinadamu uliopotoka upitie hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho. Mwanadamu amepotoka kwa kiwango cha juu sana. Wote ni wana wa Shetani, ambao walimsaliti Mungu. Iwapo hukumu na kuadibu kwa uadhama na ghadhabu ya Mungu hakukuwapata, basi ni vipi ambavyo wangeweza kusujudu mbele ya Mungu katika kutii kulikokamilika? Na ni vipi ambavyo wangeupata utakaso na wokovu halisi? Hii ndio maana tabia ya Mungu ya haki, hukumu, kuadibu, na ghadhabu ambayo imefichuliwa katika siku za mwisho imekuwa wokovu mkuu wa ubinadamu uliopotoka, na ni baraka za Mungu kwa mwanadamu kabisa. Mungu kufichua tabia Yake ya haki kwa mwanadamu ni upendo Wake wa kweli na upendo Wake kamili kwa mwanadamu.

kutoka katika “Ni Hatua Tatu Tu za Kazi ya Mungu ambazo Ni Kazi Yake Kamili ya Kumuokoa Mwanadamu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha

Tanbihi:

1. “Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

Maudhui Yanayohusiana