Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ni Lazima Mtu Ajue Kwamba ni Hatua Tatu Tu za Kazi ya Mungu ambazo Ni Kazi Yake Kamili ya Kumuokoa Mwanadamu

5

Ni Lazima Mtu Ajue Kwamba ni Hatua Tatu Tu za Kazi ya Mungu ambazo Ni Kazi Yake Kamili ya Kumuokoa Mwanadamu

Mazungumzo ya Mungu ya Hatua tatu za kazi Yake yanatosha kikamilifu kwetu kuona wazi kuwa zimejengwa Hatua kwa Hatua, na kila Hatua inahusiana kwa karibu na inayofuata. Kila Hatua ya kazi Yake ni ya utendaji na ya maana sana, na ni Hatua hizi tatu tu za kazi ambazo ni kazi kamili ya kumuokoa mwanadamu, na Hatua tatu za Mungu za kazi ni mpango Wake wa usimamizi wa kuokoa mwanadamu. Ndio maana kuelewa tu Hatua hizi tatu kwa kweli ni kuelewa kazi ya Mungu, na ni kwa njia hiyo tu inawezekana kuelewa kikamilifu tabia ya haki ya Mungu na asili Yake. Hivyo, ni lazima tuwe na maarifa na ufahamu ulio dhahiri kwa asili na umuhimu wa kila Hatua ya kazi ya Mungu, na ni wakati huo tu ambapo tunaweza kwa kweli kutambua kuwa ni Hatua hizi tatu tu za kazi ya Mungu ambazo ni kazi kamili ya kumuokoa mwanadamu. Kwa kila Hatua ya kazi ya Mungu sote tunaweza kuona kwa wazi jinsi amefaulu katika vita dhidi ya nguvu za uovu za Shetani. Mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na kwa kila Hatua ya kazi Yake kumekuwa na watu wengi ambao wamechukua jukumu la shetani, pepo mbaya, wakifanya juhudi sana kukatiza na kusumbua kazi Yake, na pia wamechanganya, kushawishi wajiunge, kudhibiti, na kutumia watu wa Mungu waliochaguliwa, wakijaribu kuharibu kazi ya Mungu. Hata hivyo, Mungu ni Mwenye enzi, Mungu Aliye mwerevu, na ametumia ujanja wa Shetani kila wakati kama huduma ya kutimiza kazi Yake ya kumkomboa na kumwokoa mwanadamu. Katika kazi Yake katika Enzi ya Neema, Alimtumia Shetani kufanya huduma na kupitia kukana kwa Yuda na kumfanya Bwana Yesu Kristo kusulubiwa msalabani, Alikamilisha kazi Yake ya ukombozi. Katika Enzi ya Ufalme, kupitia ukatizaji, hujuma, na kuchanganyikiwa kulikoletwa na wapinga Kristo, viongozi wa uongo, na aina zote za roho wachafu, Huwafundisha watu Wake waliochaguliwa na kuwafanya kuwa wakamilifu ili waelewe ukweli, waweze kumtambua Shetani, kuchukia uovu, kukwepa joka kuu jekundu, na kuingia katika ukweli wa maneno Yake. Mwishowe, huwafanya watu Wake waliochaguliwa kuwa kamili na kuwaleta katika ufalme. Kuzielewa Hatua tatu za kazi ya Mungu ya kumuokoa mwanadamu ni ya maana sana. Hatuwezi tu kuona kudura na hekima ya Mungu yalipo, lakini hata zaidi, tunaweza kuelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na Alicho ambayo yanafichuliwa katika kila Hatua ya kazi Yake. Kwa njia hii matunda ya ufahamu wetu wa kweli wa Mungu yanaweza kuzaliwa. Ukweli ni kuwa, mchakato wa kupitia Hatua tatu za kazi ya Mungu ni mchakato wa kumuelewa Mungu, na pia ni utaratibu wa mitazamo ya watu na tabia za maisha kupitia mabadiliko ya polepole ili kupata wokovu na kufanywa kuwa wakamilifu. Ni baada tu ya watu kupitia kazi ya Mungu katika siku za mwisho ambapo watakuwa wameokolewa kwa kweli na kupatwa kikamilifu na Mungu, ili kamwe wasitende dhambi na kumpinga Mungu. Hii ni kwa kuwa tabia za kishetani za ubinadamu potovu zimebadilishwa na wana ufahamu halisi wa Mungu. Kamwe tena hawamfafanui na kumpinga Mungu kwa kuzingatia mawazo na fikra za wanadamu, na haijalishi jinsi Mungu huwaongoza na jinsi Yeye hubuni na hupanga mambo, wataweza kuwa watiifu mbele Zake na moyo wa uchaji. Watu hawa tu ndio kwa kweli wanaoyafuata mapenzi ya Mungu, na ambao wanaweza kupata baraka Zake. Ni wale tu ambao kwa kweli hupata wokovu wa Mungu ambao wanaweza kuingia katika mapumziko yaliyotolewa na Mungu na kwa kweli kupata hatima yao ya mwisho. Hakuna shaka kuhusu hii.

Mungu amefanya Hatua tatu za kazi katika wokovu Wake wa mwanadamu, na Hatua hizi tatu za kazi zimewaruhusu watu kwa kweli kuelewa tabia Yake ya haki na hekima Yake na kudura Yake, na hivyo kumgeukia na kuokolewa. Hii ndio maana kuzielewa Hatua tatu za kazi ya Mungu ni muhimu sana.

kutoka katika “Ni Hatua Tatu Tu za Kazi ya Mungu ambazo Ni Kazi Yake Kamili ya Kumuokoa Mwanadamu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha

Maudhui Yanayohusiana