Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ufahamu Unaohitajika kwa Kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

4

Iwapo tunaweza kuyatafakari kwa dhati maneno ya Mwenyezi Mungu yakifichua umuhimu na asili ya kazi Yake katika Enzi ya Sheria, tutaweza kutambua kikamilifu kuwa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria ilikuwa kazi Yake ya mwanzo ya kumwongoza mwanadamu baada ya kumuumba. Yehova alikuwa wa milele, Mungu mmoja tu na wa pekee katika Enzi ya Sheria aliyejitokeza kwa Waisraeli, Ambaye kwanza aliwaongoza kutoka kwa udhibiti na utumwa wa mfalme wa Misri, na kisha Akatoa sheria na amri kwa Waisraeli, hivyo Akianzisha mwongozo wa kibinafsi wa Mungu wa maisha ya mwanadamu. Katika enzi ya Sheria, Mungu Alitoa sheria na amri nyingi ambazo mwanadamu ni lazima azizingatie, na kati yake, aina tatu za muhimu zaidi zilikuwa: Kwanza zilikuwa Amri Kumi; za pili zilikuwa Sabato; za tatu zilikuwa dhabihu, ambazo kwanza zilikuwa sadaka za dhambi, sadaka za amani, na sadaka za kuteketezwa. Matakwa haya matatu yaliyotolewa na Mungu yalikuwa kazi Yake ya Kwanza katika enzi ya Sheria, na umuhimu mkuu wa matakwa Yake matatu ulikuwa ishara za kwanza kuwaelekeza Waisraeli wa wakati huo kuhusu jinsi ya kuishi ulimwenguni. Kinachofuata, tutazungumza kuhusu ufahamu fulani wa umuhimu mkuu wa matakwa haya ya kimsingi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria.

1. Umuhimu wa Amri Kumi zilizotolewa na Mungu wakati wa Enzi ya Sheria ulikuwa wa kina. Maudhui yake yalikuwa:

Usiwe na miungu mingine isipokuwa mimi.

Usijitengenezee sanamu yoyote ya kuchonga, au mfano wowote wa kitu chochote ambacho kiko juu mbinguni, au ambacho kiko chini ulimwenguni, au ambacho kiko majini chini ya ulimwengu. Usiviinamie, wala kuvihudumia: kwani Mimi Yehova Mungu wako ni Mungu aliye na wivu, naadhibu watoto kwa sababu ya makosa ya wazazi hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wale ambao wananichukia; Na nawaonyesha rehema maelfu ya wale ambao wananipenda, na kuzitii amri zangu.

Usilitaje bure jina la Yehova Mungu wako; kwani Yehova hatakosa kumchukulia hatia yule anayelitaja bure jina Lake.

Ikumbuke siku ya sabato, kuifanya kuwa takatifu. Utafanya kazi siku sita, na kuifanya kazi yako yote: lakini siku ya saba ni sabato ya Yehova Mungu wako: hupaswi kufanya kazi yoyote siku hiyo, wewe, wala mwanao wa kiume, wala binti yako, mtumishi wako wa kiume, wala mtumishi wako wa kike, wala ng’ombe wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako: Kwani katika siku sita Yehova aliumba mbingu na nchi, bahari, na vitu vyote vilivyomo, na akapumzika siku ya saba: ndiyo maana Yehova aliibariki siku ya sabato, na akaitukuza.

Waheshimu baba na mama yako: ili siku zako zipate kuwa ndefu katika nchi ambayo Yehova Mungu wako anakupa.

Usiue.

Usizini.

Usiibe.

Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako.

Usitake sana nyumba ya jirani yako, usimtake sana mkewe wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume, wala mtumishi wake wa kike, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala lolote lililo la jirani yako” (Kutoka 20:3-17).

Hizo ndizo Amri kuu na zinazofahamika zaidi ambazo Mungu Alitumia kuwaelekeza watu katika Enzi ya Sheria. Amri Kumi za Mungu ambazo Alianzisha za mwanadamu mpotovu ni rahisi na wazi, za maana kabisa, hutofautisha kwa dhahiri uzuri na uovu, na ni wazi na za kuheshimika. Amri Zake Kumi hujumuisha kikamilifu haki, kanuni za mbinguni na dunia, yanayotia moyo kwa kutisha na ya haki, na maadili. Watu wanaweza kuona kutoka kwa hii kuwa Mungu ni mwaminifu, mwenye haki, mtakatifu na Mungu ambaye huchukia maovu. Amri Kumi huwakilisha kikamilifu matakwa na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, uumbaji Wake. Ni fupi, zina mengi, na ni pana, na zote ni za haki na za kuheshimika, mambo mazuri ambayo yanaweza kudhibitishwa kupitia dhamiri na akili za watu. Umuhimu wa Amri Kumi ni wa kina. Kila amri ina maana sana, na zote zinaweza kuwafanya watu kumuelewa Mungu, kuepuka uovu, kujua yale ambayo Mungu huchukia na yale ambayo huwa Anapenda, na yale ambayo mwanadamu anapaswa kuunga mkono. Wale wote walio na dhamiri na wana akili wanapaswa kukaribisha kwa shangwe na kusherehekea Amri Kumi zilizotolewa na Mungu, ambazo zimewaruhusu watu kuishi kwa kudhihirisha mshabaha wa ubinadamu wa kawaida chini ya mwongozo wao. Bora watu waishi kulingana na Amri Kumi, wana uwezo kamili wa kupata baraka za Mungu. Hii ni kweli. Iwapo kila nchi ulimwenguni ingeweza kuanzisha sheria zao za kikatiba na kutawala nchi yake kulingana na Amri kumi, kwa hakika ingepata baraka za Mungu na nchi yao ingekuwa na utaratibu zaidi. Na iwapo ingeweza kujumuisha Amri Kumi katika vitabu vyao vya shule ili kila mtu azikubali kutoka utotoni, ingeweza kumwabudu Mungu. Hii ingekuwa hata ya maana zaidi. Iwapo watu wa nchi zote wangekuwa wanaishi duniani kulingana na kanuni za Amri Kumi, Mwanadamu kwa hakika hangekuwa mpotovu kama alivyo leo. Lakini kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani ni kwa kina sana, ni kudhibitiwa kikamilifu na Shetani kwa mwanadamu tu ambako kumesababisha ulimwengu mzima kuwa chini ya giza cha uovu kinachoogofya. Hii ndio maana ilikuwa vigumu sana kukubaliwa na kuungwa mkono kwa Amri Kumi kwa mwanadamu aliyepotoka sana katika Enzi ya Sheria. Matokeo ya pekee ambayo zilipata ni kuwafanya watu kuzitambua dhambi zao, lakini kazi ya Mungu iliendelea yenyewe hatua kwa hatua, polepole, ikijijenga yenyewe, kila Hatua ikisaidia hiyo nyingine. Sheria na amri zilizotolewa na Mungu ni lazima zitimizwe.

2. Kanuni ya kutii sabato pia ni muhimu sana. Mungu alirudia kusema matakwa Yake mara nyingi kuwa mwanadamu aiheshimu Sabato, na Yehova akasema: “Kwa kweli mtaadhimisha Sabato zangu; kwa sababu ni ishara kati yangu na ninyi katika vizazi vyenu nzima; ili muweze kufahamu kwamba mimi ni Yehova anayewatakasa. Kwa hiyo mtaadhimisha Sabato; kwani ni takatifu kwenu: kila anayeinajisi bila shaka atauawa: kwani yeyote afanyaye kazi yoyote siku hiyo, nafsi hiyo itaondolewa kutoka watu wake. Kazi inaweza kufanywa siku sita; lakini siku hiyo ya saba ni Sabato ya pumziko, iliyo takatifu kwa Yehova; yeyote afanyaye kazi yoyote katika siku ya Sabato bila shaka atauawa. Kwa sababu hiyo Waisraeli wataadhamisha Sabato, kuizingatia Sabato hiyo katika vizazi vyao nzima, kama agano la daima. Ni ishara kati yangu na waisraeli daima; kwa kuwa Yehova aliumba mbingu na dunia katika siku sita, na katika siku ya saba alipumzika, na akachamngamshwa” (Kutoka 31:13-17). Watu wa Mungu waliochaguliwa wanapaswa kuwa wazi kuwa umuhimu wa Mungu kumhitaji mwanadamu kuiheshimu Sabato ni wa kina. Mungu alipoiumba mbingu na ardhi na vitu vyote, Alifanya hivyo kwa siku sita. Alipumzika siku ya saba. Hii ndio maana Mungu pia huwahitaji watu kufanya kazi kwa siku sita na kupumzika siku ya saba. Hii haina tu upendo wa Mungu, lakini pia ina umuhimu wa kina. Bila shaka, Mungu kumhitaji mwanadamu kuiheshimu Sabato ni ushuhuda kwa mwongozo Wake kwa maisha ya mwanadamu. Hufichua kikamilifu utunzaji Wake, fikira na upendo Wake kwa mwanadamu ambao huna mipaka. Hataki watu kuwa na haraka kila wakati, kuwa wanafanya kazi jua linapochomoza na kupumzika tu jua linapotua, kuishi tu kwa lengo na maana ya chakula, nguo, na makao ya kutosha, na kuzilisha familia zao. Siku ya Mungu ya kupumzika pia ilikuwa ya kumpa mwanadamu siku ya kupumzika, ambayo ndio maana Aliamrisha kuwa watu waiheshimu Sabato. Hii kwa kweli ni muhimu.

3. Kuhusu kanuni za sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani, bila kujali ni nani kati ya Waisraeli alitenda dhambi iliyokatazwa na Munyu Yehova, na bila kujali iwapo alikuwa anafahamu kuwa alikuwa ametenda dhambi au la, ilikuwa lazima aende mbele ya kasisi na kutoa sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya amani kwa Mungu ili dhambi yake isamehewe. Hii iliwaruhusu watu kuona kuwa tabia ya Mungu huwa haina tu haki na uadhama, lakini pia huruma na upendo. Kwa kuwa watu wamepotoshwa na Shetani, ni kawaida kwao kutenda dhambi, lakini Mungu alianzisha sadaka ya dhambi, sadaka ya amani, na sadaka ya kuteketezwa kwa mwanadamu, na haijalishi ni aina gani ya dhambi watu hutenda, bora watoe sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya amani, wanaweza kusamehewa kikamilifu na Yeye. Hii inatosha kuwafanya watu kuijua kuwa tabia ya Mungu kwa mwanadamu mpotovu hujumuisha huruma na wema Wake. Mungu huwa hawashutumu watu bila sababu, na hasa huwa hawapi watu adhabu kwa upole. Kutoka kwa hii, utunzaji na ulinzi wa Mungu, na rehema Yake na baraka kwa mwanadamu ni dhahiri hata zaidi. Hii huonyesha kikamilifu kuwa kanuni iliyomfanya Mungu kuanzisha sadaka hizi za dhambi kwa mwanadamu mpotovu ilikuwa kazi Yake ya kuyaongoza maisha ya watu.

Kazi yote aliyoikamilisha Mungu katika Enzi ya Sheria ilikuwa kumuongoza mwanadamu katika njia inayofaa ya maisha ya binadamu, kuwaruhusu watu wote kuishi mbele Yake, na kupata baraka Zake. Haya ndiyo mapenzi Yake. Katika Enzi ya Sheria, Mungu Alizitumia sheria na kanuni kuongoza maisha ya Waisraeli duniani. Kimsingi, hii ilikuwa ikitengeneza njia kwa kazi ya Mungu ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Kwanza, ilikuwa muhimu kuwafanya Waisraeli kusongea mbele ya Mungu na kumkubali, hii ni kusema, kumkubali Mungu Muumbaji, na kujua jinsi watu wanapaswa kuishi mbele Zake. Bila shaka, huu ulikuwa ushuhuda wa kweli wa Mungu kuyaongoza maisha ya watu duniani. Haukufichua tu upendo Wake kwa mwanadamu, lakini hata zaidi, uliwaruhusu watu kuelewa kuwa Mungu hakuiumba mbingu, dunia, vitu vyote, na mwanadamu tu, lakini pia huwa anawaongoza watu kujua jinsi ya kuishi, na jinsi ya kuishi mbele ya Mungu na kuzipata baraka Zake. Kwa njia hii, watu wanajua jinsi ya kuishi mbele ya Mungu, jinsi ya kumwabudu, jinsi ya kuzipata baraka Zake, na jinsi ya kuishi ili kupata amani, maisha marefu na furaha. Hii kwa kweli ni ya maana sana kwa wanadamu wapotovu. Iwapo wanadamu wote wangeishi kulingana na sheria na amri zilizopeanwa na Mungu, hawangekuwa wamepotoshwa sana na Shetani kiwango kuwa hawana mshabaha wowote wa binadamu, na ulimwengu hungekuwa na giza na uovu kama ilivyo leo. Lingekuwa jambo la kufaa sana iwapo watu wangeishi chini ya mwongozo wa Mungu! Kama vile tu Mwenyezi Mungu alisema: “Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli” (Maono ya Kazi ya Mungu (3)). Hii inaonyesha kuwa katika kufanya kila moja ya Hatua tatu za kazi ya Mungu, Mungu Hupanua polepole mawanda ya kazi Yake, na mwishowe kuwaokoa wanadamu wote kuacha kikamilifu ushawishi wa Shetani na kukigeukia kiti cha enzi cha Mungu kikamilifu. Huu ndio mpango wa usimamizi wa kumuokoa mwanadamu.

Iwapo ningejumuisha umuhimu mkuu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria kwa maneno machache, ilikuwa kazi ya kuwaongoza watu katika jinsi ya kuishi duniani baada ya Mungu mwanzo kumuumba mwanadamu. Kazi Yake katika Enzi ya Sheria hapo mwanzo ilisisitiza umuhimu mkuu wa “kuongoza.”

kutoka katika “Ni Hatua Tatu Tu za Kazi ya Mungu ambazo Ni Kazi Yake Kamili ya Kumuokoa Mwanadamu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha

Maudhui Yanayohusiana