Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kwa Nini Mungu alifanya kazi Yudea katika Enzi ya Neema?

3

Kwa Nini Mungu alifanya kazi Yudea katika Enzi ya Neema?

Mara ya kwanza Nilipokuja miongoni mwa binadamu ilikuwa katika Enzi ya Ukombozi. Bila shaka Nilikuja miongoni mwa jamii ya Wayahudi; kwa hivyo watu wa kwanza kumwona Mungu Akija ulimwenguni walikuwa Wayahudi. Sababu Yangu ya kufanya kazi hii mwenyewe ilikuwa kwa sababu Nilitaka kutumia kupata mwili Kwangu kama sadaka ya dhambi katika kazi Yangu ya ukombozi. Kwa hivyo watu wa kwanza kuniona Mimi walikuwa Wayahudi wa Enzi ya Neema. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza Mimi kufanya kazi Nikiwa katika mwili.

kutoka katika “Inapokuja kwa Mungu, Ufahamu Wako Ni Upi?”

Hakuna kilichokuwa cha ishara zaidi ya awamu ya kwanza iliyofanyika katika Israeli: Waisraeli walikuwa watakatifu sana na wenye upotovu wa chini zaidi kuliko watu wote, na hivyo pambazuko la kipindi kipya katika nchi hii kilibeba umuhimu mkubwa. Inaweza kusemwa kwamba mababu wa wanadamu walitoka Israeli, na kwamba Israeli, ilikuwa watani wa kazi ya Mungu. Hapo mwanzo, watu hawa walikuwa watakatifu sana, na wote walimwabudu Yehova, na kazi ya Mungu ndani yao iliweza kuzaa mazao makubwa. Biblia nzima inarekodi kazi ya enzi mbili: Moja ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria, na moja ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema. Agano la Kale hurekodi maneno ya Yehova kwa Waisraeli na kazi Yake katika Israeli; Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu huko Uyahudi. Lakini kwa nini Biblia haina majina yoyote ya Kichina? Kwa sababu sehemu mbili za kwanza za kazi ya Mungu zilifanyika katika Israeli, kwa sababu watu wa Israeli walikuwa wateule—ambayo ni kusema kwamba wao walikuwa wa kwanza kukubali kazi ya Bwana. Walikuwa wenye upotovu wa chini zaidi ya wanadamu wote, na hapo mwanzo, walikuwa na nia ya kumtazamia Mungu na kumheshimu Yeye. Walitii maneno ya Bwana, na daima walitumika katika hekalu, na walivaa mavazi ya kikuhani au mataji. Walikuwa watu wa kwanza kabisa kuabudu Mungu, na chombo cha kwanza kabisa cha kazi yake. Watu hawa walikuwa kielelezo na mfano wa kuiga kwa wanadamu wote. Walikuwa kielelezo na mfano wa kuiga wa utakatifu na haki. Watu kama Ayubu, Ibrahim, Lutu, au Petro na Timotheo—wote walikuwa Waisraeli, na vielelezo na mifano mitakatifu zaidi ya watu wote. Israeli ilikuwa nchi ya kwanza ya kuabudu Mungu miongoni mwa wanadamu wote, na watu wengi wenye haki walitoka hapa kuliko mahali pengine popote. Mungu Alifanya kazi kati yao ili aweze kusimamia vizuri mwanadamu katika nchi zote na katika siku zijazo. Mafanikio yao na haki ya ibada yao ya Yehova yaliandikwa kwenye kumbukumbu, ili waweze kuhudumu kama vielelezo na mifano kwa watu waliokuwa nje ya Israeli wakati wa Enzi ya Neema; na matendo yao yamezingatia miaka elfu kadhaa ya kazi, mpaka hivi leo.

kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)”

Maudhui Yanayohusiana