8. Kuna tofauti ipi kati ya mtu mwaminifu na mtu mdanganyifu?

Maneno Husika ya Mungu:

Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme. Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama una rekodi ya kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kama umemtii Mungu kikamilifu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa, jinsi ilivyoandikwa katika rekodi ya majaliwa yako.

Umetoholewa kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mtu mdanganyifu atamlaghai yeyote kwa hila zake, wakiwemo jamaa yake—hata wana wake mwenyewe. Bila kujali uko wazi kwake kiasi gani, atakuchezea. Hii ndiyo sura ya kweli ya asili yake—yeye ni wa asili hii. Ni vigumu kubadilika na yu hivi kila wakati. Watu waaminifu huenda wakati mwingine watasema kitu kijanja na cha hila, lakini mtu huyu huwa mwaminifu kiasi; yeye hushughulikia mambo moja kwa moja na hajinufaishi kutoka kwa wengine kwa njia isiyo ya haki katika shughuli zake nao. Anapozungumza na wengine, yeye hasemi vitu kimakusudi ili kuwajaribu; anaweza kuufungua moyo wake na kuwasiliana na wengine, na kila mtu husema yeye ni mwaminifu sana. Kuna nyakati nyingine ambazo yeye huzungumza kwa udanganyifu fulani; hiyo tu ni dalili ya asili potovu na haiwakilishi asili yake, kwa sababu yeye si mtu mdanganyifu.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuijua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kwa sababu ya tofauti katika asili kati ya watu waaminifu na watu wadanganyifu, tabia zao na mienendo yao pia ni tofauti sana. Ndani ya kanisa, watu waaminifu hukamilishwa kwa urahisi, wakati ambapo watu wadanganyifu hawakamilishwi kwa urahisi. Hii ni kwa sababu watu waaminifu wako tayari kukubali ukweli na wanaweza kuweka ukweli katika vitendo, lakini watu wadanganyifu huona vigumu kuweka ukweli katika vitendo, hata wakikubali ukweli. Watu waaminifu wanaweza kumpa Mungu mioyo yao katika imani yao kwa Mungu, lakini watu wadanganyifu hawawezi. Watu waaminifu wanaweza kutoa kila kitu ili kujitumia kwa ajili ya Mungu, wakati ambapo watu wadanganyifu ni wepesi wa kuomba kitu kama malipo na kuweka masharti. Mioyo ya watu waaminifu ni safi na ya kweli, lakini mioyo ya watu wadanganyifu ni yenye usaliti na ya kubadilika badilika. Watu waaminifu hutumia jitihada zote kumridhisha Mungu wakati wowote anapohitaji kitu kutoka kwao, wakati ambapo watu wadanganyifu hufanya wajibu wowote wanaoufanya ovyoovyo na kuweka mguu mmoja katika mlango ili kuhakikisha kuwa wana njia ya kutoka nje. Watu waaminifu ni wenye kujali sana kuhusu uaminifu katika usemi na tendo, na hawajaribu kumdanganya Mungu au watu wengine, wakati ambapo watu wadanganyifu humdanganya kila mtu bila haya, na kwao jambo hili ni sawa ilimradi wafikie malengo yao wenyewe. Watu waaminifu ni wakarimu sana wanapofanya ushirika na wengine, hawabishani juu ya hasara au faida za binafsi, na wao hukuza uaminifu kwa kutilia mkazo hisia, lakini watu wadanganyifu daima hushindana na wengine kupata faida, na wao ni wepesi wa kuchezacheza na watu wengine. Watu waaminifu wanaweza kufungua mioyo yao na kuzungumza yaliyo ndani ya mioyo yao katika wao kuwashughulikia wengine, na kuwa waaminifu na wazi, lakini watu wadanganyifu huhodhi madhumuni maovu ambayo wao huwaficha watu wengine, na hawawezi kuelewana na wengine. Watu waaminifu ni wanyofu na wenye uwazi katika kauli na tabia zao, na ni wenye hakika na wasema kweli, lakini watu wadanganyifu ni wa kukwepa na wao huhodhi nia za usaliti katika kauli na tabia zao, na wao husema jambo moja na kufanya jingine. Watu waaminifu ni safi na wanyofu, wasio na hatia na wakunjufu, na Mungu na watu wengine wanawapenda, lakini watu wenye udanganyifu huhodhi nia mbaya, wao hutekeleza jukumu kulingana na hali ya mambo, wao hufanya ishara kubwa, kuna uongo na unafiki mwingi sana ndani yao, na Mungu na watu wengine huwachukia. Maonyesho haya yote ndiyo tofauti kati ya watu waaminifu na watu wadanganyifu.

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Kama watu si waaminifu, Mungu hafurahishwi nao na hawataweza kusimama imara katika umati. Watu waaminifu hawapendwi na Mungu tu, lakini pia na wengine. Kwa nini watu waaminifu wanapendwa na wengine? Kipengele kimoja ni kwamba wao ni wa kutegemewa. Unaposhirikiana nao, unahisi mtulivu na imara, na huna wasiwasi. Huhangaiki kuhusu shida za baadaye, huwi na wasiwasi kwamba watajaribu na kukudanganya au kukudhuru. Jambo kuu ni kwamba watu waaminifu wanaweza kuwasaidia wengine, kufungua mioyo yao kwa watu wengine, na kuwa wa manufaa kwa wengine. Kwa sababu watu waaminifu wanapenda ukweli na wanaweza kutenda ukweli wanapomwamini Mungu, na Mungu huwapenda watu waaminifu, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao. Roho Mtakatifu afanyapo kazi ndani ya mtu mwaminifu atapata neema ya Mungu, aweze kuelewa ukweli, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu halisi. Hii ndiyo maana wengine huwapenda watu waaminifu. Aidha, kushirikiana na watu waaminifu kunakuruhusu kujifunza jinsi ya kutenda, jinsi ya kufanya, jinsi ya kutenda ukweli, na hatimaye kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu wa kawaida. Kwa nini watu huwachukia watu wadanganyifu? Kwa nini Mungu huwadharau watu wadanganyifu? Maonyesho ya upotovu wa watu wadanganyifu ni yapi? Asili na kiini chao ni kipi? Wanawaletea wengine nini? Mtu mdanganyifu, kutokana na asili ya tabia yake potovu, ni mwenye ubinafsi mno. Anafanya kila kitu kwa ajili yake, anatafuta anasa zake mwenyewe tu, hafikirii wengine, hajali wengine wakiishi au kufa. Huyu ni aina ya mtu aliye na ubinafsi na mwenye kustahili dharau kabisa. Mtu asiye mwaminifu akishika madaraka ndani ya kanisa, je, watu wateule wa Mungu watapata faida yoyote? Hafikirii iwapo watu wateule wa Mungu wanaweza kupata chochote kupitia kula na kunywa maneno ya Mungu au la, iwapo wanaweza kupata ukweli au la, kuingia katika uhalisi, au kuingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu na kuokolewa. Kile anachofikiri ni, “Alimradi nina anasa na hadhi, alimradi ninaweza kujitokeza katika umati na kuwadhibiti wengine, nimeridhika na hilo ni sawa!” Alimradi tamaa zake mwenyewe za mwili zinafikiwa basi amemalizana na shughuli yake; hazingatii iwapo watu wateule wa Mungu wanaishi au kufa. Je, hiki si kipengele muhimu kabisa cha mtu mdanganyifu? Kwa hiyo, kiini cha asili ya mtu mdanganyifu ni kujifikiria mwenyewe tu, kutafuta raha za mwili kwa ajili yake mwenyewe, na kutojali hisia za wengine.

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa Mtu Mwaminifu Pekee Ndiko Kuwa Mfano wa Binadamu wa Kweli” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha XIII

Watu waaminifu hufuatilia ukweli kwa sababu wanapenda ukweli. Je, watu wasio waaminifu? Hawapendi ukweli. Wanapenda mafundisho. Wanapenda kuelezea watu vitu na kuwafanyia watu vitu. Wanapenda kuringa. Kwa hivyo, wanalenga kunena. Je, huku si kuwa mtu bandia? Je, huku si kuwa mtu mjanja? Watu wajanja wanashughulika kuhusu sura yao ya nje. Kama tu Mafarisayo, waliomba ili wengine wangeweza kuwaona. Waliomba katika mikungamano ili kila mtu angeweza kuwaona, ili watu kila mahali wangeweza kuwaona. Walionekana kuwa wenye kumcha Mungu sana kwa nje! Lakini walikuwa wakifanya nini kwa kweli? Walikuwa wadanganyifu kabisa na bandia kabisa. Watu waaminifu hupenda ukweli. Wakiwa mbele ya Mungu, hawana fikira zingine ila kutafuta ukweli, kuelewa mapenzi ya Mungu na wana hiari ya kumridhisha Mungu. Hawahifadhi kila aina za njama janja, hawana mawazo mengi sana ya kibinafsi na yenye kustahili dharau. Wana mioyo safi. Katika kila kitu, wanatafakari tu fikira hii moja: “Nawezaje kumridhisha Mungu? Mapenzi ya kweli ya Mungu ni yapi?” Kama hawaelewi, wanaendelea kuomba na kuifikiria bila kusita hadi waielewe. Je, si watu kama hawa ni watu waaminifu? Watu waaminifu hupenda ukweli, hivyo bila shaka watafuatilia ukweli. Katika maombi yao mbele ya Mungu, hawaombi chochote kingine kando na kufuatilia na kutafuta ukweli. Ukiwauliza kutofuata ukweli ama kutoelewa mapenzi ya Mungu katika maombi yao, watahisi kwamba hawana chochote cha kusema, kwani wanahisi kwamba hivi ni vitu tu wanavyoweza kufanya pekee mbele ya Mungu, wanahisi hakuna haja na ni bure kufanya kitu kingine kando na vitu hivi. Hawako tayari kufanya vitu vya uongo. Watu hao wajanja hawako hivi. Daima wanaringa na kujigamba mbele ya Mungu, kuongea kuhusu fikira zao wenyewe, kuonyesha uwezo wao, na kutangaza mafanikio yao. Kwa kweli, kila kitu wanachofanya ni kwa ajili ya wengine kuona, wanataka wengine wawapende, wawasifu na kuwasikiza. Wale wote ambao hawatafuti ukweli, ambao hawafuatilii kuelewa mapenzi ya Mungu, ambao hawana kiu ya ukweli, ni watu wajanja, watu bandia, watu wanafiki….

Umetoholewa kutoka katika “Vipengele Kumi Ambavyo Lazima Mtu Afanye Mazoezi ya Kuingia Katika Ili Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha V

Iliyotangulia: 7. Mtu mdanganyifu ni nani? Kwa nini watu wadanganyifu hawawezi kuokolewa?

Inayofuata: 9. Mtu anafaaje kutenda kuingia kuwa mtu mwaminifu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

3. Ni nini hasa mtu anayefuata mapenzi ya Mungu? Na ushahidi wa kweli wa imani katika Mungu ni nini?

Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na ukosefu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake wa Mungu. Je, huu si upendo mkamilifu wa Mungu? Je, hii si ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo wa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki.

2. Ni nini lengo na umuhimu wa Mungu kuwa mwili nchini China ili kufanya kazi katika siku za mwisho?

Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utukufu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki