X. Jinsi ya Kutambua Wachungaji wa Uongo, Wapinga Kristo, na Makristo wa Uongo

1. Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kutenda kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Kama huwezi kutofautisha ni uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana. Huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga, na huduma ya aina hii huenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho yao mengi ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufichua fikira zao, sembuse kuwapogoa watu kwa ajili ya upungufu wao wa dhambi. Wengi wanaowafuata wanahudu kwa vipaji vyao, na yote wanayotoa ni fikira za kidini na nadharia za theolojia, ambazo haziambatani na uhalisi na haziwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, lakini wanalitumia kanisa vibaya, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao ni doezi katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila dhidi ya ndugu zao na kuwadanganya, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Je, wewe hujaribu kuwapumbaza watu kwa kufanya hivi? Je, unafanya maonyesho matupu, bila dutu ya kuyasitiri? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kuwaongoza wengine katika njia sahihi, na watawapotosha. Je, hili halileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa za watu na kuwaruhusu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuendelea kwa namna hii kutazalisha mafundisho mengi, , ambazo zitawafanya watu wakuchukie. Hivyo ndivyo ulivyo udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli unadhalilisha.

Kimetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli? Watu wa aina hii ni wa namna sawa na Paulo.

Kimetoholewa kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

8. Dhihirisho la majivuno ni kumwasi na kumpinga Mungu. Watu wanapokuwa na majivuno, wa kujikweza, na wa kujidai, wao huelekea kuanzisha falme zao huru na kufanya mambo jinsi wanavyotaka. Wao pia huwavuta wengine katika mikono yao wenyewe na kuwavuta katika kumbatio lao. Watu wanapoweza kufanya mambo ya aina hii, kiini cha majivuno yao ni kile cha malaika mkuu. Majivuno yao na kujikweza kwao kunapofika kiwango fulani, basi hilo huamua kwamba wao ni malaika mkuu na watamweka Mungu kando. Ikiwa una tabia ya aina hii ya majivuno, basi Mungu hatakuwa na nafasi moyoni mwako.

Tumehubiri injili tena na tena kwa viongozi wengi katika jamii za dini, lakini bila kujali jinsi tunavyoshiriki ukweli na wao, wamekataa kuukubali. Kwa nini hivi? Ni kwa sababu majivuno yao yamekuwa tabia yao mbaya na Mungu hayuko tena mioyoni mwao! Watu wengine wanaweza kusema: “Watu walio chini ya uongozi wa baadhi ya wachungaji katika ulimwengu wa dini kweli wana msukumo mwingi. Inaonekana kwamba wana Mungu kati yao!” Haijalishi jinsi mahubiri ya wachungaji hao yanavyoweza kuwa makubwa, je, wanamjua Mungu? Kama kweli wangekuwa wanamcha Mungu mioyoni mwao, wangewafanya watu wawafuate na kuwatukuza? Je, wao wangewahodhi wengine? Je, wangethubutu kuwawekea vikwazo wengine wanaotafuta ukweli na kuchunguza njia ya kweli? Kama wanaamini kuwa kondoo wa Mungu kwa kweli ni wao na kwamba kondoo Wake wote wanapaswa wawasikilize, je, wao wenyewe hawatendi kama Mungu? Watu kama hawa ni wabaya hata zaidi kuliko Mafarisayo. Je, wao sio wapinga Kristo? Kwa hiyo, kwa sababu ya asili yao ya majivuno, inaweza kuwadhibiti wafanye mambo ambayo yanamsaliti Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Asili yenye Majivuno ya Mwanadamu Ndiyo Chanzo cha Upinzani Wake kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

9. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo ambavyo Mungu anafanya kutoka ndani ya mwili Wake wa nyama. Katika wakati huo, fikira zote za mwanadamu zinakuwa povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. … Wale wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndiyo wanadamu kama hao watahukumiwa.

Kimetoholewa kutoka katika “Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?

Kimetoholewa kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

Kimetoholewa kutoka katika “Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili

14. Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe.

…………

Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo. Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake. …

Kazi na maonyesho ya Kristo huamua dutu Yake. Yeye Anaweza kukamilisha kwa moyo wa kweli kile Alichoaminiwa kufanya. Anaweza kumwabudu Mungu mbinguni kwa moyo wa kweli, na kwa moyo wa kweli Atafute mapenzi ya Mungu Baba. Yote haya yanaamuliwa na dutu Yake. Na vile vile ufunuo Wake wa asili pia unaamuliwa na dutu Yake; sababu ya ufunuo Wake wa asili kuitwa hivyo ni kwa sababu ya maonyesho Yake siyo maigizo, au matokeo ya elimu na mwanadamu, au matokeo ya miaka mingi ya kukuzwa na mwanadamu. Hakujifunza au kujivika nayo Yeye Mwenyewe; badala yake, ni asili ndani Yake.

Kimetoholewa kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, “Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu!” Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake.

Kimetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Iliyotangulia: IX. Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Maisha ya Petro

Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp