Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

51. Nilipitia Wokovu wa Mungu

Cheng Hao    Mji wa Yongzhou, Mkoa wa Hunan

Kwa neema ya Mungu, mimi na mke wangu tulipandishwa vyeo hadi kwa timu ya injili ya pili ili kutimiza wajibu wetu. Muda mfupi uliopita, mke wangu alipandishwa cheo kuwa mkurugenzi wa timu, huku mimi, kutokana na kiburi changu mwenyewe na utukutu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupelekwa nyumbani kutafakari juu ya matendo yangu. Kutokana na kwamba mimi na mke wangu tulianza kutimiza wajibu wetu wakati mmoja, lilikuwa jambo gumu kukubali kumuona akipandishwa cheo wakati nilifukuzwa kutoka kwa wajibu wangu. Machozi yalidondoka machoni mwangu nilipofikiri: "Mambo yangu yamekwisha. Mungu anatenganisha kila mmoja kwa jinsi yake na, kuzingatia kuwa nimefukuzwa, hii ni hakika kwamba nimefichuliwa na kuondoshwa. Aa! Nani angefikiri kwamba baada ya miaka yote hii, maisha yangu kama muumini yangeishia kwa kutofaulu kabisa. Yote ninayoweza kufanya sasa ni kusubiri adhabu yangu." Kisha nikaenda nyumbani na moyo mzito. Kuanzia wakati huo kwendelea nikawa nimetatizika katika kushindwa na kujawa na suitafahamu na lawama kwa Mungu. Nilikuwa nimetumbukia katika giza bila matumaini.

Siku moja, nikapata vifungu viwili vinavyofuata vya neno la Mungu kwa bahati: “Sijawahi kusema kuwa hamkuwa na mategemeo, sembuse kwamba mlipaswa kuangamizwa au kupotea; je, Nimetangaza hadharani jambo hilo? Wewe husema kuwa huna tumaini, lakini si hili ni hitimisho lako? Je, si hii ni athari ya mawazo yako mwenyewe? Je, hitimisho lako lina maana?” (“Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini. Je, hili si la kujiadhibu? … Huelewi kazi ya Mungu na huyaelewi mapenzi ya Mungu katu; hata zaidi, huelewi nia nzuri ambazo Mungu ameweka katika miaka Yake 6,000 za kazi ya usimamizi” (“Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nikisoma vifungu hivi, nilitambua kwa mshangao: Mungu hazungumzi juu yangu? Mara tu nilipoarifiwa kwamba kanisa lilikuwa limenifukuza, nilikisia na kuhitimisha kuwa nilikuwa nimefichuliwa na kuondoshwa na kupoteza imani katika kutafuta ukweli. Niliishi katika hali ya kudumu ya uhasi na kutoelewana, kama nimekubali bila kulalamika kabisa kushindwa kwangu mwenyewe. Wakati huo, nilitazama moyoni mwangu, nikiuliza: "Je, unaelewa kwa kweli ni kwa nini umekutana na balaa hii? Je! Unaelewa kwa kweli mapenzi ya Mungu? Bila shaka hapana! Sielewi! Basi kwa nini nifanye makisio ya kishenzi na ufafanuzi kwa maneno usio na msingi? Je, si huku kulikuwa ni kuwa na kiburi sana, udanganyifu mno? Je, si nilikuwa nimejishusha katika mahali hapa pa mateso ya giza? Upumbavu jinsi gani, jinsi nilivyokuwa na upuuzi!" Kwa hiyo, nilikwenda mbele ya Mungu kwa sala, nikiomba nuru Yake ili nipate kufichua mapenzi Yake katika ufunuo huu wa hivi karibuni. Baadaye, niliona kifungu hiki cha neno la Mungu: “Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kumfinyanga mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. … Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu” (“Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ya dhati yaliufurahisha moyo wangu na kuniamsha kutoka kwa kuishiwa imani kwangu kulikokuwa kumetiwa ganzi. Kama ilivyobainika, ingawa hali yangu ilionekana kuwa ya kutia hofu kwa ukaguzi wa kwanza, ilikuwa ni Mungu kwa kweli akiniletea upendo Wake, na akinipa wokovu Wake. Haikuwa, kama nilivyofikiria, kwamba ningeondoshwa. Nilikuwa mwenye kiburi na mgumu—nikitimiza wajibu wangu kwa kuzembea na utundu bila kuwa na subira. Mungu hangevumilia kuniona nikiendelea kukanyagwa na Shetani. Hakuweza kuvumilia kuniona nikizidi kuzama chini zaidi na Yeye hasa hakuweza kuvumilia kuniona nikikabiliwa na adhabu kwa kuikosea tabia ya Mungu kupitia vitendo vya kiburi kisichozuilika. Hivyo, kupitia hukumu na kuadibiwa, Aliniletea wokovu, akanibariki kwa neema Yake ya kuokoa na kunisaidia kuyatoroka mishiko ya upotovu wa Shetani. Kufukuzwa kwa kanisa kulikuwa, kweli, wokovu mkuu mno wa Mungu. Jinsi nilivyozidi kuwa na kiburi, ndivyo Mungu alivyozidi kutengeneza mazingira ili kukabiliana na makosa yangu. Aliruhusu tamaa zangu kubaki bila kutimizwa ili moyo wangu uliokufa ganzi uanze kuhisi maumivu. Alitenda kupitia maumivu haya ili kunifanya kutafakari juu ya matendo yangu, kuelewa kiini cha asili yangu potovu na kutafuta ukweli ili kufanikisha mabadiliko katika tabia yangu. Hii ndiyo ile kazi halisi ya wokovu ambayo Mungu aliniletea. Yote aliyoyafanya yalikuwa ni utunzaji na upendo kwangu. Vinginevyo, bado ningekuwa naishi katika dhambi isiyojali, bado nikitenda bila kuwa na subira. Mwishowe, vitendo vyangu vingekuwa vimeikosea tabia ya Mungu na ningekuwa nimeondoshwa na Mungu. Wakati huu, nilikuja kuona kwamba wokovu wa Mungu ulikuwa halisi. Hakuna kitu cha uongo au kitupu kuhusu upendo wa Mungu—ni kweli na halisi. Mimi, hata hivyo, nilikosa kuona kazi ya Mungu na wokovu Wake. Nilikosa kutafuta nia yenye ari katika wokovu wa Mungu, badala yake nilijifafanua kupita kiasi mara kwa mara huku nikimwelewa Mungu visivyo na kumlaumu na kuishi kwa uzembe bila rajua. Nilikosa busara kiasi gani! Nilikuwa mtu asiyefaa kupokea hukumu ya Mungu na kuadibiwa.

Mungu mpendwa, asante! Kupitia uzoefu huu, ninatambua kwamba wokovu Wako ni wa kweli na hukumu Yako na kuadibu vimejaa upendo. Bila hukumu Yako na kuadibu, singewahi kamwe kujitazama kwa kweli. Ningendelea kuishi katika upotovu, hali yangu ikiendelea kuharibika, kukanyagwa na Shetani na hatimaye kubebwa naye. Kupitia uzoefu huu, nilitambua pia kuwa kiini Chako ni upendo na kwamba matendo Yako yote yanalenga kuwaokoa wanadamu. Mungu, ninaapa kujiwekeza kikamilifu katika kutafuta ukweli na kuanza upya. Bila kujali matokeo ni yapi, ninaapa kutimiza wajibu wangu wa kiumbe ili kuyaridhisha mapenzi Yako.

Iliyotangulia:Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

Inayofuata:Jitiishe Mwenyewe ili Kufundisha Wengine Nidhamu

Unaweza Pia Kupenda