Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

87. Hukumu Ni Mwanga

Zhao Xia Mkoa wa Shandong

Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” na “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na maraf