Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Hukumu Inafichua Haki ya Mungu

1 Umeme unaangaza kutoka Mashariki, ukiiangaza dunia potovu ya zamani na kuifanya mbingu na dunia mpya. Kristo wa siku za mwisho Anaonyesha ukweli ili kuhukumu na kuwaokoa binadamu. Watu wa Mungu wameamshwa na maneno ya Mungu, tunafungua macho ya roho zetu na kutazama kwa karibu: Enzi ya Ufalme imewadia, na hukumu imeanza na nyumba ya Mungu. Tunapitia kuadibu na hukumu mbele ya kiti cha Kristo. Kwa kukubali hukumu na majaribu ya maneno ya Mungu, tunaijua haki ya Mungu. Mioyo yetu isiyohisi imeamshwa na maneno ya Mungu na tunaanguka chini mbele za Mungu. Tunatii kwa urahisi hukumu na kuadibu kwa Mungu ili kutakaswa na kukamilishwa na Mungu.

2 Kupitia raundi nyingi za kuadibu na usafishaji hatimaye tunapata utakaso. Nikikumbuka kazi ya Mungu na kutafakari juu ya upendo wa Mungu, nahisi mimi ni mdeni sana. Katika imani yangu ya zamani katika Bwana nilikuwa natamani tu Aje, ili ninyakuliwe na kupata taji. Nilijitahidi na kufanya kazi kwa bidii, nikijishuhudia, nikifikiria kwamba bado nilikuwa namtumikia Mungu. Nilijawa na udanganyifu na kujaribu kujadiliana na Mungu, wakati wote nikisema nampenda Mungu, nisijue aibu. Ni kwa hukumu ya Mungu tu ndipo naona wazi ukweli wa upotovu wa kumpinga Mungu. Naona aibu sana na sistahili kuwa mwanadamu, siwezi kuthubutu kumkabili Mungu. Napaswa kulaaniwa kwa kile nilichofanya, nawezaje kustahili kuingia katika ufalme wa Mungu? Kwamba nimeishi hadi leo ni upendo na huruma kubwa ya Mungu.

3 Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, hatimaye naelewa mapenzi Yake. Ufunuo Wake mkali na hukumu kuu vyote ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu. Nachukia ujinga na upofu wangu wa zamani, kwamba sikujua upendo wa Mungu. Majaribu yalipotokea, nilimwelewa vibaya na kumlaumu Mungu, sikuelewa nia Yake ya dhati. Kwamba naweza kutakaswa na kuokolewa leo ni kwa sababu ya upendo wa Mungu kabisa. Naona kwamba tabia ya Mungu ni takatifu, yenye haki, ya kuheshimiwa na kupendwa. Hakuna maneno yanayoweza kueleza kupitia ukuu wa wokovu wa Mungu. Natafuta kumjua Mungu na kumpenda kwa kweli, na mimi nitalifia hili kwa furaha. Watu wa enzi ya mwisho wamekamilishwa na Mungu, tutampenda na kumshuhudia Mungu milele!

Iliyotangulia:Kutiwa Moyo na Upendo wa Mungu

Inayofuata:Amua Kuwa Mtu Mwaminifu

Maudhui Yanayohusiana

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  Ⅰ Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  Ⅰ Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwe…

 • Upendo Safi Bila Dosari

  I Upendo ni hisia safi, safi bila dosari. Tumia moyo, tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza. Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga. Tumia moyo, …

 • Umuhumi wa Maombi

  I Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…