Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

757 Jinsi ya Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha ya Kutii

1 Sasa vimo vyenu vimewekwa kwa mtihani wa vitendo, ili kuona kama kanisa linaweza kujengwa na iwapo mwaweza kutii kila mmoja au la. Kukitazamwa kutoka kipengele hiki, kutii kwako kwa kweli ni kutii ambako unachukua na kuchagua—ingawa unaweza kuwa na uwezo wa kutii mtu mmoja, unaweza kuona ni vigumu kumtii mtu mwingine. Kwa kweli hakuna njia ambayo unaweza kuwa mtiifu wakati unategemea dhana za kibinadamu. Hata hivyo mawazo ya Mungu kila mara hupita yale ya mtu! Kristo Alitii hadi kifo na Akafa msalabani. Kristo Hakusema lolote kuhusu hali yoyote au sababu, mradi ilikuwa mapenzi ya Baba Yake, Alitii bila kusita.

2 Utii wako wa sasa ni mdogo mno. Ninawaambia nyinyi nyote, utiifu si kutii watu walio nje, ni kutii maisha ya ndani yalio ndani yenu na ni kumtii Mungu Mwenyewe. Maneno Yangu yanawafanya upya na kuwabadilisha kutoka ndani, vinginevyo nani angemtii nani? Nyinyi nyote ni waasi kwa wengine. Lazima mchukue wakati wa kuifahamu hii, kutii ni nini na jinsi mnaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kutii. Lazima mje mbele Yangu zaidi na mshiriki jambo hili, na polepole mtakuja kulielewa, na kwa hiyo kuachilia dhana na uchaguzi ndani yenu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 20” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Wanadamu Hawana Ufahamu wa Mapenzi ya Mungu

Inayofuata:Unajua Kudura Yako Itakuwa Ipi?

Maudhui Yanayohusiana