Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

161 Angalia Mbele Uanzapo Kazi

1

Mvua inanyesha kwa vishindo vidogovidogo nje ya dirisha na kunyunya ardhini.

Mawazo yangu kuhusu nyumbani yanaibuka ghafla akilini na sauti ya matone ya mvua.

Nimekuwa nikikimbia miaka hii yote, je, familia yangu iko sawa?

Je, mama na babangu wameota mvi zaidi?

Je, mwanangu ni mtiifu, ni mrefu kiasi gani sasa?

Nataka sana kupiga simu na kuongea nao.

Lakini serikali ya CCP huchunguza simu na inaweza kutia mbaroni wakati wowote.

Ninaweza tu kuwafikiria kimoyomoyo kwa kimya.

2

Kwa uchungu wangu ninamwomba Mungu na kutafuta ukweli.

Ninauona upendo wa Mungu na utunzaji Wake kwa wanadamu.

Ili kuwaokoa wanadamu, Alijinyenyekeza ili kuwa mwili, kunena maneno.

Yeye huvumilia fedheha kubwa na hupitia dhiki pamoja nasi.

Yeye bado hutulisha na kutunyunyizia kwa bidii licha ya uasi wetu.

Anatumai kuwa hivi karibuni tutaweza kukua katika maisha yetu.

Utawala na mipango ya Mungu ya hatima ya wanadamu ni ya kuaminika na ya haki.

Kila kitu kiko mikononi mwa Mungu, hakuna kitu ambacho hakiwezi kuachwa.

3

Ninaposhikilia maneno ya Mungu mikononi mwangu, nafikiri juu ya upendo Wake.

Kila hatua ninayochukua Mungu huushikilia mkono wangu, akinielekeza mbele.

Wakati ambapo kimo changu ni kidogo maneno ya Mungu yananifariji na kunitia moyo.

Ninapokuwa dhaifu yananipa nuru na riziki ya ukweli.

Ninapokuwa na kiburi Mungu hunipogoa na kunishughulikia, kunifunza nidhamu na kunirudi.

Majaribio yanaponipata maneno ya Mungu hunitia nguvu na hunisaidia kusimama imara.

Kila jambo, kila wakati ninapokua,

kuna upendo na gharama ambayo Mungu amenilipia.

4

Ninapotafakari juu ya maneno ya Mungu, ninaguswa na upendo Wake.

Maneno ya Mungu huhukumu na kuadibu ili kuamsha mioyo ya wanadamu.

Yeye hutuonya kwa uvumilivu, Akisubiri toba na mabadiliko yetu.

Tutaelewa lini juhudi njema za Mungu za kuwaokoa wanadamu?

Hakuna mtu ambaye, baada ya kuanza kazi, na kungalia nyuma, anastahili ufalme wa Mungu.

Kuteseka ili kupata ukweli kuna maana kubwa mno.

Sitaki tena kumfanya Mungu anisikitikie.

Nitaacha mitego yote ya mwili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu.

Nitajitoa kueneza injili ya ufalme wa Mungu.

Nitalipa upendo wa Mungu, nitafikia matarajio ya gharama ya thamani kuu ambayo Amelipa.

Iliyotangulia:Mfuate Mungu kwa Karibu

Inayofuata:Wakati wa Kuachana

Maudhui Yanayohusiana

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  1 Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwen…

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…