Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

326 Vitu Vyote Vyafanywa Upya Kupitia Maneno ya Mungu

1 Ndani ya maneno Yangu, milima hupinduliwa, maji hutiririka kinyumenyume, mwanadamu huwa mtiifu, na maziwa huanza kutiririka bila kusita. Ingawa bahari isiyo tulivu huenda kwa hasira kuelekea mbinguni, ndani ya maneno Yangu bahari za aina hii hutulia kama upande wa juu wa ziwa. Kwa kupunga mkono Wangu kidogo tu, upepo mkali kabisa hutokomea na kutoka Kwangu mara moja, na ulimwengu wa mwanadamu hurejesha utulivu wake mara moja. Lakini Ninapotoa ghadhabu Yangu, milima hutenganishwa mara moja, ardhi huanza kutetemeka mara moja, maji hukauka mara moja, na mwanadamu huzingirwa na maafa mara moja. Kwa ajili ya ghadhabu Yangu, huwa Mimi sisikilizi vilio vya mwanadamu, huwa sitoi msaada ili kujibu vilio vyake, kwani hasira Yangu inapanda.

2 Wakati majira ya machipuko yanaenea kwenye ardhi, Mimi hupeleka mwangaza kwa siri na kimya ulimwenguni, ili, duniani, mwanadamu awe na hisia ya ghafla ya usafi hewani. Mimi huachilia mbubujiko wa mvua juu yao, na viwambo vyao vya masikio vinavunjwa kwa ajili ya mvua na radi wanapolala. Huku wakiwa na hofu, hawana wakati wa kujikinga, na hugubikwa na mvua kubwa. Papo hapo, yote yaliyo chini ya mbingu hufagiliwa katika ghadhabu Yangu yenye hasira. Watu hawalalamiki tena kuhusu mwanzo wa mvua kubwa, na ndani yao wote, uchaji huzaliwa. Kwa sababu ya uvamizi huu wa ghafla wa mvua, idadi kubwa ya watu wanazama ndani ya maji yanayonyesha kutoka mbinguni, na kuwa maiti ndani ya maji.

3 Naangalia dunia nzima na kuona kuwa wengi wanazinduka, kuwa wengi wanatubu, kuwa wengi wanatafuta chanzo cha maji ndani ya mashua ndogo, kuwa wengi wananisujudu Mimi ili kuomba msamaha Wangu, kuwa wengi wameona mwangaza, kuwa wengi wameona uso Wangu, kuwa wengi wana ujasiri wa kuishi, na kuwa ulimwengu mzima umebadilishwa. Kufuatia mbubujiko huu mkubwa wa mvua, vitu vyote vimerudi kuwa jinsi vilivyokuwa katika akili Yangu, na haviasi tena. Kabla ya muda mrefu, ardhi yote imejaa sauti za vicheko, na kila mahali duniani kuna hali ya sifa, na hakuna popote ambapo hapana utukufu Wangu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 16” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Mungu Mwenyewe Akujapo Duniani

Inayofuata:Mungu Arudipo Sayuni

Maudhui Yanayohusiana

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…