Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

6. Mungu Wetu Anatawala Kama Mfalme

Mungu mwenyezi, Baba aishiye milele, Mfalme wa Amani,

Mungu wetu anatawala kama Mfalme juu ya vitu vyote!

I

Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

Mungu aishiye milele, Mfalme wa Amani, Mungu wetu anatawala kama Mfalme juu ya vitu vyote!

Miguu ya Mwenyezi Mungu juu ya Mlima wa Mizeituni, juu ya Mlima wa Mizeituni.

Ni mzuri vipi! Njooni mumsikilize! Sisi walinzi tunapaza sauti zetu juu,

tunapaza sauti zetu juu, tunaimba pamoja, kwani Mungu amerejea Zayuni.

Tumeona kwa macho yetu wenyewe ukiwa wa Yerusalemu!

Tuimbe pamoja nyimbo za furaha, kwani Mungu ametufariji,

Amekomboa Yerusalemu.

Katika macho ya mataifa yote, Mungu ameutoa mkono Wake mtakatifu,

Ameonekana jinsi Alivyo kweli.

Wokovu wa Mungu unaonekana mwisho wa dunia.

II

Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu!

Kutoka mbele ya kiti Chako cha enzi, Roho saba wanatumwa kwa makanisa kila mahali,

wanatumwa kwa makanisa kila mahali, ili kufanya mafumbo Yako yote kufichuliwa.

Unaketi juu ya kiti Chako kitukufu,

Ukitawala juu ya ufalme Wako, Ukiufanya usimame imara kwa haki na uadilifu,

Ukiyafanya mataifa kuinama mbele Yako, kuinama mbele Yako.

Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu! Wewe umefungua ukanda wa wafalme,

ili mbele Yako milango ya miji yao ifunguliwe na kutofungwa kamwe.

Kwani mwangaza Wako umekuja, umekuja, mwangaza Wako wa mtukufu umekuja mbele ukiangaza.

III

Giza linaifunika nchi, watu wamefunikwa na huzuni.

Aa … Lakini Unaonekana, Unaangaza mwanga Wako juu yetu.

Mungu, Unaonekana, Unaangaza mwangaza Wako juu yetu.

Utukufu Wako uko katika udhihirisho wa nafsi zetu.

Mataifa yote yanakuja katika mwangaza Wako,

wafalme wao wanauendea mwangaza uliotumwa na Wewe.

Unainua macho Yako kutazama kando Yako, wana Wako wamekusanyika karibu na Wewe.

Wana Wako wote wanakuja kutoka mbali, mabinti Wako wanakuja pia, wakiwa wamebebwa mikononi Mwako.

Mwenyezi Mungu! Ni upendo Wako mkuu ambao umetushikilia kwa uthabiti.

Ni Wewe unayetuongoza mbele, mbele kwenye njia ya ufalme.

Litukuzwe neno Lako takatifu linalotuchoma tena na tena.

Mwenyezi Mungu! Shukrani ziwe Kwako, sifa Kwako.

Shukrani na sifa, sifa Kwako Wewe.

Acha sisi, na moyo mmoja wa kweli, mtulivu, na mwaminifu,

tukutazame Wewe, tutoe ushuhuda Kwako, tukuinue Wewe, tukuimbie sifa.

Acha sisi tujijenge wenyewe katika muungano wa upatanifu,

ili karibuni tuweze kufanywa wa kufurahisha, wa kufurahisha Kwako.

Tuweze kufanywa wa kufurahisha, wa kufurahisha Kwako.

Mapenzi Yako, bila kuzuiwa, yatendeke juu ya dunia.

kutoka katika "Tamko la Ishirini na Tano" katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Mungu Wetu Anatawala kama Mfalme

Inayofuata:Ngurumo Saba za Radi

Maudhui Yanayohusiana