Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 88. Kulipa Gharama ili Kupata Ukweli ni Muhimu Sana

Sio rahisi kwa vijana kuendeleza kazi; wengi wao hawadumishi mwendo. Ni lazima moyo wako uwe mtulivu, lazima uweze kudumisha mwendo na uwe tayari kutumia muda kwake. Wengine hujiburudisha au kuwachezea wengine, lakini wewe unasema, "Siwezi, sina wakati. Biashara yangu ina shughuli sana. Nendeni mkajiburudishe. Ni lazima niipange biashara yangu.” Unaweza tu kufaulu kwa kushughulika na kujitolea kwa biashara yako. Kwa kweli, hukosi nguvu sasa, wala hukosi ujuzi wa kitaalamu. Ili kuboresha hali yako ya kitaaluma, unaweza kufanya baadhi ya utafiti na ujifunze. Ni yapi zaidi, una msingi huu, akili hii, ujuzi huu maalum; unachokosa kwa kweli ni kutumia wakati na nguvu. Vijana hujifunza kidogo kuhusu mambo ya kitaalamu na huelewa baadhi ya ujuzi, hivyo ni rahisi zaidi kwao kufaulu kuliko ilivyo kwa watu wazima? Nchi zinapomchagua raisi, kuna yeyote wa umri wa miaka 20 au 30 ambaye huchaguliwa? (La.) Mbona hivyo? Hawajahitimu vya kutosha katika uwanja wowote. Hawana tajriba ya kutosha, akili zao hazijakomaa, hawaoni mambo kwa upana; mambo kama ujasiri, umaizi, hekima au uwezo bado hayajakomaa. Zaidi ya hayo, kuna sababu kuu kwa nini mambo yako hivyo, watu wakiwa vijana, huwa na msukumo kuhusu mambo mengi. Na sababu nyingine ni kuwa, watu wakiwa vijana, kuna mambo mengi ulimwenguni ambayo bado hawajapitia au kukumbana nayo hapo awali, kwa hivyo mambo mengi yatakuwa yanawatia majaribuni na kuwavutia. Hilo ni kusema, ni vigumu sana kwa vijana kufaulu katika jambo lolote. Haijalishi kile ambacho umesoma, au kile ulichotaalimikia, ni vigumu kufaulu kwa chochote kizuri au muhimu, kuendeleza kazi, na majaribu ni mengi sana. Kwa jumla, watu katika umri wao wa miaka ya 50, 60, 70 au 80 huwa na tajriba nyingi sana za mambo ya ulimwengu na, kwa jumla, mtazamo wao wa ulimwengu uko imara. Wamepitia mambo katika ulimwengu wa nje kama vile ndoa, kushindwa na vikwazo, na aina zote za majaribu na vivutio, na wameyafaulu. Kwa watu wa umri wenu, karibu umri wa miaka 20, kuna mambo mengi sana katika ulimwengu wa nje ambayo ni maajabu kwenu; mnataka kupitia kila kitu, mnahisi kila kitu kikiwa kipya kwenu na mnapenda sana kujua kila kitu. Huna tajriba yake, hivyo daima iko katika akili yako, unahisi kwamba ulimwengu wa nje katika kupumbaza kwake kote sio lazima uwe mbaya hivyo, na sio lazima uwe wa kutisha sana. Hasa, ndani ya mazingira haya katika jamii, watu katika kikundi cha umri wenu hawana uwezo wa kutambua sawasawa mambo wanayosikia na kuona, na hawajui ni mambo yapi ambayo ni majaribu, au ni mambo yapi yatawaletea huzuni au kuwapotoza. Hivyo, kusema kiasi, vijana ni dhaifu sana kuliko watu wazima na wako katika hatari kuu sana. Kuna mambo machache ambayo watu katika kikundi hiki cha umri hufahamu katika mawazo yao, mambo machache ambayo mioyo yao huelewa na ambayo mioyo yao imejiandaa kwayo, na mambo mengi katika ulimwengu huu yako katika kiwango kisichojulikana na hayajulikani kwao, hivyo kuna mambo mengi ambayo kamwe hawawezi kuelewa kabla wawe na tajriba ya au wakumbane nayo, na kamwe hawawezi kujua mambo haya kwa hakika yanahusu nini. Hivyo, iwapo vijana wako katika mazingira ya kawaida, basi wataona ikiwa vigumu sana kusimama imara. Iwapo umeshawishika kwa miaka kadhaa kanisani, katika mazingira haya yaliyo na ukweli, kwa angalau miaka 8 au 10, basi moyo wako utakuwa umetulia na utakuwa umekita mizizi katika familia ya Mungu. Iwapo hutaweza kutuliza moyo wako katika aina hii ya mazingira, hata hivyo, basi utajipata katika shida na hatari kuu.

Kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wako ndiyo njia sahihi katika maisha, ndiyo sahihi kuchagua na, kwa huruma za Mungu, watu wana fursa hii ya kutekeleza wajibu wa binadamu aliyeumbwa. Kwa watu katika umri mchanga kama nyinyi ambao, inaweza kusemwa, mko katika upeo wa ujana wenu, ili kuweza kutekeleza wajibu wenu ni huruma za Mungu, na pia mnajaribu kushirikiana katika kufanya hivi. Lakini iwapo utadhibitiwa na kuzuiliwa kimakosa na baadhi ya masuala madogo, iwapo huwezi kuendelea kutekeleza wajibu wako na suala hili dogo liathiri wajibu wako, au labda lisumbue wajibu wako au hata kuutamatisha wajibu wako—hii haitakuwa aibu? Hii itakuwa sikitiko, aibu. Hivyo, ni lazima muombe pamoja mara kwa mara na mara nyingi kutulia; msifikirie kuhusu matatizo hayo ambayo hayawahusu au yale ambayo hampaswi kuwa mnafikiri kuyahusu sasa, na mfunge vipengele hivyo vya mioyo yenu. Mngali wachanga na wa miaka michache, kwa hivyo msiwe na wasiwasi sana wa kufikiri kuhusu mambo haya. Mambo makubwa maishani sio ndoa tu, kazi na matarajio ya siku sijazo, au kutulia na kuishi kwa amani. Wala kutokuwa na uvumilivu wa kupata nafasi yako katika jamii sio jambo la pekee. Haya sio mambo ya muhimu zaidi. Mambo muhimu zaidi ni yapi? Hapo awali, ndoa na mazishi yalikuwa mambo makubwa; mambo haya ndiyo makubwa sasa? (La.) Mambo makubwa zaidi ni yapi? (Kwanza, muiheshimu imani ya Mungu ndani yetu, na mtekeleze wajibu na shughuli ambazo binadamu aliyeumbwa anapaswa kutekeleza.) Hili ndilo azimio mnalopaswa kuwa nalo. Sasa mnamwamini Mungu na mnatekeleza wajibu wenu, hivyo maisha yenu yameanza kwa mwelekeo ulio sahihi. Hili ni kuu, na ni sahihi. Hivyo,ni nini mnachopaswa kufanya baada ya hili? Je, mnafahamu? (Weka msingi kwa njia ya kuingia katika maisha.) Hili ni sahihi. Weka misingi yako katika njia ya kutafuta ukweli, hakikisha lengo na mwelekeo wa maisha yako, uruhusu ukweli kuweka msingi katika moyo wako na, kwa njia hii, kwa hakika utakuwa mtu ambaye Mungu huchagua, mtu ambaye Mungu amejalia. Ni lazima kwanza muweke misingi. Misingi yenu sasa bado sio imara. Kamwe msijali kuhusu dhoruba, mpulizo kidogo wa upepo unaweza kuwatingisha wakati wowote, hivyo inaweza kusemwa kuwa bado hamjaweka misingi, na hii ni hatari sana. Wekeni lengo lenu la maisha, wekeni mwelekeo ambao mnatafuta, na muweke njia ambayo ni lazima muifuate katika maisha haya. Wekeni lengo hili na jambo kubwa katika maisha, tulieni kwa miaka, na mfanye kazi kwa bidii, tumieni, fanyeni juhudi na mlipe gharama ya suala husika na kwa lengo hili; msifikiri sasa kuhusu jambo lingine lolote. Mbona hampaswi kufikiri kuhusu jambo lingine lolote? Iwapo utaendelea kufikiri kuhusu mambo hayo mengine, basi suala husika halitakuwa jambo lako kuu, badala yake litakuwa la baadaye. Iwapo bado utaendelea kufikiri kuhusu kupata kazi, kupata pesa nyingi, kutajirika, kupata mahali thabiti pa usalama katika jamii, kupata nafasi yako mwenyewe, na pia kufikiri kuhusu kuolewa na kupata mume au mke, haya ni mambo makubwa mangapi? Na kisha unataka kufikiri kuhusu kupata ujuzi na uwezo katika siku sijazo, jinsi ya kuwa mtu aliyejitokeza, na unataka kusaidia na kukuza jamii katika siku zijazo na kuwapa wazazi wako maisha mazuri. Hutakuwa umechoka? Moyo wako ni mkubwa kiasi kipi? Je, mtu huwa na kiwango kipi cha nguvu katika maisha? Watu huwa na nguvu nyingi zaidi katika miaka yao mingapi, na ni miaka mingapi ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa miaka yao bora zaidi? Katika maisha mazima ya mtu, wakati rahisi zaidi, wakati ambao nguvu yao husitawi zaidi, ni wakati ambapo wako katika miaka yao ya 20, na zaidi kabisa hadi umri wa miaka 40. Katika wakati huu, ni lazima mfahamu ukweli mnaopaswa kuelewa katika imani yenu kwa Mungu, na kisha muingie katika uhakika wa ukweli, mkubali hukumu na kuadibu kwa Mungu na mkubali kusafishwa na Mungu na majaribu—ni nini ambacho lazima mtimize kwa kufanya hivi? Hamtamkana Mungu hata hali iweje—hili ni la muhimu zaidi; kando na hili, haijalishi kitakachowavuta au kuwaburuta, au iwapo baadaye mtaolewa na kupata mume au mke, hamtakata tamaa kuhusu wajibu wenu na kukata tamaa kuhusu vitu ambavyo mwanadamu aliyeumbwa anapaswa kufanya; na zaidi ya hayo, iwapo wakati fulani katika siku sijazo Mungu hatawataka, bado mtaweza kuutafuta ukweli na kutafuta kutembea kwa njia ya kumcha Mungu na kuepuka uovu. Ni lazima mtie bidii kwa vipengele hivi; iwapo mtafanya hivyo, basi hamtaishi miaka hii bure.

Na baadhi ya watu bado wamechanganyikiwa, wakiota siku yote. Wanasema, "Bado kuna muda mwingi kabla ya kazi ya Mungu kufika mwisho. Ni kawaida kula, kunywa, kuoa na kujitolea katika ndoa, na muwe au msiwe na mimi, haileti utofauti wowote." Ni kweli kwamba haileti utofauti wowote ukiwa au usipokuwa nao. Lakini kuna wakati ambao Mungu humuokoa mwanadamu, na wakati ambao ni wa kazi ya Mungu kufikia kikomo, kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza kuokolewa; Yeye anamchukua tu mtu huyo mmoja na kuwaharibu wengine wote—hii ni tabia ya Mungu. Mtu hawezi kuitambua na hawezi kuielewa. Ni watu wangapi walikufa wakati wa Nuhu? Nuhu alikuwa akijenga safina kwa zaidi ya miaka 100, na watu hao wote hawakuwa wametubu. Mwishowe, Mungu alimuokoa Nuhu na familia yake tu ya watu wanane, na baada ya watu hawa wanane kuingia katika safina, ni nini basi kilichotendeka kwa wale wote waliobaki? (Wote waliangamia kabisa.) Wale katika ya wanadamu ambao wameshindwa kuokolewa ni wadudu na mchwa machoni pa Mungu. Huku Mungu akimuokoa mtu, tabia Yake ni yenye huruma, ya kupenda, na ya kuvumilia; lakini kazi ya Mungu ya kumuokoa mtu inapokamilika, Havumilii tena na Yeye huondoa uvumilivu wake, na ni ghadhabu na uadhama wake tu ambayo hubaki. Nyakati hizi mnazoishi sasa kwa kweli ni nyakati nzuri sana. Katika wakati huu ambao kazi ya Mungu ni muhimu zaidi, mko tu katika umri unaofaa, mliweza kuupata na nyote mnaweza kutekeleza wajibu wenu. Haijalishi ni taaluma gani mlizosomea, kile ambacho mmemudu au ni ujuzi upi maalum mlionao, kwa njia ya taaluma zenu wenyewe maalum mumekuja katika nyumba ya Mungu kutekeleza wajibu wenu. Hii ndiyo huruma ya Mungu na ni fursa ambayo haiji kila siku. Matendo ya Mungu hayapendelei yeyote. Ni Mwenye huruma kwako na Hukuruhusu kufurahia baraka hii, sio ili uweze kutosheleza mwili wako na sio ili uweze kuishi maisha ya kutosheka na kutofanya juhudi zozote za kuendelea. Haijalishi ni aina gani ya njia Mungu atakupa, haijalishi jinsi Alivyo mwenye huruma kwako, mwishowe ana mapenzi haya tu, ambayo ni wewe kuelewa ukweli, ili uweze kuyaelewa mapenzi yake na kuelewa ukweli katika mazingira haya ambayo yanafaa kwa ukuaji wako. Maneno ya Mungu na ukweli wa Mungu huletwa kwako na yanakuwa maisha yako, na unaweza kumtii na kumuogopa Mungu. Licha ya umri wako mchanga, azimio lako ni kuu, kama yalivyo maisha yako, shauku lako na moyo wako wa kumuogopa Mungu. Basi hili ni kuu, na Mungu ameridhika. Mungu angesema kuwa huruma Zake kwako si za bure. Mungu huvuna mavuno, huzaa matunda na huona matokeo pamoja na wewe; gharama ambayo Yeye hulipa si bure. Mungu anafurahi na ana raha kuona hilo. Huu ni ukuu na mpango wa Mungu, kwa hiyo ni jambo ambalo mtu anaweza kuchagua?

Gharama ambayo Mungu hulipia kila mmoja wenu haijakuwa tu miongo iliyopita tangu mzaliwe. Haijakuwa miongo hiyo tu. Kama Mungu anavyoona, umekuja katika ulimwengu huu mara nyingi na umepata mwili tena mara nyingi. Je, ni nani anayehusika na suala hili? (Mungu.) Mungu ndiye anayehusika nalo, hivyo unafahamu nini kulihusu? Hujui chochote kulihusu. Kila unapokuja ulimwenguni, Mungu hupanga kila kitu Yeye Mwenyewe. Hupanga miaka utakayoishi, aina ya familia utakayozaliwa ndani, utakapooa na kutulia katika ndoa, utakachofanya ulimwenguni, utakachotegemea kuishi, na Mungu hukufungulia njia ili uweze kukamilisha kazi yako katika maisha haya bila tatizo. Wakati unaofuata unapopewa jukumu ulimwenguni, Mungu hutimiza mipango Yake kwa ajili ya maisha yako kulingana na mipango unayopaswa kuwa nayo na ambayo anapaswa kukutengenezea. Hivi tu, Hukupangia mambo mara nyingi sana na, mwishowe, unazaliwa katika enzi hii ya siku za mwisho na unazaliwa katika aina hii ya familia, na Mungu anakuruhusu uende sambamba na kazi yake, umsikize Akizungumza na kuisikia sauti Yake, na hivyo umeishi hadi sasa. Hujui umekuja ulimwenguni mara ngapi, ni mara ngapi ambapo umbo lako limebadilika, umeishi katika familia ngapi, ni enzi ngapi na ni koo ngapi umepitia. Mkono wa Mungu umekushikilia kila mara na Mungu amekulinda kila mara. Ni kiwango gani cha juhudi ambacho Mungu anapaswa kutumia kwa mtu! Baadhi ya watu husema, "Nina umri wa miaka 60, hivyo Mungu ametumia miaka 60 kwangu, Amenitunza na kunilinda kwa miaka 60 na kudhibiti hatima yangu kwa miaka 60.” Je, hili si jambo la ujinga kusema? Si suala la maisha ya wakati mmoja tu ndio Mungu hudhibiti hatima ya mtu na kumtunza na kumlinda. Iwapo lingekuwa suala la maisha ya wakati mmoja, la kipindi kimoja tu cha maisha, basi Mungu hangekuwa Mungu na hangekuwa na aina hii ya mamlaka au uwezo, na haingesemwa kuwa Mungu hutawalavitu vyote, kuwa hutawala kila kitu. Juhudi ambazo Mungu hufanya na gharama ambayo huwa Anakulipia sio tu kupanga vitu ambavyo unafanya katika maisha haya. Yeye hutenda kwa mwoyo na hutenda kwa kutumia maisha Yake Mwenyewe kama gharama, Akiongoza kila mmoja na kupanga maisha yote ya kila mtu. Hivyo, tukizingatia juhudi ambazo Mungu hufanya na gharama ambayo Yeye hulipa kwa niaba ya mwanadamu, na pia ukweli wote na maisha ambayo Yeye humpa mtu, iwapo watu hawatatimiza wajibu wa mtu aliyeumbwa katika nyakati hizi za mwisho na iwapo hawatamrudia Muumbaji, basi haijalishi ni maisha mangapi au ni enzi ngapi watakazoishi, si wao ndio watakuwa wamepoteza? Je, si watakuwa hawastahili gharama ambayo Mungu huwalipia? Hawastahili kabisa gharama anayowalipia Mungu. Kwa hivyo, katika maisha haya—Sizungumzi kuhusu maisha yoyote yaliyopita, lakini katika maisha haya—iwapo kwa ajili ya kazi yako mwenyewe huwezi kuacha vitu unavyopenda au iwapo huwezi kuacha vitu hivi vya nje—vitu hivi vya raha na maisha ya familia—iwapo huwezi kuacha vitu hivi kwa ajili ya gharama ambayo Mungu hukulipia au kulipa upendo wa Mungu, basi hakuna jambo lolote zuri kukuhusu kabisa! Kwa kweli kila gharama unayolipa inastahili. Ikilinganishwa na gharama ambayo Mungu hulipa kwa niaba yako, kiwango hicho kidogo unachotoa au unachotumia hufikia kiwango kipi? Kuteseka kwako hafifu hufikia kiwango kipi? Je, unajua Mungu ameteseka kwa kiwango kipi? Kuteseka hafifu ambako huwa unavumilia hakufikii kiwango chochote. Zaidi ya hayo, sasa unatimiza wajibu wako na unapata ukweli, hivyo mwishowe ni wewe utakayekuwa umebaki. Wakati huu, haijalishi iwapo utateseka au kulipa gharama, kwa hakika unashirikiana na Mungu, na unafanya chochote ambacho Yeye hukwambia ufanye kwa kuyatii maneno Yake; tenda kulingana na maneno Yake, usimkaidi Mungu, na usifanye chochote kinachomhuzunisha Yeye. Unaposhirikiana na Yeye, ni lazima uteseke kwa kiasi fulani na uache baadhi ya vitu, kuacha na kutoa baadhi ya vitu—kuacha umaarufu na faida, vyeo, mali na raha za dunia, hata ndoa, kazi na matarajio yako ya baadaye ya kilimwengu. Je, Mungu anajua unapoacha vitu hivi? Je, Anaweza kuona? (Ndio.) Na Anapoona hili, Atafanya nini? (Mungu anapendezwa. Mungu anafurahi.) Mungu hachukui tu mtazamo, Yeye huchukua hatua, la sivyo, matakwa Yake kwa mwanadamu hayangekuwa na maana. Yeye hafurahi tu, Akisema, “Gharama Niliyolipa inaonyesha matokeo. Mtu huyu yuko tayari kushirikiana na Mimi na ana azimio hili. Nimempata mtu huyu.” Kama Mungu amefurahi, Ameridhika au Anahisi kufarijika, huwa hachukui tu aina moja ya mtazamo—huwa Anachukua hatua. Huruma za Mungu kwa mwanadamu, upendo Wake kwa mwanadamu, rehema Zake kwa mwanadamu zote sio aina ya mtazamo tu; ni ukweli. Ukweli gani? Mungu huyaweka maneno Yake ndani yako ili uweze kupata nuru dani mwako, ili uweze kuona kupendeza kwa Mungu, ili uweze kuona kabisa jinsi ulimwengu ulivyo, ili moyo wako uweze kuchangamshwa na hivyo uweze kuyaelewa maneno ya Mungu na uelewe ukweli. Basi, si umepata kile ambacho unapaswa kupata? Hii sio tu aina ya mtazamo wa Mungu, ni mtazamo tu? Je, umepata nini? (Ukweli.) Umepata kile ambacho ni cha thamani zaidi. Mungu anapoona kuwa ni vyema, huwa Anachukua mtazamo fulani. Wakati huohuo wa kuchukua mtazamo, Yeye pia Huchukua hatua, kama tu vile watu husema, “Huwezi tu kuchukua mtazamo, ni lazima pia uchukue hatua fulani ya kiutendaji.” Watu husema, "Siutaki. Sitaki chochote. Sitaki chochote cha Mungu." Na Mungu husema, “Haikubaliki. Ni lazima Nikupe zawadi—hiki ndicho unachostahili.” Hivyo unapata faida. Unapata nini? Unapata ukweli, unapata maisha, unapata maarifa ya Muumbaji—basi bado ungali mtupu ndani? Je, hujatajirishwa ndani yako? Na mara unapotajirishwa ndani, basi si unaishi maisha ya thamani?

Ayubu aliomba ng'ombe na kondoo waliokuwa kote milimani, au utajiri mkubwa wa familia? (La.) Aliomba nini? Kumcha Mungu na kujiepusha na uovu. Kulingana na Mungu, Mungu alisema kwamba aliona ni vyema, na basi mwishowe Alifanya nini? Je, Alinena maneno hayo machache tu na kisha huo ukawa mwisho? Mungu alichukua hatua; Alichukua hatua gani? Mungu alimtuma Shetani kumjaribu Ayubu, na kuchukua ng'ombe na kondoo wake waliokuwa kote milimani, mali na vitu vyake, watoto wake na wafanyakazi wake, na haya yalikuwa majaribio ya Mungu kwa Ayubu. Mungu alitaka nini kwa kumfanya Ayubu kupitia majaribio haya? Mungu alitaka ushuhuda wa Ayubu. Na Mungu alimpa Ayubu nini wakati huo? Watu wanafikiri, “Mungu alimpa Ayubu nini wakati huo? Ng'ombe na kondoo wake wote walichukuliwa. Hakumpa Ayubu chochote.” Hapa kuna kitu alichopewa Ayubu, na kulikuwa na zawadi, na bado hakuna anayeweza kuona wazi zawadi ambayo Mungu alimpa Ayubu. Mungu alitaka ushuhuda wa Ayubu hivyo Mungu alimpa Ayubu zawadi ya fursa; Hii ilikuwa fursa gani? Ilikuwa Ayubu awe na ushuhuda wa Mungu mbele ya Shetani na mbele ya wanadamu wote, kuwa shahidi kwa ukweli kwamba Ayubu alimcha Mungu na kujiepusha na uovu, na kuwa shahidi kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu na mwaminifu. Hiki ndicho Mungu alimpa Ayubu? Iwapo Mungu hakumpa Ayubu fursa hii, Shetani angethubutu kusonga dhidi yake? Hakika Shetani hangethubutu, na hii ni hakika asilimia 100. Na iwapo Shetani hangethubutu kumjaribu, bado Ayubu angekuwa na fursa hii? Hangekuwa na fursa hii. Hivyo, Mungu alimpa Ayubu aina hii ya fursa ili kuthibitisha kwa umati kuwa njia aliyoifuata Ayubu—njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na uovu—ilikuwa njia sahihi, kwamba ilikuwa inakubalika kwa Mungu na kwamba Ayubu alikuwa mtu mwaminifu na mkamilifu. Umati uliona haya yote, Mungu aliona haya, na Ayubu alichukua fursa hii na hakumsikitisha Mungu; alikuwa shahidi wa Mungu, alimpiga Shetani, akamshinda Shetani na Mungu aliona kwamba ilikuwa vyema. Hivyo, mwishowe, Mungu alimpa Ayubu chochote kama zawadi? (Ndio.) Ni nini kilichokuwa zawadi ya pili ya Ayubu kutoka kwa Mungu? Mungu alisema kwamba Ayubu alimcha Mungu na kujiepusha na uovu na alikubaliwa na Mungu, kwamba Ayubu alikuwa shahidi wa Mungu mbele ya Shetani, na kuwa kila alichoamini kilikuwa kizuri, na Mungu alipendezwa na kufurahi, na Alichukua aina hii ya mtazamo. Je, Mungu hakuchukua hatua nyingine zaidi baada ya kuuchukua mtazamo huu? Mungu alifanya nini? Hamkifahamu sana kitabu cha Ayubu. Ni katika hali zipi ambapo Ayubu alisema, “Nimesikia habari zako kwa kusikia kwa masikio: lakini sasa macho yangu yanakuona” (Ayubu 42:5)? (Baada ya Mungu kunena na yeye.) Mungu alinena na yeye na kufichua mgongo Wake kwa Ayubu. Je, hii haikuwa zawadi ya Ayubu kutoka kwa Mungu? Kuna yeyote ambaye alikuwa amewahi kumuona Mungu kabla ya Ayubu? Hakuna aliyekuwa ameiona nafsi halisi ya Mungu hapo awali, ikijumuisha mgongo wa Mungu. Ayubu aliuona mgongo wa Mungu na kuisikia sauti yake, na hiki si kitu ambacho mtu aliyeumbwa hutamani sana kukipata? Ayubu alipata hili, hivyo mnamuonea wivu? (Ndio.) Ni vigumu kupata hili, sivyo? Hivyo ni vipi ambavyo mtu anaweza kupata fursa hii, huruma hii na zawadi hii? Ni lazima uwe na ushuhuda wa Mungu; Ni lazima uwe shahidi wa Mungu miongoni mwa majaribu ya Shetani, ni lazima utembee katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na uovu na ni lazima usimame mbele za Mungu na umfanye kusema kuwa Anachoona ni chema na umfanye Apendezwe na kufurahi. Anapoona kuwa kila unachofanya ni kizuri na ushuhuda wako ni mzuri, Anaposema umekamilika, kuwa wewe ni mtu anayetafuta ukweli, basi utapata haya yote. Baada ya Ayubu kuuona mgongo wa Yehova, zawadi ya Mungu iliishia pale? Mungu alifanya nini baada ya hayo? Alimbariki Ayubu na mali nyingi zaidi kuliko aliyokuwa nayo hapo mbeleni, sivyo? Hivyo ni kusema, alikuwa mwenye mali kuliko mbeleni. Sema kwanza alikuwa kama milionea, hivyo sasa alikuwa labda zaidi ya bilionea. Unaona, kwa mtu anayemcha Mungu na kujiepusha na uovu, kuwa bilionea ni kitu rahisi kutimiza. Hizi ndizo huruma za Mungu!

Kile ambacho Mungu humpa mwanadamu huzidi kile ambacho anaomba au kutamani, lakini iwapo utapenda kupata zawadi inayozidi unachoomba au kutamani, basi lazima uifuate njia ya Mungu. Sio suala rahisi kuifuata njia ya Mungu—ni lazima ulipe gharama. Hata hivyo, gharama hii hailipwi bure—unafidiwa. Watu hufikiri kila mara kuwa Mungu huchukua tu aina ya mtazamo kwao, kuwa Hafanyi chochote, lakini Yeye tu hukaa mahali pamoja kila wakati, Akichunguza na kutazama. Hivi ndivyo ilivyo kweli? La, sivyo. Mungu ni kama mzazi kwa mwanadamu. Unawasikiliza wazazi wako, unakuwa na tabia njema, unatekeleza wajibu wako mzuri, na unateseka sana kutembea katika njia sahihi. Kwa hiyo hilo huwafanya wazazi wako kuhisi vipi? Mioyo yao huvunjika kwa upendo, na wangetoa maisha yao kwa ajili yako ili kupunguza kuteseka kwako, kukufanya ule vyema, uvae nguo nzuri na ujifurahishe. Hawataki uteseke kutokana na umaskini wowote. Huu ndio moyo walio nao wazazi wako. Na ikilinganishwa na hii, moyo wa Mungu unaweza kuwa hata mwema zaidi, wa kupendeza zaidi, mzuri zaidi. Moyo wa Mungu hauwezi kuwa chini ya hii. Kuhusu kikundi chenu cha umri, je, hamuwezi kushukuru kwa ajili ya baadhi ya vitu vingine vizuri ambavyo wazazi wenu huwafanyia? Kwa hiyo zaidi ya yote, tumia utunzaji wa wazazi wako kwako kuushukuru moyo wa Mungu. Kwa mfano wakati wewe ni mgonjwa na unalala kitandani, wazazi wako huhisi vipi? Hawahisi kwenda kazini, na iwapo huwezi kula pia wao hawawezi. Kabla ya wewe kuweza kutembea au kutambaa, walikushikilia kila usiku. Wakati ambapo hungeweza kula hata chembe cha chakula, walikulisha kutoka kwa kinywa chao wenyewe; hii ndiyo aina ya moyo walio nao. Ulipokua na kuweza kutembea, kila wakati walikuwa wakiogopa kwamba ungegongwa na vitu. Ulipofanya hivyo, mioyo yao ilivunjika kwa upendo, na wangekusugua pale ulipogongwa na kupigapiga sakafu na kukubembeleza. Iwapo ulilia, mioyo yao ilivunjika. Iwapo uliteseka kutokana na kosa lolote, wangekuwa tayari mara moja kupigana vita vyako. Unapokua na wanakuona ukiteseka, au wakuone ukiwa umechoka kutoka kazini, wako na hamu ya kukaa na wewe siku yote, bila kula au kunywa chochote wao wenyewe, kuwa karibu na wewe na kukupikia, kufua nguo zako, kukutumikia, kuwa mjakazi wako, kutuliza mateso yako, na hata kutamani kuwa wangeteseka kwa niaba yako; huu ndio moyo walio nao. Na iwapo wazazi wanaweza kuwa hivi kwa watoto wao, basi Mungu anaweza kuwa zaidi vipi kwa wanadamu? Mungu anaweza tu kuwa mkubwa zaidi, halisi zaidi. Hawezi kuwa chini ya jinsi wazazi walivyo kwa watoto wao, kwani kwa kawaida kutakuwa na vitu kwa watu ambavyo watu wengine hawawezi kuvishughulikia, ilhali Mungu hushughulikia watu kwa kila njia iwezekanayo. Wazazi wako walikuzaa na hukuchukulia kama mwili na damu yao wenyewe. Wanakupenda, wanakutunza na kukulinda sana. Kwa hiyo Niambie, mwanadamu ni nani kwa Mungu, kama mwanadamu aliumbwa kwa mikono Yake Mwenyewe? Mtu ni mwili na damu ya Mungu Mwenyewe. Ingawa si kama hali ya mtu pale ambapo watoto wameunganishwa na wazazi wao kupitia kuzaliwa kwa mwili na damu na kwamba Mungu hutumia mkono Wake kumuumba mwanadamu, ni kwamba Mungu anapumua pumzi Yake ndani ya mwanadamu, na Anaweka matarajio Yake kwa mwanadamu. Hili ni kusema, mwanadamu amepewa matumaini ya Mungu, Mungu ana matakwa kwa mwanadamu na Huweka imani Yake kwake. Sio suala rahisi sana kwa kuwa Mungu anamuumba mwanadamu na kupumua pumzi Yake ndani ya mwanadamu, na kwa hali yoyote Mungu ni Mwenye uwezo sana, kwa hiyo iwapo Hakutaka wanadamu hawa, basi Angeumba wengine tu. Baada ya kuwaumba wanadamu, Aliwaweka katika moyo Wake. Wanadamu ni nyama na damu Yake na ni wenza Wake; pia wao ndio walioaminiwa na wanaobeba matumaini yote ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi, na mwishowe Anataka kuona matumaini na kupata matokeo kutoka kwa wanadamu. Kwa kuzingatia dhana hii, jaribuni kuthamini matakwa na mapenzi ya Mungu, na basi hamtakuwa na kuthamini kwa kina zaidi)? Hebu tuchukue mfano. Ili kumweka mtoto wao shuleni na kujipatia sifa, mtoto wao anaposoma, wazazi wako hapo kando yake wakimfukuta, kisha kumpa shira, kisha faluda ya mayai iliyotiwa mvuke, kisha kukwaruza mwasho wake, kisha kuwakanda. Hawajui cha kufanya kwa matokeo bora. Mioyo yao huwa naye kila wakati, na ulimwengu wao humzunguka. Ulimwengu wa wazazi wako hukuzunguka, na je, hawaweki matarajio kwako na kukuamini na matumaini yao? Iwapo huwasikilizi na huwatii kila wakati, je, hawahuzuniki? Je, hawasikitiki? Hivyo basi, kwa kutumia wazo hili, fikiria kuhusu moyo wa Mungu. Mungu huona wanadamu na, haijalishi jinsi ulivyo mzee, nyote ni watoto machoni pa Mungu. Unasema una miaka 80 na Mungu anasema wewe bado ni mtoto. Unasema una miaka 20 na Mungu anasema wewe hata ni mtoto zaidi. Mungu hatofautishi kati ya umri; machoni Pake wanadamu wote ni wachanga, wote ni watoto, na hivi ndivyo Yeye huwachukulia wanadamu. Kwa hivyo, machoni pake, wewe ni mwili na damu Yake, mwenzi Wake. Kwa hiyo unawezaje kustahili kuwa mwili na damu Yake, mwenza Wake, muwe watu wanaopendeza roho Yake na kumridhisha? Je, hili si swali ambalo wanadamu wanastahili kulizingatia na kulitafakari?

Mungu huchukulia wanadamu kuwa mwili na damu Yake, kama wenza Wake, kama wanaobeba gharama iliyo na uchungu ambayo Mungu hulipa, hivyo Mungu ana moyo wa aina gani? Mungu ana hali gani ya akili na Mungu ana aina gani ya mtazamo kwa watu hawa ili Aweze kuwa na kiwango hiki cha uhusiano nao? Mungu ana moyo gani Anapokuwa na kiwango hiki cha uhusiano? Je, watu wanaweza kuuthamini kikamilifu? Mtu anaweza kusema, “Sijamuona Mungu, na siwezi nikatambua chochote ambacho Mungu amenifanyia katika maisha yangu machache yaliyopita.” Lakini unaishi sasa, kwa hiyo unaweza kutambua mwongozo wa Mungu na gharama Anayokulipia sasa? Unaweza kuelewa hili? (Ndio.) Ni sawa iwapo unaweza kuelewa hili, na hili linathibitisha kuwa wewe si mjinga. Inatosha kuweza kuyaelewa haya yote, na inastahili kabisa kuacha kila kitu na kumfuata Mungu.

Iliyotangulia:Sura ya 62. Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa Wengine

Inayofuata:Sura ya 91. Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu