Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

603 Watu Hawatilii Maanani Uwepo wa Mungu

1 Kila siku Natazama juu ya uso wa ulimwengu, na kila siku Nafanya kazi Yangu mpya kati ya mwanadamu. Ilhali watu wote “wanafanya kazi kwa kujitolea,” na hakuna anayetilia maanani mienendo ya kazi Yangu ama kugundua hali ya vitu zaidi ya wao wenyewe. Ni kana kwamba watu wanaishi katika mbingu mpya na dunia mpya waliotengeneza wenyewe, na hawataki mtu mwingine kuingilia kati. Wote wameshiriki katika kazi ya kujifurahisha, wanajitamani wakifanya “mazoezi ya kimwili.” Kweli hakuna mahali Pangu katika moyo wa mwanadamu? Mimi hakika sina uwezo wa kuwa mtawala wa moyo wa mwanadamu? Roho ya mwanadamu kweli imemwacha? Nani amewahi kuyatafakari kwa makini maneno kutoka kwa mdomo Wangu? Nani amewahi kutambua ombi la moyo Wangu? Je, moyo wa mwanadamu kweli umechukuliwa na kitu kingine? Wakati mwingi sana Nimepaza sauti Nikimwita mwanadamu, lakini je, kuna yule ambaye amehisi huruma?

2 Mara nyingi Nimevunjwa matumaini na mwanadamu, mara nyingi Nimekasirishwa na utendaji kazi wake duni, na ni mara nyingi Nimesikitishwa na unyonge wake. Mbona Siibui hisia ya kiroho katika moyo wa mwanadamu? Mbona Siuvutii upendo katika moyo wa mwanadamu? Mbona mwanadamu hataki kunichukulia kama kipenzi chake? Je, moyo wa mwanadamu sio wake mwenyewe? Je, kitu kingine kimechukua makao katika roho yake? Mbona mwanadamu anaomboleza bila kukoma? Ni kwa nini yeye ana taabu? Mbona, wakati yuko na huzuni, hajali uwepo Wangu? Je, Mimi humdunga kisu? Je, Nimemwacha kwa kupenda Kwangu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 25” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Asili Yako ni Potovu Sana

Inayofuata:Kuwa na Hekima na Utii Mipangilio Yote ya Mungu

Maudhui Yanayohusiana