1. Kwa nini serikali ya CCP hukandamiza na kumtesa vikali Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Hiki ni kizazi kibaya” (Luka 11:29).

“Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1Yohana 5:19).

“Na hii ndiyo shutuma, ya kwamba mwanga umekuja duniani, na wanadamu walipenda kiza badala ya mwanga, kwa kuwa vitendo vyao vilikuwa viovu. Kwa kuwa kila mtu afanyaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwa mwanga, vitendo vyake visije vikashutumiwa” (Yohana 3:19-20).

“Na hilo joka kubwa likarushwa nje, yule nyoka mzee, anayeitwa Ibilisi, na Shetani, ambaye analaghai dunia nzima” (Ufunuo 12:9).

Maneno Husika ya Mungu:

Udhihirisho wa joka kuu jekundu ni upinzani Kwangu, ukosefu wa ufahamu na utambuzi wa maana ya maneno Yangu, mateso ya mara kwa mara Kwangu, na kutafuta kutumia njama ili kuzuia usimamizi Wangu. Shetani anadhihirika kama ifuatavyo: kupambania mamlaka na Mimi, kutaka kuwamiliki watu Wangu wateule, na kutoa maneno hasi ili kuwadanganya watu Wangu. Udhihirisho wa ibilisi (wale ambao hawalikubali jina Langu, ambao hawaamini, wote ni mapepo) ni kama ifuatavyo: kupenda raha za mwili, kujiingiza katika tamaa mbaya, kuishi chini ya utumwa wa Shetani, wengine kupinga na wengine kuniunga mkono (lakini kutothibitisha kwamba wao ni wana Wangu wapendwa). Udhihirisho wa malaika mkuu ni kama ifuatavyo: kuzungumza kwa kiburi, kuwa asiyemcha Mungu, mara nyingi kuchukua sauti Yangu kuwahubiria watu, kuzingatia tu kuniiga kwa nje, kula kile Ninachokula na kutumia kile Ninachotumia; kwa ufupi, kutaka kuwa sawa na Mimi, kuwa mwenye tamaa ya makuu lakini kukosa ubora Wangu na kutokuwa na maisha Yangu, kuwa bure. Shetani, ibilisi, na malaika mkuu ni maonyesho ya mfano hasa wa joka kuu jekundu, kwa hiyo wale ambao hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi wote ni watoto wa joka kuu jekundu: Hiyo ni hivyo kabisa! Hawa wote ni adui Zangu. (Hata hivyo mivurugo ya Shetani haihusishwi. Ikiwa asili yako ni ubora Wangu, hakuna mtu anayeweza kuibadilisha. Kwa sababu sasa bado unaishi katika mwili, mara kwa mara utakabiliwa na majaribu ya Shetani—hii haiwezi kuepukika—lakini lazima daima uwe makini.) Kwa hiyo, Nitawaacha watoto wote wa joka kuu jekundu nje ya wazaliwa Wangu wa kwanza. Asili yao haiwezi kubadilika daima, nao ni ubora wa Shetani. Ni ibilisi wanayemdhihirisha, na ni malaika mkuu wanayeishi kwa kumdhihirisha. Hii ni kweli kabisa. Joka kuu jekundu Ninayezungumzia si joka kuu jekundu lolote fulani; badala yake ni pepo mbaya anayenipinga Mimi, ambaye kwaye “joka kuu jekundu” ni kisawe. Hivyo roho zote nje ya Roho Mtakatifu ni roho mbaya, na zinaweza pia kusemwa kuwa ni watoto wa joka kuu jekundu. Haya yote yanapaswa kuwa wazi kabisa kwa kila mtu.

Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 96” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[1] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[2] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliyepo katika utumwa bila heshima amemfanya Mungu mtumwa—hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani. Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini usimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini usababishe matamanio makubwa kiasi hicho kwa Mungu? Kwa nini umfanye Mungu kuita tena na tena? Kwa nini umlazimishe Mungu kuwa na wasiwasi kwa sababu ya Mwana Wake mpendwa? Katika jamii hii ya giza, kwa nini mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba?

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Bora[a] vimepeleka fikira za mwanadamu na mawazo yake katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Kwa ukosefu wa kujua wa mwanadamu, mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje ya moyo wake na kuumiliki yeye mwenyewe kwa furaha ya ushindi tangu wakati huo, mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na uso wa mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa tena hata na chembe ya uhuru na hakuwa na njia ya kujikwamua kutokana na taabu za mfalme wa mashetani. Hakuwa na budi ila kuchukuliwa mateka papo hapo, kujisalimisha na kuanguka chini kwa kutii mbele yake. Hapo zamani, wakati moyo na nafsi ya mwanadamu vilikuwa vichanga, mfalme wa mashetani alipanda ndani yake mbegu ya saratani ya ukanaji Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuwa na kuhisi aibu yoyote au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Kuna wale hata wanaofoka kauli kama zifuatazo, kauli ambazo hazifai kutamkwa. “Mwanadamu alitoka kwa nyani katika nyakati zilizopita, na dunia leo inatoka kwa mfululizo wa jamii zizizostaarabika kuanzia takribani miaka mingi isiyohesabika. Iwapo nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Kwa nyuma, inamfanya mwanadamu kuning’iniza kwenye ukuta au kuweka kwa meza ili kutoa heshima na kumtolea sadaka. Wakati huo huo anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[3] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[4] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa,[5] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutaleta kutimia kwa matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyoovyo? Amemharibu mwanadamu kwa kiwango kama hicho mwanadamu hajui ’mahali pa raha zote, na amekuja kuwa mfu na asiye na hisia. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusitoe nafsi zetu zote kumwangamiza yeye na kumchoma ili kuondoa kabisa hofu yote ya hatari ya siku zijazo na kuruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa mapema? Genge hili la waovu limekuja katika dunia ya wanadamu na kusababisha hofu na shida kubwa. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kumeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda.[6] Hiyo kwa vyovyote vile ni rahisi! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu Aliibuka mshindi muda mrefu uliopita, Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kutoka juu hadi chini na kutoka mwanzo hadi mwisho, Shetani amekuwa akivuruga kazi ya Mungu na kutenda katika upinzani Kwake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[7] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu ya furaha ya kutamanisha, wakati mfalme wa mashetani ameendelea kucheka vibaya, kana kwamba njama zake za kupotosha zimefanikiwa. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani, kwa kishindo, kuangamiza kila kitu kuhusu Mungu, na kwa mara nyingine kuchafua na kumwangamiza; nia yake ni kubomoa na kuvunja kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” na kazi yake miongoni mwa wanadamu ulimwenguni? Anawezaje kumruhusu Mungu kuufichua uso wake wa kutisha? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya mahakama yake ya kifalme duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai![8] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemchezea mwanadamu sana kiasi kwamba mwonekano wake umekuwa ule wa mnyama wa mashambani, mbaya sana, na kutoka athari ya mwisho ya mwanadamu asilia imepotea. Aidha, wanatamani kuwa wa nguvu za ukuu duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu kiasi kwamba isiweze kusonga mbele kiasi kidogo na wanamfunga mwanadamu kwa mkazo kama wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi mbaya sana na kusababisha majanga mengi sana, je, bado wanatarajia kitu tofauti na kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha!

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.

Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake maovu. Kati ya vitendo vyote vya maovu ambavyo Shetani ametekeleza kwa binadamu—kutoka kwa jitihada zake za mapema za kudanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, hadi ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kutambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua hali halisi ya uovu wa Shetani; hakuna hata moja inayoshindwa kuthibitisha hoja kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata moja hushindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inasalimisha maovu yake, inadumisha maendelezo ya vitendo vyake vya maovu, inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Wao ni katili kwa Mungu, na ndio wale ambao hasira ya Mungu itaangamiza. Ingawaje Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake kali ni mbinu ya kutoa nje asili yake mbovu. Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa.

Kimetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

1. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.

2. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

3. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.

4. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.

5. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.

6. “Pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda” ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.

7. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.

8. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”

a. Vitabu Vinne na Maandiko Matano Boara ni vitabu vyenye mamlaka ya Ukonfushashi nchini China.

Iliyotangulia: 5. Matokeo ya mtu kuwa chini ya uongo na udhibiti wa Mafarisayo na wapinga Kristo wa dunia ya dini, na iwapo anaweza kuokolewa

Inayofuata: 2. Sababu ya ulimwengu wa kidini daima kumkana, kumkataa na kumhukumu Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Tofauti muhimu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu

Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki