Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

144 Naahidi Maisha Yangu Kumfuata Kristo

1 Bara China, ambapo mapepo wa serikali ya China hushika mamlaka, kwa kweli ni mahali pa giza na hofu. Ninahubiri na kushuhudia kuonekana na kazi ya Mungu, lakini nawindwa na serikali. Mara nyingi mimi husikia sauti za ving’ora vya polisi, na huwa katika hatari ya kukamatwa na kufungwa kila wakati. Uchina ni kasri la mapepo, ambapo Shetani anashikilia madaraka; haina mahali pa usalama kwa Wakristo. Ni lini nitaweza kukusanyika na kutekeleza wajibu wangu kwa kawaida, na kusiwe tena na haja ya kujificha kutoka kwa polisi kuepa kukamatwa? Ni lini nitaweza kusoma maneno ya Mungu kwa amani, na kuacha kulazimika kuishi kama mzururaji? Hii “uhuru wa kidini na haki ya kuishi” ni nini? Ni upuuzi tu wa kudanganya wa mfalme wa ibilisi. Ni nani katika ulimwengu huu mpana anayejua mateso wanayopitia Wakristo wa China?

2 Nina bahati namna gani kuwa nimekutana na kuonekana na kazi ya Mungu, lakini nawindwa na kukandamizwa na joka kubwa jekundu, nikilazimishwa kuondoka nyumbani kwangu na kuwatamani sana wapendwa wangu. Nawadharau mapepo wa serikali ya China kwa ukatili wao. Nikikabiliwa na mateso, ugumu na majaribu, naona wazi sura za kutisha za mapepo hawa. Njia ya mbinguni ni ngumu, iliyojaa milima na mabonde—lakini kuwa na Mungu pamoja nami huupa moyo wangu amani. Katikati ya shida, nafurahia upendo wa Mungu; nikifikiria neema Yake, kuna utamu moyoni mwangu. Kwamba nimeepuka mara kwa mara kutoka kwenye koo la chui ni kwa sababu kabisa ya Mungu kunijali na kunilinda kwa siri. Katikati ya hatari ya kudumu na shida, maneno ya Mungu yameimarisha imani yangu. Kwa kuona kwamba Mungu ni mwenye kudura, na Anatawala vyote, nimeazimia hata zaidi kumfuata.

3 Nimekuwa na mateso ya kutosha kutokana na kuadhibiwa na serikali ya China; hili linaonyesha kuwa mimi ni mdogo sana wa kimo. Katikati ya majaribu na usafishaji, mwili wangu ni dhaifu; nafichua uhasi mwingi na malalamiko mengi. Hata hivyo, kwa wakati unaofaa, maneno ya Mungu yananipa nuru na kuniangaza, yakinipa nguvu na kuniwezesha nisimame imara. Katika shida, nafurahia upendo na ulinzi wa Mungu na kulidharau joka kubwa jekundu hata zaidi. Kukabiliwa na majaribu kunaniruhusu nielewe ukweli mwingi; tabia yangu potovu inasafishwa, na ninaacha vyote kumfuata Kristo. Nimekuwa uso kwa uso na Mungu, na ingawa njia ya mbinguni ni ngumu na yenye shida, natambua kuwa Kristo ndiye ukweli—na hata ikiwa lazima niozee gerezani, naahidi maisha yangu kumfuata Kristo hadi mwisho kabisa.

Iliyotangulia:Maneno Katika Mioyo ya Wakristo

Inayofuata:Watakatifu Katika Enzi Zote Wanazaliwa Upya

Maudhui Yanayohusiana

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga. Maneno Yako ya…

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…