Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maneno Mashuhuri Kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

XI Maneno Bora Zaidi Juu ya Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli

(II) Maneno Juu ya Kumwomba na Kumwabudu Mungu

11. Maombi si aina ya tambiko; ni ushirika wa kweli kati ya watu na Mungu, na huwa na umuhimu wa kina. Tunaweza kuona nini kutoka kwa maombi ya watu? Tunaweza kuona kuwa wao wanamtumikia Mungu moja kwa moja. Ukitazama maombi kama tambiko, basi bila shaka hutamtumikia Mungu vyema. Ikiwa maombi yako hayafanywi kwa ari au kwa dhati, basi inaweza kusemwa kwamba kutoka kwa mtazamo wa Mungu, wewe kama mtu hupo; hali ikiwa hivyo, utakuwaje na Roho Mtakatifu akifanya kazi kwako? Matokeo yatakuwa kwamba baada ya kufanya kazi kwa muda fulani, utachoka. Kuanzia sasa na kuendelea, bila maombi, hutaweza kufanya kazi. Ni sala ndiyo huleta kazi, na sala ndiyo huleta huduma. Ikiwa wewe ni mtu ambaye huongoza na mtu anayemtumikia Mungu, ilhali hujawahi kujitoa kwa sala wala hujawahi kuwa makini katika maombi yako, basi njia ambayo unatumia kuhudumu itaishia kukusababisha uanguke. … Ikiwa unaweza kuja mbele ya Mungu mara kwa mara, na unaweza kumwomba mara nyingi, inathibitisha kwamba wewe unamchukulia Mungu kama Mungu. Ikiwa mara nyingi unajifanyia mambo na ikiwa mara kwa mara unapuuza kuomba, kufanya hiki na kile bila Yeye kufahamu, basi humtumikii Mungu; bali, unatekeleza tu biashara yako mwenyewe. Hivyo, je, hutahukumiwa? Kutoka nje, haitaonekana kana kwamba umefanya chochote cha kuvuruga, wala haitaonekana kwamba umemkufuru Mungu, lakini utakuwa unatenda tu mambo yako mwenyewe. Kwa kufanya hivyo, je, hukatizi? Hata kama, kwa juu, inaonekana kana kwamba hukatizi, kiasili unampinga Mungu.

kutoka katika “Umuhimu na Mazoea ya Sala” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

12. Baada ya Mungu kuwaumba wanadamu na kuwapa roho, Aliwaagiza kwamba ikiwa hawangemwita Mungu, basi hawangeweza kuunganishwa na Roho Wake na hivyo “televisheni ya setilaiti” kutoka mbinguni haingepokelewa duniani. Wakati Mungu hayupo tena katika roho za watu kuna kiti kitupu kinachoachwa wazi kwa ajili ya vitu vingine, na hivyo ndivyo Shetani anavyotwaa fursa hiyo kuingia ndani. Wakati watu wanapowasiliana na Mungu kwa mioyo yao, Shetani huingia katika hofu kubwa na huharakisha kuhepa. Kupitia wa vilio vya wanadamu Mungu huwapa kile wanachohitaji, lakini “Hakai” ndani yao kwanza. Yeye daima huwapa tu msaada kwa sababu ya vilio vyao na watu hupata ujasiri kutoka kwa nguvu hizo za ndani ili Shetani asithubutu kuja hapa “kucheza” apendavyo. Kwa njia hii, ikiwa watu daima wanaunganishwa na Roho wa Mungu, Shetani hathubutu kuja kuvuruga. Bila vurugu ya Shetani, maisha yote ya watu ni ya kawaida na Mungu ana fursa ya kufanya kazi ndani yao bila vizuizi vyovyote. Kwa njia hii, kile Mungu anataka kufanya kinaweza kutimizwa kupitia kwa wanadamu.

kutoka katika “Sura ya 17” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

13.

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Kuhusu Desturi ya Sala

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli. Watu humwomba Mungu tu wakati kitu kinawatendekea. Katika wakati huu wote, umewahi kweli kumwomba Mungu? Je, umewahi kutoa machozi ya uchungu mbele ya Mungu? Je, umewahi kujijua mwenyewe mbele ya Mungu? Je, umewahi kumwomba Mungu maombi ya kutoka? Kuomba hufanyiwa mazoezi polepole: Ikiwa kwa kawaida huombi nyumbani, basi hutakuwa na njia yoyote ya kuomba kanisani, na kama kwa kawaida huombi wakati wa mikusanyiko midogo, basi hutaweza kusali wakati wa mikusanyiko mikubwa. Ikiwa kwa kawaida humkaribii Mungu au kutafakari juu ya maneno ya Mungu, basi hutakuwa na chochote cha kusema wakati wa kuomba—na hata kama utaomba, utakuwa tu unaunga mkono kwa maneno matupu; hutakuwa unaomba kwa kweli.

Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema. Hii ndiyo maana ya kuomba kwa kweli. Baada ya kuomba kwa kweli, moyoni mwako utahisi kuwa na amani, na kufurahishwa; nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka, na utahisi kwamba hakuna kitu chochote katika maisha yako yote kinachostahili au ni muhimu zaidi kuliko kumpenda Mungu—na yote haya yatathibitisha kuwa maombi yako yamekuwa yenye ufanisi. Je, umewahi kuomba kwa njia hiyo?

Na je, kuhusu maudhui ya sala? Unapaswa kuomba, hatua kwa hatua, kwa mujibu wa hali yako ya kweli na kile kinachotakiwa kufanywa na Roho Mtakatifu, na unapaswa kuwasiliana kwa karibu na Mungu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa mwanadamu. Unapoanza kufanya mazoezi ya maombi yako, kwanza peana moyo wako kwa Mungu. Usijaribu kufahamu mapenzi ya Mungu; jaribu tu kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu. Unapokuja mbele za Mungu, sema hivi: “Ee Mungu! Leo tu ndio natambua kuwa nilikuwa nikikuasi. Mimi kweli ni mpotovu na mwenye kustahili dharau. Awali, nilikuwa nikipoteza muda wangu; kuanzia leo nitaishi kwa ajili Yako, nitaishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na kuridhisha mapenzi Yako. Ningependa Roho Wako afanye kazi ndani yangu daima, na daima aniangaze na kunipa nuru, ili nipate kuwa na ushuhuda wenye nguvu na unaosikika mbele Zako, unaomruhusu Shetani kuuona utukufu Wako, ushuhuda Wako, na thibitisho la ushindi Wako ndani yetu.” Wakati unapoomba kwa njia hii, moyo wako utawekwa huru kabisa, baada ya kuomba kwa njia hii, moyo wako utakuwa karibu na Mungu, na kwa kuomba hivi mara kwa mara, Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila shaka. Ikiwa daima wewe humwita Mungu kwa njia hii na kufanya azimio lako mbele ya Mungu, siku itawadia ambapo azimio lako litaweza kukubalika mbele ya Mungu, wakati moyo wako na nafsi yako vyote vitapokelewa na Mungu, na hatimaye utakamilishwa na Mungu. Sala ni ya muhimu sana kwenu. Unapoomba, unapokea kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo moyo wako unaguswa na Mungu, na nguvu za upendo kwa Mungu ndani yako huchipuka. Ikiwa hutaomba kwa moyo wako, ikiwa hutafungua moyo wako kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi ndani yako. Ikiwa, baada ya kusali, umesema maneno yote yaliyo ndani ya moyo wako na Roho wa Mungu hajafanya kazi, ikiwa huhisi kutiwa moyo ndani, basi hili linaonyesha kwamba moyo wako hauna ari, kwamba maneno yako si ya kweli, na bado wewe ni mchafu. Ikiwa, baada ya kusali, unafurahishwa, basi sala zako zimekubaliwa na Mungu na Roho wa Mungu amefanya kazi ndani yako. Kama mtu ambaye huhudumu mbele ya Mungu, huwezi kuwa bila sala. Ikiwa unaona ushirika na Mungu kama kitu ambacho kina maana na cha thamani, ungeweza kuacha sala? Hakuna mtu anayeweza kuwa bila mawasiliano ya karibu na Mungu. Bila sala, unaishi katika mwili, unaishi katika utumwa wa Shetani; bila sala ya kweli, unaishi chini ya ushawishi wa giza. Natumaini kwamba ndugu wanaweza kuomba kila siku. Huku si kuzingatia mafundisho ya dini, hata hivyo, bali matokeo ambayo yanapaswa kutimizwa. Je, uko tayari kuacha usingizi kidogo na anasa, kusema sala za asubuhi wakati wa alfajiri na kisha kufurahia maneno ya Mungu? Ikiwa utaomba na kula na kunywa maneno ya Mungu, katika njia hii, kwa moyo safi, basi utakubalika zaidi na Mungu. Ikiwa unafanya hivyo kila siku, ukijizoeza kumpa Mungu moyo wako kila siku na kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi ufahamu wako wa Mungu utaongezeka bila shaka, na utaweza kufahamu vizuri zaidi mapenzi ya Mungu. Unapaswa kusema: “Ee Mungu! Ningependa kutimiza wajibu wangu. Ili Uweze kutukuzwa ndani yetu, na Uweze kufurahia ushuhuda ulio ndani yetu, kikundi hiki cha watu, naweza tu kutoa nafsi yangu yote kwako. Nakuomba Ufanye kazi ndani yetu, ili niweze kukupenda na kukuridhisha kwa kweli, na kukufanya Uwe lengo ambalo ninafuatilia.” Wakati ambapo unakuwa na mzigo huu, Mungu atakufanya uwe mkamilifu bila shaka; hupaswi tu kuomba kwa ajili yako mwenyewe, bali pia kwa ajili ya kutenda mapenzi ya Mungu, na kwa ajili ya kumpenda Yeye. Hiyo ndiyo aina ya sala ya kweli kabisa. Je, wewe huomba ili kutenda mapenzi ya Mungu?

Hapo awali, nyinyi hamkujua jinsi ya kuomba, na mlipuuza maombi; leo, lazima mjitahidi kabisa kujifundisha kuomba. Ikiwa huwezi kuwa na ujasiri wa kumpenda Mungu, basi unawezaje kuomba? Unapaswa kusema: “Ee Mungu! Moyo wangu hauwezi kukupenda kweli, nataka kukupenda lakini sina nguvu. Napaswa kufanya nini? Napenda Ufungue macho ya roho yangu, napenda Roho Wako auguse moyo wangu, ili mbele Yako nivuliwe hali zote za kutoonyesha hisia, na nisishurutishwe na mtu yeyote, jambo, au kitu; nauweka moyo wangu wazi kabisa mbele Yako, ili nafsi Yangu yote ijitoe mbele Yako, na Uweze kunijaribu vile Utakavyo. Sasa, siwazii matarajio yangu, wala sifungwi na kifo. Kwa kuutumia moyo wangu ambao unakupenda, napenda kutafuta njia ya uzima. Vitu vyote na matukio viko mikononi Mwako, majaliwa yangu yako mikononi Mwako, na, zaidi ya hayo, maisha yangu yanadhibitiwa na mikono Yako. Sasa, nafuatilia kukupenda Wewe, na bila kujali kama Wewe unaniruhusu kukupenda, haijalishi jinsi Shetani anavyoingilia, nimeamua kukupenda Wewe.” Unapokabiliwa na mambo kama hayo, unasali kwa njia hii. Ikiwa utafanya hivyo kila siku, nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka polepole.

Mtu huingiaje katika sala ya kweli?

Wakati unaomba, moyo wako lazima uwe na amani mbele ya Mungu, na lazima uwe mwaminifu. Wewe kweli unawasiliana kwa karibu na kuomba na Mungu; usimdanganye Mungu kwa kutumia maneno ya kupendeza. Sala lazima ilenge kile ambacho Mungu anataka kukamilisha leo. Mwombe Mungu akupe nuru na mwangaza mwingi zaidi, na ulete hali halisi na matatizo yako mbele za Mungu kuomba, na ufanye azimio mbele za Mungu. Sala sio kufuata utaratibu, bali ni kumtafuta Mungu kwa kutumia moyo wako wa kweli. Omba kwamba Mungu aulinde moyo wako, na Aufanye uwe na amani mara nyingi mbele za Mungu, Akuwezeshe kujijua, na kujidharau, na kujitupa katika mazingira ambayo Mungu amekuwekea, hivyo kukuruhusu uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu na kukufanya mtu anayempenda Mungu kweli.

Ni nini umuhimu wa sala?

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato ambao mtu huguswa na Roho wa Mungu. Inaweza kusemwa kwamba wale ambao hawana sala ni wafu wasio na roho, ushahidi kwamba hawana uwezo wa kuguswa na Mungu. Bila sala, watu hawawezi kupata maisha ya kawaida ya kiroho, sembuse kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu; bila sala, wao huvunja uhusiano wao na Mungu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu. Ukiwa mtu anayemwamini Mungu, kadri unavyoomba, ndivyo unavyozidi kuguswa na Mungu. Watu kama hao wana azimio kubwa zaidi na wanaweza kupokea zaidi nuru ya hivi karibuni kutoka kwa Mungu; kwa hivyo, watu kama hawa pekee ndio wanaweza kukamilishwa mapema iwezekanavyo na Roho Mtakatifu.

Je, ni matokeo gani yanayofaa kutimizwa kwa sala?

Watu wanaweza kutekeleza mazoea ya sala na kuelewa umuhimu wa sala, lakini matokeo yanayofaa kutimizwa kwa sala sio jambo rahisi. Sala sio jambo la kupitia urasmi wa kisheria, au kufuata utaratibu, au kukariri maneno ya Mungu, ambalo ni kusema, sala haimaanishi kuiga maneno kama kasuku na kuwaiga wengine. Katika sala, lazima umpe Mungu moyo wako, ukishiriki maneno yaliyo ndani ya moyo wako na Mungu ili uweze kuguswa na Mungu. Ikiwa maombi yako yatakuwa na matokeo, basi lazima yategemee usomaji wako wa maneno ya Mungu. Ni kwa kuomba tu katikati ya maneno ya Mungu ndipo utaweza kupokea nuru na mwangaza zaidi. Sala ya kweli huonyeshwa kwa kuwa na moyo ambao unatamani sana matakwa yaliyowekwa na Mungu, na kuwa tayari kutimiza matakwa haya; utaweza kuchukia yote ambayo Mungu huchukia, kwa msingi huo utakuwa na maarifa, na utajua na kuelewa wazi kuhusu ukweli ulioelezwa na Mungu. Kuwa na azimio, na imani, na maarifa, na njia ya kufanya mazoezi baada ya kuomba—huku tu ndiko kuomba kwa kweli, na sala kama hii tu ndiyo inaweza kuwa na ufanisi. Lakini sala lazima ijengwe juu ya msingi wa kufurahia maneno ya Mungu na kuwasiliana kwa karibu na Mungu katika maneno Yake, moyo wako ukiweza kumtafuta Mungu na kuwa na amani mbele ya Mungu. Sala kama hiyo tayari imefikia kiwango cha kuwasiliana kwa kweli na Mungu.

Maarifa ya msingi kuhusu kuomba:

1. Usiseme kijinga chochote kinachokuja kwenye akili. Lazima kuwe na mzigo ndani ya moyo wako, ambalo ni kusema, lazima uwe na lengo wakati unapoomba.

2. Sala zako zinapaswa kuwa na maneno ya Mungu; lazima zitegemezwe kwa maneno ya Mungu.

3. Wakati unapoomba, huwezi kurudia mambo ya kale; hupaswi kuleta vitu ambavyo vimepitwa na wakati. Unapaswa kujifunza hasa kunena maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu; wakati huo tu ndipo utaweza kufikia kiwango cha ushirika wa kweli na Mungu.

4. Sala ya kikundi inapaswa kulenga kiini, ambacho lazima kiwe kazi ya Roho Mtakatifu leo.

5. Watu wote wanapaswa kujifunza jinsi ya kuwaombea wengine. Wanapaswa kupata sehemu katika maneno ya Mungu ambayo wanataka kuombea, ambayo kwayo lazima wawe na mzigo, na ambayo lazima waiombee mara nyingi. Hili ni dhihirisho moja la kujali mapenzi ya Mungu.

Maisha ya maombi ya kibinafsi yanategemea kuelewa umuhimu wa sala na maarifa ya msingi ya sala. Lazima mwanadamu aombee dosari zake mara kwa mara katika maisha yake ya kila siku, na lazima aombe juu ya msingi wa maarifa wa maneno ya Mungu ili kutimiza mabadiliko katika tabia yake ya maisha. Kila mtu anapaswa kuanzisha maisha yake ya maombi, anapaswa kuombea maarifa kutegemea maneno ya Mungu, anapaswa kuomba ili kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu. Weka hali zako za kweli mbele ya Mungu, na uwe wa vitendo, na usitilie maanani mbinu; la muhimu ni kupata maarifa ya kweli, na kupata maneno ya Mungu kwa kweli. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ya kiroho lazima aweze kuomba kwa njia nyingi. Sala ya kimya, kutafakari maneno ya Mungu, kuja kuijua kazi ya Mungu, na kadhalika—kazi hii inayolengwa ya kuwasiliana kwa karibu, ni ili kutimiza kuingia katika maisha ya kawaida ya kiroho, kuifanya hali yako mwenyewe mbele za Mungu iwe bora zaidi, na kusababisha maendeleo makubwa zaidi katika maisha yako. Kwa kifupi, yote unayoyafanya—kama ni kula na kunywa maneno ya Mungu, au kuomba kimya au kutangaza kwa sauti—ni ili kuona wazi maneno ya Mungu, na kazi Yake, na kile Anachotaka kutimiza ndani yako. La muhimu zaidi, ni ili kufikia viwango ambavyo Mungu anahitaji na kuyapeleka maisha yako kwa kiwango kinachofuata. Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake. Hivyo, jambo muhimu sana kuhusu kuomba ni kusema maneno ya moyo wako wa kweli kwa Mungu, kumwambia Mungu kuhusu dosari zako au tabia ya kuasi na kujifungua kabisa kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo Mungu atakuwa na hamu ya sala zako; la sivyo, basi Mungu atauficha uso Wake kutoka kwako. Kigezo cha chini kabisa cha sala ni kwamba lazima uweze kuuweka moyo wako kwa amani mbele za Mungu, na hupaswi kuondoka kwa Mungu. Pengine, wakati huu, hujapata mtazamo mpya au wa juu, lakini lazima utumie sala ili mambo yaendelee kama yalivyo—huwezi kurudi nyuma. Hili ndilo jambo dogo zaidi ambalo unapaswa kutimiza. Ikiwa huwezi kufanikisha hata hili, basi inathibitisha kwamba maisha yako ya kiroho hayajaingia katika njia sahihi; kwa hiyo, huwezi kushikilia maono yako ya mwanzo, na kuondolea imani kwa Mungu, na uamuzi wako hatimaye hutoweka. Kuingia kwako katika maisha ya kiroho kunadhihirishwa na iwapo sala zako zimeingia katika njia sahihi au la. Watu wote lazima waingie katika uhalisi huu, lazima wafanye kazi ya kujifunza wenyewe kwa kufahamu katika sala, sio kusubiri kwa kukaa tu, lakini kwa ufahamu watafute kuguswa na Roho Mtakatifu. Wakati huo tu ndipo watakuwa watu wanaomtafuta Mungu kwa kweli.

Unapoanza kuomba, lazima uwe mwenye uhalisi, na usitake kufanya kupita kiasi; huwezi kufanya madai ya ubadhirifu, ukitumaini kwamba mara tu utakapofungua kinywa chako utaguswa na Roho Mtakatifu, utapata nuru na mwangaza, na kupewa neema nyingi. Hilo haliwezekani—Mungu hafanyi mambo yaliyo ya rohoni. Mungu hutimiza sala za watu kwa wakati Wake mwenyewe na wakati mwingine Yeye hujaribu imani yako kuona kama wewe ni mwaminifu mbele Zake. Unapoomba lazima uwe na imani, uvumilivu, na azimio. Watu wengi wanapoanza kujifunza kuomba, hawahisi kuwa wameguswa na Roho Mtakatifu na hivyo huvunjika moyo. Hili halikubaliki! Lazima uwe na nia ya kutobadili msimamo, lazima ulenge kuhisi mguso wa Roho Mtakatifu, na kutafuta na kuchunguza. Wakati mwingine, njia unayofuata ni ile isiyo sahihi; wakati mwingine, misukumo na dhana zako haviwezi kusimama imara mbele za Mungu, na hivyo Roho wa Mungu hakusisimui; vivyo pia kuna nyakati ambapo Mungu huangalia kama wewe ni mwaminifu au la. Kwa kifupi, lazima ujitahidi zaidi katika kujifunza. Ikiwa utatambua kuwa njia unayoifuata ni ya kuacha maadili, unaweza kubadilisha jinsi unavyoomba. Maadamu unatafuta kwa kweli, na unatamani kupokea, basi Roho Mtakatifu atakuingiza kwenye ukweli huu. Wakati mwingine unasali kwa moyo wa ukweli lakini huhisi kama umeguswa hasa. Katika nyakati kama hizi lazima utegemee imani yako, na uamini kwamba Mungu anayaangalia maombi yako; lazima uwe na uvumilivu katika sala zako.

Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole. Maisha ya kweli ya kiroho ni maisha ya sala, na ni maisha ambayo yanaguswa na Roho Mtakatifu. Mchakato wa kuguswa na Roho Mtakatifu ni mchakato wa kubadilisha tabia ya mwanadamu. Maisha ambayo hayajaguswa na Roho Mtakatifu si maisha ya kiroho, bado ni ibada ya kidini; wale tu ambao huguswa na Roho Mtakatifu mara kwa mara, na wamepewa nuru na kuangazwa na Roho Mtakatifu, ndio watu ambao wameingia katika maisha ya kiroho. Tabia ya mwanadamu hubadilika kwa uthabiti wakati anapoomba, na kadri anavyosisimuliwa na Roho wa Mungu, ndivyo anavyozidi kuwa hai na mtiifu. Kwa hiyo, pia, moyo wake utatakaswa polepole, baada ya hapo tabia yake itabadilika polepole. Hayo ndiyo matokeo ya sala ya kweli.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Hata kama wakati watu hupiga magoti kuomba, wanaongea na Mungu katika ulimwengu usiogusika, lazima uelewe dhahiri kwamba sala zao pia ni mfano wa mkondo ambao kwao Roho Mtakatifu hufanya kazi. Watu wanapoomba na kutafuta wakati wako katika hali sahihi, Roho Mtakatifu pia Atakuwa anafanya kazi wakati huo huo. Huu ni mfano wa ushirikiano wenye muamana kati ya Mungu na mwanadamu kutoka mitazamo miwili tofauti; kwa maneno mengine, ni Mungu akiwasaidia watu kushughulikia masuala fulani. Hii ni aina ya ushirikiano kutoka kwa wanadamu wanapokuja mbele ya Mungu; pia ni aina ya mbinu ambayo Mungu Hutumia kuwaokoa na kuwasafisha watu. Zaidi, ni njia ya kuingia kunakofaa kwa watu katika maisha, na si aina ya utaratibu. Maombi sio tu ya kuhimiza shauku ya watu; ingekuwa huo tu, basi ingetosha tu kutenda kwa namna isiyo ya dhati na kusema baadhi ya misemo kwa sauti kubwa, na hakungekuwa na haja ya kuomba chochote, hakungekuwa na haja ya ibada au uchaji Mungu. Umuhimu wa sala ni wa kina sana! Ukiomba mara kwa mara, na kama unajua jinsi ya kuomba—ukiomba mara kwa mara kwa unyenyekevu na kwa busara—basi hali yako ya ndani itakuwa inayofaa hasa. Ikiwa mara kwa mara unatamka misemo hiyo wakati unaomba, bila kuwa na tatizo lolote lile na bila kuzingatia ni yepi kati ya yale usemayo katika maombi ni yenye busara, maneno yako yepi si yenye busara, na ni aina gani ya namna ya kuzungumza si ibada ya kweli, na kama wewe huko makini kila mara kuhusu mambo haya, basi maombi yako hayatakuwa na mafanikio, na siku zote utakuwa na hali ya ndani isiyo ya kawaida; hutawahi kuingia kwa undani kabisa katika mafunzo kuhusu mantiki ya kawaida ni nini, utiifu wa kweli ni nini, ibada ya kweli ni nini, na ni wapi pa kusimama katika maombi. Haya yote ni masuala magumu kueleza.

kutoka katika “Umuhimu na Mazoea ya Sala” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

15. Sala zenu hukosa mantiki mara nyingi mno; daima mnaomba kwa toni ifuatayo: “Ee Mungu! Kwa kuwa Wewe umenifanya nitekeleze wajibu huu, lazima Usababishe kila kitu ninachofanya kiwe cha kufaa ili kazi Yako isikatizwe na maslahi ya familia ya Mungu yasipate hasara yoyote. Lazima Unikinge....” Sala kama hii haina mantiki kabisa, sivyo? … Tazama maombi ya Yesu (ingawa maombi Yake hayatajwi hapa ili kuwafanya watu kuchukua pahali Pake au nafasi Yake): Katika Bustani ya Gethsemane, Aliomba, “Kama inawezekana....” Yaani, “Kama inaweza kufanywa.” Hili lilisemwa katika majadiliano; Hakusema, “Mimi nakuomba Wewe.” Kwa moyo ulionyenyekea na kwa hali ya utiifu, Alisali, “Kama inawezekana, hebu kikombe hiki cha mateso kinipite: Hata hivyo si kama nitakavyo Mimi, bali kama utakavyo Wewe” (Mat 26:39). Bado Aliomba hivi mara ya pili, na mara ya tatu Alisali hivi, “Naomba mapenzi Yako yafanyike.” Akiwa ameng’amua nia za Mungu Baba, Alisema, “Mapenzi Yako yafanyike.” Aliweza kutii kikamilifu bila kufanya uchaguzi wowote wa kibinafsi hata kidogo. Alisema, “Kama inawezekana, hebu kikombe hiki cha mateso kipite kutoka Kwangu.” Je, hiyo ilimaanisha nini? Alisali hivyo kwa sababu aliwaza juu ya mateso makubwa ya kuvuja damu msalabani hadi pumzi Lake la mwisho la kufa—na hili liligusia suala la kifo—na kwa sababu hakuwa ameng’amua kikamilifu nia za Mungu Baba. Kwa kuwa Aliweza kuomba kwa njia hiyo licha ya wazo la mateso, Alikuwa mtiifu sana kweli. Namna Yake ya sala ilikuwa ya kawaida; Hakutoa masharti yoyote katika sala Yake wala Hakusema kikombe sharti kiondolewe. Bali, lengo Lake lilikuwa kutafuta nia za Mungu katika hali ambayo Hakuielewa. Mara ya kwanza Alipoomba, Hakuelewa, naye Alisema: “Kama inawezekana … lakini kama utakavyo Wewe.” Alikuwa amemwomba Mungu katika hali ya unyenyekevu. Mara ya pili, Aliomba vilevile. Kwa jumla, Aliomba mara tatu (bila shaka, sala hizi tatu hazikufanyika katika muda wa siku tatu tu), na katika sala Yake ya mwisho, Alikuja kuelewa kabisa nia za Mungu, na baada ya hapo Hakuomba chochote tena. Katika maombi Yake mawili ya kwanza, Aliomba katika hali ya utiifu. Hata hivyo, watu hawaombi kwa njia hiyo hata kidogo. Katika maombi yao, watu husema, “Mungu, nakuomba ufanye hiki na kile, na nakuomba Uniongoze katika hili na lile, na nakuomba Uniandalie hali….” Pengine hatakuandalia hali zinazofaa na Atakuacha upitie ugumu. Kama watu daima wangesema, “Mungu, nakuomba Unifanyie maandalizi na Unipe nguvu.” Kusali kwa namna hiyo hakuna busara kabisa! Lazima uwe na busara wakati unaomba, na lazima ufanye hivyo katika kigezo kwamba unanyenyekea. Usiwekee maombi yako mipaka. Kabla hata uanze kuomba, wewe unaiwekea mpaka tayari hivi: Lazima nimwombe Mungu na kumfanya atende hiki na kile. Aina hii ya kuomba haina busara kabisa.

kutoka katika “Umuhimu na Mazoea ya Sala” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

16. Mara nyingine, wakati ambapo unafurahia maneno ya Mungu, roho yako huguswa, na wewe huhisi kwamba huna budi kumpenda Mungu, kwamba kuna nguvu nyingi ndani yako, na kwamba hakuna chochote usichoweza kuweka kando. Kama wewe unahisi hivi, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na utamwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Sisi kweli tumejaaliwa na kuteuliwa na Wewe. Utukufu Wako hunipa fahari, na inaonekana ya kuleta sifa kuu kwa mimi kuwa mmoja wa watu Wako. Nitatumia chochote na kutoa chochote ili kufanya mapenzi Yako, na nitayatoa maisha yangu yote, na juhudi za maisha yangu yote, Kwako.” Unapoomba hivi, kutakuwa na upendo usioisha na utiifu wa kweli kwa Mungu ndani ya moyo wako. Je, umewahi kuwa na tukio kama hili? Kama watu huguswa mara kwa mara na Roho wa Mungu, basi wako radhi hasa kujitolea wenyewe kwa Mungu katika maombi yao: “Ee Mungu! Ningependa kutazama siku Yako ya utukufu, na ningependa kuishi kwa ajili Yako—hakuna kilicho cha thamani au maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Wewe huniinua kwa kuniwezesha mimi kuishi kwa ajili Yako leo.” Wakati ambapo umeomba kwa njia hii, utahisi kwamba huna budi ila kutoa moyo wako kwa Mungu, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu wakati ambapo uko hai. Baada ya kunena ombi hilo, kutakuwa na nguvu isiyoisha ndani yako, na hutajua hiyo hutoka wapi; ndani ya moyo wako kutakuwa na nguvu bila kikomo, na utakuwa na hisi kwamba Mungu ni wa kupendeza sana, na kwamba Anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na tukio hilo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara kwa mara huguswa na Mungu, mabadiliko hutokea ndani ya maisha yao, wao huweza kufanya azimio lao na wako radhi kumpata Mungu kabisa, upendo kwa Mungu ndani yao ni thabiti zaidi, mioyo yao imeelekea kwa Mungu kabisa, wao huwa hawastahi familia, ulimwengu, matatizo, au siku zao za baadaye, na wao huwa radhi kutoa juhudi za maisha yote kwa Mungu. Wale wote ambao wameguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao huwa na tumaini la kufanywa wakamilifu na Mungu.

kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Huyu mwanadamu Petro alikuwa wa kimo bora sana, lakini hali yake ilikuwa tofauti na ile ya Paulo. Wazazi wake walinitesa, walikuwa wa mapepo yaliyomilikiwa na Shetani, na kwa sababu hii mtu hawezi kusema kwamba walipitisha njia kwa Petro. Petro alikuwa na busara nyepesi, alipewa akili asili, kupendwa sana kutoka utotoni na wazazi wake; baada ya kukua, hata hivyo, akawa adui zao, kwani daima alitaka kunijua, na hii ilimfanya kuwapuuza wazazi wake. Hii ilikuwa kwa sababu, kwanza kabisa, aliamini kwamba mbingu na dunia na mambo yote yako mikononi mwa Mwenyezi, na kwamba mambo yote mazuri yanatoka kwa Mungu na yanakuja moja kwa moja kutoka Kwake, bila kupitia usindikaji wowote na Shetani. Na mfano usiofaa wa wazazi wake kuwa kama kikwazo, hii ilimwezesha kwa urahisi kutambua upendo na huruma Yangu, na hivyo kuchochea ndani yake hamu kubwa zaidi ya kunitafuta. Alikuwa makini sana sio tu kula na kunywa maneno Yangu, lakini hata zaidi kufahamu nia Zangu, na daima alikuwa na busara na tahadhari katika mawazo yake, kwa hivyo daima alikuwa mwerevu kwa makini ndani ya roho yake, na hivyo aliweza kuniridhisha kwa vyote alivyofanya. Kwa maisha ya kawaida, alikuwa makini kuunganisha katika maisha[a] masomo ya wale walioshindwa katika siku za nyuma ili kujichochea mwenyewe kufanya juhudi kubwa zaidi, akihofia sana kwamba anaweza kuanguka ndani ya nyavu za ushinde. Alikuwa pia makini kupata imani na upendo wa wote ambao kupitia enzi nyingi walikuwa wamempenda Mungu. Kwa njia hii, aliharakisha maendeleo ya ukuaji wake sio tu kwa masuala hasi, lakini hasa kwa masuala chanya, hadi akawa katika uwepo Wangu mwanadamu pekee aliyenijua bora kabisa. Kwa sababu hii, si vigumu kuwazia jinsi alivyoweza kuweka yote aliyokuwa nayo mikononi Mwangu, kukosa kuwa tena bwana wake mwenyewe hata kwa kula, kuvaa, ama mahali aliishi, lakini alifanya kuniridhisha kwa mambo yote msingi ambao alifurahia fadhila Yangu. Mara nyingi Nilimweka chini ya jaribio, ambalo hakika lilimwacha nusu mfu, lakini hata katikati ya haya mamia ya majaribio, hakupoteza imani Kwangu hata mara moja ama kusikitishwa nami. Hata Niliposema nimemtupa kando, hakufa moyo wala kukata tamaa, lakini aliendelea kama mbeleni akitekeleza kanuni zake ili kunipenda kwa njia ya vitendo. Nilipomwambia kwamba, ingawa alinipenda, Sikumsifu ila Ningemtupa katika mikono ya Shetani mwishowe. Katikati ya majaribio haya, ambayo hayakufikia mwili wake lakini yalikuwa majaribio ya njia ya maneno, bado alisali Kwangu: “Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu unaweza kuteseka, natulizwa ndani ya roho yangu. Ningewezaje kutosifu hekima Yako na matendo Yako? Hata kama nitafa baada ya kuja kukujua, kamwe nitakuwa tayari. Ee, Mwenyezi! Hakika si kwamba Wewe kweli hutaki kuniruhusu nikuone? Hakika si kwamba sistahili kweli kupokea hukumu Yako? Inaweza labda kuwa kwamba kuna kitu ndani yangu usichotaka kuona?” Katikati ya majaribu ya aina hizi, hata kama Petro hakuweza kufahamu nia Zangu kwa usahihi, ni wazi kwamba aliliona kuwa suala la fahari na utukufu binafsi kutumiwa na Mimi (iwe tu kupokea hukumu Yangu ili binadamu waweze kuuona ukuu na ghadhabu Yangu), na hakuwa mwenye huzuni kwa ajili ya kuwekwa chini ya jaribio. Kwa sababu ya uaminifu wake mbele Yangu, na kwa sababu ya baraka Zangu juu yake, amekuwa mfano mwema na mfano wa kuigwa kwa mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Je, huui si hasa mfano unaopaswa kufuata?

kutoka katika “Sura ya 6” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, “Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Ninatamani tu kwamba tabia Yako ionekane ili, tabia Yako ya haki iweze kuonekana na viumbe wote, na kwamba niweze kukupenda kwa usafi zaidi kupitia hukumu Yako na nifikie mfanano wa yule mwenye haki. Hukumu hii Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako. Ningependa unihukumu hata zaidi, iwe ni kupitia mazingira ya uhasama au mateso makubwa; haijalishi ni nini Utakayofanya, kwangu ni ya thamani. Upendo Wako ni mkuu, na mimi niko tayari kujiweka katika huruma Yako bila malalamiko hata kidogo.” Huu ni ufahamu wa Petro baada ya yeye kuiona kazi ya Mungu, na pia ni ushahidi wa upendo wake kwa Mungu.

kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Nakala ya awali imeacha “katika maisha yake mwenyewe.”

Iliyotangulia:(I) Maneno Juu ya Kumwamini Mungu

Inayofuata:(III) Maneno Juu ya Kumtegemea na Kumwaminia Mungu

Maudhui Yanayohusiana