Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Kuna mengi ambayo Natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simwangamizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wake wa nguvu, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya kazi Yangu tu, na kuongea jinsi ambavyo Nimefanya, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua ndani kabisa ya nyoyo zao, na watanikumbuka katika mawazo yao. Nitakapoondoka duniani ndipo haswa Nitakapopanda kwa kiti cha enzi katika moyo wa binadamu, yaani, itakuwa wakati watu wote watanijua Mimi. Hivyo pia, itakuwa wakati wana Wangu na watu watatawala dunia. Wale ambao wananijua Mimi bila shaka watakuwa nguzo za ufalme Wangu, na wao peke yao ndio watastahiki kutawala na kuwa na mamlaka katika ufalme Wangu. Wote ambao wananijua Mimi wana nafsi Yangu, na wana uwezo wa kuishi kwa kunidhihirisha miongoni mwa watu wote. Sijali mwanadamu ananijua Mimi kwa kiwango gani: Hakuna yeyote anayeweza kuzuia kazi Yangu kwa njia yoyote, na mwanadamu hawezi kunipa usaidizi wowote wala kunifanyia lolote. Mwanadamu anaweza tu kufuata mwongozo Wangu katika mwangaza Wangu, na kutafuta matakwa Yangu kwenye mwangaza huu. Leo, watu wana sifa zinazostahili, na wanaamini wanaweza kutembea kwa maringo mbele Yangu, na kucheka na kufanya mzaha na Mimi bila kizuizi hata kidogo, na kunihutubia Mimi kama tuko sawa. Bado mwanadamu hanijui Mimi, bado anaamini kuwa kiasili sisi kadri tuko sawa, kuwa sisi sote ni nyama na damu, na sote tunaishi katika dunia ya binadamu. Uchaji wake Kwangu ni mdogo sana; ananiheshimu Mimi anapokuwa mbele Yangu, lakini hawezi kunihudumia Mimi mbele ya Roho. Ni kama, kwa mwanadamu, Roho hayupo kabisa. Kwa hivyo, hakuna mwanadamu ashawahi kumjua Roho; katika kupata mwili Kwangu, watu huona tu mwili wa nyama na damu, na hawamtambui Roho wa Mungu. Matakwa Yangu yanaweza kutimizwa kwa njia kama hii? Watu ni mabingwa wa kunihadaa Mimi; wanaonekana kama ambao wamepewa mafunzo maalum na Shetani ili kunihadaa Mimi. Lakini Shetani bado hanibabaishi Mimi. Bado Nitatumia hekima Yangu kuwashinda wanadamu wote na kumshinda ambaye anawapotosha wanadamu wote, ili ufalme Wangu uanzishwe duniani.

Miongoni mwa binadamu, kuna wale ambao wamejaribu kujua ukubwa wa nyota, au upana wa mbingu. Lakini utafiti wao haujawahi kuweza kuzaa matunda, na hawana hiari ila tu kuinamisha vichwa vyao kwa masikitiko na kukubali kushindwa. Nikiwaangalia watu wote na kuchunguza uwezo wa mwanadamu katika kushindwa kwake, Sioni yeyote yule ambaye ameniamini kabisa, hakuna ambaye ananitii Mimi na kujinyenyekeza Kwangu. Matarajio ya wanadamu ni yasiyo ya kawaida kweli! Wakati yote yalikuwa yamefunikwa na kiza, miongoni mwa wanadamu Nilianza kuonja uchungu wa dunia. Roho Wangu husafiri kote duniani na kuangalia ndani ya nyoyo za watu wote, na bado pia, Mimi huwashinda wanadamu katika mwili wangu wa nyama. Mwanadamu huwa hanioni Mimi, kwa kuwa yeye ni kipofu; mwanadamu hanijui Mimi, kwani amekuwa hana hisia; mwanadamu hunipinga Mimi, kwa kuwa yeye si mtiifu; mwanadamu huja kusujudu mbele Yangu, kwa kuwa ameshindwa na Mimi; mwanadamu huja kunipenda Mimi, kwa kuwa Nastahili kiasili kupata upendo wa mwanadamu; mwanadamu huishi kulingana na Mimi na kunidhihirisha Mimi, kwa sababu nguvu Zangu na hekima Yangu humfanya apendeze nafsi Yangu. Nina nafasi katika moyo wa mwanadamu, lakini kamwe Sijawahi kupokea upendo wa mwanadamu Kwangu katika roho yake. Kwa kweli, kuna mambo katika roho ya mwanadamu anayoyapenda kuliko yote mengine, lakini Mimi si mojawapo wa mambo hayo, na kwa hivyo upendo wa mwanadamu ni kama kiputo cha sabuni: Upepo unapovuma, hukipasua na kinaenda, kisiwahi kuonekana tena. Mtazamo Wangu kuhusu mwanadamu siku zote umekuwa thabiti na usiobadilika. Kuna yeyote kati ya wanadamu, ambaye angeweza kufanya vivyo hivyo? Machoni pa mwanadamu, Mimi sigusiki wala Mimi sionekani mithili ya hewa, na kwa sababu hii, idadi kubwa ya watu hutafuta tu katika anga isiyokuwa na mipaka, au juu ya bahari ambayo si tulivu, au juu ya ziwa tulivu, au miongoni mwa maandiko na mafundisho matupu. Hakuna mtu hata mmoja anayejua kiini cha binadamu, sembuse yeyote anayeweza kusema chochote kuhusu fumbo lililo ndani Yangu, na kwa hivyo huwa Simtaki mwanadamu afikie viwango vya juu zaidi ambavyo yeye hudhani Nahitaji kutoka kwake.

Ndani ya maneno Yangu, milima hupinduliwa, maji hutiririka kinyumenyume, mwanadamu huwa mtiifu, na maziwa huanza kutiririka bila kusita. Ingawa bahari isiyo tulivu huenda kwa hasira kuelekea mbinguni, ndani ya maneno Yangu bahari za aina hii hutulia kama upande wa juu wa ziwa. Kwa kupunga mkono Wangu kidogo tu, upepo mkali kabisa hutokomea na kutoka Kwangu mara moja, na ulimwengu wa mwanadamu hurejesha utulivu wake mara moja. Lakini Ninapotoa ghadhabu Yangu, milima hutenganishwa mara moja, ardhi huanza kutetemeka mara moja, maji hukauka mara moja, na mwanadamu huzingirwa na maafa mara moja. Kwa ajili ya ghadhabu Yangu, huwa Mimi sisikilizi vilio vya mwanadamu, huwa sitoi msaada ili kujibu vilio vyake, kwani hasira Yangu inapanda. Ninapokuwa miongoni mwa mbingu, nyota hazijawahi kutishiwa na kuwepo Kwangu kamwe. Bali, huwa zinaweka nyoyo zao katika kunifanyia kazi Mimi, na kwa hivyo, Mimi huzipa mwangaza zaidi na kuzifanya zing’are zaidi, ili zipate utukufu zaidi kwa ajili Yangu. Kadri mbingu inavyong’aa zaidi, ndivyo dunia chini yake inazidi kuwa na giza; watu wengi sana hulalamika kuwa mipango Yangu huwa hayafai, wengi wameniacha kuunda ufalme wao wenyewe, ambao wanautumia kunisaliti, na kubadili hali ya giza. Ila nani ameweza kutimiza hili kwa azma yao? Ni nani ametimiza hili kwa azimio lake? Nani anaweza kubadili yale ambayo yamepangwa na mkono Wangu? Wakati majira ya machipuko yanaenea kwenye ardhi, Mimi hupeleka mwangaza kwa siri na kimya ulimwenguni, ili, duniani, mwanadamu awe na hisia ya ghafla ya usafi hewani. Hata hivyo, wakati huo huwa Ninafunika macho ya mwanadamu, ili aone tu ukungu ukiwa umefunika ardhi, na watu na vitu vyote havibainiki. Watu kupumua tu kwa masikitiko. Mbona mwangaza uling’aa kwa muda mdogo tu? Kwa nini Mungu humpa binadamu ukungu na utusitusi tu? Huku watu wakikata tamaa , ukungu hupotea mara moja, lakini wanapoona dalili ya mwangaza, Mimi huachilia mbubujiko wa mvua juu yao, na viwambo vyao vya masikio vinavunjwa kwa ajili ya mvua ya na radi wanapolala. Huku wakiwa na hofu, hawana wakati wa kujikinga, na hugubikwa na mvua kubwa. Papo hapo, yote yaliyo chini ya mbingu hufagiliwa katika ghadhabu Yangu yenye hasira. Watu hawalalamiki tena kuhusu mwanzo wa mvua kubwa, na ndani yao wote, uchaji huzaliwa. Kwa sababu ya uvamizi huu wa ghafla wa mvua, idadi kubwa ya watu wanazama ndani ya maji yanayonyesha kutoka mbinguni, na kuwa maiti ndani ya maji. Naangalia dunia nzima na kuona kuwa wengi wanazinduka, kuwa wengi wanatubu, kuwa wengi wanatafuta chanzo cha maji ndani ya mashua ndogo, kuwa wengi wananisujudu Mimi ili kuomba msamaha Wangu, kuwa wengi wameona mwangaza, kuwa wengi wameona uso Wangu, kuwa wengi wana ujasiri wa kuishi, na kuwa ulimwengu mzima umebadilishwa. Kufuatia mbubujiko huu mkubwa wa mvua, vitu vyote vimerudi kuwa jinsi vilivyokuwa katika akili Yangu, na haviasi tena. Kabla ya muda mrefu, ardhi yote imejaa sauti za vicheko, na kila mahali duniani kuna hali ya sifa, na hakuna popote ambapo hapana utukufu Wangu. Hekima Yangu iko kote duniani, na katika ulimwengu mzima. Miongoni mwa vitu vyote, kuna matunda ya hekima Yangu, miongoni mwa watu wote, kumejaa kazi bora zaidi za hekima Yangu; kila kitu ni kama mambo yote katika ufalme Wangu, na watu wote wanakaa kwa mapumziko chini ya mbingu Zangu kama kondoo kwenye uwanja Wangu wa malisho. Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee kamwe, na hakuna mtu ambaye yuko kama alivyokuwa. Ninapumzika katika kiti cha enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima, na Nimeridhika kikamilifu, kwani kila kitu kimerejesha utakatifu wake, na Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena, na watu duniani wanaweza kuishi maisha tulivu na ya kuridhisha chini ya mwongozo Wangu. Watu wote wanasimamia kila kitu mikononi Mwangu, watu wote wamerejesha akili zao za awali na mwonekano wao wa kiasili; hawafunikwi tena na vumbi, lakini, ndani ya ufalme Wangu, ni wasafi kama lulu, kila mmoja akiwa na uso kama wa yule mtakatifu aliye ndani ya moyo wa binadamu, kwani ufalme Wangu umeimarishwa miongoni mwa binadamu.

Machi 14, 1992

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji