Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu, na hakuna mtu ambaye amewahi kunijua na kwa hivyo mtazamo wa mwanadamu Kwangu ni wa sitasita, na hauna uwezo wa kuwa kawaida. Lakini Nimekuwa Nikimlea na kumchunga mwanadamu na ni kwa sababu ya upumbavu wake ndiyo maana hana uwezo wa kuona matendo Yangu yote na kuelewa nia Zangu. Mimi Ndiye Ninayeongoza katika mataifa yote, na ndiye Mkubwa Zaidi kwa watu wote; kwa ufupi ni kwamba mwanadamu hanijui Mimi. Kwa miaka mingi Nimeishi na mwanadamu na kujionea Maisha katika dunia ya mwanadamu, lakini amekuwa Akinipuuza na kunichukulia kama kiumbe kutoka ulimwengu wa nje ya dunia. Kwa sababu hii, kutokana na tofauti za tabia na lugha, watu Hunichukulia Mimi kama mgeni barabarani. Nguo Zangu, huenda ikawa, pia ni za kipekee, hata kumfanya mwanadamu kukosa imani ya kunikaribia. Ni wakati huo ndio naona upweke wa maisha ya mwanadamu, na wakati huo tu ndio Ninapata ufafanuzi wa dhuluma katika dunia ya mwanadamu. Ninatembea katikati ya wapita njia, Nikiangalia nyuso zao zote. Ni kama kwamba wanaishi ndani ya maradhi, ambayo yanajaza nyuso zao na huzuni, na miongoni mwa adhabu, inayozuia kuachiliwa kwao. Mwanadamu hujitia pingu mwenyewe na kujifedhehesha mwenyewe. Watu wengi hujenga hisia za uwongo juu yao mbele Yangu ili Niwaunge mkono, watu wengi hujifanya makusudi kuwa wa kuhuzunisha mbele Yangu ili waweze kupata usaidizi Wangu. Nyuma Yangu, watu wote hunidanganya na kuniasi. Je, Mimi sio wa kweli? Je, huu si mkakati wa mwanadamu ili aweze kuishi? Ni nani ambaye ameweza kuishi kulingana na mfano Wangu maishani mwake? Nani ambaye ameweza kunitukuza miongoni mwa wengine? Nani amewahi kuwajibika mbele ya Roho? Nani ambaye amesimama imara kwa ushuhuda wake Kwangu mbele ya Shetani? Ni nani ameweza kuongezea ukweli kwa uaminifu wake Kwangu? Ni nani amewahi kuangamizwa na joka kubwa jekundu kwa sababu Yangu? Watu wametupa kura zao kwa shetani, wamekuwa wataalam kwa Kunipinga, na wamekuwa waanzilishi wa upinzani kuja Kwangu, na wamehitimu katika kunifanyia Mimi mzaha. Kwa ajili ya hatima yake mwenyewe, mwanadamu anatafuta hapa na pale duniani; Ninapomwita, anabaki bila fahamu ya thamani Yangu kubwa na anaendelea kuwa na Imani katika kujitegemea, asiwe mzigo kwa wengine. Matarajio ya mwanadamu ni ya thamani, lakini hakujawahi kuwa na matarajio ya yeyote ambayo yametimiza alama zote. Yote yanabomoka mbele Yangu, na kuporomoka bila sauti.

Kila siku Ninaongea, na kila siku Nafanya mambo mapya pia. Ikiwa mwanadamu hawezi kutumia nguvu zake zote, basi atakuwa na ugumu kusikia sauti Yangu na atapata ugumu kuona uso wangu. Mpendwa Anaweza kuwa sawa, na mazungumzo Yake kuwa ya upole, lakini mwanadamu hana uwezo wa kutazama kwa urahisi sura Yake tukufu na kusikia sauti Yake. Katika miaka yote, hakuna ambaye amewahi kuweza kutazama sura Yangu kwa urahisi. Niliwahi kuongea na Petro na Nikajitokeza kwa Paulo, na hakuna mwingine—isipokuwa Waisraeli—ambaye kweli amewahi kuona uso Wangu. Leo, nimekuja Mimi Mwenyewe kati ya mwanadamu kuishi pamoja na yeye. Je, hiki hakihisi kuwa kitu nadra na cha thamani kwenu? Je, hamtamani kufanya matumizi bora ya muda wenu? Je, mnataka jambo hili liwapite kwa njia hii? Inawezekana muda usimamishwe ghafula katika mawazo ya watu? Au inawezekana muda urudishwe nyuma? Au inawezekana mwanadamu awe kijana tena? Inawezekana maisha ya leo yenye baraka kuja tena? Simpatii mwanadamu “zawadi” sahihi kwa “ubadhirifu” wake. Mimi huendelea kufanya kazi Yangu tu, nimejitenga na mengine yote na sisimamishi mtiririko wa masaa kwa sababu mwanadamu ana shughuli, au kwa sababu ya sauti ya vilio vyake. Kwa miaka elfu kadhaa, hakuna ambaye ameweza kugawa nguvu Yangu, na hakuna ambaye ameweza kuharibu mpango Wangu wa asili. Nitavuka anga, na kuzunguka miaka, na kuanzisha kiini cha Mpango Wangu mzima juu na miongoni mwa vitu vyote. Hakuna ambaye ameweza kupokea utunzaji maalum kutoka Kwangu, hakuna aliyeweza kupata “tuzo” iliyo mikononi Mwangu. Na hata kama watu wamefungua vinywa vyao na kuomba Kwangu, na hata kama, bila kujali mambo mengine yote, wamenyosha mikono yao ya kufanya madai Kwangu, hakuna madai yoyote ambayo yameniathiri, na wao wote wamesukumwa nyuma na sauti Yangu "isiyo na utu." Watu wengi bado wanaamini kuwa wao ni "wachanga sana," na hivyo wanasubiri Niwaonyeshe rehema kubwa, kuwa na huruma kwao kwa mara ya pili, na wanauliza Niwaruhusu kuchukua mlango wa nyuma. Hata hivyo ni jinsi gani Mimi Nitaufanyia mpango Wangu mzaha? Je, Ninaweza kusimasisha dunia isizunguke kwa ajili ya ujana wa mwanadamu, ili aweze kuishi miaka zaidi duniani? Akili ya mwanadamu ni tata, lakini inaonekana kwamba pia kuna vitu ambavyo inakosa. Kwa sababu hii, katika akili ya mwanadamu mara nyingi huonekana "njia za ajabu" za kupinga kazi Yangu kwa makusudi.

Ingawa ni mara nyingi Nimesamehe dhambi za mwanadamu, na kumwonyesha upendeleo wa pekee kwa sababu ya udhaifu wake, mara nyingi pia Nimempa utunzaji sahihi kwa sababu ya ujinga wake. Ni rahisi kuwa mwanadamu hajawahi kujua jinsi ya kufahamu wema Wangu, hadi amezama kwenye hali yake ya sasa: amefunikwa katika vumbi, nguo zake zikiwa matambara, nywele zake zimefunika kichwa chake kama magugu yanayokua, uso wake umepakwa masizi, miguu yake imevalishwa viatu vilivyotengenezwa nyumbani, mikono yake kama makucha ya tai aliyekufa, yakining'inia kwa udhaifu katika pande zake. Nikifungua macho Yangu na kutazama, ni kama kwamba mwanadamu amepanda juu kutoka nje ya shimo lisilo na mwisho. Sina budi ila kuwa na hasira: Nimekuwa mvumilivu kwa mwanadamu, ni jinsi gani Nilimruhusu shetani kuja na kwenda kama atakavyo kutoka Ufalme Wangu mtakatifu? Ni jinsi gani nilimruhusu mwombaji kula bure katika nyumba Yangu? Ni jinsi gani nilivumilia kuwa na roho mchafu kama mgeni wa nyumba Yangu? Mwanadamu daima amekuwa "mkali kwake mwenyewe" na "mwenye upole kwa wengine," ilhali hajawahi angalau hata kidogo kuwa na adabu kuelekea Kwangu, maana Mimi ni Mungu mbinguni, na hivyo Yeye hunichukulia Mimi kwa nia tofauti, na hajawahi kuwa na upendo hata kidogo Kwangu. Ni kama kwamba macho ya mwanadamu ni majanja: Mara tu anapokutana na Mimi, uso wake unabadilika mara moja na anaongeza hisia kidogo kwa uso wake baridi na usio na hisia. Simlazimishii mwanadamu vizuizi vinavyofaa kwa sababu ya mtazamo wake kuelekea Kwangu, bali Naangalia tu angani kutoka juu ya ulimwengu na kutekeleza kazi Yangu hapa duniani. Katika kumbukumbu ya mwanadamu, sijawahi kuonyesha wema kwa mtu yeyote, lakini sijawahi pia kumtendea vibaya mtu yeyote. Kwa sababu mwanadamu hanihifadhii "kiti kitupu" ndani ya moyo wake, Nisipotahadhari na kukaa ndani yake, ananilazimisha Mimi Nitoke nje bila utaratibu, na kisha anatumia maneno ya kujipendekeza na ubembelezaji ili kufanya visingizio, akisema yeye hana uwezo wa kujitoa mwenyewe kwa ajili ya starehe Yangu. Anapoongea, uso wake mara nyingi hufunikwa na "mawingu ya giza," kana kwamba madhara yatakuja miongoni mwa wanadamu wakati wowote. Hata hivyo, bado ananiambia Mimi niondoke, bila kuzingatia hatari zinazohusika. Hata kama ninampatia mwanadamu maneno Yangu na joto la kumbatio Langu, yeye anaonekana kuwa hasikii, na hivyo haipatii sauti Yangu muda hata kidogo, na badala yake anashikilia kichwa chake huku akitoroka. Naondoka kwa mwanadamu Nikijihisi Nimesikitishwa kidogo, lakini pia nikiwa Nimeghadhabishwa. Mwanadamu wakati huo anatoweka huku kukiwa na shambulio la upepo mkubwa na mawimbi makuu. Baadaye, Ananililia Mimi, lakini ni jinsi gani yeye angebadili harakati ya upepo na mawimbi? Hatua kwa hatua, dalili zote za mwanadamu zinapotea, mpaka hapatikani mahala popote.

Kabla ya nyakati, Niliangalia nchi zote za ulimwengu kutoka juu mbinguni. Nilipanga shughuli kubwa duniani: uumbaji wa mwanadamu ambaye angependeza moyo Wangu, na ujenzi wa ufalme duniani kama ule wa mbinguni, Nikaruhusu uwezo Wangu kujaza anga na hekima Yangu kuenea kote ulimwenguni. Na hivyo leo, maelfu ya miaka baadaye, Mimi Naendelea na mpango Wangu, lakini hakuna anayejua mpango Wangu au usimamizi wa dunia, wala hawauoni ufalme Wangu duniani. Kwa hivyo, mwanadamu hukimbiza vivuli, na kuja mbele Yangu ili kujaribu kunidanganya, akitaka kulipa "gharama ya kimya" ili apate baraka Zangu za mbinguni. Kwa sababu hii, amechochea hasira Yangu na Ninamletea hukumu, lakini bado hana fahamu. Ni kana kwamba alikuwa anafanya kazi kichinichini, pasi na kutojua kabisa lililokuwa likiendelea katika ulimwengu huku akifuata ndoto na dhamira zake tu. Miongoni mwa watu wote, sijawahi kuona mtu yeyote ambaye anaishi chini ya mwanga Wangu. Wanaishi katika ulimwengu wa giza, na wanaonekana kuzoea kuishi ndani ya giza. Mwanga unapokuja wanakaa mbali, na ni kana kwamba mwanga umevuruga kazi zao; matokeo yake, wanaonekana kuudhika kidogo, ni kama mwanga umeathiri amani yao na kuwaacha bila uwezo wa kulala fofofo. Kwa sababu hii, mwanadamu anakusanya nguvu zake zote na kuuondoa mwanga. Mwanga, pia, unaonekana kukosa ufahamu, na hivyo unaamsha mwanadamu kutoka usingizini, na wakati mwanadamu anaamka, anafunga macho yake, akijawa na hasira. Kwa kiasi fulani ni kama hajafurahishwa na Mimi, lakini katika moyo Wangu najua lengo. Ninaendelea hatua kwa hatua kuimarisha mwanga, kusababisha watu wote kuishi katika mwanga Wangu, ili baada ya muda usiokuwa mrefu wazoee kujihusisha na mwanga, na, zaidi ya hapo, wote wathamini mwanga huo. Kwa wakati huu, ufalme Wangu umekuja miongoni mwa mwanadamu, watu wote wanacheza kwa shangwe na kusherehekea, ghafla dunia inajazwa na furaha, na kimya cha miaka elfu kadhaa chavunjwa kwa kuwasili kwa mwanga ...

Machi 26, 1992

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji