Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapofyatua moto, Ninaitazama kwa uangalifu dunia nzima, Ninatazama kwa uangalifu ulimwengu mzima. Wanadamu wote wananiomba Mimi, wameinua macho yao kuelekea Kwangu, wakiomba Nipunguze hasira, na kuapa kutoniasi tena. Lakini haya siyo yaliyopita; bali yaliyopo kwa sasa. Ni nani anayeweza kubadilisha mapenzi Yangu? Kwa kweli sio sala katika moyo wa mwanadamu, wala maneno yanayotoka midomoni mwao? Ni nani ambaye ameweza kuishi hadi wakati huu, isipokuwa ni kwa nguvu Zangu? Ni nani anayeishi ila kwa maneno ya kinywa Changu? Ni nani asiyekaa chini ya uangalifu wa macho Yangu? Ninapofanya kazi Zangu katika ulimwengu mzima, ni nani ambaye ameweza kuiepuka kazi hiyo? Inawezekana kuwa milima imeiepuka kutokana na urefu wayo? Inawezekana kuwa maji kwa wingi na upana wake, yameweza kuizuia kazi hii? Katika mpango Wangu, Sijawahi kuachilia kitu chochote kiende kwa wepesi, hivyo basi hakuna mtu yeyote, wala kitu chochote, ambacho kimeepuka mikono Yangu. Hivi leo, jina Langu takatifu linatukuka katika uumbaji wote, na tena, maneno ya malalamiko katika binadamu dhidi Yangu yanachipuka, na hadithi kuhusu kuwepo Kwangu ulimwenguni zimeenea miongoni mwa binadamu. Sivumilii binadamu wanapotoa hukumu dhidi yangu, wala Sivumilii wao kuugawanya mwili Wangu, wala lugha ya machungu na matusi dhidhi Yangu. Ukweli ni kuwa mwanadamu hajawahi kunifahamu Mimi, tangu awali amenikana na kuzua upinzani Kwangu, akishindwa kumpenda Roho Wangu au kuyathamini maneno ya kinywa Changu. Kwa kila tendo na hatua yake, na kwa mtazamo wake Kwangu, Nampa binadamu "tuzo" yake inayomfaa. Hivyo basi, binadamu hufanya jambo wakiwa wameweka macho kwenye tuzo yao, na wala hapana mmoja aliyefanya kazi inayohusisha kujinyima na kujitolea. Wanadamu hawana nia ya kujitoa kwa kujinyima, ila wanafurahia tuzo zinazopatikana kwa kutofanya chochote. Japo kuwa Petro alijiweka wakfu mbele Zangu, haikuwa ni kwa sababu ya malipo ya kesho, bali kwa maarifa ya leo. Binadamu hajawahi kuingia katika ushirikiano halisi Nami, lakini muda baada ya muda ameweza kukumbana Nami kwa namna ya juujuu, hivyo kufikiria bila juhudi za kupata idhini Yangu. Nimeangalia kwa kina ndani ya moyo wa mwanadamu, na kuibua undani wake wa siri “mgodi wa utajiri mwingi,” kitu ambacho hata mwanadamu mwenyewe hafahamu lakini mimi Nimefahamu upya. Hivyo basi, mpaka watakapojionea kwa macho “ushahidi wa kuonekana”, hapo tu ndipo binadamu atasitisha unafiki wa kujidhalilisha mwenyewe na, mikono iliyonyooshwa watakubali hali yao ya uchafu. Miongoni mwa binadamu, kuna mambo mengi mapya na ya kisasa yanayoningoja Mimi “niwatolee” ili kila mwanadamu astarehe. Mbali na kutia kikomo katika kazi Yangu kwa ajili ya ukosefu wa uwezo kwa mwanadamu, Ninaendelea na urekebishaji na udumishaji wake kama ilivyokuwa mpango Wangu wa awali. Binadamu ni kama mti wa matunda: bila ya kuukata na kuupogoa, mti huo hautaweza kuzaa matunda na, mwishowe, yatakayoonekana ni matawi yaliyonyauka na majani yaliyoanguka, pasipo na matunda yoyote kuanguka ardhini.

Ninapokipamba “chumba cha ndani” cha ufalme Wangu siku baada ya siku, hakuna yule ameingia katika “chumba Changu cha kazi” kwa ghafla ili kuvuruga kazi Yangu. Wanadamu wote wanafanya wawezayo kushirikiana nami, wakiwa na hofu ya “kufukuzwa” na “kupoteza nafasi zao” hivyo kufikia tamati maishani mwao ambapo wanaweza kuanguka “jangwani” anakoishi Shetani. Kwa sababu ya uoga wa mwanadamu, Ninamfariji kila siku, Nikimwegemeza katika pendo kila siku na zaidi ya yote kumwelekeza na sheria kila siku ya maisha yake. Ni kana kwamba wanadamu wote ni watoto wachanga ambao wamezaliwa sasa hivi; bila ya kupewa maziwa, watatoweka duniani humu, wasipate kuonekana tena. Kati ya maombi ya unyenyekevu ya mwanadamu, Nakuja katika ulimwengu wa mwanadamu, na moja kwa moja, mwanadamu anaishi katika ulimwengu wenye mwanga, wasifungiwe tena katika “chumba” ambako wanatoa vilio vya maombi vikielekea mbinguni. Mara tu wanaponiona, binadamu kwa kusisitiza huleta mbele Yangu “maombolezo” yaliyo mioyoni mwao, wakifungua vinywa vyao mbele Yangu wakiomba chakula kiangushwe midomoni mwao. Lakini baadaye, “hofu yao kutoweka na hali tulivu kurejea,” na hakuna wanachohitaji kutoka Kwangu tena, mwanadamu hulala fofofo au hukana uwepo Wangu, kisha kuelekea kufanya mambo yao wenyewe. Katika ile hali ya mwanadamu “kutelekeza”, ni wazi kuwa binadamu pasi na “hisia” huendeleza “haki bila mapendeleo” Kwangu. Hivyo basi, Ninapomwangalia mwanadamu katika ile hali yake ya ukosefu wa pendo Kwangu, Mimi huondoka kwa upole pasi na kurudi tena kwa wepesi katika hali yake ya maombi ya hitaji. Bila ya mwanadamu kufahamu, shida zake zinaongezeka siku baada ya siku, hivyo, katika hali yake ya kufanya kazi kwa bidii, ndipo anapofahamu uwepo Wangu, yeye, akikataa kuchukua “la” kama jawabu, kisha anashika kwa nguvu nguo Yangu na kunikaribisha kwa ukarimu nyumbani kwake kama mgeni. Lakini, ingawa anaandaa chakula kitamu mbele Yangu ili Niweze kustarehe, hajawahi kunikubali kama mmoja wa wenzi wake, badala yake akinichukulia kama mgeni ili tu apate kitu kiasi kidogo cha usaidizi kutoka Kwangu. Hivyo basi mwanadamu kwa wakati huu anaweka wazi Kwangu hali yake ya kuhurumisha, akiwa na matumaini kuwa atapata “sahihi,” na, kama yule anayehitaji mkopo kwa ajili ya biashara yake, ananikabili kwa nguvu zake zote. Katika kila ishara yake na mwenendo, Ninapata mtazamo wa nia ya mwanadamu: ni kana kwamba, katika maoni yake, Mimi sijui kusoma maana fiche iliyo juu ya uso wa mwanadamu na kufichwa nyuma ya maneno atamkayo, au jinsi ya kuangalia ndani ya moyo wa mwanadamu. Hivyo basi binadamu huweka wazi uaminifu wake Kwangu kwa kila hali tuliyoandamana, bila ya kuwacha au kusahau jambo lolote, kisha kuyaleta madai yake kwangu. Nina machukizo dhidi ya kila tendo la mwanadamu. Miongoni mwa binadamu, hakuna yeyote yule aliyefanya tendo lililonipendeza, kana kwamba wanafanya maksudi ili kuniudhi, wakiwa na kusudi la kuvutia adhabu Yangu kali: Wote wakitia gwaride kushoto na kulia mbele Yangu, wakitenda yaliyo mapenzi yao mbele ya macho yangu. Hakuna yeyote kati ya binadamu anayeishi kwa ajili Yangu, hivyo basi kuwepo kwa viumbe vyote kunakosa maana na wanadamu wanaishi kwa utupu mkuu. Hata hivyo, binadamu bado wanakataa kutoka katika hali ile ya uzinifu wakiendelea na uasi wao Kwangu wakisisitiza kukaa katika ubatili.

Katika majaribu yote wanayopitia, wanadamu hawajawahi hata siku moja kunipendeza. Kwa sababu ya ukatili wa uovu wao, mwanadamu hana jitihada yoyote ya kueneza jina Langu; ila, “anakimbia upande mwingine” akinitegemea kumpa riziki ya kila siku. Mwanadamu hanipi moyo wake wote hivyo kumuelekeza shetani kumnyanyasa hadi akapata majeraha mengi, na mwili wake kujawa na uchafu. Lakini mwanadamu bado hafahamu jinsi uso wake ulivyo mbaya: muda huu wote akimwabudu Shetani kinyume na mapenzi Yangu. Kwa sababu hii, kwa hasira Nitamtupa mwanadamu katika shimo lisilo na mwisho, asiloweza kujitoa ndani. Hata hivyo, kati ya kulia kwake kwa kuhuzunisha, binadamu bado hukataa kubadilisha mawazo yake, akidhamiria kupingana Nami hadi mwisho wa machungu yake, akiwa na kusudi la kuzidisha ghadhabu Yangu. Kwa ajili ya yale aliyoyatenda, Ninamtendea kama mwenye dhambi na kumnyima joto la kumbatio Langu. Tokea mwanzo, malaika wamenihudumia na kuniheshimu bila ya kubadili mienendo, lakini mwanadamu kila mara akifanya kinyume, kana kwamba hakutoka Kwangu, ila kazaliwa na Shetani. Malaika katika maeneo yao hunipa ibada kamili; pasi na kutatanishwa na nguvu za kishetani, wakijitahidi tu kutimiza wajibu wao. Wakiwa wamelishwa na malaika, halaiki za Wanangu na watu Wangu wote hukua kwa nguvu na wenye afya, hakuna kati yao yeyote yule aliyedhoofika kiafya. Hii ni kazi ya mikono Yangu, muujiza Wangu. Kama vile vigelegele baada ya vigelegele vya moto wa kanuni huzindua uanzilishi wa ufalme Wangu, malaika, wakiwa wanatembea katika usawa wa kifuasi, huja mbele ya jukwaa Langu kujiwasilisha kwa ukaguzi, Wangu, kwa sababu mioyo yao haina uchafu na haiabudu miungu mingine, hivyo hawaepuki ukaguzi Wangu.

Upepo mkali unapovuma kwa mayowe, mbingu hushuka ghafla, na kufanya wanadamu kukosa hewa hivyo basi hawawezi tena kuliita jina Langu jinsi wapendavyo. Bila ya kujua, binadamu wote umeanguka. Miti huyumba kila upande katika upepo. na katika kila muda matawi yanasikika kutoa sauti ya kuvunjika, na majani yote yaliyonyauka hubebwa na upepo. Dunia hujaa kiza na ukiwa mara moja, na watu wakikumbatiana kwa pamoja, wakingoja maafa yanayofuata majira ya kupukutika kwa majani kuwapata wakati wowote. Ndege milimani wakipuruka huku na kule, kana kwamba wanalia huzuni wao kwa mtu fulani; na katika pango za milima, simba hunguruma, wakiogofya watu kwa sauti zao, kufanya damu yao igande na kuogofya, ni kama kwamba kuna hisia ya kuogofya inayoashiria mwisho wa wanadamu. Bila kungojea furaha ya nia Yangu ya kuwaangamiza, binadamu wote huomba kimoyomoyo kwa Bwana Mkuu aliye mbinguni. Lakini itawezekanaje upepo mkubwa kuzuiliwa na kelele za maji yakitiririka kwenye kijito? Itawezekanaje upepo huu usimamishwe kwa sauti za sala za binadamu? Itawezekanaje hasira moyoni mwa radi kutulizwa sababu ya woga wa mwanadamu? Mwanadamu huyumba mbele na nyuma katika upepo; hukimbia huku na kule ili kujifichia mvua; na chini ya ghadhabu Yangu, binadamu hutingizika na kutetemeka, wakihofu kuwa Nitaweka mikono Yangu juu ya miili yao, kana kwamba Mimi ni ncha ya bunduki iliyoelekezwa katika kifua cha mwanadamu, na pia, ni kama yeye ni adui Yangu, ijapokuwa ni rafiki Yangu. Mwanadamu hajawahi kwa kweli kufahamu nia Yangu kwake, hajawahi hata siku moja kufahamu makusudi Yangu ya kweli hivyo basi bila ya kujua, huasi dhidhi Yangu, bila ya kujua, Hunikana, ilhali, bila kutaka, ameona kiasi cha upendo Wangu. Ni vigumu binadamu kuona uso Wangu wakati wa ghadhabu Yangu. Nimejificha nyuma ya mawingu ya hasira Yangu na Ninasimama, kati ya mingurumo ya radi, juu ya ulimwengu wote na kutuma huruma Zangu chini kwa mwanadamu. Kwa sababu ya mwanadamu kukosa maarifa kunihusu, Simwadibu kwa kukosa kujua nia Yangu kwake. Mbele ya macho ya binadamu, Mimi huweka wazi ghadhabu Yangu mara kwa mara, Ninatabasamu mara kwa mara, lakini hata anaponiona, mwanadamu hajawahi kuona upana wa tabia Yangu, na bado hana uwezo wa kusikia kelele za shangwe na uwazi, kwa kuwa amejaa upumbavu na ujinga. Ni kana kwamba umbo Langu linakaa katika kumbukumbu ya mwanadamu, na nafsi Yangu katika mawazo yake. Hata hivyo, hapana Yule ambaye amewahi kuniona kwa kweli kati ya ukuaji wa wanadamu wote, kwa sababu akili za binadamu zina upungufu wa hali ya juu. Kwa yote ambayo mwanadamu amenichambua, sayansi ya jamii ya mwandamu haina mizizi na, kufikia sasa, utafiti wake wa kisayansi haujaibua matokeo kamilifu. Na hivyo basi, mada ya "umbo Langu" imekuwa daima tupu pasiwe na yeyote wa kuijaza, hakuna wa kuivunja rekodi ya dunia kwa sababu ili mwanadamu aweze kuweka mguu wake imara katika ulimwengu wa sasa ni kifuta machozi kisichokadirika katika matukio makuu yenye majonzi.

Machi 23, 1992

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji