Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Ubinadamu wenu umepungukiwa sana, mtindo wenu wa maisha ni duni na wa hadhi ya chini sana, hamna ubinadamu, na mumekosa umaizi. Hiyo ndiyo maana mnahitaji kujitayarisha na vitu vya ubinadamu wa kawaida. Kuwa na dhamiri, mantiki na umaizi; kujua jinsi ya kuzungumza na kuyatazama mambo; kuzingatia usafi; kutenda kama binadamu wa kawaida—hizi zote ni sifa za maarifa ya ubinadamu wa kawaida. Mnapotenda kwa njia inayofaa katika vitu hivi, basi mnachukuliwa kuwa na kiwango kinachokubalika cha ubinadamu. Lazima mjitayarishe pia kwa ajili ya maisha ya kiroho. Lazima mjue kazi yote ya Mungu duniani na myapitie maneno Yake. Unapaswa kujua jinsi ya kutii mipango Yake na jinsi ya kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa. Hivi ndivyo vipengele viwili vya kile unachopaswa kukiingia leo—kujitayarisha kwa maisha ya ubinadamu, na kutenda kwa ajili ya maisha ya mambo ya roho. Vyote ni vya lazima.

Watu wengine ni wa upuuzi: Wanajua tu kujipa sifa za ubinadamu. Hakuna kasoro inayoweza kupatikana katika kuonekana kwao; mambo wanayoyasema na njia yao ya kuzungumza ni ya kufaa, na mavazi yao ni ya heshima na ya kufaa sana. Lakini ni watupu ndani yao; wanaonekana tu kuwa na ubinadamu wa kawaida kwa nje. Kuna wengine wanaolenga tu kile cha kula, kuvaa, na kile cha kusema. Hata kuna wale wanaolenga vitu kama kufagia sakafu, kutandika kitanda na usafi wa jumla pekee. Wanaweza kuwa wamejizoeza vizuri vitu hivi vyote, lakini unapowaomba wazungumze kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu ya siku za mwisho, ama ya kuadibu na hukumu, ama majaribu na usafishaji, huenda wakaonyesha hawana uzoefu hata kidogo. Unaweza kuwauliza: “Je, una ufahamu wa kazi ya msingi ya Mungu duniani? Je, kazi ya Mungu mwenye mwili leo inatofautiana vipi na kazi ya Yesu? Inatofautiana vipi na kazi ya Yehova? Je, Wao ni Mungu mmoja? Je, Amekuja kutamatisha enzi hii, ama kuwaokoa wanadamu?” Lakini watu kama hawa hawana chochote cha kusema kuhusu masuala haya. Wengine wanajivika mapambo mazuri, lakini ya juujuu: Kina dada wanajivika mapambo mazuri kama maua, na kina ndugu wanavalia kama wana wa wafalme ama wambuji wadogo matajiri. Wanajali tu kuhusu vitu vya nje, kama vitu wanavyokula na kuvalia; ndani yao, wao ni mafukara na hawamfahamu Mungu hata kidogo. Hili lina maana gani? Na kisha kuna wengine wanaovalia kama waombaji maskini—kweli wanaonekana kama watumwa wa Asia Mashariki! Je, kweli hamwelewi Ninachotaka kutoka kwenu? Shirikini kwa karibu: Mmepata nini kweli? Mmemwamini Mungu kwa miaka hii yote, lakini mmevuna hili tu—je, hamna aibu? Je, hamwoni haya? Mmekuwa mkifuatilia kwenye njia ya kweli kwa miaka hii yote, lakini leo kimo chenu bado ni cha chini kuliko cha jurawa! Watazame mabibi wadogo walio miongoni mwenu, warembo kama picha mkiwa mmevalia mavazi na vipodozi vyenu, mkijilinganisha kati yenu—na ni nini mnacholinganisha? Starehe zenu? Matakwa yenu? Je, mnadhani kwamba Nimekuja kuandikisha waonyesha mitindo? Hamna aibu! Maisha yenu yako wapi? Je, kile mnachokifuatilia si tamaa zilizopita kiasi tu? Unadhani kuwa wewe ni mrembo sana, lakini ingawa umevalia kila aina ya umaridadi, kwa kweli wewe si buu anayegaagaa, aliyezaliwa katika rundo la kinyesi? Leo, huna bahati ya kufurahia baraka hizi za mbinguni kwa ajili ya uso wako mrembo, ila kwa sababu Mungu anafanya jambo la kipekee kwa kukuinua. Je, bado huelewi ulikotoka? Maisha yanapotajwa, unafunga mdomo wako na husemi chochote, na unakimya kama sanamu, lakini bado una ujasiri wa kuvalia vizuri! Bado unataka kupaka uso wako rangi nyekundu na poda! Na watazame wambuji walio miongoni mwenu, wanaume waliopotoka wanaoshinda siku kutwa wakitembea huku na kule polepole, wakaidi, na wenye sura tepetevu usoni pao. Je, hivi ndivyo mtu anapaswa kutenda? Je, kila mmoja kati yenu, awe mwamamume ama mwanamke, anazingatia nini siku nzima? Je, mnajua mnamtegemea nani kujilisha? Tazama mavazi yako, tazama kile ulichovuna mikononi mwako, sugua kitambi chako—umefaidika nini kutoka kwa gharama ya damu na jasho ambayo umelipa katika miaka hii yote ya imani? Bado unafikiri kwenda kutalii sehemu maarufu, bado unafikiri kupamba mwili wako unukao—ufuatiliaji usio na maana! Unaombwa uwe mtu wa kawaida, lakini sasa wewe si mtu asiye wa kawaida tu, wewe ni mpotovu. Mtu kama wewe anawezaje kuwa na ujasiri wa kuja mbele Zangu? Ukiwa na ubinadamu kama huu, ukionyesha uzuri wako na kuringa kwa ajili ya mwili wako, ukiishi daima ndani ya tamaa za mwili—je, wewe si mzao wa mashetani wachafu na pepo waovu? Sitamruhusu shetani mchafu kama huyu aendelee kuishi kwa muda mrefu! Na usifikiri kwamba Sijui kile unachofikiri moyoni mwako. Unaweza kudhibiti vikali tamaa na mwili wako, lakini Nawezaje kukosa kujua fikira zilizo moyoni mwako? Nawezaje kukosa kujua tamaa zote za macho yako? Je, ninyi mabibi wadogo hamjirembeshi sana ili kuonyesha miili yenu? Wanaume wana faida gani kwenu? Je, kweli wanaweza kuwaokoa kutoka katika bahari ya mateso? Na kwa wambuji miongoni mwenu, nyote huvalia ili kujifanya muonekane waungwana na wa heshima, lakini, je, hii si hila iliyokusudiwa kuvuta macho kwa sura zenu changamfu? Mnafanya hili kwa sababu ya nani? Wanawake wana faida gani kwenu? Je, wao si chanzo cha dhambi yenu? Enyi wanaume na wanawake, Nimewaambia maneno mengi sana, lakini mmetii machache tu. Masikio yenu hayataki kusikia, macho yenu yamefifia, na mioyo yenu ni migumu kiasi kwamba kuna tamaa tu katika miili yenu, kiasi kwamba mmetegwa nayo, msiweze kutoroka. Ni nani anayetaka kuwakaribia ninyi mabuu, ninyi mnaojifurukuta katika uchafu na masizi? Msisahau kwamba ninyi tu ni wale Niliowatoa kutoka katika rundo la kinyesi, kwamba mwanzoni hamkuwa na ubinadamu wa kawaida.Ninachotaka kutoka kwenu ni ule ubinadamu wa kawaida ambao hamkuwa nao mwanzoni, si kwamba muonyeshe tamaa zenu ama muachilie miili yenu iliyooza, ambayo imeelekezwa na ibilisi kwa miaka mingi sana. Mnapojivisha nguo hivyo, je, hamwogopi kwamba mtategwa kwa kina zaidi? Je, hamjui kwamba mwanzoni mlikuwa wenye dhambi? Je, hamjui kwamba miili yenu imejaa tamaa sana kiasi kwamba hata inavuja kutoka kwa mavazi yenu, ikifichua hali zenu kama mashetani wabaya na wachafu kukithiri? Je, si kweli kwamba mnajua hili vyema zaidi kuliko yeyote mwingine? Mioyo yenu, macho yenu, midomo yenu—je, si vyote vimenajisiwa na mashetani wachafu? Je, hizi sehemu zenu si chafu? Je, unadhani kwamba alimradi hutendi, basi wewe ndiwe mtakatifu kabisa? Je, unadhani kwamba kuvalia mavazi mazuri kunaweza kuficha nafsi zenu duni? Hilo haliwezekani! Nawashauri muwe wenye uhalisi zaidi: Msiwe wadanganyifu na bandia, na msijigambe. Mnaonyeshana tamaa zenu, lakini yote mtakayopata kama malipo ni mateso ya milele na kurudiwa kikatili! Mna haja gani ya kupepeseana macho yenu na kujiingiza katika mapenzi? Je, hiki ndicho kipimo cha uaminifu wenu, kiasi cha uadilifu wenu? Nawachukia kabisa wale miongoni mwenu wanaojihusisha katika uganga na uchawi; Nawachukia sana wale wanaume na wanawake wadogo miongoni mwenu wanaopenda miili yao wenyewe. Ni vyema mjizuie, kwa sababu sasa mnahitajika kuwa na ubinadamu wa kawaida, na hamruhusiwi kuonyesha tamaa zenu—lakini mnachukua kila fursa muwezayo, kwani miili yenu imejaa sana, na tamaa zenu ni kubwa mno!

Kwa nje, maisha yako ya ubinadamu yamepangwa vizuri sana, lakini huna cha kusema unapoambiwa uzungumzie maarifa yako ya maisha; na umepungukiwa sana katika hili. Lazima ujitayarishe na ukweli! Maisha yako ya ubinadamu yamebadilika kuwa bora, na kwa hivyo pia maisha yaliyo ndani yako lazima yabadilike; badili mawazo yako, geuza maoni yako kuhusu imani katika Mungu, badili maarifa na fikira zilizo ndani yako, na ubadili maarifa kumhusu Mungu kama yalivyo ndani ya mawazo yako. Kupitia kushughulikiwa, kupitia ufunuo na ruzuku, badili kwa utaratibu maarifa yako kujihusu, kuhusu maisha ya binadamu, na kuhusu kumwamini Mungu; ufanye ufahamu wako uweze kuwa safi. Kwa njia hii, fikira alizo nazo mwanadamu zinabadilika, jinsi anavyoyaona mambo inabadilika, na mtazamo wake wa kiakili unabadilika. Ni hili tu linaloweza kuitwa mabadiliko katika tabia ya maisha. Huombwi kuyasoma maneno ya Mungu siku nzima ama uoshe nguo na kusafisha. Maisha ya ubinadamu wa kawaida lazima angalau yavumilike kwa kawaida. Aidha, unaposhughulikia masuala ya nje, lazima bado utumie umaizi na mantiki kiasi; lakini kilicho muhimu kabisa ni kwamba ujitayarishe na ukweli wa maisha. Unapojitayarisha kwa ajili ya maisha, lazima ulenge kula na kunywa maneno ya Mungu, lazima uweze kuzungumzia maarifa ya Mungu, maoni yako ya maisha ya binadamu, na hasa, maarifa yako ya kazi iliyofanywa na Mungu wakati wa siku za mwisho. Kwa kuwa unafuatilia uzima, ni lazima ujitayarishe na vitu hivi. Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, lazima utathmini uhalisi wa hali yako mwenyewe kulingana na vitu hivi. Yaani, unapogundua dosari zako wakati wa uzoefu wako wa kweli, lazima uweze kupata njia ya kutenda, uweze kupuuza nia na fikira zako zisizo sahihi. Ukijitahidi daima kupata vitu hivi na utake kuvitimiza kwa dhati, basi utakuwa na njia ya kufuata, hutahisi mwenye utupu, na hivyo utaweza kudumisha hali ya kawaida. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayebeba mzigo katika maisha yako mwenyewe, aliye na imani. Mbona watu wengine hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo baada ya kuyasoma? Je, si kwa sababu hawawezi kuelewa vitu muhimu kabisa? Je, si kwa sababu hawayachukulii maisha kwa uzito? Sasabu ya wao kutoelewa vitu muhimu na kukosa njia ya kutenda ni kuwa wanaposoma maneno ya Mungu, hawawezi kuyahusisha na hali zao wenyewe, wala hawawezi kuwa na ujuzi wa hali zao wenyewe. Watu wengine husema: “Mimi huyasoma maneno ya Mungu na kuyahusisha na hali yangu mwenyewe, na najua kwamba mimi ni mpotovu na mwenye ubora duni wa tabia, lakini siwezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu.” Umeona tu mambo ya nje kabisa; kuna vitu vingi halisi ambavyo huvijui: jinsi ya kuweka kando raha za mwili, jinsi ya kuweka kando kujidai, jinsi ya kujibadili, jinsi ya kuviingia vitu hivi, jinsi ya kuboresha ubora wako wa tabia, na kuanzia kutoka kipengele kipi. Unaelewa tu mambo machache ya nje, na yote unayoyajua ni kwamba kweli umepotoka sana. Unapokutana na ndugu zako, unazungumzia jinsi ulivyopotoka, na inaonekana kwamba unajijua na unabeba mzigo mkubwa kwa ajili ya maisha yako. Kwa kweli, tabia yako potovu haijabadilika, jambo linalothibitisha kwamba hujapata njia ya kutenda. Ikiwa unaongoza kanisa, lazima uweze kuelewa hali za kina ndugu na kuzionyesha. Je, itatosha kusema tu: “Ninyi watu ni wasiotii na wenye maendeleo kidogo mno!” La, lazima uzungumze hasa kuhusu jinsi kutotii kwao na wao kuwa wenye maendeleo kidogo mno kunavyodhihirishwa. Lazima uzungumzie hali zao za kutotii, mienendo yao ya kutotii, na tabia zao za kishetani, na lazima uyazungumzie mambo haya kwa namna ambayo wanashawishika kabisa kuhusu ukweli katika maneno yako. Tumia mambo ya hakika na mifano kutoa hoja zako, na useme hasa jinsi wanavyoweza kujiondoa kwa tabia ya uasi, na uonyeshe njia ya kutenda—hivi ndivyo jinsi ya kuwashawishi watu. Ni wale tu wanaofanya hivi ndio wanaoweza kuwaongoza wengine; ni wao tu walio na uhalisi wa ukweli.

Sasa mmepewa ukweli mwingi kupitia kufanya ushirika, na lazima uutathmini. Unapaswa kuweza kufikia uamuzi kuhusu kuna ukweli ngapi kwa jumla. Punde unapojua na wewe mwenyewe unaweza kutofautisha kati ya vipengele kadhaa vya ubinadamu wa kawaida ambao mtu anapaswa kuwa nao, vipengele vikuu vya mabadiliko ya tabia ya mtu, kuzidishwa kwa maono, na njia zenye makosa za kujua na kupitia ambazo watu wametumia katika enzi zote—ni hapo tu ndipo utakuwa kwenye njia sahihi. Watu wa dini wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu; hasa wanazichukulia Injili Nne za Agano Jipya kana kwamba ni nyuso nne tofauti za Yesu na wanazungumzia Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Haya yote ni ya mzaha kabisa, na nyote mnapaswa kuyabaini; zaidi ya hayo, lazima muwe na maarifa ya kiini cha Mungu aliyepata mwili na kazi ya siku za mwisho. Pia kuna mbinu hizo za kale za kutenda, uongo na mikengeuko hiyo inayohusiana na utendaji—kuishi ndani ya roho, kujazwa na Roho Mtakatifu, kukubali yoyote yatakayokuja, kutii mamlaka—ambayo lazima myajue; mnapaswa kujua jinsi watu walivyotenda awali, na jinsi watu wanavyopaswa kutenda leo. Kuhusu jinsi viongozi na wafanyakazi wanapaswa kushirikiana katika makanisa; jinsi ya kuweka kando kujidai na kujionyesha kuwa bora; jinsi ndugu wanavyopaswa kuishi kwa amani; jinsi ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na watu wengine na Mungu; jinsi ya kutimiza ukawaida katika maisha ya binadamu; kile ambacho watu wanapaswa kuwa nacho katika maisha yao ya kiroho; jinsi wanavyopaswa kula na kunywa maneno ya Mungu; ni maneno yapi ya Mungu yanahusiana na maarifa, ni yapi yanayohusu maono, na ni yapi kati yao yanayohusiana na njia ya kutenda—je, haya yote hayajazungumziwa? Maneno haya yako wazi kwa wale wanaofuatilia ukweli, na hakuna mtu anayetendewa kwa upendeleo. Leo, mnapaswa kukuza uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, si kutegemea akili ya kutegemeana. Katika siku zijazo, wakati hakuna mtu wa kuwaongoza, mtayafikiria haya maneno Yangu. Katika nyakati za taabu, wakati haiwezekani kuishi maisha ya kanisa, wakati ndugu hawawezi kukutana, wengi wao wakiishi peke yao, wakiweza tu kuwasiliana na watu katika maeneo yao mambo yakiwa mazuri, ni katika nyakati hizi ambapo kwa sababu ya kimo chenu cha sasa, hamwezi kabisa kusimama imara. Wakiwa katikati ya taabu, wengi huona vigumu kusimama imara. Ni wale tu wanaoijua njia ya maisha na wamejitayarisha na ukweli wa kutosha ndio wanaoweza kuendelea kusonga mbele na kufanikisha utakaso na mabadiliko kwa utaratibu. Kupitia taabu si jambo rahisi; ikiwa unafikiri kuwa utazipita kwa siku chache, basi hili linathibitisha jinsi fikira zako zilivyo rahisi! Unafikiri kwamba kwa kuelewa kanuni nyingi, utaweza kusimama imara, lakini hali si hivyo! Ikiwa hufahamu mambo ya maana katika maneno ya Mungu, huwezi kuelewa sifa muhimu za ukweli, na huna njia ya kutenda, basi wakati utakapofika na kitu kikufanyikie, utatumbukia katika vurugu. Hutaweza kuvumilia jaribio la Shetani, wala ujio wa usafishaji. Ikiwa hakuna ukweli ndani yako na huna maono, basi wakati ukifika, hutaweza kujizuia kuanguka. Utakata tamaa kabisa na kusema, “Ni sawa, ikiwa nitakufa liwalo liwe, ni heri niadhibiwe hadi mwisho kabisa! Iwe ni kuadhibiwa ama kurushwa katika ziwa la moto, litimike basi—nitayakabili mambo yanavyonijia!” Mambo yalikuwa hivi wakati wa watendaji huduma: Watu wengine waliamini kwamba walikuwa watendaji huduma kwa vyovyote vile, kwa hivyo hawakufuatilia maisha tena. Walivuta sigara na kunywa pombe, wakafurahisha miili yao, na kufanya kile walichotaka. Wengine walirudi tu duniani kufanya kazi. Mazingira yasiyokalika yako hivi pia; ikiwa huwezi kuyashinda, ukishindwa kujidhibiti hata kidogo, utakata tamaa kabisa. Ikiwa huwezi kushinda ushawishi wa Shetani, utatekwa nyara na Shetani kufumba kufumbua na kuletewa maangamizi tena. Hivyo basi, ni lazima leo ujitayarishe na ukweli; ni lazima uweze kuishi kwa kujitegemea; na unapoyasoma maneno ya Mungu, ni lazima uweze kutafuta njia ya kutenda. Ikiwa hakungekuwa na viongozi ama wafanyakazi wa kukunyunyizia na kukuchunga, unapaswa bado kuweza kupata njia ya kufuata, upate dosari zako mwenyewe, upate ukweli unaopaswa kujitayarisha nao na kutenda. Je, Mungu anaweza kumwandama mwanadamu kila wakati baada ya kuja duniani? Ndani ya fikira zao, watu wengine huamini: “Mungu, usipotufinyanga hadi kwa kiwango fulani, basi kazi Yako haiwezi kuchukuliwa kuwa iliyokamilika, kwa sababu Shetani anakushutumu.” Nakuambia, punde Nitakapomaliza kunena maneno Yangu, basi kazi Yangu itakuwa imekamilika kwa mafanikio. Wakati Sina mengine zaidi ya kusema, basi kazi Yangu itakuwa imekamilika. Mwisho wa kazi Yangu utakuwa thibitisho la kushindwa kwa Shetani, na kwa sababu hiyo, inaweza kusemekana kwamba imemalizwa kwa mafanikio, bila shutuma yoyote kutoka kwa Shetani. Lakini ikiwa bado hakuna mabadiliko ndani yenu wakati kazi Yangu imemalizika, basi watu kama ninyi hamwezi kuokolewa na mtaondolewa. Nitafanya tu kazi inayohitajika. Sitaendeleza kazi Yangu duniani hadi ushindwe kwa kiwango fulani, na nyote muwe na maarifa mazuri ya kila kipengele cha ukweli, na ubora wenu wa tabia uboreke na mnishuhudie kwa undani na nje. Hilo halitawezekana! Leo, kazi Nifanyayo ndani yenu inakusudiwa kuwaongoza hadi katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; ni kazi ya kukaribisha enzi mpya na ya kuwaongoza wanadamu katika maisha ya enzi mpya. Kazi hii inatekelezwa na kukuzwa miongoni mwenu hatua kwa hatua na moja kwa moja: Nawafunza ana kwa ana; Nawaongoza moja kwa moja; Nawaambia chochote msichokielewa, Nawapa chochote msicho nacho. Inaweza kusemekana kwamba, kwenu, hii kazi yote ni kwa ajili ya ruzuku yenu ya maisha, kuwaongoza pia katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; inakusudiwa hasa kuruzuku maisha ya kundi hili la watu wakati wa siku za mwisho. Kwangu Mimi, hii kazi yote inakusudiwa kukamilisha enzi ya kale na kukaribisha enzi mpya; kumhusu Shetani, Nilipata mwili hasa ili nimshinde. Kazi Nifanyayo miongoni mwenu sasa ni ruzuku yenu ya leo na wokovu wenu wa wakati mzuri, lakini katika miaka hii michache mifupi, Nitawaambia ukweli wote, njia nzima ya maisha, na hata kazi ya siku zijazo; hili litatosha kuwawezesha mpitie mambo kwa njia ya kawaida katika siku zijazo. Nimewaaminia maneno Yangu yote pekee. Sitoi ushawishi mwingine wowote; leo, maneno yote Ninayowazungumzia ni ushawishi Wangu kwenu, kwa sababu leo hamjapitia maneno mengi Ninenayo, na hamwelewi maana yake ya ndani. Siku moja, uzoefu wenu utatimika jinsi tu Nilivyosema leo. Maneno haya ni maono yenu ya leo, na ndiyo mtakayotegemea katika siku zijazo; ni ruzuku ya maisha leo na ushawishi wa siku zijazo, na hakuna ushawishi unaoweza kuwa bora zaidi. Hii ni kwa sababu muda Nilio nao kufanya kazi duniani si mrefu kama muda mlio nao kupitia maneno Yangu; Namaliza kazi Yangu tu, wakati ninyi mnafuatilia maisha, mchakato unaohusisha safari ndefu katika maisha. Ni baada tu ya kupitia mambo mengi ndipo mtaweza kupata njia ya maisha kikamilifu; ni hapo tu ndipo mtaweza kubaini maana ya ndani ya maneno Nizungumzayo leo. Mtakapokuwa na maneno Yangu mikononi mwenu, wakati kila mmoja wenu amepokea maagizo Yangu yote, punde Nitakapowaagizia yote Nipasayo, na wakati kazi ya maneno Yangu imemalizika, basi utekelezaji wa mapenzi ya Mungu pia utakuwa umetimizwa, bila kujali jinsi matokeo makubwa yamefanikishwa. Siyo jinsi unavyodhani, kwamba ni lazima ubadilishwe hadi kiwango fulani; Mungu hatendi kulingana na fikira zako.

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji