I. Ni Kipi Kikubwa Zaidi: Mungu, au Biblia? Ni nini Uhusiano Kati ya Mungu na Biblia?

1. Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni kufuata imani tofauti tofauti na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia. Ni kusema kwamba, kama unasema unamwamini Bwana, basi ni lazima usome Biblia, unapaswa kula na kunywa Biblia, na nje ya Biblia hupaswi kuabudu kitabu kingine ambacho hakihusishi Biblia. Ikiwa utafanya hivyo, basi unamsaliti Mungu. Kuanzia kipindi ambapo kulikuwa na Biblia, imani ya watu kwa Bwana imekuwa imani katika Biblia. Badala ya kusema watu wanamwamini Bwana, ni bora kusema kwamba wanaamini Biblia; badala ya kusema wameanza kusoma Biblia, ni bora kusema wameanza kuamini Biblia; na badala ya kusema wamerudi mbele ya Bwana, ingekuwa vyema kusema wamerudi mbele ya Biblia. Kwa njia hii, watu wanaiabudu Biblia kana kwamba ni Mungu, kana kwamba ni damu yao ya uzima na kuipoteza itakuwa ni sawa na kupoteza maisha yao. Watu wanaitazama Biblia kuwa ni kuu kama Mungu, na hata kuna wale wanaoiona kuwa ni kuu kuliko Mungu. Kama watu hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa hawawezi kuhisi Mungu, wanaweza kuendelea kuishi—lakini punde tu watakapoipoteza Biblia, au kupoteza sura na maneno maarufu sana kutoka katika Biblia, basi inakuwa ni kana kwamba wamepoteza maisha yao. Na hivyo, pale ambapo watu wataanza kumwamini Bwana wanaanza kusoma Biblia, na kuikariri Biblia, na kadri ya sehemu kubwa ya Biblia wanayoweza kukariri, ndivyo hii inathibitisha kwamba wanampenda Bwana na ni watu wenye imani kuu. Wale ambao wameisoma Biblia na wanaweza kuizungumzia kwa wengine wote ni kaka na dada wazuri. Kwa miaka yote hii, imani ya watu na uaminifu kwa Bwana vimepimwa kulingana na kiwango cha ufahamu wao wa Biblia. Watu wengi hawaelewi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini Mungu, na hawafanyi chochote zaidi ya kutafuta kiupofu dondoo ili kufasiri sura za Biblia. Watu hawajawahi kufuata mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu; muda wote huo, hawajafanya chochote, bali kujifunza na kuchunguza Biblia kwa papara, na hakuna hata mmoja ambaye amepata kazi mpya ya Roho Mtakatifu nje ya Biblia, hakuna ambaye amewahi kujitenga na Biblia, wala kuthubutu kujitenga na Biblia. Watu wamejifunza Biblia kwa miaka yote hii, wamekuja na maelezo mengi sana, na kufanya kazi kubwa sana, pia wana maoni mengi tofauti kuhusu Biblia, ambayo yamekuwa ni mdahalo usiokwisha, kiasi kwamba ziadi ya madhehebu elfu mbili yameanzishwa hadi leo. Wote wanataka kutafuta ufafanuzi maalumu, au siri za kina zaidi katika Biblia, wanataka kuichunguza, na kuipata katika usuli wa kazi ya Yehova katika Israeli, au usuli wa kazi ya Yesu katika Yudea, au siri nyingi zaidi ambazo hakuna yeyote anayejua. Watu wanavyoichukulia Biblia ni shauku na imani, na hakuna anayeweza kufafanua kikamilifu kisa cha ndani au kiini cha Biblia. Kwa hivyo, leo watu bado wana hisia zisizoelezeka za kimiujiza linapokuja suala la Biblia, na hata wana shauku nayo zaidi, na wanaiamini hata zaidi. Leo, kila mtu anataka kutafuta unabii wa kazi ya siku za mwisho katika Biblia, wanataka kugundua ni kazi gani Mungu hufanya wakati wa siku za mwisho na kuna ishara gani ya siku za mwisho. Kwa njia hii, kuabudu kwao Biblia kunakuwa na maana sana, na kadri wanaposogelea siku za mwisho, ndivyo wanavyozidi kuonyesha imani pofu kwa unabii wa Biblia, hususani ule wa siku za mwisho. Kwa imani hiyo ya upofu katika Biblia, kwa imani hiyo katika Biblia, hawana shauku ya kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Katika dhana za watu, wanadhani kwamba ni Biblia pekee ndiyo inayoweza kuleta kazi ya Roho Mtakatifu; ni katika Biblia pekee ndimo wanamoweza kupata nyayo za Mungu; ni katika Biblia pekee ndimo kulimofichika siri za kazi ya Mungu; ni kwenye Biblia pekee—na sio katika vitabu vinginevyo au watu—wanaoweza kufafanua kila kitu cha Mungu na ujumla wa kazi Yake; Biblia inaweza kuleta kazi ya mbinguni duniani; na Biblia inaweza kuanzisha na kuhitimisha enzi. Kwa dhana hizi, watu hawana shauku kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo, licha ya kiasi gani Biblia ilikuwa ina msaada mkubwa kwa watu wa wakati wa nyuma, imekuwa ni kikwazo katika kazi ya Mungu ya hivi karibuni. Bila Biblia, watu wanaweza kutafuta nyayo za Mungu mahali kwingineko, bado leo, nyayo zake zimejumuishwa na Biblia, na kupanua kazi Yake ya hivi karibuni, imekuwa na ugumu mara mbili, na mapambano magumu. Hii yote ni kwa sababu ya sura na misemo maarufu kutoka katika Biblia, vilevile unabii mbalimbali wa Biblia. Biblia imekuwa sanamu katika akili za watu, limekuwa ni fumbo katika akili zao, na hawawezi kabisa kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi nje ya Biblia, hawawezi kuamini kwamba watu wanaweza kumpata Mungu nje ya Biblia, achilia mbali kuwa na uwezo wa kuamini kwamba Mungu angeweza kujitenga na Biblia wakati wa kazi ya mwisho na kuanza upya. Hili suala haliingii akilini mwa watu; hawawezi kuliamini, na wala hawawezi kulifikiria. Biblia imekuwa kikwazo kikubwa kwa watu kukubali kazi mpya ya Mungu, na imefanya kuwa vigumu kwa Mungu kuipanua kazi hii mpya.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Huu ni ufahamu wenye makosa wa mwanadamu, na hauafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, sembuse kuona maono ambayo Yohana aliona. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. … Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Wakati wa kipindi cha Yesu, Yesu aliwaongoza Wayahudi na wale wote ambao walimfuata Yeye kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu katika Yeye wakati huo. Hakuichukulia Biblia kama msingi wa kile Alichofanya, bali Alizungumza kulingana na kazi Yake; Hakutilia maanani kile ambacho Biblia ilisema, wala hakutafuta katika Biblia njia ya kuongoza wafuasi Wake. Kuanzia pale Alipoanza kufanya kazi, Aliongoza njia ya toba—neno ambalo halikutajwa kabisa katika unabii wa Agano la Kale. Sio kwamba tu Hakutenda kulingana na Biblia, lakini pia Aliongoza njia mpya, na Akafanya kazi mpya. Na wala Hakurejelea kabisa Biblia Alipohubiri. Wakati wa Enzi ya Sheria, hakuna ambaye aliweza kufanya miujiza Yake ya kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Hivyo, pia, kazi Yake, mafundisho Yake, na mamlaka na nguvu za maneno Yake yalizidi mtu yeyote wakati wa Enzi ya Sheria. Yesu alifanya tu kazi Yake mpya, na ingawa watu wengi walimhukumu kwa kutumia Biblia—na hata wakatumia Agano la Kale kumsulubisha—kazi Yake ilipitiliza Agano la Kale; kama hii haikuwa hivyo, kwa nini watu walimwangika msalabani? Ilikuwa ni kwa sababu haikusema kitu katika Agano la Kale la mafundisho Yake, na uwezo Wake wa kuponya wagonjwa na kutoa mapepo? Kazi Yake ilikuwa ni kwa ajili ya kuongoza katika njia mpya, haikuwa ni kwa makusudi ya kufanya ugomvi dhidi ya Biblia, au kwa makusudi kujitenga na Agano la Kale. Alikuja tu kufanya huduma Yake, kuleta kazi mpya kwa wale waliomtamani sana na kumtafuta. Hakuja kufafanua Agano la Kale au kutetea kazi yake. Kazi Yake bado haikuwa ni kwa ajili ya kuruhusu Enzi ya Sheria kuendelea kukua, maana kazi Yake haikuzingatia Biblia kama msingi wake; Yesu alikuja kufanya tu kazi ambayo Alipaswa kufanya. Hivyo, Hakufafanua unabii wa Agano la Kale, wala Hakufanya kazi kulingana na maneno ya Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Alipuuzia kile ambacho Agano la Kale lilisema, Hakujalia kama lilikubaliana na kazi Yake au la, na Hakujali kile ambacho watu wengine walijua kuhusu kazi Yake, au namna walivyokuwa wakiihukumu. Aliendelea tu kufanya kazi ambayo Alipaswa kufanya, ingawa watu wengi walitumia unabii waliousema manabii wa Agano la Kale kumhukumu. Ilionekana kwa watu kana kwamba kazi Yake haikuwa na msingi, na kulikuwa na mengi ambayo yalikuwa hayapatani na rekodi za Agano la Kale. Je, haya hayakuwa makosa ya mwanadamu? Je, kuna haja ya kutumia mafundisho ya dini katika kazi ya Mungu? Je, ni lazima iwe kulingana na maneno ya unabii waliyosema manabii? Hata hivyo, kipi ni kikubwa: Mungu au Biblia? Kwa nini ni lazima kazi ya Mungu iwe kulingana na Biblia? Je, inaweza kuwa kwamba Mungu hana haki ya kuwa juu ya Biblia? Je, Mungu hawezi kujitenga na Biblia na kufanya kazi nyingine? Kwa nini Yesu na wanafunzi Wake hawakutunza Sabato? Ikiwa Angetunza Sabato na matendo mengine kulingana na amri za Agano la Kale, kwa nini Yesu Hakutunza Sabato baada ya kuja, lakini badala yake Aliitawadha miguu, Akafunika kichwa, Akavunja mkate, na kunywa divai? Je, sio kwamba haya yote hayapatikani katika amri za Agano la Kale? Ikiwa Yesu aliliheshimu Agano la Kale, kwa nini Aliyakataa mafundisho haya. Unapaswa kujua ni kipi kilitangulia, Mungu au Biblia! Kuwa Bwana wa Sabato, je, Asingeweza pia kuwa Bwana wa Biblia?

… Hivyo, Alisema: “Msidhani ya kwamba Nilikuja kuiharibu torati au manabii; Sikuja kuharibu, bali kutimiliza.” Hivyo, kulingana na kile Alichokitimiza, mafundisho mengi yalikuwa yamevunjwa. Siku ya Sabato Alipowachukua wanafunzi wake kuenda katika shamba la nafaka, walichuma na kula masuke: Alikuwa Anaivunja Sabato, na Akasema, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya sabato.” Kwa wakati huo, kulingana na sheria za Waisraeli, yeyote ambaye alikuwa haitunzi Sabato angepigwa na mawe hadi kufa. Hata hivyo Yesu, wala Hakuingia hekaluni wala Hakuitunza Sabato, na kazi Yake haikuwa imefanywa na Yehova wakati wa Agano la Kale. Hivyo, kazi aliyoifanya Yesu inapita sheria ya Agano la Kale, ilikuwa ni ya juu kuipita, na haikuwa na ulinganifu nayo. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale, Aliyakataa mafundisho hayo. Lakini Waisraeli waliishikilia Biblia vikali na wakamshutumu Yesu—je, huku hukuwa kuikataa kazi ya Yesu? Leo, dunia ya dini pia inaishikilia Biblia vikali, na watu wengine husema, “Biblia ni kitabu kitakatifu, na inapaswa kusomwa.” Baadhi ya watu husema, “Kazi ya Mungu inapaswa itetewe milele, Agano la Kale ni agano la Mungu na Waisraeli, na haliwezi kubadilishwa, na Sabato inapaswa kutunzwa siku zote!” Je, hawa sio wapuuzi? Kwa nini Yesu Hakutunza Sabato? Je, Alikuwa Anafanya dhambi? Nani anaweza kuelewa mambo hayo?

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Matamshi na kazi ya Yesu wakati huo hayakushikilia mafundisho, na hakufanya kazi Yake kulingana na kazi ya sheria ya Agano la Kale. Yalilingana na kazi iliyopaswa kufanywa kwa Enzi ya Neema. Alitenda kulingana na kazi Aliyokuwa ameleta mbele, kulingana na mipango Yake, na kulingana na huduma Yake; Hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale. Hakuna Alichofanya kilicholingana na Agano la Kale, na Hakuja kufanya kazi ili kutimiza maneno ya manabii. Kila hatua ya kazi ya Mungu haikuwa wazi ili kutimiza utabiri wa manabii wa zamani, na Hakuja kuyafuata mafundisho au kutambua makusudi utabiri wa manabii wa kale. Bado vitendo Vyake havikuvuruga utabiri wa manabii wa kale, wala havikuvuruga kazi Aliyokuwa amefanya awali. Hatua muhimu ya kazi Yake haikuwa kufuata mafundisho yoyote, na kufanya kazi ambayo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya. Yeye hakuwa nabii wala mwaguzi, ila mtendaji, aliyekuja kufanya hiyo kazi Aliyopaswa kufanya, na aliyekuja kufungua enzi Yake mpya na kufanya kazi Yake mpya. Bila shaka, Yesu alipokuja kufanya kazi Yake, pia Alitimiza maneno mengi yaliyosemwa na manabii wa zamani kwa Agano la Kale. Hivyo pia kazi ya leo imetimiza utabiri wa manabii wa zamani wa Agano la Kale. Ni vile tu Sishikilii hiyo “kalenda njano ya zamani,” hayo tu. Kwani kuna kazi zaidi ambayo lazima Nifanye, kuna maneno zaidi ambayo lazima Niwazungumzie, na kazi hii na maneno haya ni ya umuhimu mkubwa kuliko kueleza vifungu kutoka Biblia, kwa sababu kazi kama hiyo haina maana ama thamani kubwa kwenu, na haiwezi kuwasaidia, au kuwabadilisha. Ninanuia kufanya kazi mpya sio kwa ajili ya kutimiza kifungu chochote kutoka Biblia. Ikiwa Mungu alikuja duniani tu kutimiza maneno ya manabii wa Biblia, basi ni nani aliye mkuu, Mungu wa mwili ama hao manabii wa zamani. Na hata hivyo, hao manabii ni wasimamizi wa Mungu, ama Mungu ni msimamizi wa manabii? Unaweza kueleza haya maneno jinsi gani?

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Majina na Utambulisho” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni mkondo sawa, na unastahili kuukubali bila wasiwasi wowote hata kidogo; hufai ya kuchukua na kuchagua kipi cha kukubali. Ukipata ufahamu zaidi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari zaidi Kwake, basi hili silo tendo lisilohitajika? Huna haja kutafuta uthibitisho zaidi kutoka kwa Biblia; iwapo ni ya Roho Mtakatifu huna budi kuikubali, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu. … Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. … Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni Mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo?

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Wale wanaojali tu kuhusu maneno ya Biblia, wasiojali kuhusu ukweli au kutafuta nyayo Zangu—wao wananipinga, kwa kuwa wao wananizuilia Mimi kulingana na Biblia, na kuniwekea vizuizi ndani ya na Biblia, na hivyo ni wa kukufuru pakubwa dhidi Yangu. Jinsi gani watu wa aina hii wanaweza kuja mbele Zangu? Wao hawatilii maanani matendo Yangu, au mapenzi Yangu, au ukweli, badala yake wanashikilia maneno, maneno yanayoua. Jinsi gani watu kama hao wanaweza kulingana na Mimi?

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Biblia ni rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu katika Israeli, na inaandika utabiri mwingi wa manabii wa kale vilevile baadhi ya matamshi ya Yehova katika kazi Yake wakati huo. Hivyo, watu wote wanakitazama kitabu hiki kama kitakatifu (maana Mungu ni mtakatifu na mkuu). Kimsingi, hii yote ni matokeo ya uchaji wao kwa Yehova na vile walivyokuwa wanampenda Mungu. Watu wanarejelea kitabu hiki kwa namna hii kwa sababu tu viumbe wa Mungu wacha Mungu na wanampenda Muumba wao sana, na hata kuna wale ambao wanakiita kitabu hiki kitabu cha mbinguni. Kimsingi, ni rekodi tu za kibinadamu. Hakikupewa jina na Yehova Mwenyewe, wala Yehova Mwenyewe hakuongoza utengenezaji wake. Kwa maneno mengine, mwandishi wa kitabu hiki sio Mungu, bali ni wanadamu. Biblia Takatifu ni jina la heshima tu lililotolewa na mwanadamu. Jina hili halikuamuliwa na Yehova na Yesu baada ya Wao kujadiliana; si chochote zaidi ya mawazo ya kibinadamu. Maana kitabu hiki hakikuandikwa na Yehova, wala kuandikwa na Yesu. Badala yake, ni maelezo yaliyotolewa na manabii wengi wa kale, mitume na waonaji maono, ambayo baadaye yalipangiliwa na vizazi vilivyofuata na kuwa kitabu cha maandiko ya kale, ambayo kwa watu, yanaonekana kuwa matakatifu, kitabu ambacho wanaamini kimejumuisha siri nyingi ambazo hazieleweki na za kina ambazo zinasubiri kufunguliwa na vizazi vijavyo.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Agano la Kale ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Agano la Kale la Biblia linarekodi kazi yote ya Yehova wakati wa Enzi ya Sheria na kazi Yake ya uumbaji. Lote linarekodi kazi iliyofanywa na Yehova, na hatimaye linahitimisha maelezo ya kazi ya Yehova kwa kitabu cha Malaki. Agano la Kale linarekodi kazi mbili zilizofanywa na Mungu: Moja ni kazi ya uumbaji, na nyingine ni kuamrisha sheria. Zote ni kazi zilizofanywa na Yehova. Enzi ya Sheria inawakilisha kazi chini ya jina la Yehova Mungu; ni ujumla wa kazi iliyofanywa kimsingi chini ya jina la Yehova. Hivyo, Agano la Kale linarekodi kazi ya Yehova, na Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu, kazi ambayo kimsingi ilifanywa chini ya jina la Yesu. Umuhimu wa jina la Yesu na kazi Aliyoifanya imerekodiwa sanasana katika Agano Jipya. Wakati wa Agano la Kale Enzi ya Sheria, Yehova alijenga hekalu na madhabahu katika Israeli, Aliongoza maisha ya Waisraeli duniani, kuzingatia kwamba walikuwa watu Wake, kundi la kwanza la watu ambalo alilichagua duniani na ambao walikuwa wanautafuta moyo Wake, kundi la kwanza ambalo Yeye Mwenyewe aliliongoza; ni sawa na kusema, makabila kumi na mawili ya Israeli walikuwa ni wateule wa kwanza wa Yehova, na hivyo siku zote Alifanya kazi ndani yao, hadi ambapo kazi ya Yehova ya Enzi ya Sheria ilihitimishwa. Hatua ya pili ya kazi ilikuwa ni kazi ya Enzi ya Neema ya Agano Jipya, na ilifanyika kati ya watu wa Kiyahudi, kati ya mojawapo ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Mawanda ya kazi hii yalikuwa madogo kwa sababu Yesu alikuwa Mungu aliyepata mwili. Yesu alifanya kazi katika eneo lote la Yudea pekee, na Alifanya tu kazi ya miaka mitatu na nusu; hivyo, kile kilichorekodiwa katika Agano la Kale kiko mbali zaidi kupitiliza kiwango cha kazi kilichorekodiwa katika Agano la Kale. Kazi ya Yesu ya Enzi ya Neema kimsingi imerekodiwa katika Injili Nne. Njia iliyopitiwa na watu wa Enzi ya Neema ilikuwa ile mabadiliko ya juu juu katika tabia yao ya maisha, nyingi zaidi ambayo imerekodiwa katika nyaraka.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Vitabu vya injili ya Agano Jipya vilirekodiwa miaka ishirini hadi thelathini baada ya Yesu kusulubiwa msalabani. Kabla ya hapo, watu wa Israeli walisoma tu Agano la Kale. Hiyo ni sawa na kusema, mwanzoni mwa Enzi ya Neema watu walisoma Agano la Kale. Agano Jipya lilionekana tu wakati wa Enzi ya Neema. Agano Jipya halikuwepo wakati wa kazi ya Yesu; watu waliandika kazi Yake baada ya kuwa amefufuka na kupaa mbinguni. Baada ya hapo kulikuwa na Injili Nne, katika nyongeza hiyo pia kulikuwa na nyaraka za Paulo na Petro, na vile vile kitabu cha Ufunuo. Ni baada tu ya zaidi ya miaka mia tatu baada ya Yesu kupaa mbinguni, wakati vizazi vilivyofuata viliweka pamoja rekodi zao, ndipo kulikuwa na Agano Jipya. Ni baada tu ya kazi hii kukamilika ndipo kukapatikana Agano Jipya; halikuwepo hapo kabla. … Inaweza kusemwa kuwa, kile walichorekodi kilikuwa ni kulingana na kiwango chao cha elimu na tabia. Kile walichokirekodi kilikuwa ni uzoefu wa wanadamu, na kila mmoja alikuwa na namna yake ya kurekodi na kuelewa, na kila rekodi ilikuwa tofauti. Hivyo, ikiwa unaiabudu Biblia kama Mungu wewe ni mjinga na mpumbavu wa kutupwa!

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Yote yaliyoandikwa katika Biblia ni machache na hayawezi kuwakilisha kazi yote ya Mungu. Injili Nne zina chini ya sura mia moja zote pamoja ambamo mliandikwa mambo yale yaliotendeka yanayohesabika, kwa mfano Yesu Akilaani mti wa mkuyu, Petro akimkana Bwana mara tatu, Yesu Akiwaonekania wanafunzi Wake baada ya kusulubiwa na ufufuo Wake, Akifunza kuhusu kufunga, kufunza kuhusu maombi, kufunza kuhusu talaka, kuzaliwa na kizazi cha Yesu, uteuzi wa Yesu wa wanafunzi, na mengine mengi. Hata hivyo, mwanadamu anayathamini kama hazina, hata kuthibitisha kazi ya leo kulingana nayo. Hata wanaamini kuwa Yesu Alitenda kiasi tu katika muda baada ya kuzaliwa Kwake. Ni kana kwamba wanaamini kuwa Mungu anaweza kufanya hayo tu, kwamba hakuna kazi nyingine. Je huu si upumbavu?

Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Katika kusoma Biblia watu wanaweza pia kupata njia nyingi za maisha ambazo haziwezi kupatikana katika vitabu vingine. Njia hizi ni njia za maisha ya kazi ya Roho Mtakatifu ambazo manabii na mitume walizipitia katika enzi iliyopita, na maneno mengi ni ya thamani, na yanaweza kutoa kile ambacho watu wanataka. Hivyo, watu wote wanapenda kusoma Biblia. Kwa sababu kuna mambo mengi sana yaliyofichwa katika Biblia, mitazamo ya watu juu ya Biblia ni tofauti na mitazamo yao juu ya maandiko ya viongozi wa kiroho mashuhuri. Biblia ni rekodi na mkusanyiko wa uzoefu na maarifa ya watu ambao walimhudumia Yehova na Yesu katika enzi ya kale na mpya, na pia vizazi vya baadaye vimeweza kupata nuru, mwanga mkubwa na njia za kuweza kutembea kwazo. Sababu ya Biblia kuwa na hadhi ya juu kuliko maandiko ya kiongozi yeyote mkubwa wa kiroho ni kwa sababu maandiko yao yote yanatoka katika Biblia, uzoefu wao wote unatokana na Biblia, na wote wanaelezea Biblia. Na hivyo, ingawa watu wanaweza wakafaidika na vitabu kutoka kwa kiongozi yeyote wa kiroho mashuhuri, bado wanaiabudu Biblia, maana kwao, inaonekana ni ya juu sana na ya kina sana! Ingawa Biblia inaleta pamoja baadhi ya vitabu vya maneno ya uzima, kama vile nyaraka za Paulo na nyaraka za Petro, na ingawa watu wanaweza kusaidiwa na vitabu hivi, vitabu hivi bado vimepitwa na wakati, bado ni vitabu vya enzi ya kale, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, vinafaa tu kwa ajili ya kipindi kimoja, na wala sio vya milele. Maana kazi ya Mungu siku zote inaendelea, na haiwezi kusimama tu katika kipindi cha Paulo na Petro, au siku zote ibaki katika Enzi ya Neema, enzi ambayo Yesu alisulubiwa. Na hivyo, vitabu hivi vinafaa tu katika Enzi ya Neema, na wala sio kwa ajili ya Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho. Vinaweza tu kuwa na manufaa kwa waumini wa Enzi ya Neema, na sio kwa watakatifu wa Enzi ya Ufalme, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, bado havifai kwa kipindi hiki. Ni sawa na kazi ya Yehova ya uumbaji au kazi Yake katika Israeli: Haijalishi kazi hii ilikuwa kubwa kiasi gani, bado imepitwa na wakati, na muda utaendelea kuja wakati umekwishapita. Kazi ya Mungu pia ni ile ile: Ni nzuri, lakini muda utafika ambapo itakoma; siku zote haitaendelea kubaki katikati ya kazi ya uumbaji, wala katikati ya kazi ile ya msalaba. Haijalishi kazi ya msalaba inashawishi kiasi gani, haijalishi ilikuwa ya ufanisi kiasi gani katika kumshinda Shetani, hata hivyo, kazi bado ni kazi, na enzi, hata hivyo bado ni enzi; kazi siku zote haiwezi kubaki katika msingi ule ule, wala nyakati haziwezi kukosa kubadilika, kwa sababu kulikuwa na uumbaji na lazima kuwepo na siku za mwisho. Hii haiepukiki! Hivyo, leo maneno ya uzima katika Agano Jipya—nyaraka za mitume, na Injili Nne—vimekuwa vitabu vya kihistoria, vimekuwa vitabu vya kale, na inawezekanaje vitabu vya kale kuwapeleka watu katika enzi mpya? Haijalishi ni kiasi gani vitabu hivi vinaweza kuwapatia watu uzima, haijalishi vina uwezo kiasi gani katika kuwaongoza watu kwenye msalaba, ndio kwamba havijapitwa na wakati? Havijaondokewa na thamani?

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria. Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu duniani, ambayo ipo katika Injili Nne, vilevile kazi ya Paulo; je, sio rekodi za kihistoria? Kuleta mambo ya zamani leo kunayafanya yawe historia, haijalishi yana ukweli kiasi gani, bado ni historia—na historia haiwezi kushughulikia masuala ya leo. Maana Mungu haangalii historia! Na hivyo, kama unaelewa tu Biblia, na huelewi chochote kuhusu kazi ambayo Mungu anakusudia kufanya leo, na kama unamwamini Mungu, na hutafuti kazi ya Roho Mtakatifu, basi hujui inamaanisha nini kumtafuta Mungu. Ikiwa unasoma Biblia kwa lengo la kujifunza historia ya Israeli, kutafiti historia ya uumbaji wa Mungu wa mbingu na dunia, basi humwamini Mungu. Lakini leo, kwa kuwa unamwamini Mungu, na kutafuta uzima, kwa kuwa unatafuta maarifa juu ya Mungu, na hutafuti nyaraka na mafundisho mfu, au ufahamu wa historia, unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu ya leo, na unapaswa kutafuta uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Kama ungekuwa mwanaakiolojia ungeweza kusoma Biblia—lakini wewe sio mwanaakiolojia, wewe ni mmoja wa wale wanaomwamini Mungu, na utakuwa bora zaidi ukitafuta mapenzi ya Mungu ya leo.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. Leo, Mungu amefanyika mwili, na Amewachagua wateule wengine katika nchi ya China. Mungu anafanya kazi ndani ya watu hawa, Anaendelea na kazi Yake duniani, Anaendelea kutoka katika kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. Hivyo, kazi ambayo haijawahi kufanywa kabla sio historia, kwa sababu sasa ni sasa, na bado haijawa muda uliopita. Watu hawajui kwamba Mungu amefanya kazi kubwa, mpya duniani, na nje ya Israeli, yaani imevuka mawanda ya Israeli, na zaidi ya unabii wa manabii, ambayo ni kazi mpya na ya kushangaza nje ya unabii, na kazi mpya kabisa nje ya Israeli, na kazi ambayo watu hawawezi kuielewa au kufikiria. Inawezekanaje Biblia kuwa na rekodi za wazi za kazi kama hiyo? Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya. Unapaswa kuelewa ni kwa nini leo unaambiwa usisome Biblia, kwa nini kuna kazi nyingine ambayo inajitenga na Biblia, kwa nini Mungu haonekani mpya na wa kina zaidi katika Biblia, kwa nini badala yake kuna kazi kubwa zaidi nje ya Biblia. Haya ndiyo yote mnayopaswa kuelewa.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Mungu angeweza kuwa na mwanzo mpya kwa nyingi za kazi Anazotaka kufanya na mambo Anayotaka kusema. Punde Anapokuwa na mwanzo mpya, Hataji kazi Yake ya awali tena wala kuiendeleza. Kwani Mungu anazo kanuni Zake katika kazi Yake. Anapotaka kuanzisha kazi mpya, ndipo Anapotaka kumleta mwanadamu katika awamu mpya ya kazi Yake, na wakati kazi Yake imeingia katika awamu ya juu zaidi. Kama watu wanaendelea kutenda kulingana na misemo au taratibu za kale au kuendelea kushikilia kabisa kwazo, Hatakumbuka au kulisifu jambo hili. Hii ni kwa sababu tayari Ameileta kazi mpya, na ameingia katika awamu mpya ya kazi Yake. Anapoanzisha kazi mpya, Anaonekana kwa mwanadamu akiwa na taswira mpya kabisa, kutoka katika mtazamo mpya kabisa, na kwa njia mpya kabisa ili watu waweze kuona dhana zile tofauti za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hii ni mojawapo ya malengo Yake katika kazi Yake mpya. Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi; Anapofanya kazi na kuongea sio njia ya kutilia mipaka kama vile watu wanavyofikiria. Ndani ya Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa, na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye yuko hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Wakati huo, Yesu alisema kuwa kazi ya Yehova ilikuwa imebaki nyuma kwa Enzi ya Neema, kama Nisemavyo leo kwamba kazi ya Yesu imebaki nyuma. Kama kungekuwa tu na Enzi ya Sheria na siyo Enzi ya Neema, Yesu hangeweza kusulubiwa na hangeweza kuwakomboa wanadamu wote; kungekuwa tu na Enzi ya Sheria, kungekuwa na uwezekano wa mwanadamu kuendelea hadi siku ya leo? Historia inaendelea mbele; historia sio asili ya sheria ya kazi ya Mungu? Hii sio picha ya usimamizi Wake wa mwanadamu ndani ya ulimwengu mzima? Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga. Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno “mpya” na “ajabu.”

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Kwa kuwa kuna njia ya juu, kwa nini mjifunze hiyo ya chini, njia ya kale? Kwa kuwa kuna matamshi mapya, na kazi mpya, kwa nini uishi katikati ya rekodi za kale za kihistoria? Matamshi mapya yanaweza kukupa, ambayo yanathibitisha kwamba hii ni kazi mpya; rekodi za kale haziwezi kukushibisha, au kutosheleza mahitaji yako ya sasa, kitu ambacho kinathibitisha kwamba ni historia, na sio kazi ya hapa na sasa. Njia ya juu zaidi ni njia mpya zaidi, na kazi mpya, bila kujali njia ya zamani ni ya juu kiasi gani, bado ni historia ya kumbukumbu ya watu, na haijalishi ina thamani kiasi gani kama rejeleo, bado ni njia ya kale. Ingawa imerekodiwa katika “kitabu kitakatifu,” njia ya kale ni historia; ingawa hakuna rekodi yake katika “kitabu kitakatifu,” njia mpya ni ya hapa na sasa. Kwa njia hii inaweza kukuokoa, na kwa njia hii inaweza kukubadilisha, maana hii ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Mkitumia fikira zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkimwekea Mungu mipaka kabisa katika vigezo vya Biblia na kumweka katika mawanda ya kazi yenye mipaka, basi hii inathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo lisilobadilika waliloshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yeye aliyeitwa Masihi pekee ndiye Angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu binadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—hivyo Yesu asiye na hatia Alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, mwanadamu alikataa kumsamehe, naye alisisitiza kumhukumu afe na basi Yesu akasulubishwa. Kila wakati mwanadamu huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu ana ufahamu wa kina kuhusu usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwanadamu anavyo vitu vyote atendavyo Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea jambo. Bila kujali jinsi kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu kilivyo, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo kabisa wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kamilifu na Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Waovu Hakika Wataadhibiwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, na haziwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyoshawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Mungu Mwenyewe aeleze na kumfichulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa. Kazi hii ya miaka elfu sita ni ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii. Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji, na hakuna nabii wa awali ambaye amewahi kuweza kulielewa, kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho na kamwe halijawahi kufichuliwa hapo awali. Mkielewa fumbo hili na muweze kulipokea kwa ukamilifu, wale watu wote wa kidini watashindwa kwa fumbo hili. Hili pekee ndilo kuu zaidi ya maono, lile ambalo mwanadamu hutamani sana kulielewa lakini pia lile ambalo si wazi zaidi kwake.

Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Kipande cha gogo lililokufa: Nahau ya Kichina yenye maana “-siyoweza kusaidiwa.”

Iliyotangulia: Je, Utatu Upo?

Inayofuata: II. Juu ya Ukweli wa Kupata Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuhusu Maisha ya Petro

Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp