1. Sababu ya Bwana Yesu kuwalaani Mafarisayo, na ni nini kiini cha Mafarisayo

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa nini nyinyi pia mnavunja amri ya Mungu kwa utamaduni wenu? Kwani Mungu aliamuru, Akisema, Mwonyeshe babako na mamako heshima: na, Yule anayemlaani baba au mama yake, na afe hicho kifo. Lakini mnasema, Yeyote ambaye atamwambia baba au mama yake, ni zawadi, chochote ambacho ungefaidi kupitia mimi; Na asimwonyeshe baba yake au mama yake heshima, atakuwa huru. Hivyo hamjaibatilisha amri ya Mungu kwa utamaduni wenu. Nyinyi wanafiki, Isaya alitabiri vyema kuwahusu, akisema, Watu hawa wananikaribia kwa vinywa vyao, na wananiheshimu kwa midomo yao; lakini moyo wao uko mbali nami. Lakini wananiabudu bure, wakifunza mafundisho ya dini ambayo ni amri za wanadamu” (Mathayo 15:3-9).

“Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi.

“Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.

“Ole wenu ninyi, viongozi mlio vipofu, mnaosema, Yeyote atakayeapa kupitia kwa hekalu, haimaanishi chochote; lakini yeyote atakayeapa kupitia kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa kwa kiapo hicho. Ninyi mlio wapumbavu na vipofu: kwa kuwa kipi kilicho kikubwa zaidi, hiyo dhahabu, au hilo hekalu linaloitakasa dhahabu? Na, Yeyote atakayeapa kupitia kwa madhabahu, haimaanishi chochote; lakini yeyote atakayeapa kupitia kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu hiyo, amefungwa kwa kiapo hicho. Ninyi mlio wapumbavu na vipofu, kwa kuwa ni kipi kilicho kikubwa zaidi, hiyo sadaka, au hiyo madhabahu inayoitakasa sadaka? Basi yeyote anayeapa kupitia kwa madhabahu, huapa kupitia kwa madhabahu hiyo, na kila kitu kilicho juu yake. Na yeyote anayeapa kupitia kwa hekalu, huapa kupitia kwa hekalu hilo, na kupitia kwa yeye anayekaa hekaluni. Na yule anayeapa kupitia kwa mbingu, huapa kupitia kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kupitia kwa yule anayeketi juu yake.

“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, ninyi wanafiki! kwani mnatoa fungu la kumi la mnanaa na bizari na jira, na mmeacha mambo muhimu zaidi ya sheria, hukumu, fadhili, na imani: mlipaswa kuyafanya haya, na sio kutolifanya lingine. Nyinyi viongozi vipofu, mnaochunguza sana visubi, na kumeza ngamia.

“Ole wenu ninyi, waandishi na Mafarisayo, wazandiki! Kwa maana mnaosha nje ya kikombe na sahani, lakini ndani yake kumejaa kutoza kwa nguvu na kupenda zaidi ya kiasi. Ewe Farisayo aliye kipofu, osha kwanza kikombe na sahani kwa ndani, ili nje viwe safi pia.

“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, nyinyi wanafiki! Kwani nyinyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, ambayo kwa nje yanaonekana mazuri sana, lakini ndani yake mna mifupa ya wafu, na yenye uchafu wote. Hata hivyo ninyi pia mnaonekana wenye haki kwa wanadamu, lakini ndani yenu mmejaa unafiki na dhambi.

“Ole wenu, ninyi waandishi na Mafarisayo, wazandiki! kwa sababu mnajenga makaburi ya manabii, na kupamba makaburi ya wenye haki, Na kusema, iwapo tungelikuwa katika siku za baba zetu, hatungelishiriki na wao kuwaua manabii. Kwa nini mnakuwa mashahidi kwenu wenyewe, kuwa ninyi ni wana wa hao ambao waliwaua manabii. Basi kijazeni kiwango cha baba zenu. Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu? Hivyo, tazama, natuma kwenu manabii, na wanadamu wenye busara, na waandishi: na mtauwa na kusulubisha baadhi yao; na mtawacharaza baadhi yao katika masinagogi yenu, na kuwatesa kutoka mji mmoja hadi mji mwingine: Ili damu yote yenye haki iliyomwagika duniani iweze kuwa juu yenu, kuanzia damu ya Habili aliyekuwa mwenye haki hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia, ambaye mlimwua katikati ya hekalu na madhabahu. Kweli nawaambieni, Mambo haya yote yatakifuata kizazi hiki” (Mathayo 23:13-36).

Maneno Husika ya Mungu:

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki?

Kimetoholewa kutoka katika “Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu

Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.

Mafarisayo Kukemewa na Yesu

Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.

…………

Katika Biblia, tathmini ya Mafarisayo kwa Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “walisema, Yeye si wa akili sawa. … Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Mafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa ikiiga mambo au ikifikiria tu kutoka popote—ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho yao ilitolewa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele ya watu ni kana kwamba ilikuwa imeshughulikiwa vyema, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kuvumilia. Nguvu zao mchafukoge za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua maono yao binafsi yasiyo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na maumbile yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na maono yao yasiyo na misingi, ya wivu, na hali ya ubovu na ubaya na ukatili wao dhidi ya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, walimshambulia bila mpango, bila subira, kwa njia za kishenzi, na kwa makusudi ya kijicho pamoja na kutupilia mbali kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilikuwa hadi kufikia kiwango cha kutupilia mbali Roho Wake bila kubagua, Yaani, Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu. Hivi ndivyo waliyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli,” na “mkuu wa pepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa pepo. Waliweza kupatia sifa ya kazi ambayo Roho wa Mungu mwenye mwili alikuwa amevalia kama kurukwa akili. Hawakukufuru tu Roho wa Mungu kama Beelzebuli na mkuu wa pepo, lakini waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upingaji wao na kukufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kutumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na watumishi wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na mapambano yao na Mungu yasiyoisha. Kiini cha upingaji wao kwa Mungu na mwelekeo wao wa ukatili kwake Yeye, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa ya na yale waliyoyasema na kufanya, na akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusameheka ulimwenguni humu na hata ulimwengu unaokuja, kama vile tu maandiko yafuatayo yanasema: “Wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” na “Yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.”

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Huko Israeli, “Mfarisayo” lilikuwa aina ya jina la heshima. Badala yake, kwa nini sasa ni jina la kupachikwa? Hii ni kwa sababu Wafarisayo wamekuwa wawakilishi wa aina fulani ya mtu. Je, tabia za mtu wa aina hii ni gani? Wao huimba wito na hutumia lugha inayoonekana ya juu; wana ustadi wa kujifanya, wa kujionyesha wenyewe kwa namna fulani, wa kujificha na wanaibua uungwana mkubwa, utakatifu na unyofu mkubwa, ukarimu na heshima kubwa. Kwa sababu hiyo, hawatendi ukweli hata kidogo. Je, wao hutendaje? Wao husoma maandiko, wao huhubiri, huwafundisha wengine kutenda mema, wasifanye uovu, wasimpinge Mungu; wao husema mambo ya kupendeza na hutenda vizuri mbele ya wengine, lakini wakati ambapo wengine hawaoni, wao huiba sadaka. Bwana Yesu alisema “wanachuja mbu na kumeza ngamia.” Hili linamaanisha kuwa tabia zao zote zinaonekana kuwa nzuri kwa nje—wanaimba wito kwa shaufu, wanazungumza nadharia kubwa kubwa na maneno yao husikika ya kupendeza, lakini matendo yao ni machafuko yasiyo na mpangilio, yanayompinga Mungu kabisa. Tabia zao na mwonekano wao wa nje vyote ni kujifanya, vyote ni ulaghai; mioyoni mwao, hawana upendo kwa ukweli hata kidogo, wala kwa vitu chanya. Hawapendi ukweli, hawapendi yote yanayotoka kwa Mungu, na hawapendi vitu chanya. Je, wanapenda nini? Je, wanapenda usawa na haki? (Hapana.) Unawezaje kujua kwamba hawapendi vitu hivi? (Bwana Yesu alikuja kufanya kazi na kueneza injili ya ufalme wa mbinguni, lakini walimshutumu.) Je, wasingemshutumu, je, ungeweza kujua? Kabla ya Bwana Yesu kuja kufanya kazi, je, ni kitu gani kingeweza kukuonyesha kwamba hawakupenda usawa na haki? Usingeweza kujua, sivyo? Tabia zao zote ni za kujifanya, na wao hutumia kujifanya huku kwa tabia nzuri kuwalaghai wengine uaminifu wao. Je, huu sio unafiki na udanganyifu? Je, wadanganyifu kama hao wanaweza kuupenda ukweli? Je, kusudi la siri la hii tabia yao nzuri ni lipi? Sehemu moja ya kusudi lao ni kuwadanganya wengine; sehemu nyingine ni kuwalaghai wengine, kupata uaminifu wao na kuabudiwa na wao, na mwisho, kupata thawabu. Je, mbinu zao ni za busara jinsi gani kiasi kwamba wanaweza kutekeleza ujanja mkubwa kama huu? Je, basi watu kama hawa wanapenda usawa na haki? Bila shaka hawapendi. Wanapenda hadhi, wanapenda umaarufu na utajiri, na wanatamani kupokea thawabu. Je, wao huyaweka katika vitendo maneno ya Mungu yanayowaongoza watu? La, hasha. Hawaishi kwa kuyadhihirisha hata kidogo; wao hujificha na kujiwasilisha wenyewe kwa namna fulani ili kuwachezea watu shere na kupata uaminifu wao, ili kushikiza hali yao wenyewe, ili kushikiza sifa zao wenyewe. Mara tu mambo haya yanapopatikana, wao huyatumia kupata mtaji na mahali pa kupata riziki. Je, hili si jambo la kustahili dharau? Inaweza kuonekana kutoka katika hizi tabia zao zote kwamba ni kiini chao kutopenda ukweli, kwa kuwa huwa hawautii ukweli katika vitendo kamwe. Je, ishara ya kwamba wao huwa hawautii ukweli katika vitendo ni ipi? Hii ndiyo ilikuwa ishara kubwa zaidi: Bwana Yesu alikuja kufanya kazi na kila kitu Alichosema kilikuwa sahihi, kila kitu Alichosema kilikuwa ukweli. Je, waliyachukuliaje hayo? (Hawakuyakubali.) Je, hawakuyabali maneno ya Bwana Yesu kwa sababu waliamini kuwa yalikuwa na makosa, au hawakuyakubali licha ya kujua kwamba yalikuwa sahihi? (Hawakuyakubali licha ya wao kujua walikuwa sahihi.) Na ni kitu ambacho kingeweza kusababisha haya? Hawaupendi ukweli, na wanachukia mambo chanya. Yote ambayo Bwana Yesu alisema yalikuwa sahihi, bila kosa lolote, na ingawa hawakuona kosa lolote katika maneno ya Bwana Yesu ili walitumie dhidi yake, walisema, “Je, si huyu ni mwana wa seremala?” Wakaanza kutafuta makosa katika maneno ya Bwana Yesu wayatumie dhidi Yake na walipokosa kupata yoyote, walimshutumu, kisha wakafanya njama: “Msulubishe. Ni yeye au sisi.” Kwa njia hii wanajiweka dhidi ya Bwana Yesu. Ingawa hawakuamini kuwa Bwana Yesu alikuwa Bwana, Alikuwa mtu mwema ambaye hakuvunja sheria za kidunia au sheria ya Musa; kwa nini walimshutumu Bwana Yesu? Kwa nini walimtendea Bwana Yesu hivyo? Inaweza kuonekana kutoka katika jinsi watu hawa ni waovu na wabaya—ni waovu kupita kiasi! Uso mbaya ambao Mafarisayo walifunua haungeweza kuwa tofauti zaidi na kujificha kwao katika fadhila. Kuna wengi ambao hawawezi kutambua ni ipi ndiyo sura yao ya kweli na ni upi ndio uwongo, lakini kuonekana kwa Bwana Yesu na kazi Yake viliwafichua wote. Mafarisayo hujificha vizuri sana, wao huonekana wema kwa nje—kama ukweli haungefichuliwa, hakuna mtu ambaye angeweza kuwaona jinsi walivyo kwa kweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Sehemu Muhimu Zaidi ya Kuamini Katika Mungu ni Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 2. Sababu ya Mungu kulibariki tu kanisa ambalo huikubali na kuitii kazi Yake, na kwa nini dunia ya kidini imelaaniwa na Mungu

Inayofuata: 2. Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo na kiini chao ni kipi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

3. Uhusiano kati ya hatua zote tatu za kazi ya Mungu

Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo.

1. Jinsi ambavyo mtu anaweza kujua asili ya uungu ya Kristo

Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki