1. Maana ya kuokolewa na kufikia wokovu kamili

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Yule ambaye anaamini na kubatizwa ataokolewa; lakini yule ambaye haamini atahukumiwa” (Marko 16:16).

“Kwa kuwa hii ni damu yangu ya agano jipya, ambayo inamwagwa kwa ajiki ya msamaha wa dhambi” (Mathayo 26:28).

“Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21).

Maneno Husika ya Mungu:

Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi.

Kimetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi.

Kimetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Umuhimu wa kumwamini Mungu ni kuokolewa, kwa hiyo kuokolewa kunamaanisha nini? “Kuokolewa,” “kujitenga na ushawishi mwovu wa Shetani”—watu huzungumza juu ya mada hizi mara nyingi, lakini hawajui kuokolewa kunamaanisha nini. Je, kuokolewa kunamaanisha nini? Hii inahusiana na mapenzi ya Mungu. Ili kuokolewa, kuzungumza kwa lugha ya wenyeji, kunamaanisha unaweza kuendelea kuishi, na kwamba unafufuliwa. Kwa hiyo kabla ya hayo, je, umekufa? Unaweza kuzungumza, na unaweza kupumua, kwa hivyo unawezaje kusemekana kwamba umekufa? (Roho imekufa.) Kwa nini inasemekana kwamba watu wamekufa ikiwa roho yao imekufa? Msingi wa msemo huu ni upi? Kabla ya kuokolewa, wako wapi? (Wanamilikiwa na Shetani.) Watu wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Wanategemea nini ili kuishi? (Falsafa na sumu za Shetani.) Wanategemea asili yao ya kishetani na asili potovu ili kuishi. Mtu anapoishi kwa kufuata mambo haya, nafsi yake nzima—mwili wake, na vipengele vingine vyote kama vile roho na mawazo yao—wako hai au wamekufa? Kutoka katika mtazamo wa Mungu, wao ni wafu. Kwa juu juu, unaonekana kuwa unapumua na kufikiria, lakini kila kitu unachokifikiria daima ni kiovu; unafikiria kuhusu vitu ambavyo vinamwasi Mungu na vya ukaidi dhidi ya Mungu, vitu ambavyo Mungu huchukia, hukirihi, na kushutumu. Machoni pa Mungu, mambo haya yote si ya mwili tu, bali pia ni ya Shetani na ya pepo kikamilifu. Kwa hiyo watu ni nini machoni pa Mungu? Je, wao ni wanadamu? La, wao si wanadamu. Mungu huwaona kama pepo, kama wanyama, na kama Shetani, Shetani waishio! Watu wanaishi kulingana na vitu na asili ya Shetani, na machoni pa Mungu, wao ni Shetani waishio waliovalia miili ya binadamu. Mungu huwafafanua watu kama hao kama maiti zinazotembea; kama wafu. Mungu anafanya kazi Yake ya sasa ya wokovu kuwachukua watu kama hawa—maiti hizi zinazotembea zinazoishi kwa kufuata tabia zao za kishetani na kwa kufuata viini vyao vipotovu vya kishetani—Anawachukua hawa wanaodaiwa kuwa wafu na kuwageuza kuwa walio hai. Hii ndiyo maana ya kuokolewa.

Sababu ya kumwamini Mungu ni kupata wokovu. Kuokolewa kunamaanisha kuwa unageuka kutoka kuwa mtu aliyekufa hadi kuwa mtu aliye hai. Maana ya hili ni kwamba pumzi yako inafufuliwa, na wewe unakuwa hai; unaweza kumwona Mungu, unaweza kumtambua, na unaweza kusujudu ili umwabudu Yeye. Moyoni mwako huna upinzani zaidi dhidi ya Mungu; humkatai tena, humshambulii tena, au kumuasi tena. Watu kama hawa tu ndio walio hai kwa kweli machoni pa Mungu. Mtu akisema tu kwamba anamkubali Mungu na anaamini moyoni mwake kwamba kuna Mungu, basi ni mmoja wa walio hai au la? (La, sio.) Kwa hiyo watu walio hai ni wa aina gani? Je, walio hai wana uhalisi wa aina gani? Angalau, walio hai wanaweza kuzungumza lugha ya binadamu. Hiyo ni nini? Inamaanisha kwamba maneno wanayotamka yanahusu mawazo, fikira, na utambuzi. Watu walio hai hufikiri na kufanya nini mara nyingi? Wanaweza kujihusisha na shughuli za binadamu, na kutimiza wajibu wao. Asili ya kile wanachofanya na kusema ni ipi? Ni kwamba kila kitu wanachofichua, kila kitu wanachofikiria, na kila kitu wanachofanya kinafanywa na asili ya kumcha Mungu na kuepuka uovu. Ili kuliweka kwa usahihi zaidi, kila tendo na kila wazo lako hakihukumiwi na Mungu au kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; badala yake, yanaidhinishwa na kusifiwa na Mungu. Hiki ndicho watu walio hai hufanya, na pia ndicho ambacho watu walio hai wanapaswa kufanya.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuwa Mtiifu Kwa Kweli Pekee Ndiyo Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani mwanadamu anaishi katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake.

Kimetoholewa kutoka katika “Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni kitu chenye najisi. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi na kuna maonyesho mengi sana ya mwili; hii ndiyo maana Mungu hudharau mwili wa mwanadamu kwa kiwango fulani. Watu wanapotupa mambo machafu, potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini bado wasipoachana na uchafu na upotovu, basi bado wanamilikiwa na Shetani. Ujanja, udanganyifu, na ukora wa watu yote ni mambo ya Shetani. Wokovu wa Mungu kwako ni ili kukuokoa kutoka katika mambo haya ya Shetani. Kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa; yote inafanywa ili kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini hadi kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena pingu na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unamilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na huwezi kupokea urithi wa Mungu. Mara tu unapotakaswa na kufanywa mkamilifu, utakuwa mtakatifu, utakuwa mtu wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na kuwa mtu anayemfurahisha Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale wasiofuata maarifa ya mambo katika Roho, wasiofuata utakatifu, na wasiofuata kuishi kulingana na maisha ya ukweli, wanaotosheka na kushindwa kwa upande wa kanusho, na wasioweza kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu na kuwa binadamu watakatifu—hawa ni watu ambao hawajaokolewa. Kwani, kama hana ukweli, mwanadamu hataweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu; wale watakaoweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu pekee ndio wale ambao wameokolewa. Ninalotaka Mimi ni watu kama Petro, watu wanaofuata kufanywa wakamilifu. Ukweli wa leo unatolewa kwa wale ambao wanautamani na kuutafuta. Wokovu huu unapewa wale ambao wanatamani kuokolewa na Mungu, na haujakusudiwa kuwafaidi tu, lakini ili pia ili mpatwe na Mungu. Mnampata Mungu ili Mungu pia awapate. Leo nimenena hayo maneno kwenu, na mmeyasikia, na mnafaa kutenda kulingana na maneno haya. Mwishowe, mkiweka maneno haya katika matendo ndipo nitakapowapata nyinyi kupitia katika maneno haya; na pia, mtakuwa mmepata maneno haya, kumaanisha, mtakuwa mmepata wokovu mkuu. Punde mtakapofanywa wasafi, mtakuwa wanadamu halisi. Kama huwezi kuishi kulingana na ukweli, ama kuishi kulingana na aliyefanywa mkamilifu, basi inaweza kusemwa kuwa wewe si binadamu, ila wewe ni mfu anayetembea, mnyama, kwa sababu huna ukweli, ni kusema huna pumzi ya Yehova, na basi wewe ni mtu aliyekufa ambaye hana roho! Ingawa unaweza kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa, unachopata ni wokovu kidogo, na hujakuwa kiumbe chenye roho. Ingawa umepata adabu na hukumu, tabia yako haijafanywa upya ama kubadilishwa kama matokeo; umebaki tu ulivyokuwa, bado wewe ni wa Shetani, na wewe si mtu aliyetakaswa. Wale tu waliofanywa wakamilifu ndio wenye thamani, na watu tu kama hao ndio wamepata maisha ya kweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 3. Tofauti kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya Neema na katika Enzi ya Ufalme

Inayofuata: 2. Tofauti muhimu kati ya kuokolewa na kufikia wokovu kamili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

2. Tofauti kati ya kazi ya wale wanaotumiwa na Mungu na kazi ya viongozi wa kidini

Kazi inayotekelezwa na yule anayetumiwa na Mungu ni kwa ajili ya kushirikiana na kazi ya Kristo au Roho Mtakatifu. Mtu huyu anainuliwa na Mungu miongoni mwa wanadamu, yuko pale kuongoza wateule wote wa Mungu, na pia yeye anainuliwa na Mungu ili kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu. Na mtu kama huyu, ambaye anaweza kufanya kazi ya ushirikiano wa mwanadamu, matakwa mengi zaidi ya Mungu kwa mwanadamu na kazi ambayo Roho Mtakatifu lazima Afanye miongoni mwa wanadamu inaweza kutimizwa kupitia kwake.

2. Maana ya kweli ya kunyakuliwa, na jinsi mtu anavyoweza kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu

Sisi ni kundi la watu wa kawaida tu, waliomilikiwa na tabia potovu ya kishetani, wale waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na wale maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati tulipomkataa na kumshutumu Mungu, lakini sasa tumeshindwa na Yeye. Kutoka kwa Mungu tumepokea uzima, njia ya uzima wa milele. Licha ya mahali ambapo tunaweza kuwa duniani, licha ya mateso na dhiki tunazovumilia, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu pekee!

2. Lengo na umuhimu wa Mungu kupata mwili nchini China ili kufanya kazi katika siku za mwisho

Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utukufu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki