Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu
Baada ya kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwa kusoma maneno ya Mungu na kusikiliza mahubiri, nilikuja kuelewa umuhimu wa kufuatilia kuwa mtu mwaminifu katika imani ya mtu, na kwamba ni kwa kuwa mtu mwaminifu tu ndipo mtu anaweza kupata wokovu wa Mungu. Hivyo nikaanza kushiriki kuwa mtu mwaminifu katika maisha halisi.