Ubia wa Kweli

15/01/2018

Fang Li Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan

Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha. Lakini kama ukweli ulivyofichua, ubia wenye kuridhisha kwa kweli haukuwa kama kitu chochote nilichosadiki.

Siku moja katika mkutano, mshirika wangu alionyesha baadhi ya dosari zangu mbele ya mkuu wetu, akisema nilikuwa na kiburi, wa kutokubali ukweli, mwenye kudhibiti, mwenye kutiisha…. Kumsikia akisema hivyo kulinikasirisha mno, na nikawaza: “Jana nilikuuliza kama ulikuwa na maoni yoyote kunihusu, ulisema hapana, lakini sasa, mbele ya mkuu wetu, unasema mengi hivyo! Huo ni unafiki mkubwa!” Nilidhani mshirika wangu na mimi tulikuwa na uhusiano wa amani, lakini alikuwa na maoni mengi sana kunihusu, ambalo lilithibitisha kuwa bado kulikuwa na kutoelewana kati yetu na kwamba uhusiano wetu haukuwa wa amani hata kidogo. Kama nimekabiliwa na ukweli wa mambo, sikuweza kujizuia tena kurejelea tabia yangu mwenyewe katika ubia huo: Katika mikusanyiko, ingawa ndugu yangu alifanya ushirika pia, alinena kidogo, kwa sababu nilizungumza kwa mingi ya mikutano na ni kwa nadra nilimpa nafasi ya kuongea; kazini kweli tulijadili matatizo yoyote yaliyotokea, lakini maoni yetu yalipotofautiana, daima nilishikilia maoni yangu na kuyakataa yake, na masuala yalitatuliwa wakati ndugu yangu alipoacha kubishana; kutoka kwa nje hakukuwa na ubishi au migongano kati yetu, lakini ndani daima kulihisi kama kulikuwa na kizuizi kati yetu, kitu kilichotusimamisha kuwa wazi kabisa. Ni hapo nilipotambua kwamba wakati sisi wawili tulionekana kuwa washirika waliofanya kazi pamoja, kwa kweli nilikuwa nikitoa maagizo yote, na kamwe hakupata nafasi ya kutimiza wajibu wake kweli. Nilidhani uhusiano wetu ulikuwa wa washirika wawili kukamilishana na kuwa sawa, lakini kwa kweli ulikuwa ni wa kiongozi na aliyeongozwa. Ukweli ulinifichulia kuwa kile nilichokifikiria kama ubia wenye kuridhisha yalikuwa tu ni matendo ya juujuu. Kwa hiyo, kwa hakika ubia wenye kuridhisha ni nini? Nilitafuta majibu ya swali langu katika neno la Mungu, na nilipata maneno haya, “Mmesikiliza mahubiri mengi, na mna uzoefu kiasi kuhusu kufanya huduma. Msipojifunza kutoka kwa kila mmoja, msaidiane, na kufidiana dosari zenu mnapofanya kazi makanisani, basi mnawezaje kupata mafunzo yoyote? Wakati wowote mnapokabiliwa na chochote, mnapaswa kufanya ushirika ninyi kwa ninyi ili maisha yenu yaweze kufaidika. Aidha, mnapaswa kufanya ushirika kwa makini kuhusu mambo ya aina yoyote kabla kufanya maamuzi yoyote. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo mnawajibikia kanisa badala ya kutenda kwa uzembe tu. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukusanyika pamoja na kushiriki kuhusu masuala yote mnayogundua na matatizo yoyote mliyokumbana nayo katika kazi yenu, na kisha mnapaswa kuwasiliana kuhusu nuru na mwangaza ambao mmepokea—huu ni utendaji wa msingi wa huduma. Lazima mfanikishe ushirikiano wa upatanifu kwa ajili ya kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na ili muwahimize ndugu zenu mbele. Mnapaswa kushirikiana, kila mmoja akimrekebisha mwenzake na kufikia matokeo bora ya kazi, ili kuyatunza mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo maana ya ushirikiano wa kweli, na ni wale tu wanaoshiriki katika ushirikiano huo ndio watakaopata kuingia kwa kweli” (“Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kupima kwa uangalifu maneno ya Mungu, moyo wangu kwa ghafla ulielewa. Ubia wa kweli una maana kwamba washirika wanaweka kazi ya kanisa kwanza; kwa maslahi ya kanisa na maisha ya ndugu wa kiume na wa kike, wanaweza kufanya ushirika wao kwa wao na kukamilisha udhaifu wa wao kwa wao, ili matokeo bora yaweze kufanikishwa katika kazi yao; hawana kutoelewana au chuki dhidi ya wao kwa wao na hawadumishi tofauti yoyote katika hadhi. Kwa kulinganisha tabia yangu mwenyewe na hiyo, nilihisi aibu na majuto yasiyosemeka. Kuangalia nyuma kwa tabia yangu, nilitambua sikuwahi kuzingatia maslahi ya kanisa kamwe, daima nilijiweka kwanza, niliongoza kwa kuegemea hadhi yangu na kwa uangalifu nilitunza sifa yangu mwenyewe na cheo, na niliogopa tu kwamba wengine wangenidunisha au kuniangalia kwa dharau, na ushirika wangu na ndugu wa kiume na wa kike haukuwa wa kukamilishana au kuendeshwa kwa njia ya usawa, kwa hiyo haukuwahi kufanikisha kamwe kusudi la kuingia kwa pamoja neno la Mungu, kwa kitegemeo cha pande mbili. Wakati kwa nje mshiriki wangu nami tulionekana kuwa tukijadili jinsi ya kufanya kazi yetu, katika moyo wangu sikuyakubali mawazo yake, na hatimaye niliyashikilia mawazo yangu mwenyewe badala ya kuzingatia kile kilichokuwa bora kwa kazi ya kanisa; ingawa wakati mwingine nilimuuliza aonyeshe dosari zangu, badala ya kuzikubali, daima nilibishana, nikatetea mambo, na kujitetea mwenyewe, mambo ambayo yalimwekea vikwazo na kumfanya awe na hofu sana ya kuzungumza nami wazi na kutotaka kutaja dosari zangu tena, ambayo yalisababisha kutoelewana kati yetu na kutugharimu uwezo wa kukamilisha kazi ya kanisa kwa dhamira moja. Miongoni mwa ndugu zangu wa kiume na wa kike nilitenda hata na kiburi zaidi na ubora, daima nikidhani kwamba nilikuwa kiongozi wao kwa sababu ufahamu wangu mkubwa wa ukweli ulinistahilisha kuwaongoza. Nikiwa nao, sikuonyesha kabisa unyenyekevu au utafutaji wa kweli, badala yake nikijifikiria kuwa stadi wa ukweli na kusisitiza kwamba kila mtu anisikilize. … Hapo ndipo nilipogundua kuwa ubia wangu katika huduma haukuwa na kiini chochote cha ubia, au kwa maneno mengine makubwa, nilikuwa nikijihusisha na udhalimu na udikteta. Kutenda jinsi hiyo kama kiongozi na mshirika sio tofauti na jinsi joka kubwa jekundu hushikilia mamlaka! Joka kubwa jekundu huweka udhalimu katika matendo, likisisitiza mamlaka ya mwisho katika vitu vyote na likihofia kusikiliza sauti ya umma au kutawala kupitia kanuni za kisiasa tofauti na zake. Na mimi, nikiwa na hadhi yangu ndogo niliyo nayo leo, nataka kuwa msimamizi wa eneo finyu ninalolidhibiti. Kama siku moja nitamiliki mamlaka, nitakuwaje tofauti na joka kubwa jekundu? Nikifikiri juu ya yote haya, kwa ghafla nilihisi hofu. Kuendelea jinsi hii kungekuwa hatari mno, na ikiwa singebadilika, mwisho wangu ungekuwa sawa na wa joka kubwa jekundu—kuadhibiwa na Mungu.

Baada ya kutambua yote haya, sikushikilia tena maoni yoyote dhidi ya ndugu yangu. Badala yake, nilikuwa na shukrani kwa Mungu kwa kunisaidia kujijua mwenyewe katika mazingira kama hayo na kwa kunionyesha hatari ndani yangu. Baadaye, niliposhirikishwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike, nilijifunza kujishusha, kuwa na moyo wa kuyatunza mapenzi ya Mungu kuwajibika katika kazi yangu, na kusikiliza zaidi maoni ya wengine, na baada ya muda fulani, nilitambua kwamba aina hii ya matendo haikunipa tu ufahamu kamili zaidi mzima wa ukweli, pia ulinileta karibu na ndugu zangu wa kiume na wa kike na ulituruhusu kushiriki waziwazi zaidi. Na nikiwa na aina hizi za matunda kuonyesha, hatimaye nilielewa jinsi inavyoweza kuwa vizuri kufanya huduma ya mshirika kulingana na matakwa ya Mungu!

Ninashukuru kwa kupata nuru kutoka kwa Mungu, ambako hakukunisaidia tu kuelewa ubia wa kweli wenye kuridhisha, lakini hata zaidi kulinisaidia kuona tabia yangu potovu ya kiburi ikifichuliwa katika huduma yangu mwenyewe na mshirika wangu, na kulinionyesha kuwa wakati wanadamu wapotovu wanapotwaa mamlaka, matokeo yake ni sawa na joka kubwa jekundu. Natumaini ninaweza kuondosha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yangu, kuingia katika huduma ya kweli ya ubia, na hatimaye kuwa mtu anayemtumikia Mungu ambaye analingana na moyo wa Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kiini cha Kutumia Mamlaka Vibaya Kwa Ajili ya Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

Ee Mungu, asante kwa nuru Yako ya haraka, kwa kuzuia tabia yangu ya ubaguzi, kwa kuniruhusu kuona vyema zaidi uso wangu wa Shetani ukitenda kama adui Yako. Kuanzia siku hii kwendelea, ninapenda kufuata mabadiliko katika tabia, na wakati ninapokutana na watu au vitu ambavyo havinipendezi, nitajifunza kujiweka kando, kuunyima mwili, na katika vitu vyote kuyalinda maslahi ya kanisa, kufanya kila linalowezekana ili kutimiza majukumu yangu.

Wivu—Ugonjwa Sugu Wa Kiroho

He Jiejing Jiji la Hezhou, Mkoa wa Guangxi Dada mmoja na mimi tuliunganishwa ili tusahihishe makala pamoja. Tulipokuwa tukikutana,...

Umuhimu wa Uratibu katika Huduma

Hivi karibuni kanisa lilitoa mpangilio wa kazi likihitaji viongozi wa kanisa katika ngazi zote kuanzisha mbia (mfanyikazi mwenza kufanya kazi pamoja nao). Wakati huo, nilifikiri kwamba huu ulikuwa mpangilio mzuri. Nilikuwa wa ubora wa tabia wa chini na nilikuwa na kazi nyingi; kwa kweli nilihitaji mbia wa kunisaidia kukamilisha kila aina ya kazi kanisani.

Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

Maneno ya kawaida “Wote huwekelea mizigo kwa farasi anayekubali” ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp