Ni kwa Kuingia Katika Ukweli Mimi Mwenyewe tu Ndio Ninaweza Kuwasaidia Wengine

15/01/2018

Du Fan Mkoa wa Jiangsu

Hivi karibuni, kanisa moja lilikuwa linakipiga kura ili kumchagua kiongozi mpya, lakini kiongozi aliyeongoza alienda kinyume na kanuni za kanisa, akitumia njia yake mwenyewe kutekeleza upigaji kura. Wakati ndugu fulani wa kiume na wa kike walipotoa maoni yao, sio tu kwamba hakuyakubali, lakini alisisitiza kushikilia njia yake mwenyewe. Baadaye kanisa lilitupwa katika mchafuko kwa ajili ya vitendo vya kiongozi huyo. Nilipopata kujua, nilikasirika kabisa: Mtu anawezaje kuwa mwenye kiburi mno na wa kujidai? Kutekeleza wajibu wa kiongozi wa kanisa bila Mungu ndani ya moyo wake, kuangalia kwa dharau mipango ya kazi, kupinga na kukataa mapendekezo ya ndugu wa kiume na wa kike—ni nani mwingine wa kulaumiwa kwa mchafuko wa kanisa ila wewe! Papo hapo nilimtuma mtu kuwasiliana kwa karibu na kiongozi wa kanisa na, wakati ule ule, nikapitia neno la Mungu kutafuta ukweli unaohusika ambao ningeuibua na kiongozi ili kumridhisha kuhusu makosa yake. Baadaye usiku huo, nilikwenda na kukutana na kiongozi. Wakati wa ushirika, nikamwambia kwa sauti ya mashtaka, nikishindwa kuzuia hasira yangu mwenyewe. Nilishangaa kuwa, dakika kumi katika mkutano wetu, kiongozi ghafla aliinuka na kutimua nje akiwa na machozi machoni mwake. Ndugu aliyekuwa ameenda kumfuata alirudi baadaye kidogo na kusema, “Amekwenda na anajua amefanya makosa.” Nilikuwa siachilii, nikiguta kwa hasira: “Kuhusu suala muhimu jinsi hii la kanuni, uko tayari kuacha mambo tu kama hayajatatuliwa? Jinsi wewe ulivyo mwenye kiburi mno na wa kujidai! Unaenda kinyume na kanuni za kanisa na humruhusu mtu mwingine awe na maoni. Je! Unapaswaje kupata kitu chochote kifanywe wakati ujao? Ni matarajio ya hatari kweli! Hili halitakuwa sawa hasa, kama utatoka nje kwa hasira bila kusema, itanilazimu kukuandikia barua tu.” Papo hapo, nikaketi na kumwandikia barua ambamo kwa ishara nilikubali kuwa mtazamo wangu katika ushirikiano haukuwa bora na nikauliza msamaha wake. Katika barua hiyo, nilizungumzia pia masuala yake, nikitoa mfano wa kanuni ili kutambua tatizo hilo. Nilidhani kwamba nilikuwa nimeyashughulikia mambo vizuri sana. Kwa upande mmoja, nilionyesha kuwa niliweza kuacha ubinafsi wangu mwenyewe na kupata ufahamu wa kina kujihusu, wakati huo huo nikitumia ukweli kutatua masuala. Baada ya kuona jinsi nilivyoshughulikia mambo, kiongozi huyu bila shaka angeridhika na kupata ufahamu mpya, nilifikiri.

Siku moja, nilipokuwa nikiwasiliana kwa karibu juu ya jambo hili na kiongozi wangu, kiongozi aliniuliza jinsi nilivyoingia katika ukweli wakati wa kutatua suala hili. “Niliingiaje katika ukweli? Nilifanya kazi mbaya? Je! Matendo yangu yalikuwa yasiyofaa?” Nilijihisi kuchanganyikiwa kidogo. Kiongozi huyo aliendelea: “Sio suala la jinsi ulivyotatua suala hili vizuri, lakini badala yake, katika kutatua suala hilo, je, ulilitumia hadhi yako na uwezo kuwashawishi wengine au ulitumia ukweli kumkuza na kumshuhudia Mungu, na kuwaruhusu wengine kupata kujijua kwa kina? Kwa juu, inaonekana kama kwamba wewe ulikuwa ukiwasiliana kwa karibu katika neno la Mungu, lakini kwa kweli ulikuwa unajaribu kumfanya ashindwe na mtazamo wako tu. Kwa nini aliishia kwenda? Ni wazi kuwa aliondoka kwa sababu hakuweza kukubali hoja yako, hakuridhika. Kama tunajishughulisha tu na kuwasiliana ukweli kwa karibu na wengine na kupuuza kuzingatia upotovu wetu wenyewe, kupuuza kujijua wenyewe, na kufanya kazi kwa ajili ya kuifanya tu, huenda tusijifunze chochote kipya na kutopata mabadiliko yoyote katika tabia yetu wenyewe. Kwa maana hii, si sisi ni kama Paulo, ambaye alitoa mwongozo kwa wengine lakini, ambaye, katika huduma ya Mungu, alijishikilia zaidi njia zake potovu? Katika kiburi chake, akawa mtu ambaye alimwamini Mungu na bado alimpinga Mungu, akifikia mwisho wake kwa kuangamia kabisa.” Ushirika huu ulikuwa kama wito ukinitikisa kutoka kwa usingizi mrefu. Kweli, wakati Mungu alileta hali hii kwangu, sikutafuta ukweli au kutafuta nia ya Mungu, sikufikiria jinsi ya kuingia katika ukweli mwenyewe au kutafakari juu ya majibu yangu mwenyewe yenye mhemko kwa hali hiyo. Yote niliyoweza kufanya ilikuwa ni kufikiria jinsi ya kutatua matatizo ya watu wengine. Kwa maana hii, nilikuwa nikizingatia hamu ya Mungu ya kuwaleta wengine mbele Yake? Au badala yake nilikuwa nikitumia hadhi yangu kuwalazimisha wengine kuukubali mtazamo wangu? Nilipotoshwa na Shetani, bila ukweli, ubinadamu au sababu. Mimi pia nilikuwa mwathiriwa. Nilikuwaje bora kuliko mtu mwingine yeyote? Sikuwa na maarifa ya binafsi, ufahamu wa ukweli. Bila kutambua, nilikuwa nimechukua sauti kali na kukasirika, nikiitukuza hadhi yangu katika kuwaonya wengine. Kiburi changu cha kishetani na majivuno vilikuwa vimefichuliwa! Wakati dada yangu alipotimua akilia, sikufikiria juu ya matendo yangu, badala yake nikimchukia na kukasirika sana. Je, si tabia yangu ilifanana na vitendo vya kikatili vya joka kubwa jekundu?

Namshukuru Mungu kwa ajili ya uongozi Wake. Uzoefu huu ulinipa nuru kwa umuhimu wa kuingia katika uhalisi wa ukweli. Ni kwa kuingia tu katika uhalisi wa ukweli tunapoweza kupokea ulinzi wa Mungu na kutompinga Mungu. Katika mahubiri ilisemwa: “Watu wengi hugeuka viongozi wa uongo au wapinga Kristo kwa sababu hawafuatilii ukweli kwa kweli na, kwa sababu hiyo, hawana uhalisi hata chembe wa ukweli. Mara tu wanapopata hadhi na kuwa na mamlaka fulani wao huanza kutenda kwa utukutu, kuwa juu zaidi ya wote, kujipa hadhi juu ya wengine na kutamani radhi ya hadhi. Mwishowe, watu kama hao huchukiwa sana na kukataliwa na wateule wa Mungu, hatimaye wakishindwa kabisa. Hili linaweza kuwa labda tukio adimu? Kwa nini watu hawawezi kujirudi? Kuna haja gani ya kumwamini Mungu ili kupata mamlaka tu, kushika madaraka na kutamani radhi ya hadhi? Hii ni tabia ya watu wa ubinafsi, duni na waovu, ni tamaa duni ya wale wanaoitembea njia ya mpinga Kristo” (“Unapaswa Kupata Uzoefu na Kuingia kwa Uhalisi wa Ukweli wa Neno la Mungu Ili Uweze Kupata Ukamilifu wa Mungu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Kupitia kifungu hiki niligundua kwamba wale ambao hawaingi katika ukweli, baada ya kupata hadhi, watajitangaza kuwa mfalme na kwa majivuno watatumia hadhi yao kuwakandamiza, kuwasingizia, na kuwadhibiti wengine. Hatimaye watakuwa viongozi wa uongo na wapinga Kristo. Sio mamlaka yaliyowaharibu watu hawa, lakini matokeo yasiyoepukika ya kushindwa kutafuta ukweli! Ingawa inaweza kuonekana kama uzoefu huu haukuwa mbaya sana, hali yangu ya akili na asili ya kweli katika kumpinga Mungu bila kukanushika inaashiria kwamba nilikuwa nikiitembea njia ya upinzani kwa Kristo. Kama sikuwa na mwelekeo wa Mungu, bila shaka singekuwa nimetambua upumbavu wangu na bado ningekuwa nikiishi katika hali ya kujidai. Kuendelea kupitia njia hiyo, hatimaye ningefichuliwa na kufutwa! Wakati ninapofikiria jinsi mambo yangeishia, jambo hili huniogofya. Jinsi niliyoitembelea nilivyopitia matatizo, nikimwamini Mungu kwa miaka mingi sana na bado kutoweza kujua jinsi ya kuingia katika uhalisi kama Paulo, ambaye aliishi ndani ya dhana ya kufikiriwa, lakini aliendelea kumwamini na kumtumikia Mungu kulingana na tabia yake ya kawaida na asili iliyopotoka. Nisipogeuza hali ya mambo ya leo, huenda nikajipata nimehukumiwa kwa laana ya milele. Katika siku zijazo, nahitaji kuweka umuhimu zaidi juu ya kuingia binafsi na ukimbizaji wa ukweli.

Muda mfupi baada ya haya yote kufanyika, nilipokea barua kutoka kwa dada ambayo ilianza kwa kusema kuwa alikuwa na shida kuelewa ukweli na kuomba mwongozo wangu. Baada ya kusoma barua hiyo, nilipandwa na hasira tena: Wewe ni mtu mwenye kiburi jinsi gani! Huwezi kushirikiana vizuri na hao viongozi wa kanisa na wafanyakazi. Kila wakati wanapokupa mapendekezo wewe hutoa tu udhuru, ukiendelea kufanya mambo kiholela. Kazi ya injili unayowajibikia haijafanikiwa na makanisa daima hutoa taarifa juu ya hali yako. Leo unaniandikia kuniuliza mwongozo: Una uhakika unaweza kukubali mwongozo wangu? Unafikiri kwamba kila kitu ambacho umekifanya kimekuwa cha kufaa na sawa na kushindwa kwako kote kumesababishwa na watu wengine kutoweza kutenda ukweli: Ni kiasi gani unajijua mwenyewe? … Jinsi nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kukasirika, ningehisi miale ya ghadhabu ikiwaka moyoni mwangu: Si uliniomba nikupe mwongozo? Nimekuwa nikitaka kuzungumza nawe kwa muda sasa, leo hatimaye nina nafasi. Nikaandika kazi zangu za sasa na kuanza shughuli za kutafuta maneno ya Mungu yanayohusiana na hali yake ambayo ningeweza kudondoa ili kumshawishi. Ilielekea kwamba, nilivyozidi kutafuta vifungu vilivyofaa, ndivyo nilivyozidi kuvikosa—nilikanganyika na vilikopotelea vifungu vyote ambavyo kwavyo nilikuwa na ufahamu fulani. Nilipokuwa tu nimeanza kupata wasiwasi, ghafla nilihisi kufedheheka: Ni wapi unatafuta neno la Mungu? Hapa mtu huyu yuko mbele yako, huwa unaingiaje katika ukweli? Kwa nini daima unajaribu kutatua matatizo ya watu wengine? Umefichua nini ndani yako? Wakati huo, moyo wangu ulitulizwa na nikaanza kufikiria kwangu mwenyewe: Je! Umesahau tayari kilichotokea wakati wa mwisho? Usifanye kazi kwa ajili ya kufanya tu—tatua masuala yako mwenyewe kabla ya kujaribu kuwasaidia wengine. Wakati huu, nilifikiria nyuma kifungu hiki cha neno la Mungu: “Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwa mtu kutojijua. Uponye ugonjwa wako mwenyewe kwanza, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako. … Je, maisha ya mtu ambaye hawezi kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu yanaweza kukomaa? Hapana, hayawezi. Lazima uishi kwa kutegemea maneno Yangu kila wakati. Katika maisha, lazima maneno Yangu yawe kanuni yako ya vitendo. Yatakusababisha kuhisi kuwa kufanya mambo kwa njia fulani ni kile Mungu anafurahia, na kufanya mambo kwa njia nyingine ni kile Mungu anachochukia; polepole, utakuja kutembea katika njia sahihi” (“Sura ya 22” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Lazima uwe na ufahamu wa watu ambao huwa na ushirika nao na ushirika kuhusu masuala ya kiroho katika maisha, ni hapo tu unapoweza kuruzuku maisha kwa wengine na kufidia mapungufu yao. Hupaswi kuchukua sauti ya kuhubiri nao, ambao kimsingi ni msimamo mbaya kuwa nao. Katika ushirika ni lazima uwe na ufahamu wa mambo ya kiroho. Lazima uwe na hekima na kuwa na uwezo wa kuelewa ni nini kilicho katika mioyo ya watu wengine. Lazima uwe mtu mwafaka kama utawatumikia wengine na lazima ufanye ushirika na kile ulicho nacho” (“Sura ya 13” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalikuwa wazi kama ziwa la mlimani na yalinisaidia kutambua upungufu wangu mwenyewe: Wakati ninapokumbana na hali yoyote, huwa sina ufahamivu wangu kamwe na huwa siweki umuhimu wowote juu ya kile ninachokifichua ndani yangu. Kimsingi, sina Mungu ndani ya moyo wangu na sijui jinsi ya kumtegemea Yeye. Aidha, sielewi maneno mengi sana ya Mungu na siwezi kuona vitu au kutenda kulingana na maneno ya Mungu. Mungu hutaka kwamba tuishi kulingana na neno Lake wakati wote wa kila siku na kwamba tulichukue neno la Mungu kama mwongozo ambao tunapaswa kujiongozea. Yeye hutaka kwamba tufanye kile Anachopenda na kuacha kile ambacho hakiambatani na nia Yake. Je, si Mungu huyachukia yale niliyoyafichua kujihusu leo? Je, matendo yangu leo yalikuwa yakitimizaje wajibu wangu? Hapana, kwa dhahiri nilikuwa nikitenda uovu. Baadaye nilisoma “Kanuni za Kuwasaidia Wengine Kwa Moyo wa Upendo,” na kanuni ya kwanza ilisema: “Ni lazima utofautishe aina tofauti za watu kulingana na neno la Mungu. Kwa wale ambao kwa kweli humwamini Mungu na kuukubali ukweli, ni lazima uwasaidie kwa moyo wa upendo na uaminifu.” (Utendaji na Mazoezi kwa Mwenendo Wenye Maadili). Nilipata pia maneno haya ya Mungu, “Katika maneno ya Mungu, ni kanuni ipi iliyotajwa kuhusiana na jinsi watu wanapaswa kutendeana? Kipende kile ambacho Mungu anapenda, na ukichukie kile ambacho Mungu anachukia. Yaani, watu wanaopendwa na Mungu, ambao kweli hufuatilia ukweli na kufanya mapenzi ya Mungu, ndio ambao unapaswa kuwapenda hasa. Wale wasiofanya mapenzi ya Mungu, wanaomchukia Mungu, wasiomtii, na wale Anaowachukia ndio wale ambao sisi pia tunapaswa kuwadharau na kuwakataa. Hiki ndicho neno la Mungu linahitaji” (“Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kwa sababu Mungu anatupenda, Yeye huwa mwili na kujificha Mwenyewe kwa unyenyekevu, akifanya chochote ili kuuokoa binadamu wote. Yeye huchukia vipengele viovu vya wanadamu, lakini husikitikia udhaifu wao, bila kuwashughulikia watu kamwe kuhusu upotovu wao, lakini daima Akiwatia moyo watu kwa maonyo madogomadogo ya ari, mafundisho yasiyokwisha na upendo ili watambue makosa ya njia zao na kutafuta njia mpya ya kwendelea mbele. Mungu hunipa neema Yake, huniinua na kuniruhusu kutimiza wajibu huu ili niweze kupenda kile ambacho Mungu hupenda, kuwasaidia na kuunga mkono ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa moyo wenye upendo wanapokabiliwa na shida na kuwatendea watu wote kwa moyo mwaminifu. Mimi, hata hivyo, nilikwenda kinyume na kanuni Zake: Kwa sababu tu nilikuwa na hadhi ndogo na niliona kuwa wengine walikuwa wameonyesha upotovu wao kiasi, nilikosa kuuhurumia udhaifu wao, lakini badala yake nilitumia neno la Mungu kama silaha ya kuwakandamiza na kuwalazimisha wakubaliane nami. Si hiki ni kitendo cha chuki? Kwa ghafla nilihisi kutahayarishika na kuaibika juu ya kiburi na ujinga wangu. Baadaye, nilisoma kifungu cha neno la Mungu kutoka kwa Kanuni ya 43, “Kanuni ya Kushiriki Kutoka Moyoni”: “‘Kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu’ kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako. Na baada ya hayo, wengine wanatambua mambo haya, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli” (“Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kupitia kula na kunywa neno la Mungu, nilijifunza jinsi ya kuwasiliana kwa karibu na dada yangu kwa namna ambayo ingekuwa ya manufaa kwake. Wakati huu, nilipochukua kalamu, nilihisi msisimko wa up endo ukifurika ndani yangu. Nilihisi hamu kubwa ya kuufunua moyo wangu katika majadiliano na dada yangu. Wakati huu, nilijadili utambuzi wangu juu ya tabia yangu yenye kiburi na asili yangu ya majivuno na katili—sikuwa nimewatendea ndugu wa kiume na wa kike kwa usahihi, nikikosa kuonyesha upendo na huruma kwao. Katika barua niliandika yafuatayo: Kwa hakika namshukuru Mungu kwa kukuweka mbele yangu, akiniruhusu kuona uovu ndani ya moyo wangu. Kama kiongozi, sina ukweli au uhalisi. Sistahili kuwa kiongozi, kwa sababu nilishindwa kuwajibikia wajibu ambao Mungu alinipa—nilishindwa kutenda kama mtumishi mbele ya Mungu. Badala yake, nilichukua wajibu wangu kama cheo cha mamlaka, hadhi, nikijiona kuwa juu ya wengine. Nilipoona barua yako, nilijaa dharau na hukumu, na hata nikaamini kwamba nilikuwa na mamlaka ya kukupogoa na kukushughulikia. Jinsi nilivyokuwa na kiburi na majivuno! Kwa ukweli, upungufu wako ulikuwa pia upungufu na makosa yangu. Wakati mimi na ndugu zangu wa kiume na wa kike hatuwezi kufanya kazi pamoja kwa mpangilio wa kuridhisha, huyu ni Mungu akionyesha ukweli kwamba maafa haya yote ya dhiki yalikuwa matokeo ya kutoweza kwangu kuingia katika ukweli kwa ushirikiano wenye kuridhisha. Asante Mungu kwa ufunuo huu, ambao ulinisaidia kutambua kwamba licha ya kumwamini Mungu kwa miaka mingi, bado sijapata ufahamu juu ya wokovu wa Mungu wa wanadamu. Bado sijaielewa nia ya Mungu katika kuwaokoa wanadamu. Sijui ni kwa njia gani mwanadamu anapaswa kuokolewa na kukamilishwa. Kutokana na haya, katika hali yoyote ninayoweza kuikabili, sijaweza bado kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, kushughulikiwa na kupogolewa. Badala yake, daima mimi hugaagaa katika mambo ya juujuu. Kama haungekuwa umenituma barua hii kunifichua, singekuwa nimeona asili ya suala langu. Hebu sote tufanye mazoezi ya kuingia katika uhalisi wa ukweli siku zijazo.

Wakati kwa kweli nilipoiacha nafsi yangu, nikaja kujijua na kujichangua, na kutumia hali halisi ambayo nina uzoefu nayo kuwasiliana kwa karibu na kuingia katika ukweli na dada yangu, nilijihisi kuwa na mwenye hekima kabisa na kuwa na amani na kuona kuwa hakukuwa na umbali na utengano kati yetu. Kwa kweli niliona alama ya baraka ya Mungu katika hali ambazo nilitenda ukweli. Ni kwa njia ya mwongozo wa mfululizo wa Mungu na kupata nuru tu, ambapo mimi, ambaye ningeweza kuzungumza juu ya ukweli tu lakini sio kuutumia, ambaye nilipitia uzoefu kwa kutoonyesha hisia bila kuingia katika uhalisi wa ukweli, polepole nilianza kuboreka. Niliona tabia takatifu na ya haki ya Mungu katika uzoefu wangu wa zamani. Kama vile tu kifungu katika mahubiri kilisema, “Popote palipo na upotovu, patakuwa na hukumu, popote palipo na uovu, patakuwa na kuadibu” (“Zile Hatua Tatu za Kazi ya Mungu tu Ndizo Kazi Kamili ya Wokovu wa Wanadamu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Pia nilikuja kuwa na ufahamu zaidi na zaidi kwamba hukumu ya Mungu na adabu ndivyo tu tunavyovihitaji. Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu ni zawadi ya wokovu mkubwa na neema. Ni kwa kupokea hukumu hii na kuadibiwa tu tunapoweza kupokonywa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, tuondoe giza, tutafute mwanga na ukweli, tuingie katika ukweli, na tutende ukweli. Naomba kwamba hukumu na adhabu ya Mungu vinifuate popote nitakapokwenda, ili niweze kupata usafi na kuishi kama mwanadamu wa kweli.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

Ilikuwa ni katika ufunuo wa Mungu ambapo hatimaye nilitambua asili yangu ya kishetani ya kiburi na hali ya kutojali: sikuwa na chembe ya uchaji mbele ya Mungu. Niligundua wakati huo huo kwamba mawazo ya mwanadamu ni shimo la maji ya kunuka. Njia yangu “iliyofanywa kwa werevu”, bila kujali ni nzuri kiasi gani, ilikuwa matakwa ya Shetani, na ingeweza tu kumchukiza Mungu. Ingeweza tu kumkosea Yeye na kuvuruga kazi Yake.

Kuwa Mtu Mwaminifu Ni Kuzuri Kweli!

Kwa njia hii nilitenda kama mtu mwaminifu, yule ambaye kweli alitenda kulingana na matakwa ya Mungu, na biashara ikawa bora zaidi na zaidi. Nilijua kwamba hii ilikuwa baraka ya Mungu. Mungu hakunipa vitu yakinifu tu. Muhimu zaidi pia Alinifundisha jinsi ya kutenda. Katika dunia halisi kweli ni vizuri kutenda kama mtu mwaminifu kulingana na neno la Mungu!

Kupitia Upendo Maalum wa Mungu

Jiayi Mji wa Fuyang, Mkoa wa Anhui Asili yangu ni ya kiburi hasa; bila kujali ninafanya nini, mimi daima hutumia werevu na ujuzi wa...

Nilipitia Wokovu wa Mungu

Mungu mpendwa, asante! Kupitia uzoefu huu, ninatambua kwamba wokovu Wako ni wa kweli na hukumu Yako na kuadibu vimejaa upendo. Bila hukumu Yako na kuadibu, singewahi kamwe kujitazama kwa kweli. Ningendelea kuishi katika upotovu, hali yangu ikiendelea kuharibika, kukanyagwa na Shetani na hatimaye kubebwa naye. Kupitia uzoefu huu, nilitambua pia kuwa kiini Chako ni upendo na kwamba matendo Yako yote yanalenga kuwaokoa wanadamu. Mungu, ninaapa kujiwekeza kikamilifu katika kutafuta ukweli na kuanza upya. Bila kujali matokeo ni yapi, ninaapa kutimiza wajibu wangu wa kiumbe ili kuyaridhisha mapenzi Yako.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp