Ubia wa Kweli
Fang Li Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
He Jiejing Jiji la Hezhou, Mkoa wa Guangxi
Dada mmoja na mimi tuliunganishwa ili tusahihishe makala pamoja. Tulipokuwa tukikutana, nilitambua kuwa haikujalisha kama ilikuwa ni kuimba, kucheza ngoma, kupokea neno la Mungu, au kuwasiliana ukweli, huyu dada alikuwa bora kuniliko katika kila kipengele. Ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji wote walimpenda na wangezungumza naye. Kwa sababu ya hili, moyo wangu ulikuwa na wasiwasi sana na nilihisi kama nilikosa kuthaminiwa—hata kufikia kiasi kwamba nilifikiri kuwa mradi alikuwa huko, hakukuwa na nafasi yangu. Moyoni mwangu nilianza kuhisi kuchoshwa naye na kutotaka kuandamana naye katika kutimiza wajibu wetu. Nilitumaini kwamba angeondoka ili kwamba ndugu wa kiume na wa kike wangenipenda na kuniheshimu sana.
Siku moja, kiongozi alituzuru. Kwa sababu ya hali yake hasi, huyu dada aliomba kuhamishiwa kwa kazi tofauti. Baada ya kusikia akisema hivi, nikawa na msisimko mno. Niliwaza: Nilikuwa nikitumaini daima ya kwamba ungeenda. Ukienda, basi nitayaondokea mashaka yangu. Kwa hiyo, nilikuwa na shauku ya kiongozi huyu kumpa kazi nyingine mara moja. Hata hivyo, mambo yaliniendea kinyume na matarajio na kiongozi hakukosa tu kumpa kazi mpya, lakini kwa uvumilivu aliwasiliana naye ukweli na kumsaidia kubadilisha hali yake. Nilipoona hayo, nilihisi kuwa na wasiwasi hasa, na nikatumaini hata zaidi kuwa huyu dada angeondoka. Nikafikiri: Ni lini nitaweza kuyaondokea mashaka haya kama haendi wakati huu? Hapana, ni lazima nifikirie njia ya kumfanya aondoke haraka. Kwa hiyo, nilitumia fursa wakati huyu dada hakuwepo ili kumpa kiongozi maelezo zaidi, nikisema: “Hali yake mbaya mara nyingi humzuia katika kulenga wajibu wake. Sasa amepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na tayari imeathiri kazi ya kanisa ya kuhariri na kukusanya makala. Ni heri umpe kazi mpya. dada X anaweza kuwa na thamani bora ya kukuza kuliko dada niliyewekwa naye.” Mara tu nilipomaliza kusema hili, neno la Mungu liliingia ndani yangu likinishutumu: “Wanadamu dhalimu! Kuwafumba watu macho na kula njama, kupokonyana na kunyang’anya mmoja kutoka kwa mwingine, kung’ang’ania umaarufu na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amezungumza, hakuna hata mmoja ambaye ameacha kufanya upumbavu. … Ni wangapi wasiowakandamiza na kuwatenga wengine ili kulinda vyeo vyao wenyewe?” (“Waovu Hakika Wataadhibiwa” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kukabiliana na maneno ya hukumu ya Mungu, nilihisi kama Mungu alikuwa akinikaripia kwa ukali uso kwa uso. Kwa ghafla nilianza kutetemeka kwa hofu na sikuweza kujizuia kuhisi woga kwa maneno ambayo nilikuwa tu nimeyasema. Si mimi ni kama watu wanaofichuliwa na neno la Mungu ambao “Ni wangapi wasiowakandamiza na kuwatenga wengine ili kulinda vyeo vyao wenyewe?” Nilipoona kwamba dada niliyekuwa nikifanya kazi naye alikuwa bora zaidi kuniliko katika kila kipengele na kwamba ndugu wa kiume na wa kike wote walimpenda, nilikuwa na wivu moyoni mwangu. Nilikuwa nimechoshwa naye, nikambagua, na kutarajia kuwa angeondoka hivi karibuni ili kwamba ningeyaondokea mashaka yangu. Ili kuwafanya ndugu wa kiume na wa kike kunisikiliza ili kwamba ningejisikia kama nilikuwa na hadhi nikiwa nao, nilitumia hali mbaya ya dada huyu kwa manufaa yangu na kumsengenya kwa kiongozi kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya kanisa. Lilikuwa jaribio langu la bure la kutumia kiongozi kumwondoa yule dada kabisa. Mwenendo wangu ulifunua kabisa sura yangu ya kweli na kufichua tabia yangu mbovu ya kishetani. Ili kubuni udikteta, joka kubwa jekundu hutumia njia yoyote muhimu ili kuwaondoa wapinzani kabisa. Ili kuwa kiini cha ndugu zangu wa kiume na wa kike na kuwafanya watake kuwa karibu nami, kwa hila niliwaondoa kabisa wale ambao hawakuwa na faida kwangu. Joka kubwa jekundu lina wivu kwa wale walio wakubwa kuliliko na huwaangamiza wale wenye malengo mema. Mimi pia nilikuwa na wivu kwa dada huyu kwa sababu alikuwa bora zaidi kuniliko katika kila kipengele na nilitumia mbinu za kusikitisha kumwondoa kabisa. Joka kubwa jekundu huwahukumu na kuwaua watu kwa matilaba yake mwenyewe. Ili kupata matilaba yangu mwenyewe, kwa makusudi nilitia chumvi mambo kumhusu dada huyu. Mwenendo wangu ulikuwa sawa na ule wa joka kubwa jekundu. Kanisa lilikuwa limetupangia kufanya kazi pamoja ili tuweze kusaidia na kuauniana, ili tuweze kufanya kazi nzuri kwa moyo na akili moja ili kumpendeza Mungu. Ilikuwa pia ili tuweze kutumia nguvu zetu ili kufidia udhaifu wa mwingine ili tuweze kuelewa na kupata ukweli zaidi na kubadilisha tabia yetu. Lakini sikuwa na ufahamu wa mapenzi ya Mungu hata kwa kiwango kidogo. Nilipoona huyu dada alikuwa katika hali mbaya, sio tu kuwa sikutegemea upendo kumsaidia, lakini pia nilitarajia abadilishwe kwa haraka ili kuilinda nafasi yangu, kiasi kwamba ningetumia njia yoyote ili kufanikisha malengo yangu mwenyewe. Kama sitaharakisha na kutubu, ni lazima hatimaye niangamizwe pamoja na joka kubwa jekundu.
Asante Mungu! Hukumu Yako na kuadibu vimeniamsha wakati ufaao kunifanya nione wazi uso wangu uliotoka katika upotovu wa Shetani, na kupitia kwa hili kuniwezesha kukuza chuki ya kweli kwa asili yangu ya kishetani. Kuanzia wakati huu kwendelea, nitageuka kutoka kwa asili ya Shetani iliyo ndani yangu. Sitajipignia mwenyewe tena. Natumaini kufanya kazi vyema na dada huyu ili kutimiza wajibu wetu na kumridhisha Mungu. Nitakuwa tayari zaidi kutafuta ukweli na kutupa sumu ya joka kubwa jekundu, na hivyo kuishi kama mtu halisi ili kumfariji Mungu!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Fang Li Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi...
Maneno ya kawaida “Wote huwekelea mizigo kwa farasi anayekubali” ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine.
Ee Mungu, asante kwa nuru Yako ya haraka, kwa kuzuia tabia yangu ya ubaguzi, kwa kuniruhusu kuona vyema zaidi uso wangu wa Shetani ukitenda kama adui Yako. Kuanzia siku hii kwendelea, ninapenda kufuata mabadiliko katika tabia, na wakati ninapokutana na watu au vitu ambavyo havinipendezi, nitajifunza kujiweka kando, kuunyima mwili, na katika vitu vyote kuyalinda maslahi ya kanisa, kufanya kila linalowezekana ili kutimiza majukumu yangu.
Hivi karibuni kanisa lilitoa mpangilio wa kazi likihitaji viongozi wa kanisa katika ngazi zote kuanzisha mbia (mfanyikazi mwenza kufanya kazi pamoja nao). Wakati huo, nilifikiri kwamba huu ulikuwa mpangilio mzuri. Nilikuwa wa ubora wa tabia wa chini na nilikuwa na kazi nyingi; kwa kweli nilihitaji mbia wa kunisaidia kukamilisha kila aina ya kazi kanisani.