Njia ya Pekee ya Kuepuka Maafa

14/01/2018

Chaotuo Mji wa Xiaogan, Mkoa wa Hubei

Tangu Tetemeko la Ardhi la Sichuan la Mei 12, daima nimekuwa na hofu na wasiwasi kwamba siku moja huenda nikakumbwa na maafa. Hasa kwa vile nimeona maafa yakiongezeka, na matetemeko ya ardhi yakiwa ya mara kwa mara, hofu yangu ya maangamizi imekuwa hata wazi zaidi. Matokeo yake ni kuwa, mimi hutumia siku nzima nikitafakari ni tahadhari gani ambazo napaswa kuchukua ili kujilinda iwapo tetemeko la ardhi litazuka.

Siku moja, wakati wa chakula cha mchana, dada wa familia mwenyeji wangu aliwasha TV kama kawaida, na mtangazaji wa habari alitokea tu kuwa akizungumza juu ya hatua za usalama kwa tetemeko la ardhi. Katika tukio la tetemeko la ardhi, unapaswa kukimbia nje kwa haraka katika sehemu wazi ili kuepuka kujeruhiwa na jengo likianguka. Ikiwa huwezi kutoroka wakati ufaao, unapaswa kujificha chini ya kitanda, meza au kwa kona…. Baada ya kusikia hili, nilihisi kama nilipata suluhisho la kuokoa maisha, na kwa haraka nikaweka hatua hizi za tahadhari kwa kumbukumbu, hivyo ningeokoa maisha yangu iwapo tetemeko la ardhi lingetokea. Nilirudi kwa chumba changu baada ya chakula cha mchana, na nikaangalia kwa makini kote ndani na nje ya nyumba na nilisikitishwa sana na yale niliyoyaona: Kulikuwa na vikorokoro tele chini ya kitanda, na hakukuwa na nafasi ya ziada ya kujificha. Nikiangalia nje ya nyumba, kiasi cha mita mia kadhaa kutoka mahali niliposimama majengo yote yalikuwa ya ghorofa 5 au 6 kwenda juu, na yalikuwa yamesongamana pamoja. Hata kama ningehama jengo langu, bado huenda ningepondwa hadi kufa. Ilionekana kana kwamba kutimiza wajibu wangu hapa kungekuwa hatari sana. Ingenibidi nimsubiri kiongozi wa wilaya kuja na kunibadilisha kwa familia mwenyeji wa vijijini. Njia hiyo, kama tetemeko la ardhi lingetokea, ingekuwa rahisi kukimbia kwa nafasi wazi. Lakini ilinitokea kwamba: Kazi yangu ya kusahihisha makala ilihusisha hasa kukaa ndani ya nyumba—hata kwa kuishi vijijini maisha yangu bado yangekuwa hatarini. Ni vyema kumwambia kiongozi wa wilaya kunihamisha hadi kwa timu ya injili. Hivyo angalau ningekuwa nje mchana kutwa, na ingekuwa salama kuliko kukaa nyumbani. Jambo la pekee lilikuwa, sikujua kiongozi wa wilaya angekuja lini. Bado nilihitaji kuandaa makazi kwa wakati uliopo. Na hivyo, niliishi kwa hofu kila siku, na sikuweza kusahihisha makala yangu.

Kisha siku moja, nikasoma kifungu kinachofuata katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako”: “Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu.” “Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yakanichangamsha. Kama ilivyoelekea, Mungu husababisha maafa—maafa hayo hutoka kwake. Mungu anataka kutumia maafa kuuangamiza binadamu hawa waovu na wapotovu. Hili ndilo Mungu anataka kufanya katika siku za mwisho. Waumini hawajui jambo hili, na wao hudhani kuwa haya ni maafa ya kawaida. Kwa hiyo wao hutumia njia za kibinadamu, jitihada za kibinadamu kujilinda wenyewe wakati wanapokabiliwa na maafa. Wanafikiri wanaweza kuepuka uharibifu wa maafa mbalimbali kwa kufanya hivyo. Na mimi, ambaye nilikuwa mjinga, niliamini Mungu lakini sikuijua kazi ya Mungu hata kidogo. Nilikuwa nikifikiri kuwa yote niliyohitaji kufanya ni kufuata hatua za tahadhari za wasioamini na ningeepuka mateso yaliyoletwa na majanga na kuishi. Kwa hakika ulikuwa ni upuuzi kwamba ningekuwa na mtazamo sawa na wasioamini! Si ningepaswa kujua ya kwamba kama watu hawatekelezi wajibu wao kwa uaminifu na kushindwa kufanya matendo mema, hawataonekana machoni mwa Mungu kama wema? Bila kujali jinsi wanadamu wanaweza kuwa na nguvu, jinsi hatua zao za tahadhari zilivyo za juu, au jinsi gani mipango yao ya kujiokoa ilivyo timamu, mwishoni hakuna kuyatoroka maafa hayo ambayo Mungu huyapatilizia mwanadamu. Kutoka kwa majibu yangu mbalimbali kwa tishio la maafa, ilikuwa dhahiri kwamba sikuwa na imani halisi katika Mungu. Sikuwa na ufahamu halisi wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho na wa uweza Wake na ukuu. Sikukujua ni nani ambaye Mungu analenga kuangamiza katika maafa, au ni nani ambaye Mungu anataka kuokoa, wala sikutambua kwamba katika maafa, ni wale tu ambao ni waaminifu kwa Mungu na wameandaa matendo mema ya kutosha wanaookolewa katika maafa. Kwa hiyo, wakati tishio la maafa lilipotishia, badala ya kutafakari kama nilikuwa nimetayarisha matendo mema au la, nilikuwa mwaminifu kwa Mungu, nilitafuta ukweli na nilikuwa nimepokea wokovu wa Mungu, nilitumia muda wangu wote nikitafakari njia za kujiokoa. Bila ukweli, hivi ndivyo tulivyosikitisha!

Wakati wa Nuhu, wakati Mungu alipoangamiza dunia na mafuriko, kwa sababu Nuhu alimwogopa Mungu na kukaa mbali na uovu, alijenga safina kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, alitumia kila kitu kutokana na ombi la Mungu, na alionyesha uaminifu wake wa juu, alionekana na Mungu kama mtu nzuri. Kwa hiyo, maafa yalipofika, wanakaya wake wote wanane walinusuriwa. Wakati huu, nilikumbuka kilichojadiliwa katika “Ushirika na Mahubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha,” “Usipotayarisha matendo yoyote mazuri, wakati maafa yatakapobisha, moyo wako utakuwa na hofu kubwa mchana kutwa. Bila matendo mema, moyo wa mtu hauhisi faraja, na hana imani au amani moyoni mwake. Kwa sababu hajatayarisha matendo mema, hakuna amani halisi au furaha moyoni mwake. Waovu wana dhamiri ya hatia, na ni waovu kwa moyo. Jinsi wanavyozidi kutenda matendo mabaya, ndivyo wanavyozidi kujihisi wenye hatia zaidi na kuwa wenye woga zaidi. Ikiwa unataka kuufanya moyo wako kuwa na faraja na amani maafa yanapokuja, unahitaji kufanya matendo mazuri zaidi na kuandaa matendo mema zaidi sasa. Ni hapo tu utakapojisikia kuwa na amani na faraja katika moyo wako wakati maafa yanapobisha” (“Maana Muhimu katika Kuandaa Matendo Mema” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha II). Nilipofikiri juu ya jinsi nilivyokuwa nikihisi mwenye wasiwasi na kuchanganyikiwa mchana kutwa, nikihofia kifo changu mwenyewe katika maafa, nilitambua ni kwa sababu sikuwa nimetimiza wajibu wangu kwa uaminifu na sikuwa nimeandaa matendo yoyote mazuri. Katika kufanya kazi yangu, kweli sikuwa nimewahi kamwe kubeba mzigo kwa kazi nilizoaminishiwa na kanisa. Sikuwa nimewahi kutimiza majukumu yangu kwa moyo mwaminifu kwa Mungu. Badala yake, nilikuwa nimemdanganya na kushughulika na Mungu kwa sababu ya kudekeza kwa mwili. Sikufanya mengi na makala niliyotumiwa, lakini niliyasahihisha kihobelahobela na nilitaka tu kukamilisha kazi yangu. Nilipoona jinsi makala yaliyoandikwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike yalivyovurugika, sikuwaongoza na kuwasaidia kwa juhudi, lakini niliandika tu maoni machache, bila kujali kama waliyaelewa au kama yangefaa. Badala yake, niliyarudisha makala hayo kwa haraka, na hatimaye nilipokea makala yaliyopungua zaidi na zaidi ya kuhariri. Matokeo yake yalikuwa, kazi ya uhariri ilikaribia kusimama. Hata hivyo, sikutafakari juu ya matendo yangu, wala sikujaribu kutambua na kurekebisha chanzo cha tatizo hilo, lakini nilimlaumu kiongozi, nikidai kuwa matatizo yalitokea kwa sababu hakuweka umuhimu katika kazi ya uhariri. Nilikisiaje kumridhisha Mungu kwa vitendo kama hivyo na hivyo kufarijiwa moyoni mwangu? Kwa njia hii, ningewezaje kuonekana katika macho ya Mungu kama mtu mwema? Kama nikiendelea kwa njia hii na sifuatilii ukweli vizuri, nishindwe kuwa mwaminifu kwa yale ambayo nimeaminishiwa na kanisa, na sitayarishi vitendo vizuri vya kutosha, hakika nitashindwa kukwepa ghadhabu ya adhabu ya Mungu kwa waovu hata kama nitafuata zile tahadhari zilizowekwa na watu wa kidunia wakati maafa yanapobisha.

Namshukuru Mungu kwa uongozi Wake kwa kufungua akili yangu kuniruhusu nielewe kwamba ni kwa kufanya kazi yangu vizuri tu na kufanya matendo mema ninapoweza kupata ukombozi kutoka kwa mateso yaliyoletwa na majanga na kuponyoka na maisha yangu. Hii ndiyo njia moja tu na ya pekee. Katika siku zijazo, napenda kufuatilia ukweli kwa usawa, kuwa mwaminifu iwezekanavyo katika kutimiza wajibu wangu, na kuandaa matendo mema maridhawa ili kumridhisha Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu

Asante, Mwenyezi Mungu! Ni Wewe uliyenitunza na kunipa nuru na kuniongoza kujitoa katika pingu ambazo zilikuwa zimenidhibiti kwa miaka mingi sana, kuniruhusu kutoka katika ukungu. Zamani, sikukujua Wewe na mara nyingi niliishi katika kutoelewa, nisiweze kuamini neno Lako na kulichukulia kama tu la kuliwaza na kuwatia watu moyo. Sikulichukulia neno Lako kama ukweli na uzima, na zaidi sikukuchukulia wewe kama Mungu. Lakini Ulinivumilia, na Ulikuwa mwenye subira kwangu. Ulinipa nuru na kuangaza mwanga Wako kwangu, ili kwamba niwe na ufahamu kidogo wa kiini Chako cha haki na uaminifu. Hii hasa ni mfano kamili wa upendo Wako kwa mwanadamu.

Kushikilia Wajibu Wangu

Na Yangmu, Korea ya Kusini Nilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu....

Kiini cha Kutumia Mamlaka Vibaya Kwa Ajili ya Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

Ee Mungu, asante kwa nuru Yako ya haraka, kwa kuzuia tabia yangu ya ubaguzi, kwa kuniruhusu kuona vyema zaidi uso wangu wa Shetani ukitenda kama adui Yako. Kuanzia siku hii kwendelea, ninapenda kufuata mabadiliko katika tabia, na wakati ninapokutana na watu au vitu ambavyo havinipendezi, nitajifunza kujiweka kando, kuunyima mwili, na katika vitu vyote kuyalinda maslahi ya kanisa, kufanya kila linalowezekana ili kutimiza majukumu yangu.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp