Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Moto Ulioshtua Taifa katika Wilaya ya Ji, Mji wa Tianjin

53

Chen Yao, Tianjin

(Chanzo: Fotolia)

Jengo la Laide lilikuwa mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya ununuzi katika wilaya ya Ji. Juni 30, mwaka wa 2012 ilikuwa ni Jumamosi, na Laide lilikuwa na ukuzaji wa bidhaa, hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya wateja. Wakati fulani baada ya saa tisa alasiri hiyo, jengo likashika moto ghafla. Mkuu wa jengo, akiogopa kuwa wateja katika machafuko haya wangechukua vitu au kutolipa, alifunga na kuweka vizuizi kwa lango kuu kwenye ghorofa ya kwanza, na kuwafukuza wateja hadi ghorofa ya pili na ya tatu. Kitu ambacho hakikutarajiwa ni kwamba moto ulikuwa mkali zaidi na zaidi, hatimaye ukifika kiwango cha kutodhibitika kabisa. Umeme katika jengo lote ukazima. Kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya nne, lifti zilikuwa mbovu, na mlango wa kuingia uliofungwa kwenye ghorofa ya kwanza haungefunguka. Moshi mweusi ulitapakaa jengo zima, cheche ziliruka hadi kwa anga. Ndimi kubwa za moto ziliruka kutoka kila dirisha, moshi ulifunika wilaya, hewa iliwasonga watu koo kwa mita mia kadhaa. Wakati huo watu wengi walionaswa juu ya ghorofa ya tatu waliamua kutoroka kwa kuruka kutoka kwa jengo, na wengine walikufa walikoanguka, shani ya kuogofya hiyo.

Ingawa idara ya moto haikuwa mbali na jengo hilo, ikiwa ni dakika kumi tu kwa kutembea, kulikuwa na dakika 25 baina ya wito wa msaada na malori ya moto kufika. Uokoaji ulikuwa tayari umecheleweshwa. Waokozi waliongeza ngazi hadi ghorofa ya tatu, lakini waliowaokoa watu saba au wanane tu kabla ya moto kuifanya ngazi kuwa moto sana, hivyo wale wao wa mwisho walianguka kutoka kwa ngazi na kufa papo hapo. Na ndani watu wengi waliokuwa wamenaswa walipunga mikono kwa wayowayo madirishani wakitafuta msaada, lakini baada ya muda mfupi hakukuwa na mkono wowote uliopunga ulioonekana …

Moto huu mkubwa uliwaka kutoka saa tisa na nusu adhuhuri hiyo hadi saa tatu usiku huo. Kulikuwa na zaidi ya watu mia tatu waliokufa moto ndani ya jengo (idadi halisi bado haijadhibitishwa, lakini serikali ya CCP ilitoa taarifa ya watu 10 tu). Kulikuwa na mtu ambaye aliipigia familia yake simu mnamo saa tisa jioni, lakini familia yake ilipompigia simu baadaye saa kumi na moja hakuna aliyejibu. Familia moja ya watu saba ilikuwa imeenda Laide kufanya ununuzi pamoja, na familia hiyo nzima ilikufa katika moto huo. … Kuna visa vingi sana vya huzuni.

Wakati moto ulipoanza tu, watu fulani waliweka janga hili kwa mtandao, na papo hapo, maneno “Moto katika Laide” yaliitetemesha wilaya ya Ji na kulishtua taifa. Watu wa wilaya ya Ji walishikwa na hofu kubwa, nao walikuwa katika hali ya kushtuka, watu wengi walikurupuka kuwatafuta wenzao wa familia.

Ingawa maafa hayo yaliwaogofya na kuwaumiza watu wa kawaida, kwa mintarafu ya ndugu wa kiume na wa kike walio na imani katika Mwenyezi Mungu, wengi waligundua wokovu na ulinzi mkubwa wa Mungu katika maafa haya, na kuona matendo ya kimiujiza ya Mungu. Dada Gao na mama yake walikuwa wamepokea kazi ya Mungu ya siku za mwisho karibuni mnamo Juni, mwaka wa 2012. Katika moto huu waliona matendo ya Mungu, na wakawa na hakika zaidi juu ya kazi mpya ya Mungu. Dada mkubwa, mamake Gao, ana umri wa miaka 73 mwaka huu, na ana matatizo kiasi ya kutembea. Yeye hutembea kwa fimbo, lakini kwa kawaida angeanguka mara chache. Mnamo siku ya tarehe 29 Juni, mamake Gao kwa ghafla alianguka kwa sakafu bapa. Ingawa hakuvunjika mifupa yoyote, ni kupokea chubuko kubwa tu, hakuweza kujitunza, na alihitaji dada Gao awe kando ya kitanda chake. Siku iliyofuata (siku ya moto), dada mwingine alimpigia simu dada Gao na kusema kuwa alitamani suruali katika Laide, akimwomba dada Gao kuja aandamane naye kuinunua. Dada Gao akasema: “Mama yangu anahitaji mtu wa kumtunza kwa sasa, hivyo ninahitaji kukaa naye. Itakubidi uende peke yako!” Huyu rafiki alikuwa amemwomba dada Gao msaada kabla, na hakuwahi kukataa kamwe. Lakini wakati huu kwa sababu mama yake alihitaji utunzaji, alikataa ombi la rafiki yake mwema.

Ni baada tu ya kusikia kwamba kulikuwa na moto katika Laide ndio dada Gao alitambua ghafla: Wakati wote huu bila kujua alikuwa chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu alikuwa ameizuia njia yake kupitia kwa udhaifu wa mama yake. Kama angekuwa ameambatana na rafiki yake kwa kituo cha ununuzi, bila ya shaka angekufa katika moto. Mungu alitumia njia Zake maalum kuyalinda maisha yake, Mungu kwa hakika ni wa ajabu! Hata zaidi yasiyotarajiwa, jioni baada ya moto mamake dada Gao angeweza kutoka kitandani na kutembea. Baadaye, kupitia ushirikiano na ushirika mamake Gao mzee alielewa nia njema ya Mungu, akisema: “Ingawa nilipatwa na uvimbe kiasi, Mungu alitumia udhaifu wangu ili kumwokoa binti yangu. Asante Mwenyezi Mungu!”

Dada Gao aliongeza kuwa yule rafiki mwema ambaye alikuwa amemwalika kwenda naye Laide siku hiyo (ambaye pia alimwamini Mwenyezi Mungu) pia alipata ulinzi wa Mungu kimiujiza. Kuona kuwa dada Gao hangeenda, yule rafiki alikuwa amempigia simu mume wake, kumtaka aandamane naye kununua ile suruali moyo wake uliyoitaka. Mnamo saa nane u nusu adhuhuri mumewe akafika nyumbani na kujaribu kumharakisha, lakini ghafla alipoteza hisia yake ya haraka, akamwambia mumewe: “Labda baadaye.” Saa tisa jioni, mumewe akamwuliza tena, na tena akamwambia asubiri kidogo. Mumewe alipomwuliza mara ya tatu, dada Gao hatimaye akaandamana naye kwa gari kwelekea Laide. Nusu njia kwelekea huko waliona moshi mweusi ukitoka upande wa Laide, na baada ya kuuliza, aligundua kwamba kituo hicho cha ununuzi kilikuwa kimeshika moto. Dada Gao hakuweza kujizuia na alisema: “Asante Mungu kwa kunilinda!” Wakati huo huo yeye alitambua kwamba kuahiri kwake kulikuwa na asili yake katika ustadi wa Mungu, na hakukuwa matokeo ya hiari yake mwenyewe.

Nguvu za Mungu ziko kila mahali; hekima ya Mungu haiwezi kueleweka na kiumbe yeyote. Ingawa mara nyingi sisi humsahau Mungu katika maisha yetu ya kila siku, Mungu hututunza daima, akitulinda, akiwa kwa upande wetu, bila kutuacha kamwe. Tukimwamini Mungu, wakati maafa yanapotokea, Mungu atatuokoa kwa njia zote na kutuponya kutokana na maafa. Mnamo siku ya moto, ndugu wengi wa kiume na wa kike waliyaona matendo ya Mungu. Dada mmoja alikuwa katika Laide akinunua bidhaa, na aliitwa nje kwa simu ili kufanya kitu fulani wakati huo huo wa kipeo, moto ukiwa nyuma yake hasa. Dada mwingine alikuwa njiani kutoka kwa jengo lake kwenda Laide, na ghafla akahisi maumivu ya tumbo, kiasi kwamba aligeuka moja kwa moja na kurudi, na hakuenda, na hivyo aliepukwa maafa. … Kwa dhahiri, katika maafa ni Mungu tu aliye kimbilio letu la kweli, mnara wetu wenye nguvu, kwa sababu Mungu amesema: “Mimi tu Ndiye wokovu wa pekee wa mwanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la pekee mwanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa mwanadamu. Bila Mimi, mwanadamu atasimama mara moja. Bila mimi, mwanadamu atakumbana na msiba mkuu huku akikanyagwa na mapepo. … Maafa haya yatatekelezwa Nami na ni wazi kwamba Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamtaweza kutenda kwa Wema mbele Yangu, hamtaweza kuyaepuka maafa” (“Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari” katika Neno Laonekana Katika Mwili).

Moto umetupatia nuru: Hata kama mifuko ya mtu fulani imejaa fedha, anatukuzwa, anaweza kufurahia maisha ya kujistarehesha na ya kisasa, na huheshimiwa sana na kuonewa kijicho, anapokabiliwa na maafa yote haya yanavunjika. Katika moto, miongoni mwa wale ambao hawakuweza kustahimili joto la moto na kupoteza maisha yao kwa kuruka kutoka kwa jengo hilo, miongoni mwa wale ambao maisha yao yalikwisha kwa kutokuwa na matumaini walipokuwa walipunga mikono kwa majonzi madirishani, wengine walikuwa na pesa na hadhi, baadhi yao walikuwa wazuri na waliovalia mavazi ya kupendeza, baadhi yao walikuwa na familia zao…. Hata hivyo, moto ulipoongezeka, ukichoma kwa pande zote, hakuna walichokuwa nacho kingeweza kuwaokoa kutoka kwa ndimi hizo za moto. Ni kama maneno ya Mungu: “Wale wanaoishi nje ya neno Langu, waliokimbia mateso ya majaribu, si wao wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale na pasipo na pahali pa kupumzika, wala pasiwe na neno Langu la kufutia machozi. Ingawa kuadibu Kwangu na usafishaji hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wanatangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli?” (“Maana ya Mwanaadamu Halisi” katika Neno Laonekana Katika Mwili).

Ndugu zangu wapendwa, moto wa wilaya ya Ji umepita, lakini kwa ruhusa ya Mungu, na kwa onyo na kumbusho la Mungu kwetu. Wakati huo huo, ni wokovu wa Mungu wa upendo kwetu. Ningependa tulizingatie na kwalo kujua nia njema ya Mungu, kuweka muda zaidi na jitihada katika kutafuta ukweli, kutembelea njia sahihi ambayo Mungu huongozea maisha yetu kusonga mbele. Ni kwa njia hii tu tunapoweza kupokea ahadi na baraka za Mungu. Wakati huo huo, acha iwe kwamba Mungu huhamasisha roho zetu, akituacha tuokoe roho zaidi kati ya maafa haya ya mara kwa mara, tukileta faraja kwa moyo wa Mungu uliohuzunika na kusumbuka.

Maudhui Yanayohusiana

 • Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

  Kwamba neno la Mungu huahidi watu kwamba Mungu hutunza na hulinda, kwamba Mungu hutawala vyote, kamwe halitakuwa tena fungu la maneno tu kwangu. Katikati ya maafa haya nilipata nuru kwa wingi. Nilipata uzoefu kwamba tukiweka mustakabali na jaala zetu mikononi mwa Mungu, sio kuandaa mbadala na mipango kwa ajili yetu wenyewe, lakini kutafuta ukweli na kumridhisha Mungu kikamilifu, basi bila kujali ni hali ipi Mungu atatufadhili, kutulinda, na kutusaidia wakati wa matatizo yoyote. Kwa sababu Mungu ni mwenye haki kwa kila mtu.

 • Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

  Na hivyo ilikuwa kwamba tulikuwa kwa mvua kwa masaa matano mfululizo. Kwa kweli, kufikia wakati huo waokozi wachache walikuwa tayari wametuona, lakini kwa kuona jinsi mkondo wa maji ulivyokuwa na nguvu, walihofia kusombwa na maji, hivyo badala yake wakaangalia tu kutoka mbali bila kuja kutuokoa. Yamkini, wanapokabiliwa na maafa, kila mtu ni mwenye ubinafsi na wasiojiweza; watu hawawezi kabisa kuokoana wao kwa wao. Ni Mwenyezi Mungu pekee Aliye chanzo chetu cha uzima; zaidi ya hayo, Yeye ndiye pekee Ambaye anaweza kutuokoa mapema. Kumwacha Mwenyezi Mungu ni kufa.

 • Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

  Katika siku za nyuma sikuweza kufungua kinywa changu kuhubiri, sikuthubutu kuzungumza. Kwa njia ya uzoefu huu mimi sitarudi nyuma tena; niko tayari kuweka jitihada zote kuchukua uzoefu wangu na kushuhudia. Kwa kuwa niliona na kupata uzoefu wa wokovu wa Mungu na upendo Wake wa kweli na halisi zaidi katika jaribio la maafa, ninawezaje kukosa kuwa na ushuhuda Kwake?

 • Kupitia Utunzaji wa Uangalifu wa Mungu wa Wokovu wa Mwanadamu katika Maafa

  Kwa njia ya uzoefu huu nilielewa kweli kwamba Mungu hushusha maafa sio kuwaangamiza wanadamu lakini kuathiri wokovu wao. Kwa upande mmoja, Yeye hutupa tahadhari, watoto tulio vipofu na waasi ambao humwamini Yeye lakini bado tuko shingo upande na humdanganya na kumsaliti Yeye. Kwa upande mwingine, ni zaidi kuziokoa roho zote fukara ambazo kwanza zilikuwa Zake lakini bado zinaishi chini ya utawala wa Shetani. Njia hii ya wokovu ina utunzaji mwingi wa uangalifu wa Mungu.