Naona Ukweli wa Upotovu Wangu

13/01/2018

Imeandikwa Na Li Heng, Mkoa wa Jiangsu

Miongoni mwa maneno ambayo kwayo Mungu humfichua mwanadanu nilipata kifungu hiki: “Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu” (“Sura ya 36” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilidhani maneno haya ya Mungu yalikusudiwa kuwafichua wale wakanaji Mungu watawala wa mabavu, kwa sababu wao huyakomesha mawazo ya watu na kwa ukali kuwakataza watu kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu; wao huwatesa kikatili watu wa Mungu wateule, wao huivuruga na kuiharibu kazi ya Mungu popote wanapoweza, wao hufanya mambo mengi maovu na ni wakaidi na wasiomcha Mungu, wakimpinga Mungu katika kila kitu. Mimi, kwa upande mwingine, ni muumini wa Mungu ambaye hutimiza wajibu wake kanisani, na ingawa nina tabia potovu, sijakaribia kuwa muovu kama wao—ningewezaje kuwa mfano halisi na mtoto wa joka kubwa jekundu? Hayo yalikuwa hivyo mpaka nilipofichuliwa na kazi ya Mungu, na ni hapo tu nilipojua kwamba asili yangu ilikuwa sawa na ile ya joka kubwa jekundu, na kwamba nilikuwa, bila shaka, mfano halisi wa joka kubwa jekundu.

Kulikuwa na shemasi fulani katika kanisa letu ambaye ailiyefungwa kikiki na kuzuiwa na familia yake. Kwa sababu hiyo, hakuwa mwangalifu sana katika kutimiza wajibu wake, na mara nyingi alisahau kuhudhuria mikutano ya vikundi. Nilifanya ushirika naye, nikisema, “Hufai kutowajibika sana au kuwa hobelahobela na wajibu wako. Wewe ni shemasi wa kanisa na una jukumu kwa maisha ya ndugu na dada zetu. Mungu amekuaminia agizo muhimu kama hilo, na Mungu atalikirihi jambo hili na atachukia ukilipuuza!” Baada ya kumpa ushirika huu, hakukosa tu kuukubali, lakini pia alitoa visingizio na alitoa sababu za kunikanusha. Niliwaza, “Yeye hana upatanifu na Mungu. Hawezi kuwa mtu ambaye Mungu anataka kumwokoa, anaweza kweli? Kwa hakika hafai kutumiwa na Mungu, au mtu aliyefichuliwa na kuondoshwa na Mungu?” Nilianza kuangalia kwa makini mtu wa kuchukua nafasi yake katika kanisa letu. Mara tu nilipopata mtu aliyefaa kwa kazi hiyo, nilipanga kumwondoa. Lakini kwa wakati uliopo hapakuwa yeyote aliyefaa, hivyo chaguo langu la pekee lilikuwa ni kufanya ushirika naye tena. Baadaye alielewa kuwa alikuwa ameshindwa kutimiza wajibu wake na hakuwajibika na alikuwa mvivu, na alitaka kulipia makosa yake ya zamani. Lakini bado, daima nilihisi kama haikutosha, na sikuwa na upendo mwingi kwake baada ya hayo. Wakati mmoja, nilimtakaa afanye mkutano na familia moja mwenyeji ambayo ilikuwa mbali kidogo na pale alipoishi, lakini alikataa na hakutaka kwenda. Hasira moyoni mwangu ilifurika aliposema hilo. Nilijiwazia: “Wewe ni mwenye kuchagua mno katika kutekeleza wajibu wako, kufanya kile unachotaka na kupuuza kile usichotaka. Huna hata chembe ya utii na wewe hukanusha chochote unachoambiwa. Kanisa haliwahitaji kama wewe, na unafaa ufukuzwe tu. Kwa vyovyote, umejiletea haya kwa kutotekeleza wajibu wako vizuri.” Ingawa nilijua kuwa kuwafukuza watu kiholela huhitilafiana na kanuni, wazo hili lilikuwa imara na liliendelea kuja katika mawazo yangu, sikuweza kulidhibiti, na moyoni mwangu lilinisumbua daima, na hali yangu ikadhoofika kwa kasi. Nikiwa katika maumivu, nililoweza kufanya lilikuwa kuja mbele ya Mungu na kumwomba, “Ee Mungu! Huyu dada hanisikilizi, kwa hiyo ninahisi kama nataka kumfukuza haraka iwezekanavyo. Najua kwamba wazo hili si sahihi, lakini siwezi kujizuia. Ee Mungu! Nakuomba Uniniokoe na uniruhusu nimwendee huyu dada kwa njia sahihi, na Usiache nifanye chochote kinachokuasi.” Baada ya kuomba, nilijihisi mtulivu zaidi, na hamu yangu ya kumfukuza haikuwa na nguvu kama awali.

Kisha kifungu cha maneno ya Mungu kikaibuka katika mawazo yangu, “Udhihirisho wa joka kuu jekundu ni upinzani Kwangu, ukosefu wa ufahamu na utambuzi wa maana ya maneno Yangu, mateso ya mara kwa mara Kwangu, na kutafuta kutumia njama ili kuzuia usimamizi Wangu. Shetani anadhihirika kama ifuatavyo: kupambania mamlaka na Mimi, kutaka kuwamiliki watu Wangu wateule, na kutoa maneno hasi ili kuwadanganya watu Wangu” (“Sura ya 96” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinishtua. Je, si ufunuo wangu ulikuwa wa joka kubwa jekundu kabisa? Joka kubwa jekundu, hata hivyo, lilikuwa na uwezo wa kufanya mambo ambayo sikuwa nimeyafanya. Niliwazia jinsi Mungu hutekeleza kazi Yake ya siku za mwisho ili kumwokoa mwanadamu, na bado joka kubwa jekundu kwa hasira huwakandamiza, huwatesa kikatili watu wa Mungu wateule, likifanya yote liwezalo kueneza uvumi ili kulikashifu na kuliaibisha Kanisa la Mwenyezi Mungu na kuwavuruga watu ili wasimwamini na kumfuata Mungu, likijaribu kuchukua fursa zao za kuokolewa, likiivuruga na kuiingilia kazi ya Mungu. Si hayo hasa ndiyo niliyokuwa nikiyafanya? Nilipoona kwamba dada yangu alikuwa na dosari fulani, sikufanya ushirika juu ya ukweli kwa sababu ya upendo ili kumsaidia atambue makosa yake, kuelewa mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, na kuweza kuitii kazi ya Mungu; badala yake, nilizikuza kuzichambua kupita kiasi dosari zake na nilitaka kuifuata tamaa yangu mwenyewe kumfukuza na kuharibu nafasi yake ya kuokolewa. Si nilikuwa nikijaribu kuivuruga na kuiharibu kazi ya Mungu ya wokovu kati ya wanadamu? Si kwa kweli nilikuwa mfano halisi wa joka kubwa jekundu? Katika mahubiri fulani, nilisoma, “Angalia jinsi joka kubwa jekundu humtesa Mungu na jinsi huwatesa kwa ukatili watu wateule wa Mungu, kisha angalia jinsi wewe hupinga na kuasi dhidi ya Mungu na jinsi usivyoweza kuelewana kwa amani na watu walioteuliwa na Mungu. Umejazwa na mifundo na una ubinafsi mno. Una tofauti gani na joka kubwa jekundu? … Watu wengi huwa hawatambui sumu za joka kubwa jekundu ambazo hujificha ndani yao. Wao daima hufikiri kuwa joka kubwa jekundu ni ovu mno, na kwamba watakapomiliki mamlaka, watakuwa bora zaidi kuliko joka kubwa jekundu; lakini hiyo ndiyo hali kweli? Ungeshika mamlaka hivi sasa, ni kiasi gani ungekuwa bora zaidi kuliko joka kubwa jekundu? Unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko joka kubwa jekundu? Ukweli ni kwamba joka kubwa jekundu kushika mamlaka hakuna tofauti na wanadamu wowote wapotovu wakishikilia mamlaka. Ikiwa joka kubwa jekundu linaweza kuwaua watu milioni 80, ni wangapi utakaowaua ukishikilia mamlaka? Wakati kundi moja linapoinuka kukupinga, utasema, ‘Kuua kundi si jambo kubwa, joka kubwa jekundu liliua watu milioni 80. Mimi ninaua tu kundi ndogo, hiyo ni idadi kidogo sana kuliko joka kubwa jekundu.’ Wakati watu milioni 10 watainuka kukupinga, utasema, ‘Naweza kuwaua hawa watu milioni 10 pia, kwa sababu nisipofanya hivyo, nitawezaje kushikilia mamlaka?’ Je, huoni tatizo hapa? Wakati huna mamlaka yoyote, hufanyi maovu yoyote, lakini hakuna uhakika kwamba hutafanya matendo maovu utakaposhika mamlaka, kwa sababu asili za mwanadamu zote ni sawa” (“Jinsi Watu Wanavyopaswa Kushirikiana na Kazi ya Mungu ya Kumkamilisha Mwanadamu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III). Kupitia kupata nuru na mwangaza wa maneno ya Mungu na uchambuzi wa mahubiri haya, hatimaye niliona kwa dhahiri tabia yangu halisi, kwamba nilikuwa mfano halisi wa joka kubwa jekundu, na kwamba asili yangu potovu haikuwa tofauti na asili ya joka kubwa jekundu. Dada yangu alipokuwa haelewi ukweli kwa dhahiri na alikuwa hobelahobela na asiyewajibika katika wajibu wake, sikumsaidia kwa moyo wa upendo hata kidogo, lakini badala yake nilimsemeza bila kuridhika kwa sauti yenye nguvu. Na aliponipinga na hakufuata na kuitii mipango yangu, nilikasirika na kumshutumu kama mtu aliyefichuliwa na kuondoshwa na Mungu, nia mbovu iliibuka moyoni mwangu na nilitaka kumfukuza kanisani. Si nilikuwa natenda kama joka kubwa jekundu, na sera zake za “Kujitukuza mimi pekee,” “Wale wanaotii watafanikiwa, huku wale wanaopinga wataangamia,” “Piga chuku ubora wa kitu” na “Waue ovyoovyo watu wengi wasio na hatia”? Hii yote ni mifano hasa ya sumu za joka kubwa jekundu! Joka kubwa jekundu huwaua wengi wasio na hatia na huwaua watu wasiohesabika; halijawahi kuyatilia maanani maisha ya watu, na yeyote asipokubaliana nalo au kulitii, au kulikosea kwa namna fulani, basi humuua. Kama ningekuwa mamlakani, ningekuwa sawa tu na joka kubwa jekundu, na hakungekuwa na uovu ambao singeutenda na ningetenda kwa njia isiyobashirika. Isingekuwa kwa ajili ya mipango ya kazi na kanuni zilizowekwa na kanisa vikinizuia, na ndugu na dada zangu wakinisimamia, bila shaka ningekuwa nimeshamtoa dada yangu mhanga zamani sana. Kutoka kwa fikira na mawazo yangu mwenyewe, niliona kuwa, kwa kuwa nilikuwa nimefichua mambo kama hayo, basi niliyohitaji tu ingekuwa mamlaka na madaraka ili kuweza kufanya matendo sawa na ya joka kubwa jekundu, ya kuwaua watu wengi wasio na hatia. Kupata nuru na uongozi wa Mungu viliniwezesha kujua asili na kiini changu vibaya na viovu, na ilikuwa ni hukumu ya Mungu na kuadibu vilivyonipa fursa ya kutubu. Moyo wangu ulijaa shukrani kwa Mungu, na pia nilikuja kuyachukia na kuyatubu matendo yangu hata zaidi.

Uzoefu huu ulinipa ufahamu wa kweli wa kiini changu kipotovu. Niliona kwamba kwa hakika nilikuwa mtu bila mantiki au dhamiri, bila shaka uzao wa joka kubwa jekundu. Lakini pia lilinifanya kuhisi kuwa bila kujali jinsi kuchomwa na maneno ya Mungu kunavyoweza kuwa au kama kunakubaliana na mawazo ya mwanadamu, kila tamko ndilo linaloishi milele, ukweli usiobadilika, na siku moja wanadamu wapotovu watashawishika kabisa. Ee Mungu! Nataka kutekeleza wajibu wangu vizuri kukulipa kwa neema ya wokovu Wako, nataka kupatana na ndugu na dada zangu na kufidia makosa yangu ya zamani, na kuwa mtu mpya ambaye hukufariji Wewe.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ulinzi wa Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya...

Hukumu ni Mwanga

Zhao Xia Mkoa wa Shandong Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Kama vile...

Kuwa Mtu Mwaminifu Ni Kuzuri Kweli!

Kwa njia hii nilitenda kama mtu mwaminifu, yule ambaye kweli alitenda kulingana na matakwa ya Mungu, na biashara ikawa bora zaidi na zaidi. Nilijua kwamba hii ilikuwa baraka ya Mungu. Mungu hakunipa vitu yakinifu tu. Muhimu zaidi pia Alinifundisha jinsi ya kutenda. Katika dunia halisi kweli ni vizuri kutenda kama mtu mwaminifu kulingana na neno la Mungu!

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp