Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ni Nini Ambacho Kimeidanganya Roho Yangu

4

Xu Lei Mji wa Zaozhuang, Mkoa wa Shandong

Siku moja nilipokea taarifa kutoka kwa kiongozi wangu mkubwa, ikinitaka nihudhurie mkutano wa wafanyikazi wenza. Kwa kawaida hili ni tukio la kufurahisha, lakini mara tu nilipofikiria jinsi kazi yangu hivi karibuni ilikuwa machafuko kabisa, sikuweza kujizuia kuhisi wasiwasi. Kama mkuu wangu angejua jinsi sikuwa nimemaliza kazi yoyote yangu, bila shaka angehitaji kunishughulikia, na huenda hata kunibadilisha na mwingine kazini. Ningefanya nini basi? Siku iliyofuata nilikwenda kwa mkutano na moyo mzito. Nilipofika huko, nikaona kwamba mkuu wangu alikuwa bado hajafika, lakini baadhi ya wafanyakazi wenzangu walikuwa hapo tayari. Niliwaza: “Sijui kazi yoyote yao iko katika hali gani. Katika mkutano wa mwisho, niliwasikia wakisema jinsi karibu walikuwa wamefanya kazi yao, na wakati huu lazima kwa kweli wawe wameimaliza yote. Kama wamemaliza kazi yao yote na ni mimi tu ambaye ni mbaya sana, basi niko kwa shida kubwa.” Nilishangaa basi kwamba, wakati tulipokuwa pamoja tukizungumza juu ya hali zetu wenyewe za kazi, wengi wa wafanyakazi wenzangu walikuwa wakisema jinsi hawakuwa wamemaliza sehemu fulani za kazi zao. Niliposikia jambo hili, moyo wangu uliokuwa mzito sana kabla kwa ghafla ulihisi wepesi sana. Niliwaza: “Yaonekana kuwa hakuna mtu aliyemaliza kazi yake, sio mimi tu. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi basi. Hatuwezi kubadilishwa sote.” Sehemu kubwa ya hisia zangu zisizokuwa na utulivu wakati huo zilitoweka papo hapo.

Nilipokuwa tu nikianza kupata starehe katika hali yangu ya kujifariji, kifungu katika ushirika kutoka hapo juu kilizurura ndani ya mawazo yangu: “Mtu akileta maoni ya kidunia katika familia ya Mungu, basi hizo ni dhana na yanamdharau Mungu. Watu wengi wana maoni sawa juu ya mambo kama wasioamini. Kwa sababu hawana ukweli ndani yao, mara tu wanapokuja katika familia ya Mungu wao hutumia maoni ya kidunia ili kutazama kazi ya familia ya Mungu, kutoa maoni juu ya mambo ya familia ya Mungu, matokeo yake yakiwa ni wao kusita, kujisababisha wao daima kuwa dhaifu na hasi, kushindwa kufuatilia ukweli au kulipa gharama. Je, si hili limesababishwa na ujinga wao?” (“Jinsi ya Kujua Dhana za Wanadamu na Hukumu” katika Ushirika na Mahubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha III). Maneno haya yalinifanya nifikiri juu ya mjibizo wangu muda mfupi uliopita. Nilipofikiria jinsi nilivyokuwa sijamaliza kazi yangu, moyo wangu ulijihisi kuwa mzito sana na sikuweza kuacha kuwa na wasiwasi. Lakini nilipojua kwamba wafanyakazi wenzangu pia hawakuwa wamemaliza kazi yao, mara moja nilihisi utulivu, na nikawaza kwa dhamiri nyepesi kwamba sio mimi tu ambaye kazi yake haikuwa imefanikisha chochote. Kama mkuu wetu angekuwa atushughulikie, basi kila mtu angekuwa na mgao wake. Kwa kuwa wengi wetu sana hatukuwa tumemaliza kazi yetu, msimamizi wetu kwa hakika hangetubadilisha wote. Je, si kufikiria kwa aina hii kulitawaliwa na maoni ya Shetani: “Sio dhambi kama kila mtu huitenda”? Si kwa kweli nilikuwa nikitumia maoni ya Shetani kupimia kanuni za kazi ya kanisa? Nilikuwa nimetumia maoni yenye mantiki ya Shetani kwa kanisa, nikiyatumia kujiliwaza, kujipendeza—lakini si nilikuwa nikijidhuru tu? Kwa kweli nilikuwa kipofu sana na mjinga! Nikifikiria nyuma, kulikuwa na nyakati nyingi nilipokubali utawala wa maoni haya ya Shetani ili kujifariji. Kwa muda mfupi, niliishi katika mwili bila kuingia kwa maisha na, ingawa nilikuwa na wasiwasi juu ya wokovu wangu mwenyewe, nilipoona baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike pia kutokuwa wameingia katika ukweli, sikuwa na wasiwasi na niliacha kujihangaisha. Nilidhani kwamba kama watu wengi sana hawakuwa wameingia katika uzima, basi Mungu hangetuchekecha, Angetucheka? Kwa hivyo, niliishi katika hali ya kiholela ya kujishughulisha mno na mambo, kutowajibikia maisha yangu. Nilipokuwa sijaandika makala yoyote kwa muda mrefu na nilikuwa na hisia za kujishutumu mwenyewe, ningewaona ndugu fulani ambao pia hawakuwa wameandika chochote, na shutuma katika moyo wangu ingetoweka. Ningewaza: Sio jambo kubwa kutoandika makala na, hata hivyo, sio mimi pekee ambaye hajaandika moja. Wakati sikuona matokeo yoyote kamwe kutoka kwa kazi yangu ya injili, ningehisi wasiwasi. Lakini nilipoona kazi ya injili ya maeneo mengine bila matokeo yoyote pia, ningehisi utulivu, nikidhani kwamba kila mtu alikuwa jinsi hii, kwamba haikuwa mimi tu ambaye hakumleta mtu yeyote kanisani. … Wakati huo, niliona kuwa maoni ya Shetani—“Sio dhambi kama kila mtu huitenda”—yalikuwa yamekita mizizi moyoni mwangu sana. Chini ya utawala wa maoni haya, nilikuwa daima nikijipendeza nilipokuwa nikitekeleza kazi zangu, sikuwa nikitia bidi yote katika kazi na sikuwa nikitafuta matokeo bora zaidi. Haikusababisha hasara kubwa tu kwa kazi ya kanisa, lakini pia iliisababishia hasara kubwa sana kwa maisha yangu mwenyewe. Kwa sababu nilikuwa nimekubali sumu ya dhana yenye kosa ya Shetani—“Sio dhambi kama kila mtu huitenda”—Sikuwa nimechukua mzigo halisi katika kazi yangu kwa kanisa, mara zote nikiridhika na kazi ya shingo upande na sikuwa nikitafuta matokeo yoyote; nilikuwa nimepoteza dhamiri na mantiki ambavyo kila mmoja wa viumbe wa Mungu ni lazima wawe navyo. Kwa sababu nilikuwa nimekubali pingu za maoni ya Shetani ya “Sio dhambi kama kila mtu huitenda,” daima nilikuwa nikiboronga tu katika harakati za mimi kumfuata Mungu. Sikuwa nimechukulia imani yangu kwa Mungu kuwa ya thamani yoyote hata kidogo, sikutafuta ukweli kwa bidii, sikujali kuhusu au kuzingatia kuingia kwangu mwenyewe kwa maisha; sikuwa na lengo la kufuatilia, sikuwa na mwelekeo katika maisha. Niliboronga tu na kuishi kwa kufanya kiwango cha chini sana. Ni hapo tu nilipoona kwamba nilikuwa nimedhuriwa vibaya sana na maoni ya Shetani ya “Sio dhambi kama kila mtu huitenda” na nilikuwa nimepoteza dhamiri kabisa, mantiki, uadilifu na heshima ambazo mtu wa kawaida anapaswa kuwa nazo. Nikifikiria kwa makini, nilikuwa nikiishi ndani ya mawazo yangu na dhana zangu wakati wote, nikiamini “Sio dhambi kama kila mtu huitenda,” kwamba kama watu wengi wakifanya dhambi hiyo basi Mungu atatuacha tuponyoke kupitia kwa wavu na bila kumfanya mtu yeyote awajibike, bila kufikiria kamwe kama Mungu angewatendea watu kwa njia hii au la. Wakati huo, sikuweza kujizuia kufikiria maneno ya Mungu, ambayo yanasema: “Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo” (“Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalifanya nitetemeke kwa hofu, kwa kuwa niliona kwamba tabia ya Mungu haitamruhusu mtu yeyote afanye kosa na kwamba Yeye hatategemeza uamuzi Wake juu ya kama kumwangamiza mwanadamu kwa msingi wa idadi ya wenye dhambi au la. Nikifikiria nyuma, watu wa siku za Nuhu walikuwa wenye dhambi na wazinzi, wakipotoka sana kiasi kwamba Mungu aliwaangamiza wote walioishi wakati huo ila familia ya Nuhu. Uharibifu Wake wa mji wa Sodoma pia ulikuwa hivi. Sasa watu katika siku za mwisho wamefikia bilioni kadhaa, idadi iliyozidi kwa mbali ile ya siku za Nuhu. Lakini Mungu hajaweka sheria Yake kando na kuonyesha rehema kwa sababu kuna watenda dhambi wengi katika siku za mwisho; kwa watu hawa Mungu ana chuki, karaha na kuwakataa tu. Mwishonwe, mbali na wachache ambao wanaweza kuokolewa, Mungu atawaangamiza kabisa wale wote watakaobaki. Ni hapo tu nilipoona jinsi nilivyokuwa nimeelewa kidogo sana tabia ya Mungu. Sikuelewa kwamba Mungu ni mwenye haki, Mungu ni mtakatifu ambaye hamruhusu mtu afanye kosa, kiasi kwamba nilikuwa nimeduwazwa na uongo wa Shetani na nilikuwa nimeangukia mipango yake ya hila. Leo, kama haingekuwa kupata nuru ya Mungu, ningekuwa bado ninaishi katika dhambi bila kufikiri kuwa ilikuwa dhambi, mwishowe nikiadhibiwa na Mungu bila hata kujua kwa nini ningekufa—kwa kweli ilikuwa hatari sana!

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa nuru Yake ambayo ilinifanya niamke kutoka kwa udanganyifu wa Shetani na kutambua kwamba “Sio dhambi kama kila mtu huitenda” ilikuwa kabisa ni dhana ya uasi ya Shetani. Ulikuwa mpango wa hila wa Shetani wa kuwadhuru na kuwaangamiza wanadamu. Aidha, niliona kwamba Mungu ni mwenye haki, kwamba tabia ya Mungu haitaruhusu kosa lolote, kwamba Mungu atategemeza uamuzi wa mwisho kwa upande wa wanadamu kama wana ukweli au la, na kwamba Yeye hataonyesha huruma ya kipekee kwa mtu ambaye hana ukweli. Kuanzia leo kwendelea, napenda kufanya jitihada kabisa katika kutafuta ukweli, katika kutafuta kumjua Mungu, kutegemeza mtazamo wangu wa mambo yote kwa maneno ya Mungu, kutumia maneno ya Mungu kama kiwango ambacho kwacho nitajifanyia matakwa makali, kuacha uongo wote na udanganyifu wa Shetani, na kutafuta kuwa mtu anayeishi kwa kutumainia ukweli.

Maudhui Yanayohusiana

 • Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

  Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

 • Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

  Maneno ya Mungu tena yalinileta kwa ufahamu wa jinsi huduma yangu kwa Mungu kwa kweli ilikuwa ni kujishuhudia mwenyewe na kujiinua na yalinisaidia kuona matokeo mabaya ya tabia hii. Maneno ya Mungu yalinisaidia kuona kwamba asili yangu, kama ile ya malaika mkuu, ingeweza kuniongoza kuwa gaidi dhalimu, na kwamba ningeweza kusababisha maangamizi makubwa. Nilifikiria kuhusu jinsi huduma yangu kwa Mungu haikutimizwa kulingana na kanuni sahihi za huduma; haikuwa ikimwinua Mungu na kumshuhudia Mungu, si kufanya wajibu wangu. Badala yake, siku zangu zilitumiwa kujionyeshwa mwenyewe, kujishuhudia mwenyewe, kuwavuta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele yangu. Je, si aina hii ya huduma ni ya kudharauliwa?

 • Kutambua Kuwa Niliitembea Njia ya Mafarisayo

  Ee, Mwenyezi Mungu! Niko tayari kugeuza nia zangu mbovu na dhana chini ya uongozi wa neno Lako. Niko tayari kutimiza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa na kufuata mfano wa Petro kwa kufanya kile ninachopaswa kufanya kwa kupitia njia ya kumpenda Mungu, bila tena kufanya kazi katika nafasi yangu kama kiongozi, na kufanya kila ninaloweza kutafuta na kuendelea mbele kwelekea njia ya Petro!

 • Huyu Ni Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

  Kutoka leo, napenda kuchukua kirai “tafuta ukweli na kuwa na hisi ya haki” kama vigezo vya mwenendo wangu, kutafuta kuingia ndani zaidi katika ukweli, kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kujitahidi kuwa mtu mwema kwa dhati hivi karibuni ambaye yu dhahiri juu ya upendo na chuki na ambaye ana hisi ya haki.