Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Chochote Mungu Asemacho Ndiyo Hukumu Hasa ya Mwanadamu

22

Xunqiu Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan

Nilikuwa nikidhani kwamba Mungu alimhukumu na kumuadibu mwanadamu wakati tu Alipoufichua upotovu wa asili wa mwanadamu au alipoeleza maneno mkali ambayo yaliuhukumu mwisho wa mwanadamu. Ilikuwa ni baadaye kabisa tu ambapo tukio moja liliponiongoza kutambua kwamba hata maneno mapole ya Mungu pia yalikuwa ni hukumu na kuadibu Kwake. Niligundua kuwa kila neno Alilolisema Mungu ni hukumu Yake kwa mwanadamu.

Hivi karibuni, dada mzee wa familia ya mwenyeji alipata kuhusika na hisia za kimwili, na kwa sababu hiyo aliteseka sana. Niliwasiliana naye kwa karibu mara kadhaa, lakini ilionekana kuwa bure. Alibaki vile vile. Pole pole nikakosa subira, nikifikiria mwenyewe, “Nimezungumza nawe mara kadhaa, lakini hujabadilika. Labda huna shauku katika ukweli. Sitawasiliana nawe kwa karibu tena.” Baada ya hapo, sikuhisi tena kuwa radhi kujihusisha naye na ni mara chache sana nilishughulika naye. Siku moja, dada mwingine ambaye nilishirikiana naye alipendekeza kwamba tulipaswa kuomba na dada huyo mzee. Baada ya kusikia hivyo, nilihisi maudhi, “Kwa nini? Ingekuwa ni kupoteza wakati kukaa pamoja naye, na sala zetu hazingezaa matunda.” Kwa kweli nilijua hili lilifichua kiburi changu, kilichokuwa ni tabia ya Shetani. Nilikuwa nawadharau wengine na kutoonyesha upendo kwa wengine. Hata hivyo, sikuweza tu kuzuia hili. Tulipoomba pamoja, bado niliona ugumu kuachia huru mawazo na hisia zangu za ndani sana kiasi kwamba nilizama katika giza la kiroho na sikuweza kuhisi kuwa Mungu alikuwa pamoja nami. Aidha, nilihisi kusongwa ndani kana kwamba moyo wangu ulizuiwa na haungeweza kuachiliwa. Baadaye, niliomba mbele ya Mungu juu ya mashaka yangu, “Mungu, nilikuwa nafahamu kiburi na ukatili wangu. Sikuonyesha nadhari wala wema kwa dada yule mzee. Lakini nilishindwa tu kujibadilisha. Mungu, nakusihi Wewe unipe nuru kuhusu ukweli na kujijua vyema.” Nilipokuwa nikitoa hiyo sala, nilikumbuka visivyo dhahiri maneno ya Mungu. Mara moja nikafungua kitabu cha neno la Mungu na kupata kauli zifuatazo: “Mbona inasemwa kwamba kiwango cha uamuzi wako kumpenda Mungu, na iwapo kweli umeukataa mwili, kinategemea iwapo una chuki bila sababu kwa ndugu zako, na iwapo, kama una chuki bila sababu, unaweza kuweka kando chuki bila sababu kama hiyo. Ambayo ni kusema, wakati uhusiano wako na ndugu zako ni wa kawaida, basi hali zako mbele ya Mungu pia ni za kawaida. Wakati mmoja wa ndugu zako ni dhaifu, hutamchukia, kumdharau, kumtania, ama kutomthamini. Ikiwa unaweza kumsaidia, utawasiliana nay…. Ukihisi huwezi kumkimu, basi unaweza kumtembelea. Si lazima hili lifanywe na kiongozi wa kanisa—ni jukumu la kila ndugu kufanya kazi hii. Ukiona kwamba kaka au dada yuko katika hali mbaya, unapaswa kumtembelea. Hili ni jukumu la kila mmoja wenu” (“Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, onyo dogo kwamba “wakati uhusiano wako na ndugu zako ni wa kawaida, basi hali zako mbele ya Mungu pia ni za kawaida” lilichapiwa akilini mwangu kwa njia fulani ya wazi. Nilikuwa nikitafuta huku nikifikiria sana kanuni hii. Kupitia kupewa nuru na Roho Mtakatifu, nilihisi kuwa kanuni hii iliyoonekana kuwa ya wazi kwa kweli ilijumuisha uadhama na hukumu, na iliuchoma moyo wangu kama upanga. Mungu daima kwa dhahiri alikuwa amemwambia mwanadamu kwamba ni kwa msingi wa maneno ya Mungu tu wanadamu wanapoweza kuanzisha uhusiano wa kawaida miongoni mwa ndugu wa kiume na kiume, na uhusiano wa mtu huyo na Mungu utakuwa wa kawaida mradi uhusiano wake na ndugu wa kiume na wa kike ulikuwa wa kawaida. Nilipoelewana na wengine, yote niliyothibitisha ilikuwa ni tabia potovu ya Shetani, hasa katika kudharau na kuwakataa wengine. Sikukuwa na uhusiano wa kawaida na watu, kwa hiyo ningewezaje kufurahia uhusiano wa kawaida na Mungu? Lilikuwa jukumu lisilobadilika la mtu kuwatembelea na kuwatumikia ndugu wa kiume na wa kike ambao walikuwa baridi na dhaifu. Yalikuwa ni maisha ya kuishiwa na watu wanaotaka kumpenda Mungu; mwenendo wa ndugu wa kiume na wa kike waliopendana. Kwa kulinganisha, sikujali kabisa nilipopata habari kuhusu hali mbaya ya dada mzee. Ingawa nilionekana kuwasiliana nawe kwa karibu, ndani kabisa sikufanya hivyo kwa moyo uliompenda Mungu. Sikujaribu kadri ilivyowezekana kumsaidia na kumtegemeza. Sikuwasiliana naye kwa karibu kwa uvumilivu kwa moyo mwema au ufahamu wa mtu ambaye alikuwa ameteseka—mtu ambaye alikuwa ameishi katika giza—kumsaidia kutoka kwa hali hasi. Hata niliamua kuwa huyu dada mzee hakuwa na nia ya kuutafuta ukweli, na kwa hiyo nilimdharau na kumuepuka. Kwa hiyo nilipoteza uhusiano mzuri na Mungu na nikawa wa kustahili kuadibu Kwake. Niliteseka kutokana na giza la kiroho. Si ni kweli kwamba tabia ya Mungu ilikuwa imenijia? Nilivyozidi kuifikiria, ndivyo nililivyozidi kuhisi kabisa kuwa kanuni hii hii ni hukumu ya uso kwa uso ya Mungu kwangu. Nilitahayari na kuona majuto kwa kina. Ubinadamu wangu umepungukiwa sana! Kisha, hata hivyo, uchaji wangu kwa Mungu ukainuka wenyewe na sawia. Nikagundua kwamba tabia ya Mungu ni moja ya uadhama na ghadhabu. Niligundua kwamba Mungu kweli ni mwenye haki mno na mtakatifu. Mungu aliweza kupekua ndani ya kila wazo, hivyo hapakuwa na utorokaji kutoka kwa hukumu Yake.

Hukumu ya maneno ya Mungu ilinisaidia kuacha chuki yangu dhidi ya yule dada mzee. Hivyo, nilipata radhi ya kuwasiliana naye kwa roho ya upendo na wema. Bila kutarajia, hata hivyo, kabla ya wasiliana naye kwa karibu tena, huyu dada mkubwa alikuwa amepokea nuru kutoka kwa Mungu na akayaondokea mashaka yake hasi kwa kuomba na kusikiliza nyimbo za neno la Mungu. Wakati huo, nilijihisi kufurahishwa kwamba hali yake ilikwishakuwa nzuri kabisa. Nilifurahi kwamba Mungu alikuwa ametuongoza, kama Atakavyo daima. Pia nilihisi kutaharishwa tabia mbovu ambayo nilikuwa nimeonyesha.

Nilimshukuru Mungu! Licha ya ukweli kwamba nilikuwa nimeonyesha uasi na upotovu tu wakati wa uzoefu huu, nilijifunza kuwa maneno ya Mungu makali kidogo yalikuwa pia ni hukumu Yake kwa mwanadamu na kuadibu kwa mwanadamu, na kwamba kila neno kutoka Kwake linakusudiwa kuwa la hukumu ya wanadamu. Sitaangalia tena kamwe maneno ya Mungu kwa dhana yangu mwenyewe. Nitakubali hukumu ya Mungu na kuadibu katika maneno na utii kamili. Nitatambua na kupokea ukweli zaidi ili kubadilisha tabia yangu haraka iwezekanavyo.

Maudhui Yanayohusiana

 • Mama wa “Vijijini” Akutana na Binti Mkwe wa “Mjini”

  Kupitia uzoefu wangu, kwa kweli nilihisi furaha ambayo huja kutokana na kuliweka neno la Mungu katika vitendo. Maneno ya Mungu kwa kweli yanaweza kutubadilisha na kutuokoa, yakituwezesha kuishi maisha yenye furaha na yenye baraka. Sasa familia yangu inaweza kuishi pamoja kwa upatanifu, na kwa ajili ya hilo namshukuru Mungu kwa dhati kwa kuniokoa. Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!

 • Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)

  Nina wana wawili wa kiume na wameachana na mwaka mmoja. Ili kuwalea kuwa watu waliostaarabika, wenye tabia nzuri, watu wema ambao wataweza watajijengea jina katika jamii na kufanikiwa, walipokuwa na umri wa miaka miwili, nilijadiliana na mume wangu juu ya kuwatafutia shule nzuri ya chekechea. …

 • Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

  Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kuliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha.

 • Kanuni Zangu za Maisha Ziliniacha Nikiwa Nimeharibika

  Maneno ya kawaida “Wote huwekelea mizigo kwa farasi anayekubali” ni ambayo mimi binafsi ninayafahamu sana. Mimi na mume wangu sote tulikuwa hasa watu wasio na hatia: Wakati wa masuala yaliyohusisha faida au hasara yetu binafsi, hatukuwa aina ya watu wa kubishana na kusumbuana na wengine. Pale ambapo tuliweza kuwa wavumilivu tulikuwa wavumilivu, pale ambapo tungeweza kuwa na fadhila tulifanya tulivyoweza kuwa na fadhila. Kama matokeo yake, mara nyingi tulijipata tukiwa tumedanganywa na kudhulumiwa na wengine.