Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

51

Zhang Jin, Beijing

Agosti 16, 2012

Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.

Ilikuwa Julai 21, mwaka wa 2012. Siku hiyo mvua ya mfoko ilinyesha, na nilikuwa tu nje nikitimiza wajibu wangu. Baada ya saa 10 alasiri, mvua ilikuwa bado haijaisha. Wakati mkutano wetu ulipomalizika, niliikabili mvua bila woga na kupanda basi kwelekea nyumbani. Wakati nikisafiri, mvua ikawa nzito zaidi na zaidi, na wakati basi lilipofika kituo cha basi kabla ya changu, dereva alituambia sisi sote abiria, “Basi hili haliwezi kwendelea zaidi; barabara imeporomoka huko mbele.” Hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kufanywa, kwa hivyo sikukuwa na chaguo ila kushuka kutoka kwenye basi na kutembea njia yote. Bila kudhubutu kumwacha Mungu, nilikuwa ninaendelea kuomba moyoni mwangu. Kutokana na nguvu ya gharika, maji yalikuwa yamemeza barabara kabisa. Nilijaribu kuendelea kwa kushikilia nguzo za saruji zilizosimama kwa safu kando ya barabara, nikisonga mbele hatua kwa hatua. Wakati huo, nikasikia mtu akipiga ukelele nyuma yangu, “Acha kusonga mbele! Haraka; geuka na kurudi! Huwezi kupita; maji hayo yana uketo na mkondo una kasi sana. Ukikusomba, sitaweza kukuokoa!” Wakati huo, hata hivyo, singesonga mbele wala kurudi nyuma, kwa sababu maji yalikuwa tayari yamefika kifuani mwangu. Sikudhubutu kutembea zaidi, hivyo yote niliyoweza kufanya ni kumwomba Mungu na kumsihi Yeye afungue njia yangu kupitia: “Mungu! Umeyaruhusu mazingira haya kunifika, na ikiwa nitaishi au kufa iko mikononi Mwako sasa. Kama kiwango cha maji kingeshuka kwa nusu futi tu, ningeendelea kutembea mbele. Mungu, fanya Unavyotaka; Niko tayari kuaminisha maisha yangu Kwako!” Baada ya kufanya sala hii, nilijihisi mnyamavu na mtulivu. Nilikumbuka mojawapo ya maneno ya Mungu: “Mbingu na ardhi na vitu vyote vimeasisiwa na kukamilishwa na maneno ya kinywa Changu na na Mimi chochote kinaweza kufanikishwa” (Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni). Maneno ya Mungu yalinipa imani na ujasiri. Kwa kuwa mbingu na ardhi na vitu vyote viko mikononi mwa Mungu, nilijua kwamba bila kujali jinsi gharika hiyo ilivyokuwa katili, haingeepuka mpango wa Mungu. Hakuna yeyote ambaye angetegemewa tena; mwanangu wa kiume, binti yangu … hakuna yeyote ambaye angeweza kumtunza mwenzake. Niliamini kuwa mradi nilimtegemea Mungu, hakukuwa na shida ambayo singeweza kuipita. Wakati ule ule, muujiza ukafanyika. Mkondo ukapungua zaidi na zaidi mpaka haukuwa tena mkali kama ilivyokuwa wakati mfupi awali, na nguzo za saruji zilizosimama kwa safu kando ya barabara zimefichuliwa hatua kwa hatua. Kwa hakika, kiwango cha maji kilishuka kwa nusu futi kutoka kiwango cha kifua changu. Na hivyo tu, niliondoka mahali hapo, hatua kwa hatua, chini ya uongozi wa Mungu. Isingekuwa kwa sababu ya huruma na ulinzi wa Mungu, sijui ambako gharika ingenipeleka. Kutoka kwa kina cha moyo wangu, nilionyesha shukrani yangu na sifa, nikimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa ya pili katika maisha.

Baadaye, nikasikia maelezo ya mtoto wangu kuhusu mvua hiyo: Siku hiyo, baada ya kurudi nyumbani kutoka kutimiza wajibu wake, alikwenda msalani kwanza. Mara tu alipotoka chooni na kurudi kwenye chumba chake alisikia sauti kubwa nje. Alipotoka nje kwenda kuangalia, aliona kwamba jengo zima la choo lilikuwa limeanguka kabisa chini ya maji. Isingekuwa kwa ulinzi wa Mungu, angekufa. Ilikuwa hasa kama Mungu alivyosema katika mojawapo ya maneno Yake: “vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, vitafanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Msisimko wa kuzidi kiasi niliouhisi ndani ya moyo wangu hakika hauwezi kuelezwa kwa maneno.

Kupitia matukio haya mawili, imani yangu imekuwa imara hata zaidi. Siku hiyo, Mungu alikuwa ameniruhusu kuokoka maafa hasa kuniruhusu mimi kutoa ushahidi kwa ajili Yake. Siwezi kupuuza dhamiri yangu. Ninapoangalia nyuma juu ya jinsi nilivyokuwa na ubinafsi, ukatili, na hali ya kujidai nilivyokuwa awali kwa kawaida nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, ninatambua kuwa sikuhisi kamwe busara ya Mungu ya umuhimu au kushiriki mawazo ya Mungu. Kuanzia sasa kwendelea, napenda kutubu na kubadilika. Nitatumia uzoefu wangu binafsi kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu, na kufanya wajibu wangu katika kazi ya kueneza injili.

Maudhui Yanayohusiana

 • Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

  Tabia ya Mungu ni haki na, hata zaidi, upendo. Bila kujali Yeye hufanya nini, ni wokovu kwangu; ni kuniruhusu kumjua Yeye, kumtii Yeye, na kumpenda. Sasa, baada ya kupata uzoefu wa kazi ya Mungu na kufurahia ukarimu Wake, matumaini yangu tu ni kufanya liwezekanalo ili kutimiza majukumu yangu kama kiumbe kilichoumbwa ili kuulipa upendo wa Mungu, ili kuuridhisha moyo wa Mungu, na kutenda sehemu yangu katika kueneza injili ya ufalme wa Mungu.

 • Moto Ulioshtua Taifa katika Wilaya ya Ji, Mji wa Tianjin

  Nguvu za Mungu ziko kila mahali; hekima ya Mungu haiwezi kueleweka na kiumbe yeyote. Ingawa mara nyingi sisi humsahau Mungu katika maisha yetu ya kila siku, Mungu hututunza daima, akitulinda, akiwa kwa upande wetu, bila kutuacha kamwe. Tukimwamini Mungu, wakati maafa yanapotokea, Mungu atatuokoa kwa njia zote na kutuponya kutokana na maafa. Mnamo siku ya moto, ndugu wengi wa kiume na wa kike waliyaona matendo ya Mungu.

 • Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

  Kwa kweli tuliona upendo na wokovu wa Mungu. Kama haingekuwa Mungu kutuchunga na kutulinda hakuna hata mmoja wetu angeweza kuishi. Familia nzima ilimshukuru Mungu kwa dhati. Ni Mungu aliyetupa fursa hii ya maisha, tunapaswa kuihifadhi kwa upendo, na kufanya liwezekanalo kuanzia sasa kuendelea ili kufanya wajibu wetu na kumridhisha Mungu!

 • Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

  Kwamba neno la Mungu huahidi watu kwamba Mungu hutunza na hulinda, kwamba Mungu hutawala vyote, kamwe halitakuwa tena fungu la maneno tu kwangu. Katikati ya maafa haya nilipata nuru kwa wingi. Nilipata uzoefu kwamba tukiweka mustakabali na jaala zetu mikononi mwa Mungu, sio kuandaa mbadala na mipango kwa ajili yetu wenyewe, lakini kutafuta ukweli na kumridhisha Mungu kikamilifu, basi bila kujali ni hali ipi Mungu atatufadhili, kutulinda, na kutusaidia wakati wa matatizo yoyote. Kwa sababu Mungu ni mwenye haki kwa kila mtu.