Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

218 Kubadilishwa kwa Hukumu

1 Nilimwamini Bwana kwa miaka mingi, kila wakati nikitamani sana thawabu za Bwana na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Nilijitahidi na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya sifa na hadhi, na kamwe sikuyatia maneno ya Mungu katika vitendo. Nilisema nilimpenda Mungu, lakini majaribu yalipokuja, moyo wangu ulijawa suitafahamu na malalamiko. Nikibishana na Mungu, nilisema vitu vingi vya uasi. Kwa kupitia hukumu mbele ya kiti cha Kristo, nilipata kujijua mwenyewe. Maneno ya Mungu yalikuwa kama upanga mkali wenye makali kuwili ulioupasua moyo na roho yangu. Hukumu kali ya Mungu iliweka wazi ukweli wa unafiki wangu. Nilijishughulisha huku na kule ili nipate baraka, lakini nilisema niliteseka kwa ajili ya upendo wangu kwa Mungu. Sikuwa mwaminifu, na kila kitu nilichofanya ilikuwa ili kumdanganya na kumhadaa Mungu. Nilimwamini Mungu lakini nilifanya mapatano na Mungu—sikuwa na dhamiri au mantiki hata kidogo. Nilimwumiza Mungu sana na nikapoteza ubinadamu wangu kabisa, na nilijawa majuto. Bila mahali pa kuficha aibu yangu, nilianguka mbele za Mungu na nilikuwa tayari kukubali hukumu ya Mungu.

2 Mungu anapitia aibu na uchungu mkubwa mno ili kuwaokoa wanadamu. Anavumilia auitafahamu na malalamiko ya mwanadamu, na Anasubiri kimya mwanadamu aamke. Hukumu na kuadibu kwa Mungu ni ili tu wanadamu waweze kupata ukweli na uzima. Sasa kwa kuwa ninaelewa bidii nyingi ambazo Mungu huweka, nimeazimia kufuatilia ukweli. Kwa kupitia hukumu na majaribu, tabia zangu potovu zinatakaswa. Kujiendesha kulingana na ukweli wa maneno ya Mungu humfurahisha Mungu na kunipa hisia tamu zaidi moyoni mwangu, na ni sasa tu ndipo nafahamu kwamba hukumu na majaribu ni baraka za Mungu. Upendo wa Mungu ni halisi sana—tutakosaje kutoa shukrani na sifa? Niko tayari kuutoa moyo wangu na mwili wangu kutangaza na kumshuhudia Mungu ili nilipe upendo Wake. Nitakumbuka vyema kusihi kwa Mungu na kutekeleza wajibu wangu kwa uaminifu kumridhisha Mungu. Nitayajali mapenzi ya Mungu na kutoa ushuhuda mzuri na mkuu kwa ajili Yake. Ingawa njia ina milima na mabonde, natamani kumpenda Mungu milele.

Iliyotangulia:Hukumu Iliuzindua Moyo Wangu

Inayofuata:Maneno ya Mungu Yaliuzindua Moyo Wangu

Maudhui Yanayohusiana

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. 1 …

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…